Kikwete amefanikisha lipi tangu aingie madarakani!?

kawaida ya viongozi wa TZ baada ya nyerere ni kuharibu hasa inapokuja awamu ya pili ya uongozi.najua huyu bwana ataendelea lakini namuonea huruma rais atayekuja 2015 kazi atakayokuwa nayo ya kujenga nchi ni kubwa sana.sasa naanza kujua kwanini watu wa pwani wanawadharau sana wakwere.pwani mkwere hata akiwa na PHD ya Neuro Surgery utamjua kwa uswahili wake tu.ovyo kabisa
 
kUBWA ANALOJIVUNIA BWANA JK NI KUWA KIONGOZI WA KWANZA WA KIAFRICA KUINGIA IKULU YA MAREKANI CHINI YA OBAMA, VINGINEVYO ,HAKUANA, NI SIFURI KABISA
 
Ndugu zanguni nimeona sasa nianze kuangalia hii miaka mitano inaishia sioni allicchokifanya rais wetu ukiacha safari za nje za kila siku..labda tusaidiane kwa hili...nimejaribu kuangalia hata miradi ya mikoani kama mmoja wa juzi mradi wa maji...alieenda kufungua lakini umeanzishwa na fisadi BWM.
Chuo kikuu cha DODOMA kakuta BWM akamalizia...kila sehemu yeye anamalizia nini anachoakianzisha yeye mwenyewe awe ameweka pale kwa ajili ya safari na PER DIEM....../

Hekima yangu inaniambia kuwa hoja hii ikijadiliwa vizuri italeta heshima kwetu zote ndani ya jamii forum na pia itabadili fikara za watu ambao wana mapenzi yasiyokuwa na mashiko. Binafsi nimekuwa najiuliza anachokifanya mkuu wetu sijakijua labda bado anajipanga. Historia inaonyesha kuwa kipindi cha pili kwa watawala wetu ni kipindi kinachotumika kujilimbikizia mali kwa wote wanaomzunguka mkuu wa kaya na yeye mwenyewe.

Kama BWM angepewa kipindi kimoja tu bila kujijua, angekuwa mtawala bora wa karne lakini kipindi cha pili kiliharibu kabisa kazi zake nzuri za kipindi cha kwanza.

Labda umefika wakati wa watanzania kumpima vyema raisi wtu na kuamua ama awe wa kipindi kimoja au vipindi viwili. hapa hoja ya vyama isiingie kabisa, hoja hii ni kwa masilahi ya taifa na vizazi vyetu sote.

Wale wanaofaidikwa utawala uliopo, wajue wana nafasi ya kufaidi zaidi ya hicho kama watasaidia dhamira ya dhati ya kulikomboa taifa hili.

MIAKA MITANO KWA UHAI WA MWANADAMU NI MINGI SANA, mtoto aliyezaliwa wakati kikwete anachaguliwa leo hii ana mabadiliko mengi sana ingawaje kila kitu anafanyiwa VIPI KWA TAIFA LINALOENDESHWA NA WTU WAZIMA.

HOJA HII NI MUHIMU,IJADILIWE.
 
Kama Mtanzania namba moja tunamfikiria hivi, hajafanya chochote miaka 4 ya utawala wake, tuwafikirieje wale mamilioni waliomsikiliza, kumuamini, kumuunga mkono, kumchagua na kumshangilia mwaka 2005?

JK ni kioo tu. Ambaye hajafanya chochote miaka 4 iliyopita ni sisi wenyewe.
 
Jamani mimi nadhani mnasahu mengine makubwa ambayo Mh. Rais wetu ameyafanya.

Mambo ya diplomasia. Ni mambo ambayo kwa juu juu yanaweza yasionekane machoni petu, kwani kwa siye tuliowengi tumezoea kuona majengo na vitu vingine vinavyoonekana ndiyo tunakubaliana na utendaji kazi wa mtu.

Mh. Rais Kikwete ameonesha diplomasia ya hali ya juu sana kwa yote aliyojihusisha nayo. Hata lile swala la kukomboa visiwa vya Comoros ni moja ya mambo ya kidiplomasia baina ya Mataifa.

Ni kweli vita ya kukomboa visiwa vile imegharimu Taifa letu mabilioni, bila kusahau maisha ya askari wetu. Najua GT ni moja ya wachache waliopinga sana hii vita, ila ukweli wa mambo ni kwamba this is one of the biggest diplomatic endeavours our country has ever engaged in. Pro na cons za hii vita zimeongelewa kwenye thread husika.

Kuna swala la mazungumzo ya kuiwezesha Kenya kuepukana na civil war. Credit nyingi amepewa Koffi Anan, lakini ukweli unabakia palepale kwamba, Tanzania under Kikwete ilikuwa mstari wa mbele kuona suluhisho linapatikana mara moja.

Kingine ni diplomasia katika mikutano mbalimbali ndani na nje ya Afrika. Ndiyo, kwamba katika kufanikisha haya safari nyingi ambazo nyingine tunazipinga vikali zilijitokeza. Hata hivyo hatuna budi kukubali na kutambua mambo ya kuendeleza diplomasia yanayojitokeza au kuendana na mawasiliano ya aina hii.

Uhuru wa vyombo vya habari. Nadhani hili swala ni kubwa kuliko wengi wetu tunavyofikiria. Bila kuwezesha hili liwepo, hivi sasa sidhani kama tungelikuwa tunaandika haya mambo hapa JF under Mh. Mkapa au Mwl. Nyerere! Mh. Rais Kikwete amebariki uwepo wa uhuru wa vyombo vya habari. Kitu cha kuzidi kuombea kitokee kuhusiana na hili akiwa bado yuko madarakani ni kule kubadilishwa/kurekebishwa kwa Sheria ya vyombo vya habari ya 1976. Tuzidi kumsihi Mh. JK afanikishe hili.

SteveD.
 
Ndugu zanguni nimeona sasa nianze kuangalia hii miaka mitano inaishia sioni allicchokifanya rais wetu ukiacha safari za nje za kila siku..labda tusaidiane kwa hili...nimejaribu kuangalia hata miradi ya mikoani kama mmoja wa juzi mradi wa maji...alieenda kufungua lakini umeanzishwa na fisadi BWM.
Chuo kikuu cha DODOMA kakuta BWM akamalizia...kila sehemu yeye anamalizia nini anachoakianzisha yeye mwenyewe awe ameweka pale kwa ajili ya safari na PER DIEM....../


Nadhani kajitahidi kuliko marais wote duniani, kwani ni yeye pekee ambaye ameweza kutangazwa zaidi kwenye web site ya ZEUTAMU..! Ulitaka awe maarufu kiasi gani zaidi ya pale..!
 
Kukutana na watanzania ughaibuni na kuwa mtaalam wa kujibu maswali yao bila dukuduku na kuwaacha wakimshangilia na kusahau yote yanawaletea machungu huko bongo...

Aliwaambia WABONGO huko USA wasahau mambo ya ujenzi wa mabarabara ya lami maana hayo ni makubwa sana kwa wa ughaibuni kuyamudu ... wajenge vijinyumba tu bongo maana huo ndo uwezo wao baada ya kupiga box...

Haya pia ni maendeleo yake... Nani anapinga?
 
kuna mahakama ya biashara natumai ilikuwa ndo moja ya focus ya jamaa ili kuvutia uwekezaji na kuspeed up economic growth..(BEST programme hiyooooooooo)

So tayari uchumi umekua?

najua mwaka huu tu uchumi wetu utashuka kwa zaidi ya asilimia 2% ( sijui wajumbe mnasemaje hapo) mahakama hiyo imeleta tija gani; ni nani y upo hapo mahakamani na unaweza kutupa labda kwa uelewa wako mpaka sasa wamevutiwa wawekezaji wangapi au ndio mawazo ya kufikirika tu
 
Amefanya mengi tatizo alituhahidi mengi zaidi. Tatizo ni mfumo mzima wa uongozi Tanzania, "IT CAN BE DONE-PLAY YOUR PART" Deep Green bado imeshika hatamu so yeye kama yeye hawezi kufanya mageuzi katika kipindi hiki kifupi cha 4 yrs. Lets help him from our base as individual.
 
Na John Kibaso
MwanaHALISI

NIMELAZIMIKA kuandika makala hii baada ya kubaini upotoshaji mkubwa kutoka kwa baadhi ya wasomaji wa MwanaHALISI wakichangia makala ya Salva Rweyemamu aliyempinga mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Professa Ibrahim Lipumba ambaye alisema "Rais Jakaya Kikwete ameshindwa kazi."

Nashawishika kukubaliana na Rweyemamu kuhusu utendaji kazi wa Rais Kikwete. Hakika binafsi navutiwa sana na staili ya uongozi wake; haina tofuati na utawala wa rais mtaafu wa Marekani, Bill Clinton na Marehemu John Kennedy.
Wote hawa walikuwa na falsafa ya kuwapa uhuru wa dhati raia wao na mara zote walitaka kujua watu wanasemaje (what people talk about you).

Kikwete amefanikiwa katika maeneo matatu muhimu ya kisiasa, kiuchumi na kijamii.
Kwa mtizamo wangu, Rais Kikwete amefanikiwa kumudu vizuri siasa ya nchi yetu. Nionavyo mimi anatumia mfumo wa wengi wape kwa kuzingatia miiko na maadili ya uongozi ya kutoingilia mihimili mingine ya nchi.
Ni katika utawala wa Kikwete uhuru wa dhati wa vyombo vya habari na wananchi wameweza kutoa maoni yao bila kuingiliwa na dola. Kikubwa katika siasa ya sasa ni viongozi kukubali kutoa mwanya wa mawasiliano ili wananchi waweze kupata habari sahihi (bila) kuingiliwa na dola.

Dhana ya siasa safi na uongozi bora, siri yake ni serikali kuweza kusimamia haki na usawa kwa raia na kuwapa uhuru wa kutoa maoni yao; jambo ambalo rais Kikwete ameliweza kwa kiwango kikubwa.

Hivi karibuni zimeibuliwa hoja kiasi cha kuidhalilisha serikali (lakini) bado Kikwete amekubali kuacha mlango wazi bila kukurupuka ili wananchi wapate nafasi ya kuikosoa serikali yao.
Viongozi wengi duniani hawawezi kuhimili mashambulizi. Kikwete ameweza hili.
Hata hoja ya ufisadi ambayo imekitikisa hata chama chake – Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kikwete kwa kutambua mgawanyo wa mhimili ya madaraka, ameiachia vyombo husika kufuatilia ili haki ipatikane bila kuhujumu upande wowote.

Huu ndio utawala wa sheria. Siyo busara rais kuingilia haki za watu kabla hawajapatikana na hatia kwenye vyombo husika. Huko ni kuingilia uhuru wa vyombo hivyo.

Kuhusu mafisadi ndani ya chama, hili ni tatizo kwenye vyama vingi duniani kwani mfumo wa uendeshaji vyama hautenganishi serikali na chama tawala.

Mara nyingi viongozi wa chama wanakuwa na mwingiliano na serikali. Hapa Kikwete ameruhusu vyombo vya dola kufanyakazi yao bila kuviinglia. Huwezi kuamua kuburuza mtu mahakamani bila ushahidi.

Sisi sote ni mashuhuda wa serikali ya Kikwete; hakuingilia kati kuzuia viongozi waandamizi na makada wakubwa wa chama kupelekwa mahakamani kama ilivyofanyika kwa Daniel Yona na Basil Mramba.
Kwenye nyanja ya uchumi, pamoja na uchumi wa dunia kuyumba, serikali ya Kikwete bado imehimili kusimamia mfumuko wa bei.
Hivi sasa, mfumuko wa bei unapanda kwa kasi ndogo lakini dhamira ya dhati inaonekana, kwamba unaweza kupungua. Dhamira hizo ni kwa kufanya mabadiliko kwenye mfumo wa utendaji ndani ya BoT, husuani kwenye sekta ya madini.
Dhamira ya Kikwete katika kupambana na umaskini (inajidhihirishani) pale alipotangaza bajeti mbadala sambamba na bajeti ya serikali ili kuimarisha sekta ya kilimo na sekta ya walala hoi (vulnerable).

Ni Kikwete aliyetoa mabilioni ya (shilingi) ili kufikia wajasiriamali wenye kipato cha chini na kuwakopesha.

Jitihada zake zimeenda mbali kwa kuimarisha Saccos na uanzishaji wa Benki za Wananchi. Hizi ni jitihada zinazoleta matumaini.
Tatizo la kuyumba kwa uchumi limezikumba nchi nyingi hata nchi kubwa matajiri za Magharibi.

Hivi karibuni Rais Obama alitangaza kuongeza bajeti ya kukwamua hali hiyo mbaya katika nchi yake. Hatua aliyochukua Rais Obama haina tofauti na hatua aliyochukua Kikwete. Ni vema Lipumba na wenzake wakampa muda ili mafanikio yaweze kupatikana.
Umakini wa serikali ya Kikwete umewezesha nchi yetu kusimama kidete, kupinga matumizi huria ya ardhi kwa nchi za jumuiya ya Afrika Mashariki. Huu ni uthibisho wa uamuzi wa kijasiri kupitia Kikwete.
Kwenye eneo la tatu la jamii, nathubutu kusema kwamba Kikwete amefanya mapinduzi makubwa kuhakikisha kwamba jamii inaishi kwa usalama.
Serikali ya Rais Kikwete imeweza kusimamia usalama wa raia kwa kupambana na majambazi. Bila usalama kamwe hakuna maendeleo yanayoweza kupatikana.
Serikali imejitahidi kusuluhisha migongano ya wanafunzi na migongano ya wafanyakazi.
Hapana shaka penye siasa safi na uongozi bora mara zote wafanyakazi au wanafunzi vyuoni hupewa nafasi kutoa hisia zao kupitia njia ya migomo, maandamano au press bila kubugudhiwa na dola.
Mara zote serikali ya Rais Kikwete imejitahidi kusuluhisha migongano hiyo kwa njia ya kistaarabu kwa kuweka mambo hadharani bila kukandamiza upande mwingine.
Juhudi za dhati zimeonekana katika kuongeza mara dufu shule za sekondari za Kata. Katika hili, sina budi kumpongeza aliyekuwa waziri mkuu Edward Lowassa kwa juhudi za pamoja katika kufanikisha zoezi hili.
Ni kweli bado kuna matatizo ya hapa na pale lakini ukweli unabakia kwamba juhudi kubwa imeonyeshwa na serikali katika ujenzi wa sekondari hizi. Kila kitu kina mwanzo wake, baada ya majengo itafuata miundombinu.
Kwenye matatizo ya kijamii, siku zote Kikwete ameweza kujishusha na hata kuacha ziara zake muhimu za serikali kwenda kuhani waliopotelewa na wenziwao.
Mara nyingi viongozi wengi kwa nafasi ya urais ni nadra sana kuona wanashiriki katika shughuli za maziko, harusi au sherehe za kijamii, lakini Kikwete amedhihirisha kuenzi utamaduni wa Mwafrika wa kuwafariji wanaopatwa na matatizo bila kujali uwezo wao kiuchumi.

Nasisitiza msimamo wangu wa kukubaliana na mawazo ya Rweyemamu, kwamba Rais Kikwete, katika muda aliokaa madarakani, ameonyesha dhamira halisi ya kumudu majukumu yake kama alivyotumwa na wananchi.

Rais Kikwete anatumia busara nyingi pale anapokuwa anatoa taarifa ya serikali katika mambo ya msingi. Kikwete hakurupuki.
Ni majuzi tu amekubali kuondoa suala la ushuru lililokuwa limekwaza madhehebu ya kidini na (serikali) ikakubali kusikiliza hoja zao na hatimaye kuliondoa kwenye bajeti yake.

Naamini kwa busara zake suala la ufisadi ndani ya chama na serikali hatima yake itajulikana kwa wananchi.
Si kweli kwamba Kikwete ameshindwa kuwadhibiti mafisadi, bali ni mfumo uliolazimishwa na nchi tajiri za Magharibi ambao dhahiri ni mfumo wa kibepari.

Katika mazingira ya kawaida, inakuwa vigumu kumtambua fisadi ni yupi hasa pale mtu anapokuwa na kitega uchumi chake.
Ufisadi ni uharamia. Ni ujambazi; ni suala ambalo linahitaji nguvu za raia wote kusaidia serikali yao kulitokomeza. Ni vema basi, tumuunge mkono Kikwete ili aweze kufanikisha adhima yake ya kuutokomeza.
Mjadala unaendelea
 
Wanaombeza kikwete wakome!Nitawaeleza mafanikio yake,
KISIASA:
1.Kamaliza mpasuko wa kisiasa zanzibar kama alivyoahidi
2.Amefanikiwa kuunda tume huru ya uchaguzi ili watz wapate viongozi wanaowataka
3.Amezidi kukiimarisha chama chake kikongwe ccm na tangu ameingia madarakani hakuna makundi tena, zile kambi alizivunja palepale na sasa ccm ni kula kuku kwa mrija
4.Kafanya ziara nyingi sana marekani kwa muda mfupi kuliko marais wote waliotangulia na hii imetusaidia kupata ufadhili mkubwa na umaskini umepungua sana
5.Alizingatia zaidi uwezo katika kuteua wateule wa kumsaidia kuendesha nchi,hakujali rafiki zake wala watu wa dini yake na ndio maana serikali yake iko imara
6.Mafisadi wote wamekamatwa na wamefikishwa mahakamani kama vile kagoda,meremeta,downs&richmond ambao waliibia taifa fedha nyingi
KIJAMII:
1.Ameongeza vitanda mahospitalini na hakuna tena wagonjwa wanaolala chini au wanaolala wa3 kitanda kimoja
2.Hospitali za serikali dawa ni bure kama serikali inavyosema na zote zinapatikana
3.Hospitali kuna vifaa vyote muhimu kwa wagonjwa
4.Shule zimekuwa nyingi kuliko melezo kwani kila mtanzania sasa anapata elimu
5.Kuna waalimu wa kutosha katika kila shule
6.Vitabu vya kiada na ziada vipo vya kutosha labda washindwe walimu wenyewe
7.Katika shule kuna maabara ili nchi iendane na karne hii ya sayansim na technolojia
8.Walimu na madaktari wameboreshewa maslahio yao japo kwa sasa yanakaribia ya waheshimiwa wabunge
9.Amekemea sana kuhusu mambo ya kuigawa jamii kama vile dini,alikataa katakata kuweka mambo ya dini kwenye ilani ya chama chake ccm
KIUCHUMI:
1.Kauli mbiu yetu ya maisha bora kwa kila mtz sasa imetimia wote tu mashahidi
2.Hakuna tena mikataba ya kinyonyaji maana aliahidi kupitia mikataba yoye ya madini
3.Pesa walizorudisha mafisadi zimepelekwa kwenye kilimo sote tunajua na tumeona jinsi kilimo kinavyozidi kuliongezea taifa pato lake
4.Bei za pembejeo za kilimo zimepungua sana ili kufanikisha kilimo kwanza
5.Sasa kuna umeme wa kutosha na wa uhakika na hatutegemei tena kusumbuliwa na dharula itakayo tulazimisha kuagiza tena mitambo ya poormond badala ya richmond
6..................
Add more mafanikios on jk's leadership...........
 
wanaombeza kikwete wakome!nitawaeleza mafanikio yake,
kisiasa:
1.kamaliza mpasuko wa kisiasa zanzibar kama alivyoahidi
2.amefanikiwa kuunda tume huru ya uchaguzi ili watz wapate viongozi wanaowataka
3.amezidi kukiimarisha chama chake kikongwe ccm na tangu ameingia madarakani hakuna makundi tena, zile kambi alizivunja palepale na sasa ccm ni kula kuku kwa mrija
4.kafanya ziara nyingi sana marekani kwa muda mfupi kuliko marais wote waliotangulia na hii imetusaidia kupata ufadhili mkubwa na umaskini umepungua sana
5.alizingatia zaidi uwezo katika kuteua wateule wa kumsaidia kuendesha nchi,hakujali rafiki zake wala watu wa dini yake na ndio maana serikali yake iko imara
6.mafisadi wote wamekamatwa na wamefikishwa mahakamani kama vile kagoda,meremeta,downs&richmond ambao waliibia taifa fedha nyingi
kijamii:
1.ameongeza vitanda mahospitalini na hakuna tena wagonjwa wanaolala chini au wanaolala wa3 kitanda kimoja
2.hospitali za serikali dawa ni bure kama serikali inavyosema na zote zinapatikana
3.hospitali kuna vifaa vyote muhimu kwa wagonjwa
4.shule zimekuwa nyingi kuliko melezo kwani kila mtanzania sasa anapata elimu
5.kuna waalimu wa kutosha katika kila shule
6.vitabu vya kiada na ziada vipo vya kutosha labda washindwe walimu wenyewe
7.katika shule kuna maabara ili nchi iendane na karne hii ya sayansim na technolojia
8.walimu na madaktari wameboreshewa maslahio yao japo kwa sasa yanakaribia ya waheshimiwa wabunge
9.amekemea sana kuhusu mambo ya kuigawa jamii kama vile dini,alikataa katakata kuweka mambo ya dini kwenye ilani ya chama chake ccm
kiuchumi:
1.kauli mbiu yetu ya maisha bora kwa kila mtz sasa imetimia wote tu mashahidi
2.hakuna tena mikataba ya kinyonyaji maana aliahidi kupitia mikataba yoye ya madini
3.pesa walizorudisha mafisadi zimepelekwa kwenye kilimo sote tunajua na tumeona jinsi kilimo kinavyozidi kuliongezea taifa pato lake
4.bei za pembejeo za kilimo zimepungua sana ili kufanikisha kilimo kwanza
5.sasa kuna umeme wa kutosha na wa uhakika na hatutegemei tena kusumbuliwa na dharula itakayo tulazimisha kuagiza tena mitambo ya poormond badala ya richmond
6..................
Add more mafanikios on jk's leadership...........

kijamii...... Suala la ujambazi na ufisadi amefanikiwa mkuu???
 
Na kwa kuomba misaada nchi za nje amefanikiwa kwa kuonesha kuwa yeye ni Matonya nambari wani...
 
basi tu ingekuwa open debate ya hali ya sasa nadhani lazima ngumi zingekuwa zinapigwa! lazima haiwezekani ukamfananisha JK na Clinton au Kennedy! people are not serious wakishiba wao hawaelewi maisha ya watanzania wengine!

Huyo mwandishi anatafuta kula, na hii si ajabu maana hata mbwa akitaka attention ya bosi wake anachezesha mkia!
 
_hamnamadawati.jpg


Shule ya msingi kunzugu ipo ndani ya wilaya ya Bunda tarafa ya serengeti.

Hasa katika idara hii ya elimu, bado kabisa Kikwete hajafanikiwa. Hadi leo hii bado watoto wanakaa chini hakuna desk. Vigogo wapo tu wanafisadi nchi.
 
Ngoja kwanza niende kilabuni pale uwanja wa fisi nikapate kill-me-quick kidogo. Nikishapata chupa kadhaa basi huenda nikayaelewa vizuri niliyosoma hapo juu kwa sababu sasa hivi wakati akili yangu bado i timamu, mambo hayo hayapandi kabisa.
 
na sasa inajengwa barabara ya lami kabisa kupitia ikulu ya kwake,si mlimsikia Sendeka? na si mlisikia majibu ya Sitta baada ya kupokea riport ukweli upo palepale.Sendeka hakukosea wala serikali haikukosea,
''mwenye macho haambiwi tazama'',nchi isha uzwa hii.....
Kwa kuongezea, kujenga ikulu kijijini kwao msoga/msata. Waliomtangulia wote, mwalimu, ruksa na anbem hawakuthubutu kufanya hivyo huyu peke yake ndio ameliweza. I think he should be remembered for that. Nchi chovu na ya kimaskini kama hii rahisi (sio rais) kujenga 14 presidential houses kijijini kwake si kitu kidogo ati. Hivi kwa wanaojuwa zinazinduliwa lini rasmi? I would wish to attend.
 
Huyu mtu naona akili pamoja na mawazo yake yamestuck coz while tunaenda mbele yeye yuko nyuma some mo years back,hivi anafikiri bado ni waziri wa mambo ya nje (receptionist)nini?Anachokiweza ni kupokea akina Hasheem Thabit na kutamani kuhudhuria misiba ya kina Wacko Jacko even though hawajamualika!!
 
Back
Top Bottom