Kikwete alivyomfunga mdomo Membe sakata la rada

Jamani watanzania mbona tunarudishana kulekule?? ifike sehemu tuwe tunajiridhisha tu, hatuwezi tukasubiri eti Mr. DHAIFU awataje watu ambao tayari keshawapa na vyeo tena vikubwa. Ukweli ni kwamba hawa watu walishakubaliana kulindana LIWALO NA LIWE. cha kufanya hapa tujipangeni kuwapiga chini 2015 au kabla ya hapo halafu tuwapeleke kortini. watatajana tu. hii staili ya kumuuliza mwizi kama ameiba huku unamchekea unategemea atakubali kweli?? NASHAURI TUTUMIE NGUVU NYINGI KUWAPA WATU ELIMU YA URAIA WAJUE WANAVYONYONYWA RASILIMALI ZA TAIFA LAO NA HAWA WAKOLONI WEUSI. WATAKAPOELEWA ITAKUWA RAHISI KUWAONDOA MADARAKANI NA KUWAFIKISHA KORTINI.

Unazungumza very intelligently and practically. Elimu ya uraia ndiyo suluhu kuhitimisha huu upuuzi unaoendelea hapa Tanzania. Haiwezekani nchi yetu yenye utajiri wa ajabu (mali asili) duniani kote hakuna mfano halafu CCM inatuchezwa kiasi hiki bila hata aibu. Wananchi tumekuwa wapole, waadilifu na subira nyingi lakini tunaonekana wajinga. Hatuna sababu ya kumwaga damu kudai haki yetu tutumie ustaarabu wa kupiga kura, tuwashikishe adabu CCM. Ili hii itokee kuwe na mkakati maalum wa kutoa elimu kwa umma. Hata kama wengi wamenyimwa elimu ya darasani kiana na hawa watawala wana akili za kupambanua mambo.
 
PCCB walikuwa wanafanyia uchunguzi jambo hili! halafu kesho tuambiwe PCCB inafanyia kazi jambo jingine! phew!
PCCB ina kazi ya kukamata walimu, wauguzi na manesi, period! upotevu wa fedha
Hivi clare short alipojiuzulu alikuwa mjinga! ushahidi gani na pesa zilizoibiwa zimerudishwa.

Watanzania, wakati wa ununuzi wa rada JK alikuwa waziri wa mambo ya nje. Anafahamu kila uchafu uliofanyika na nadiriki kusema yeye ni sehemu ya.

Alipoingia madarakani kitu cha kwanza ni kuonyesha hasira kuhusu wizi wa fedha za rada na kusema ni lazima zirudi. Kumbu kumbu zipo. Alifanya hivyo kuwafurahisha wananchi wamuone kiongozi mzuri na shupavu, kuwapooza wananchi

Sasa amerudi kuwafariji marafiki zake akina EC/RA/EL. Anakana hakuna wizi wakati yeye anajua wizi ulikuwepo, alishuhudia akiwa waziri na rais.

Tukifika hapo wapo wanaosema JF inaponda kila jambo, lakini tuseme ukweli hivi katika historia ya nchi hii JK atakumbukwa kwa nini zaidi ya UDHAIFU na Kudumuza nchi, zaidi ya unafiki na kulea uhalifu na wahalifu. Kuna kitu gani huyu mheshimiwa analitendea taifa ?

Kila mara nasema JK ameufanya Urais uonekane kazi ya kila mtu ndio maana kila mtu hata mjinga au mwendawazimu anafikiria kuwa na kundi ili awe Rais. Nini kitamshinda!
 
Back
Top Bottom