Kikwete alijua na kuruhusu jengo la ubalozi Italy kununuliwa

Tumeshasikia kashfa nyingi sana za huyu mshikaji, uuzaji wa wanyama pori, Richmond, miaka mitatu nje ya nchi, kashfa ya suti, mikataba mibovu ya madini, utendaji mbovu, ushikaji, wizi wa kura, mauaji ya arusha na songea, EPA. Yote haya alistahili kujiuzulu, hata likiongezeka hili nothing can be done, as usually days are going
 
Bila hizo Pesa asingeweza Kuchaguliwa; sababu walihonga, walitengeneza khanga, T-Shirt, kofia, na sherehe kila Wilaya ili ashinde....

Tatizo ni Wabaya wa Mahalu aliyekuwa ikulu ndie aliyefungua hiyo kesi na huyo Jamaa yuko Ubalozini hajabadilishwa kazi, Anaelekea Mwaka wa 6 sasa bila hata kubadilisha station.

Sina uhakika kama kweli wewe ni mtu mzima uliyefikia umri wa kupiga kura au umeshawahi kupiga kura. Katika chaguzi zote tumekuwa tukishuhudia utengenezaji wa Kofia, khanga na T-shirts kwa vyama vyote vya siasa vyenye wagombe na wengine hutengeneza hata scarf... kinachotofautiana ni viwango na wingi wa vitu hivyo na hii hutokana na uwezo wa vyama hivyo kulingana na ruzuku wanazopewa.

CHADEMA leo wanalaumiwa kwa kutumia milioni 19 kumpeleka MREMA akafanye phisibility study Arumeru ili waweza kuamua ni nani wamsimamishe kumkabili mgombea wa CCM, je hayo si matumizi ya fedha?
 
Duh, MAMA POROJO, je kudanganywa kwenyewe ni kama hii hapa chini? Yaani alidanganywa akiwa Waziri wa Mambo ya Nje na hadi leo anadanganywa akiwa Raisi - je hagutuki? Bila shaka hapa anayelaumiwa ni mzungu wa watu, LOL...

ru76er.jpg

Ni kosa la wasaidizi wa Rais ambao kwa itifaki wanatakiwa kuona haya. Jk ni binadamu kama tunavyokosea kuona mambo kwa usahihi sehemu zetu za kazi.

Hili ni suala la kuwaajibisha waliondaa shughuli hii ikiwemo benki yenyewe na pia aliyeoko pembeni mwa JK anawajibika kwa kadhia hii.
 
Tumeshasikia kashfa nyingi sana za huyu mshikaji, uuzaji wa wanyama pori, Richmond, miaka mitatu nje ya nchi, kashfa ya suti, mikataba mibovu ya madini, utendaji mbovu, ushikaji, wizi wa kura, mauaji ya arusha na songea, EPA. Yote haya alistahili kujiuzulu, hata likiongezeka hili nothing can be done, as usually days are going

Mada moja habari mbalimbali. ungepata kazi kubwa ku-defence thesis yako kama unaweza kuchanganya mambo kiasi hiki.

Hadidu ya rejea hapa ni tuhuma za udanganyifu wa ununuzi wa jengo la ubalozi wewe unachomeka mada.

hakuna jambo tunalohitimisha watanzania kazi ni kubishana bila mpangilio mwishowe tunakosa jibu la jambo lililo mbele yetu
 
Tangu lini kiongozi akiruhusu manunuzi ndio karuhusu uwizi? Akili za mahalu hazina akili. serikali ya Mkapa ndiyo iliruhusu ununuzi huu JK alikuwa mwakilishi wa serikali kuona kinachoendelea na kwa kawaida Jk alipewa briefing na wanaotuhumiwa kufanya udanganyifu..... Mahalu partners and company.

Hivi tunategemea Mahalu angeweka wazi uwizi huo au angefanya jitihada kubwa kuhakikisha briefing inaficha maswali yote ya udanganyifu?

Huyu jamaa ni profesa wa sheria wataalamu wa mambo ya kugushi duniani kote
 
kuna tapeli mmoja pale kibaha aliwaibia sana watu akijifanya yeye ni mdogo ake kikwete.sasa mahalu nae ameanza
 
True, this is too much. Kila siku Kengemumaji kazi yake ni kumtetea Kikwete...dont you see where our beloved country is headed to? Remember the buck stops with the President!

Mimi simtetei Kikwete ila ninachoshwa na jinsi watu wanavyokosa yakusema hapa JF hata kufikia hatua ya kuleta vitu vya kuokoteza okoteza tu.... mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni...

Mahalu ahukumiwe kwa makosa yake ambayo hata akiwasingizia watu wengine haitamsaidia.
 
Hakuna kesi hapa hii ni misuguano ya kisiasa na mambo ya ngono tu, haiwezekani hata siku moja balozi inunue jengo bila kumhusisha waziri wa mambo ya nje.

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Hi kesii inatakiwa kufutwa kwani Mkapa alishasign ushahidi wake kwenye affidavit akimtetea Mahalu; wafunge hii kesi inapoteza muda na fedha za wadanganyika!
 
Nashangaa kwanini mawakili wa Mahalu hawajatoa subpoena ya kumuita Rais Kikwete kuja mahakamani au kuelezea anachokijua au hata kumfanyia deposition. He is a material witness...
 
Nashangaa kwanini mawakili wa Mahalu hawajatoa subpoena ya kumuita Rais Kikwete kuja mahakamani au kuelezea anachokijua au hata kumfanyia deposition. He is a material witness...

Hansard za bunge zinasuta. Hii kesi inaanza kufanana fanana na ile ya Lema. Mbele shida, nyuma shida. Ukiishi kwa upanga utakufa kwa upanga.
 
Jk alilifahamu hilo, na inawezekana Mahalu alimzunguka akamtosa mgao....sasa hiyo ni hasira yake mzee wa kulipiza
 
Hivi Tanzania inapata kipato kikubwa kutoka balozi zake zilizoko nchi za nje? Je, nikutokana na kipato hicho kinachogharamia ununuzi wa majengo ya kibalozi huko nchi za nje au..? Je, baada ya ununuzi wa majengo hayo, kipato kinachobaki hutumikaje? Je, balozi zetu zina madeni ambayo bado hayajalipwa huko tunakowakilishwa, licha ya ununuzi wa majengo haya? Kwa nini uongozi wetu unalipa suala la ununuzi wa majengo ya kibalozi nchi za nje kipaumbele kuliko kutumia fedha hizo humu nchini kuboresha huduma za jamii? Je, Mtanzania wa kawaida ananufaikaje, kijumla, kutokana na kuwakilishwa kwa gharama kubwa kama hizo? Hivi ofisi ndogo za ubalozi wetu zikifungwa na baadhi ya majengo yaliyokwisha nunuliwa yakauzwa na fedha zikarejeshwa nchini ili kuboresha huduma za jamii, taifa litapata hasara gani? Masuala kama haya nayo pia yanastahili ufafanuzi kwa upande wa uongozi wetu.
Nashangaa kwanini mawakili wa Mahalu hawajatoa subpoena ya kumuita Rais Kikwete kuja mahakamani au kuelezea anachokijua au hata kumfanyia deposition. He is a material witness...
 
Kesi inayoondelea mahakamai dhidi ya aliekuwa balozi wa tz mjini rome prof Mahalu...leo katika utetezi wake kasema kuwa raisi kikwete by then waziri wa mambo ya njealijua na akabariki ununuzi wa jengo la ubalozi wetu Italy ambalo lilipelekea aliekuwa balozi wa wakati huo Prof mahalu kushtakiwa kwa kuliingizia taifa hasara ya mamilioni ya Euro....

Prof mahalu katika utetezi wake kasema KIkwete alipokuwa waziri wa mambo nje mnamo mwaka 2001 alitembelea nchini Italy na kukagua mjengo huo.....na aliuliza iweje ununuzi wa jengo uwe na mikataba miwili akaambiwa ni kawaida kwa ununuzi wa majengo ya bei nafuu kama lile......

kwani si kama kawa huyu mtu wa visa?alinyimwa 10% ndo anataka a mm babu seya mahalu
 
Hakuna kesi hapa hii ni misuguano ya kisiasa na mambo ya ngono tu, haiwezekani hata siku moja balozi inunue jengo bila kumhusisha waziri wa mambo ya nje.

Chama
Gongo la mboto DSM

Barabaraaaaaaaaaa! Ni visasi tu vinavyofanya kesi hii iendelee kutafuna mamilioni ya walipa kodi
 
Kesi inayoondelea mahakamai dhidi ya aliekuwa balozi wa tz mjini rome prof Mahalu...leo katika utetezi wake kasema kuwa raisi kikwete by then waziri wa mambo ya njealijua na akabariki ununuzi wa jengo la ubalozi wetu Italy ambalo lilipelekea aliekuwa balozi wa wakati huo Prof mahalu kushtakiwa kwa kuliingizia taifa hasara ya mamilioni ya Euro....

Prof mahalu katika utetezi wake kasema KIkwete alipokuwa waziri wa mambo nje mnamo mwaka 2001 alitembelea nchini Italy na kukagua mjengo huo.....na aliuliza iweje ununuzi wa jengo uwe na mikataba miwili akaambiwa ni kawaida kwa ununuzi wa majengo ya bei nafuu kama lile......

Mkuu nilikuwa nimelala na kama ndoto nikaisikia hii habari na mwishoni nikasikia kwamba kuna mtu alialikwa Ngorongoro au ni masikio yangu na ndoto tu? Naomba kuambiwa kama ilikuwa ndoto ama la. Na ni nani alialikwa Ngorongoro?
 
Sasa wangenunua vipi bila waziri na katibu mkuu kujua? Huo utetezi wa mahalu naona utamtokea puani sioni point yeyote hapo.
 
Back
Top Bottom