Kikwete alijiandaa kuhamia CHADEMA

nawaambia hivi leo, hakuna hata mmoja kati ya mapacha watatu atakae kuja kuwa rais wa hii nchi. labda kizazi hiki kiangamie chote, kije kizazi kipya. Quote me.
 
WEWE hatutaki uchafu. Tumpeleke wapi Doctor wa UKWELI!???
Miaka miwili inatosha sana kwa Lowassa kujisafisha. Itakapofika 2015, kila mtu atakuwa anamtaka Lowassa. Sasa hivi anashindwa kufanya lolote kwakuwa bado yupo ndani ya system. Mmesahau namna ambavyo Kikwete aliandaliwa kiasi cha kuonekana bonge ya kiongozi wakati kumbe hakuna kitu? Ndivyo itakavyokuwa kwa Lowassa.
 
na chadema walitanguliziwa bilioni tatu na wanamtandao
na hiyo ni open secret
but wanachama wengi hawajui
Hehe, nasikia na heirikopta ya kampeni aliyotumia Mbowe, ilikuwa imeandaliwa itumika na Kikwete kwenye kampeni. Na ililipiwa na Kikwete mwenyewe. Huyu Kikwete ni bonge ya mnafiki wazee.
 
Kwenye red, sio sahihi kwa CDM kupokea magamba kutoka CCM. Lowasa hafai tena na fikra kwamba waliobaki wote kama milioni arobani hakuna kiongozi wa kufaa CDM bali Lowasa ni mawazo mgando. Bora kutoshika dola kuliko kushika dola na viongozi makanjanja.

Kwenye blue, unatoa hilo ombi wewe ukiwa wapi? CCM au CCJ? Kwa statement yako wewe sio CDM sasa nashindwa kuelewa kivipi unaitakia CDM mema? Nafikiri ni kinyume chake.
Hakuna ushahidi wowote wa kimazingira wala wa kihalisia unaoonyesha kwamba Lowassa aliwahi kufanya ufisadi wowote. Akiwa kama waziri mkuu ilikuwa ni halali kabisa kwake kumpress msabaha aharakishe upatikanaji wa umeme. Mlitaka anyamaze kimya kama alivyonyamaza mtoto wa mkulima hivi sasa huku nchi ikiendelea kuumia na mgao mkali wa umeme?
 
Kama ufisadi ungekuwa mfumo na siyo mtu kama unavyodai,,,,sidhani kama hao wangeitwa mafisadi. Bahati mbay....ndivyo wanavyoitwawakiwa kama watu
Kwa hiyo kwa mtizamo wako mafisadi ni hao watatu tu ndani ya CCM? Akina Liyumba, Yona, Mramba, Maranda ni akina nani? Na do you know kwamba Tangu Kikwete hadi wakuu wa mikoa waliomo ndani ya CCM wanafanya ufisadi wa kutisha sana nchi hii? Kwa taarifa yako ufisadi ni mfumo. Kama chama kimerushusu huo mfumo basi utashamiri, lakini kama chama kitakuwa ngangari, kinaweza kumtimua yeyote atakayeendekeza matendo yatakayoshusha reputation ya chama. Mbona Mbeki kula A. Kusini alitimuliwa chamani kiasi cha kuachia hadi urais? CCM wanaweza kufanya hayo?

Ufisadi ni mfumo uliojichimbia na kustawisha mizizi yake ndani ya CCM. Hata wewe tukikupa madaraka leo ndani ya CCM utakwenda kuwa FIsadi tu kama alivyo NAPE. Nani alitegemea kwamba NAPE ataingia katika kundi la mafisadi wa kodi za wananchi wa nchi hii?
 
Msema hovyo naona umeoamua kutuhubiria ya Lowasa ili tumkubali mapema!! Anyway, its too early kuanza kuwasahau mashujaa kama Dr Slaa aliyetibua mambo mengi hadi neno ufisadi likaenea nchi nzima. Leo hii, ukikutana na mtu ukamuuliza kuhusu ufisadi, atakupa jibu bila kuficha maneno.
So, Let Lowasa be ex-Prime Minister, hayo mambo ya kutushawishi hapa jamvini ni mapema mno kwani kuna candidates wengi wenye sifa kemu kemu wanaoweza kuongoza hii nchi tena kwa ufanisi kuliko tunaowazungumza kila siku kwa sababu ya ushawishi wao kwa kifedha.
 
Sijawahi kusikia Lowasa akikiponda cdm. Inawezekana pia kama atakuwa na nia ya dhati ya kubadilika, na akautangazia umma kuwa anakiri kubadilika, tunaweza kumpokea cdm. Aondoke sasa madarakani na aanze harakati za kujisafisha. Kama akapewa nafasi cdm na akaharibu basi kumtosa ni jambo la kufumba na kufumbua
 
This is IMPOSSIBLE of IMPOSSIBILITIES which is ONLY possible for Impossibles! Think again, Yani sisi CHADEMA ndio tuwe wakula MAGAMBA waliojivua CCM? Patachimbika siku hiyo wakiwapokea hao MAFISADI, HAKUNA CHA MBOWE wala SLAA, Ni Bakora tu siku hiyo. Hatutaki USHENZI. hayo magamba yao ccm wayaloweke yakilainika wayale wenyewe! Nasema HATUTAKI!!! Tena dont even mention kitu kama hii ni DHAMBI.
 
na chadema walitanguliziwa bilioni tatu na wanamtandao
na hiyo ni open secret
but wanachama wengi hawajui
Hii thread imepandikizwa na makachero wa Magamba au wasafishaji wa mafisadi. Hii ni misinformation ili kuteka akili za watu na kuwageuza mawazo. Watu wanaoleta hizo hoja utakuta wana post 25 ikiwa maana ni mgeni au hataki ajulikane kama alikuwepo tayari. Tahadhari. Usidanganyike.
 
Kama ufisadi ungekuwa mfumo na siyo mtu kama unavyodai,,,,sidhani kama hao wangeitwa mafisadi. Bahati mbay....ndivyo wanavyoitwawakiwa kama watu
ndo maana tunawaita ccm mafisadi bcs ni mfumo wenu huo!
 
Chadema ina wanachama wengi sana wengine hata CDM leaders hawawajui, yes wakati hule Kikwete alitumia hadaa kama kawaida ya viongozi wa CCM na alioneka kama mtu makini hakuna mtu hakumkubali kuwa anaweza kuwa moto wa matatizo yetu kama ni wakati ule yes hata mimi ninge mkubali lakini hatukumjuwa na ndio maana hata Mbowe kaachana naye 100% amebaki na Zitto peke yake. Hana tofauti na Maalim Seif, Dr. Bilal na wanafki wengine halitudanganya na ndio maana alishinda kwa kishindo 2005.

Kati yao wote hawafai wala wasifikire siasa wakae pembeni wasubiri viongozi makini wawatie pingu, Lowasa kuja CDM ni akili mbovu ya wana-CCM wa humu JF wanadhani CDM members wote ni wajinga kama wao! huo upuuzi hauwezi kuwachanganya wana CDM huo ni mzigo wenu kila mkiutuwa chini tutawawekea kichwani mpaka mfe nao, kumbukeni kuwa Lowasa ni PM mstaafu na pia ana siri nyingi hata wizi wa Kagoda na fedha zote ambazo CCM imekuwa ikiiba kutoka serikalini kwa matumizi yake ya Kifisadi anazijuwa zote, hamtaweza kumuepuka mtakufa naye Kikwete ametumia Uislam na Uraia kumuhadaa RA ajiuzuru kuwachanganya EL na CHenge lakini bado ngoma nzito hawezi kuicheza itamtowa nyongo.

Lowasa hauziki labda ndani ya CCM ambako wanategemea wizi wa kura!
 
Taarifa za ndani, zinapasha kwamba katika harakati za uchaguzi wa Rais za mwaka 2005, Kikwete alijiandaa kuhamia CHADEMA iwapo NEC ya CCM isingempitisha kugombea Urais. Na inasemekana kwamba mkakati kabambe ulishaandaliwa na mafisadi wa CCM (Rostam na Lowassa) kuhakikisha kwamba Kikwete anashinda Urais kupitia CHADEMA. Mkapa alinusa hilo, ndiyo maana aliamua kumuacha Kikwete apite hata kama target yake ilikuwa ni Salim A SalimInasemekana pia, kwamba Mheshimiwa Mbowe alikuwa well informed kuhusu hilo, na alikuwa anasubiri tu maamuzi ya NEC ya CCM, ndipo aamue nani awe mgombea Urais kupitia CHADEMA. Kwa taarifa za ndani, ni kwamba baada ya Rostam kujiuzulu, mafisadi wengine pia kama Lowassa na Chenge watajiuzulu, na watajitahidi kutumia vyombo vya habari na pesa kujisafisha kutoka sasa hadi hapo 2014 ambapo watahamia rasmi CHADEMA. Maamuzi ya ama kuwa CHADEMA au chama kingine yatategemea pia mtizamo wa akina Mbowe na Slaa ambao wanaonekana kuwa ni threat kwa hao mapacha watatu.Binafsi ninaungana na Lowassa kuhamia CHADEMA, nina imani kwa kufanya hivyo atawezesha upinzani kushika dola kama ambavyo aliamini angemuwezesha Kikwete kushika dola kupitia CHADEMA. Tena kwa kuwa atakuwa ana kisilani na CCM Lowassa akiingia madarakani kupitia CHADEMA atahakikisha anawashughulikia wale wafujaji wa mali za umma wote waliopo CCM akiwemo na Kikwete, na kujitahidi kufanya vema zaidi katika uongozi wake ili kuwaonyesha CCM kwamba yeye si kama wao. Zaidi ya yote mimi ninamuona Lowassa kama ni strong leader, akishika nafasi ya Urais atafanya vema. Nawaombeni CHADEMA mpokeeni Lowassa.Lakini msiniulize source, sawa!!?Nawasilisha.
Unaongea upumbavu na huu ni upotoshaji wa wazi,lete source ya unachokisema usilete assumption hapa
 
Sijawahi kusikia Lowasa akikiponda cdm. Inawezekana pia kama atakuwa na nia ya dhati ya kubadilika, na akautangazia umma kuwa anakiri kubadilika, tunaweza kumpokea cdm. Aondoke sasa madarakani na aanze harakati za kujisafisha. Kama akapewa nafasi cdm na akaharibu basi kumtosa ni jambo la kufumba na kufumbua
Upo backward mkuu na unatakiwa kusoma arama za nyakati,pole sana labda aanzishe chama kingine
 
hauwezi kuwachanganya wana CDM huo ni mzigo wenu kila mkiutuwa chini tutawawekea kichwani mpaka mfe nao, kumbukeni kuwa Lowasa ni PM mstaafu !
Arafat umenifanya nicheke.......wanataka kuwakabidhi CDM mzigo wa bangi mbele ya polisi ha ha haaaa.
 
hatuwataki hao mafisadi ndani ya chadema ..waje wamchukue shibuda waondoke nao ccj bado inaexist
 
Hii thread imepandikizwa na makachero wa Magamba au wasafishaji wa mafisadi. Hii ni misinformation ili kuteka akili za watu na kuwageuza mawazo. Watu wanaoleta hizo hoja utakuta wana post 25 ikiwa maana ni mgeni au hataki ajulikane kama alikuwepo tayari. Tahadhari. Usidanganyike.
Lakini mimi nina post 88, kwa hiyo sijapandikizwa kumuuza Lowassa. Naongelea uhalisia wa mambo. Kama hutaki subiri yatakapotokea halafu utarudi hapa kunitafuta.
 
Back
Top Bottom