Kikwete, akutukanaye hakuchagulii tusi!

"Mtu ana chupa na wewe una almasi anakupa chupa unampa almasi halafu unakenua meno kama zuzu" Nyerere aliona mbali sana...

Mkuu yaani tunashangilia Presidaaa wetu kupewa jezi yenye jina lake halafu tunanyamaza wakati wao wakija kuchukua madini na gesi yetu kwa bei ya kutupa..! Halafu wanasema ati wanamuenzi Nyerere..?
 
Hiyo jezi ya kitu gani polo, ice hockey au makidamakida?

Yaani Madam Eliza ambacho cijaelewa hapo ni muingiliano uliopo kati ya Presidaaa.. huyo muzungu na hiyo jezi.. Jee huyo muzungu anamiliki timu yeyote ya michezo..? au labda Presidaaa ameomba jezi kwa ajili ya timu ya Ikulu.. au ndo ndo kwa ajili ya Barrick Gold team..?
 
Mama naye kapewa kanga.....familia hii kwa kuvaa tu hawajambo!(NB: Kwa watu wa pwani mkeo kupewa kanga na mawanaume mwingine ni kosa kubwa sana)

03%2B%5B800x600%5D.JPG
 
kwa kweli tuna safari ndefu sana mpaka ifike 2015 wengine tutakuwa tumekonda kwa presha kama hizi hivi huyu jamaa ilikuwaje akawa rahisi wetu? nasikia kichefuchefu kwa hizo picha...sasa ona wanavyodhihaki kwenye hilo tolori la kuburuzwa na faras...tanzanians job we have!
 
Mimi kuna kipindi naona Mangungo wa Msovero alikuwa na akili kuliko hawa vilaza wetu. Ingekuwa Julius umpe upuuzi kama huu asikuchanechane? Wetu kumbe rahisi si rais.
 
Kma tunamuona Rais wetu zuzu basi sisi waTanzania sjui ndio tujiiteje tuliopewa wali, T shirt na kofia af tukamchagua zuzu atuongoze na mpaka sasa bado anatuongoza. Huyu wala simlaumu. Aibu yetu wenyewe na uzuzu wetu.
 
Hivi jezi aliyowahi kuppewa Obama, Kibaki, Kagame, Museveni, na wengine wote ziko wapi? Na ni namba ngapi? Kwa nini tunapewa jezi? Nchi tuliyotembelea inapenda michezo sana au sisi tunapenda michezo sana? Au ndo hitaji letu kubwa kwa sasa? Hili tukio lina maswali mengi kuliko majibu?
 
Yaani Madam Eliza ambacho cijaelewa hapo ni muingiliano uliopo kati ya Presidaaa.. huyo muzungu na hiyo jezi.. Jee huyo muzungu anamiliki timu yeyote ya michezo..? au labda Presidaaa ameomba jezi kwa ajili ya timu ya Ikulu.. au ndo ndo kwa ajili ya Barrick Gold team..?

Jezi ni ya soka. Timu inaitwa Toronto FC inacheza ligi kuu ya Marekani na Canada ( MLS -Major League Soccer).The 'mzungu' in the picture ni Prime Minister wa Canada anaitwa Stephen Harper.
 
Jezi ni ya soka. Timu inaitwa Toronto FC inacheza ligi kuu ya Marekani na Canada ( MLS -Major League Soccer).The 'mzungu' in the picture ni Prime Minister wa Canada anaitwa Stephen Harper.

Ahsante kwa kunijuza ila linakuja swali jingine.. Jee kupewa jezi kwa Presidaaa kuna uhuciano gani na PM..? Hiyo timu inamilikiwa na na huyo PM..? Au ndio timu pekee hapo Toronto..?
 
Back
Top Bottom