Kikwete akutana na Bill Gates Dar es Salaam

BabuK

JF-Expert Member
Jul 30, 2008
1,845
329
MFUKO wa Bill na Melinda Gates utaendelea kuisaidia Tanzania katika masuala mbalimbali ya Utafiti katika sekta za afya na kilimo.

“Tuko tayari kuendelea kuisaidia Tanzania kama mtatupa vipaumbele vyenu,” Mwenyekiti
mwenza wa Mfuko wa Bill na Melinda Gates, Bill Gates alimwambia Rais Kikwete jana
mchana alipofika Ikulu kumsalimia.

Rais Kikwete amemshukuru Gates na mkewe Melinda kwa msaada wao mkubwa wanaoupatia
Tanzania.
06_11_tfhney.jpg

Gates, ambaye ni tajiri mkubwa duniani na mkewe Melinda, wapo nchini kwa ziara binafsi ya kifamilia na wametembelea mbuga za Serengeti na shughuli nyingine za kikazi, ikiwemo kukagua miradi ya Mfuko huo iliyopo nchini.

Tayari wametembelea Kituo cha Utafiti na Mafunzo katika Hospitali ya Bagamoyo mkoani Pwani, ambacho ni sehemu ya Kituo cha Utafiti cha Ifakara kilichoko Morogoro na Kituo cha Serikali cha Utafiti wa Kilimo cha Mikocheni (MARI) vinavyosaidiwa
na Mfuko huo.

Kituo cha Bagamoyo kinatafuta kinga ya malaria wakati kituo cha Mikocheni kinatafuta chanzo cha ugonjwa wa muhogo.

Wakati huo huo, Rais Kikwete anaondoka leo mchana kwenda Malabo, Equatorial Guinea kuhudhuria kikao cha kila mwaka cha wakuu wa nchi za Afrika, chini ya Uenyekiti wa Rais Teodoro Mbasogo.

Mada kuu ya kikao cha mwaka huu ni Uwezeshaji wa Vijana kwa ajili ya Maendeleo.

Rais Kikwete anatarajiwa kurejea nchini Julai 2, na Julai 3 atakuwa mgeni rasmi katika Siku ya Washirika wa Tumbaku mkoani Kagera.

Julai 4, Rais Kikwete ataongoza sherehe za ufunguzi rasmi wa barabara ya Mwandiga-Manyovu, uzinduzi wa ujenzi wa barabara ya Kidahwe-Uvinza na pia atazindua ujenzi wa daraja la Malagarasi.

Source: HABARILEO
 
The Lions Club International in collaboration with Bill Gates Foundation has set aside 10bn/- to fight against malaria and trachoma.

According to Lions Club director Manoj Shah, the money has been collected from its members and friends across the world.

Shah said his club was interested in improving health care, education, human settlements and housing.

“We are interested in seeing socio-economic challenges are smoothly addressed,” Shah said, when briefing reporters recently on the forthcoming three-day meeting which would involve club members from the East African region.

He, however, said for some years now, the Lions Club International had been in the frontline to help needy people including children with heart problems.

“We have been facilitating and supporting heart surgeries for hundreds of Tanzanian children in India,” he said, adding that the Lions Club had been also helping people with disabilities by providing them with walking tools.

Arusha New Century Lions Club president Lion Manish Chavda said despite the notable strides, the Lions Club was still facing some challenges including inability to reach out to rural communities.

He said in most cases, rural populations failed to discover diseases in early stages and some of them relied on traditional healers.

Chavda explained that rural dwellers should be sensitised on checking their health status from an early stage.

New Century Lions Club is a non-profit organisation, which has been involved in helping needy people in society.

SOURCE: THE GUARDIAN
 
ombaomba maarufu kakutana na ombwaombwa maarufu,....good
 
Nadhani ni bora tumwombe Bill Gates awe mshauri wa nchi katika kupanga jinsi ya kuendeleza nchi na siyo kutupa pesa.
Ni vizuri watanzania wakakumbuka mafundisho ya mwalimu Nyerere kuwa pesa siyo msingi wa maendeleo.
Alifundisha kuwa tunahitaji vitu 4 ili kuendelea; ardhi, watu, siasa safi na uongozi bora.
Ukiangalia utaona tunacho kitu kimoja tu sasa hivi nacho ni ardhi ingawaje viongozi wetu vipofu wanajaribu pia kuiuza kwa wageni tusibakiwe na chochote kile tena.
Watu wapo lakini, ni wa quality gani in terms of education and skills? Kuwa na population kubwa pekee is useless kama watu hao hawana elimu wala ujuzi. Nchi zenye watu wachache kama Denmark (4m), Israel (7m), South Africa (wazungu mil. 4) na kadhalika zimeendelea sana kwasababu ya ujuzi (technology). Hivyo kuna tofauti ya kuwa na watu wengi na kuwa na watu wenye ujuzi. Kuhusu siasa na uongozi bora, sina cha kuongea kwa sababu itakuwa ni kurudia wimbo tunaoimba full time kwenye forum hii.
Hivyo ni bora kina Bill Gates na mataifa yaliyoendelea wakakata mara moja misaada yote ya pesa. Watupe tu mawazo yatakayosaidia kuinua akili yetu kwanza ili tuweze kuendelea wenyewe. Otherwise tutakuwa kivutio cha utalii kama wanyama waliopo zoo na mbugani ambao wazungu watakuwa wanakuja kuangalia jinsi gani wanaishi primitive life.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom