Kikwete akubaliana na Mnyika kuondoa udhaifu, Kabaka na Werema watakiwa kutoa kauli bungeni

Paparazi Muwazi

JF-Expert Member
Dec 23, 2007
310
79
Rais Jakaya Kikwete amemuagiza Waziri wa Kazi naAjira kutoa kauli bungeni ya kubatilisha tangazo la fao la kujitoa ili wafanyakazi kuendelea kuruhusiwa kupokea fao la kujitoa.

Rais Kikwete amemuagiza pia mwanasheria mkuu wa serikali kuondoa sehemu ya sita katika muswada wa marekebisho wa sheria ya mbalimbali iliyotaka kuruhusu fao la kujitoa kwa mfuko mmoja wa PPF pekee.

Hatua hiyo imekuja siku chachebaada ya mbunge wa Ubungo kutaka Kikwete kuingilia kati kuondoa udhaifu ulioonyeshwa na SSRA, Wizara ya Kazi na Ajira na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuhusu suala hilo.

Habari kutoka vyanzo ndani ya serikali vinaonyesha kwamba Rais Kikwete alifikia uamuzi huo ili kuepusha Serikali kuingia katika mgogoro na wafanyakazi ukimhusisha yeye baada ya kubainika kwamba kwa ndiye mwenye mamlaka ya kikatiba.

Hatua hiyo inakuja siku chache kuelekea mkutano mkuu wa CCM na imetafsiriwa na wadadisi wa mambo kuwa Rais kama Mwenyekiti wa CCM ameepusha chama hicho cha wakulima na wafanyakazi kuingia katika mgogoro kuelekea mkutano huo ambao serikali itaeleza mafanikio yake katika kipindi cha miaka miwili ikiwemo kuhusu kazi na ajira.

Kwa mara ya kwanza wazo la kutaka agizo la SSRA litenguliwe na kubainisha kuwa agizo hilo halitokani na marekebisho yaliyofanyika bungeni tarehe 13 Aprili 2012 pekee bali marekebisho ya miaka ya nyuma lilitolewa la Mnyika mwanzoni mwa mwezi Agosti wakati akiomba muongozo wa Spika ambao pia alitaka kuwasilishwe muswada wa sheria kurekebisha hali hiyo.

Siku chache baadaye mapendekezo yote mawili yalichukuliwa na Mbunge wa Kisarawe Seleman Jafo katika maelezo yake bungeni aliyoyawasilisha tarehe 6 Agosti 2012 na hatimaye Spika akaliongoza bunge kuweka maazimio.

Kumbukumbu za Bunge zinaonyesha kuwa hata baada ya azimio la bunge Mnyika aliendelea kutaka kauli ya Serikali ya kutengua agizo la SSRA tarehe 7 Agosti 2012, hata hivyo Waziri hakuzingatia ndani na nje ya bunge na pendekezo hilo ndio sasa Serikali hatimaye imekubali kulitolea kauli bungeni baada ya maelekezo ya Rais Kikwete.

Suala la fao la kujitoa limeleta malumbano kwa muda toka tangazo hilo la SSRA huku upande wa Serikali pamoja na mifuko ya hifadhi ya jamii ukikataa suala hilo na wafanyakazi wakiongozwa na wafanyakazi wa migodini pamoja na wabunge wakiongozwa na Jafo na Mnyika wakitaka fao hilo lirejeshwe.

Kwa nyakati mbalimbali wabungehao wameeleza kusudio la kuwasilisha miswada binafsi ya sheria kuhusu sualahilo, wa kwanza kueleza kusudio hilo alikuwa Mnyika ambaye katika muongozo wakewa tarehe 3 Agosti 2012 pamoja na mkutano wake na waandishi wa habari baada ya muongozo huo alieleza kuwa aliandika kwa katibu wa bunge barua ya kuwasilisha muswada binafsi kwa hati ya dharura na kuanza kukusanya saini za wabunge.

Siku chache baadaye katika maelezo yake Bungeni tarehe 6 Agosti 2012 Jafo naye akataka serikali ilete muswada kwa hati ya dharura na kuahidi kwamba isingeleta angewasilisha. Mjadala wa muswada binafsi uliibuka tena baada ya tarehe 15Agosti 2012 Mnyika kueleza vyombo vya habari kuwa amewasilisha tena kusudio kwa katibu wa bunge baada ya kuona serikali haijawasilisha muswada kwa hati yadharura kama ilivyoahidi.

Siku chache baadaye Jafo naye akaeleza kwamba amewasilisha kusudio la hoja binafsi. Hata hivyo, wabunge wote wawili walitakiwa kuvuta subira serikali iwasilishe muswada huo na kuelezwa kwamba kwakuwa jambo hilo lina azimio la bunge ikiwa serikali haitaleta muswada, muswada huo ungewasilishwa na Kamati ya Kudumu ya Bunge inayosimamia suala hilo. Uamuzi wa Serikali kutoa kauli kuhusu suala hilo katika mkutano wa bunge unaondelea umezima mjadala mkali uliotarajiwa kuhusu matatizo ya wafanyakazi na mifuko ya hifadhi ya jamii nchini.

PM
 
Haya Waziri wa kazi na werema kazi ni kwenu bosi ashatoa agizo..........Fanyeni haraka tusije kuwakata vichwa tuna hasira sana kwa kutaka kutudhurumu haki zetu hivi hivi....
 
Yaani natamani kuwatundika huyo Werema na Dada yake Kabaka.Hawana uwezo na wanaburuzwa !huyo Mama alimjibu pumba za ajabu sana EL aliposema vijana wasio na ajira ni bomu kubwa liliotegwa...litalipuka soon!akabishana kwa mapovu kibao,juzi juzi JK akaliongelea kama EL alivyosema,akanywea hata comment!sasa wamekutana na Kaka Yake Werema!kazi ipo!
 
Bora serikali imeamua kulifanyia kazi suala hili maana Jafo alishataka kulifanya kuwa ndo mtaji wa kisiasa
 
Japo hujaleta source, lakini kama ni kweli basi waajiri wajiandae kukimbiwa na mifuko ya hifadhi ya jamii iandae fedha za kutosha kuwalipa watakaoacha kazi. Maana wengi wamestushwa na sintofahamu iliyojitokeza na wasingependa ku-take risk tena.
 
Sisi hatujui huyu Mhindi wetu pesa zetu anazipelekaga wapi. Kumbe ni haki ya kila mfanyakazi eee, huwa tunaambiwa ni watumishi wa serikali tu.
 
hawa watu ni wezi walikua wanataka kula hela zetu..kwa maisha ya sasa hivi ni vijana wangapi watafika miaka 55 labda asilimia 10 tu sasa hao wengine serikali ilikua inataka itafune pesa za watu sio
 
Japo hujaleta source, lakini kama ni kweli basi waajiri wajiandae kukimbiwa na mifuko ya hifadhi ya jamii iandae fedha za kutosha kuwalipa watakaoacha kazi. Maana wengi wamestushwa na sintofahamu iliyojitokeza na wasingependa ku-take risk tena.........

Ni kweli maana miaka ya nyuma fao la kujitoa lilikuwepo lakini watu walikuwa wana hiari ya kulichukua au kutokulichukua na wengi walikuwa wanajitahidi kuliacha mpaka wanapopata ajira nyingine lakini kwa mtaji huu kila ataeacha kazi anachukua chake na mwisho wa siku mifuko mifuko itafilisike.
 
Sasa kama ilikuwa ni suala la kutoa tamko tu, alikuwa wapi siku zote? Au alikuwa anapima upepo kwani alijua utapita tu!!...huu ungepita na CCM mapema sana...na pia tuwaunge mkono akina "Mnyika" na sio wale ambao kazi yao ni kukaa tu nawakilala bungeni halafu huamshwa na makofi ya wengi bila kujua kilichokuwa kinajadiliwa...big up Mnyika!!
 
Waziri kabaka alibaka wafanyakazi wa migodini kwa kukaba, ila Mnyika ka Mnyuka Sodakta, Sasa hakuna kusubiri kauli ni kwenda kuchukua Mafao tu kwa kwendaa mbeleeeeeeee, Kabaka tumeku werema na mkaeeremewaaaaaa
 
Nina mashaka na huu uzi!

Inawezekana kabisa hii mbinu ya makusudi kutupumbaza wafanyakazi!
 
OLE WAO...!!!BORA WAMEBADILISHA MSIMAMO,,, JASHO LANGU MIMI WEWE ULIPANGIE MATUMIZI ILI IWEJE ETI HAD IFKE MIAKA 60 LIFE EXPECTANCY YENYEWE KIBONGO BONGO MWACHE MWACHE EBO...!!

NA NACHUKUA CHANGU KABISAAA MANA MSHANISTUSHA,SINA IMANI NA NYIE KABISA.

:smile: :smile:
 
9 Reactions
Reply
Back
Top Bottom