Kikwete akiwa ccm au kikwete akiwa upinzani

mpuuzi

Member
May 29, 2010
99
17
Katibu Mkuu, Alhaji, Luteni Kanali Yusuph Rajab Makamba aliwahi kusema kuwa JK ndio mtaji wa kura za CCM. Jamaa nisiowaamini kabisa, REDET nao wakaja na mapambia kama hayo ya Luteni Kanali Mstafu, Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi.

Kinachoonekana hapa kuwa CCM itapata ushindi kwa sababu ya Kikwete. Sasa nauliza Swali,
Endapo Kikwete huyu akiamua kuwa mwendawazimu, ahamie upinzani, let's say TLP, na akaamua kugombea Urais, atashinda? Au kelele za Makamba na REDET bado ni porojo zile zile tulizozizoea?
 
Hapo kwenye red ndo pananitatiza.
Kuhamia upinzani ni uendawazimu au una maana gani?
 
Kila mwa CCM anajua kuwa ukienda kinyume na mkwere, umekwisha...REDET, Makamba wote vibaraka tu... wanampamba tu kwa kuwa ni Presidaa..
 
Mkuu hoja yako ngumu kidogo kuingia akilini, sababu ukitaja jk ujue umemtaja 1 presdaa anaye simamia uvundo wote unaoujua sasa. 2 m kit ccm anaye ongoza chama cha maharamia. Issue ni kwamba ataweza vipi kuhama navyo vyote hivyo vika msapoti huko TLP ili REDET waje na porojo zao
 
Mpuuzi,

Naona leo umamua kuvamia huku!! Si mseme tu kama mnataka kusaidiwa.
Acha kuuliza maswali unyojua majibu yake kaka.
Ukweli unabaki pale pale tu, agombee akiwa CCM au upinzani kwa chama chochote!!, muungwana hana uwezo wa kuongoza. Period. We mtu ameshindwa hata kupata watu "competent" kwa team yake!! We uliona wapi gari la raisi linapata breakdown mara mbili kwa siku moja!! Whether bahati mbaya au intentionally, watu katika team yake ni wazembe na ni watu wasiojua maadili ya kazi zao na kazi zao.

Muungwana ana ngekewa ya kupendwa tu.... bila sababu. Amini amini nakwambia, kuna watu mwaka 2005 walipiga kura kwa sababu muungwana aliwavutia tu. Otherwise, we now know, he does not have the capacity. Kafikishe haya..... tutamheshimu sana akikataa kugombea tena ili kubeba failures za term 1. Mods mniwie radhi kama nimemkwaza mtu, lakini hawa watu wanakwaza!!

Amani iwe kwako.
 
Back
Top Bottom