Kikwete ajisafisha Dowans

Jamani hajaongea lolote la maana na nina uhakika ndo kazidisha moto, alichofanya ni kupiga story na alikua wapi sikuzote hizo hadi aje kuongea leo? kwa nini asubiri hadi wengine wawe wakali na kukataa malipo hayo ndio leo ajitutumue azungumzie Dowans, tena kwenye sherehe za CCM ili mambo yakiwa magumu aseme kuwa alizungumza kama Mwenyekiti wa CCM na sio RAIS, na mtaamini maneno yangu

umenena ipasavyo mkuu...huyu mzee hana washauri kabisa..yaani leo ndio kavuruga kila kitu ....yaani mi natamani kutapika mapilau aliyonipikia mama gaude mara baada ya kumsikiliza huyu mzee
 
Namalizia kitimoto yangu, naskia kuna watu wamevunjwa bucha
 
Kweli mpaka sasa sijui hatma ya nchi yetu inaelekea wapi maana kila mtu anaongelea Dowans hakuna mtu anaongea ukweli kuhusu hilo.
 
Atajutia maneno yake hayo; hebu subiri uone muvi la kuanzia kesho, mi sikubali kuongozwa na mtu asiyekua na kauli kama RAIS wa nchi!! utaongeaje kama vile uko kwenye vijiwe vya kahawa? No!
 
Kama amekiri wazi kuwa Richmond/Dowans kampuni hewa, sasa basi Rostam Aziz, mbunge wake aliyehusika kuisimamia Kampuni hii feki kuchukua tenda, anamfanyaje???????????? Atueleze bayana hapo.
Amekiri kuwa Richmond ni kampuni hewa na ndiyo maana alimtahadharisha Msabaha kuhusu kuwalipa Richmond down payment, ameonekana kuutambua mkataba wa Dowans kwa kusema tumetumia umeme wa Dowans miezi tisa na kuutambua ushindi wa Dowans dhidi ya Tanesco ila baada ya malalamiko mengi ameemua serikali isiipe fedha Tanesco ili kuona jinsi ya kuweza kuepa au kupunguza malipo hayo!
 
mimi nahisi leo JK aliazima akili ya Mzee Mwanakijiji kwa muda mfupi alipokua akiongelea DOWANS
 
Kama alitilia shaka kwa nini hakuviagiza vyombo vyake vya kiinteligensia vitafute uhalali wa kampuni hiyo kumuondolea shaka hiyo ?
 
mimi nahisi leo JK aliazima akili ya Mzee Mwanakijiji kwa muda mfupi alipokua akiongelea DOWANS
Ameona hadhi yake inashahuka kila uchwao na moja ya chanzo ni Dowans. Ok amejitahidi kujisafisha sasa sijui kama wananchi watamuelewa husussni njia aliyotumia ya kuongea kupitia sherehe za chama chake.
 
Kuongelea Dowans bila kumtaja ROSTAM AZIZ ni kufanya commedy.
Alitakiwa aende hadi kwenye uliokuwa utata wa umiliki wake(japo sasa umewekwa hadharani),na kwanini wenyewe wabehave kama vile ghosts owners!...
CC ya ccm walichofanya ni kusoma majadiliano ya JF na kuibuka nayo kwenye kikao chao wakijidai pioneers.
 
Hivi huyo RA yupo kwenye sherehe? anaskilizia jamaa anavyojikanyaga tu
 
mh,kuitambua dowanz?then richmond unaikana?kwani dowanz imetokea wapi?
awamu ya kwanza,raic alisema anajfunza!bt naic utawala wa awamu ya 4 ni wa kujfunza
 
for sure makamba na mkwere wanabidi wawajibishwe,kama hatupo makini inawezekana wakaleta maafa,eti li-makamba limejidai linaongelea matokeo ya uchaguzi na li-kikwete badala ya kufanya tathmini ya chama chao na kujua kimetoka wapi,kipo wapi na kinaelekea wapi?wao wanaJipendekeza na mambo ya kitaifa ktk sherehe za chama ,hzo akili au matope?
 
Anahusika, ni kama adam na eva, hata Mungu alipowakamata wamevunja amri yake, walianza kujhtetea badala ya kuomba msamaha. Ndicho anacho fanyanya Jk. Kama alijua Richmond ni batili ilikuwaje akaruhu iuze tenda kwa Dowans. Na yote siyanajadiliwa ndani baraza lake ambalo yeye ni mwenyekiti? Hivyo kwakuwa waliamua pamoja, hata yeye ni miongoni mwa mafisadi. Hachomoki kwa hilo labda awadanganye ccm ambao walikuwa wanamsindikiza kwa makofi ya ujinga wao. Anabeza maandamano kupinga matokeo F4, kwa upande mwingine yeye anafurahia matokeo hayo. Jamaa anauwezo mdogo sana. Yawezekana ana dememtia.
 
asitufanye sisi watoto mpuuzi huyu..........aote kauli kama rais na sio kubwabwaja tu ..........aseme moja kuwa hawa jamaa wanalipwa au hawalipwi lakini kutupigisha story mchana kweupe huu ni uongo.......
 
Back
Top Bottom