jmushi1
Platinum Member
- Nov 2, 2007
- 24,989
- 22,521
Subiri FF akija hapa utasikia mambo yake, ni wazee wa gerezani tuu!Baba yake Mbowe (Mbowe Senior) ni mtu ambaye pia alistahili hiyo tuzo sema tu JK kaibadilisha imekuwa ya kichama zaidi na kuifanya ya Mawaziri Wakuu na Marais Wastaafu utadhani ndio wachapa kazi peke yao. Kama mtakumbuka Mzee Mbowe ndiye aliyekuwa anafadhili harakati zote za Mwalimu Nyerere. Ni kama Sobodo na CDM leo hii.
Mzee Edwin Mtei nae alipaswa apewe hiyo tuzo kwa mchango wake wa kusimamia sera yake ya Ubepari ambayo ilipingwa vikali na Nyerere hatimae akajiuzuru. Lakini baadae miaka ya 1990 serikali ikaanza kufanyia kazi mawazo ya Mtei. Na ndiyo inayoyatekeleza hadi leo.