Kikwete ahutubia Taifa Julai 31 - hutuba ya mwisho

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,474
39,987
Kikwete anahutubia sasa taifa, atazungumzia

a. Kura ya maoni
b. Barabara ya lami kupita serengeti
c. Uchaguzi Mkuu


Nitawaletea hotuba yenyewe baada ya hotuba kwisha.

SEHEMU YA 1
[video=dailymotion;xe7u3i]http://www.dailymotion.com/video/xe7u3i_hotuba-ya-kikwete-mwisho-wa-mwezi-j_news[/video]
SEHEMU YA 2
[video=dailymotion;xe7uuk]http://www.dailymotion.com/video/xe7uuk_hotuba-ya-kikwete-mwisho-wa-mwezi-j_news[/video]
 
Aahidi kuwa hii itakuwa hotuba yake ya mwisho kwa kipindi hiki cha miaka yake mitano ya kwanza.

Anadai matokeo ya kura za maoni zanzibar lazima yafuate kwa amani ya Zanzibar na Tanzania kwa ujumla..aufagilia utaratibu serikali chakachua akitolea mfano, S.A, Kongo, Kenya na Zimbabwe.
 
Kesho ni siku ya kuchukua form za kugombea uraisi na 31 october ni siku ya kupiga kura, ahimiza watanzania watumue haki yao ya kuchagua na kuchaguliwa katika mazingira yaliyo huru na haki.
 
apongeza sheria ya matumizi ya fedha katika chaguzi zijazo na baada ya uchaguzi wataipitia sheria hiyo ili kuiboresha zaidi, na utunzi wa sheria hiyo umekuwa wakati muafaka, awafagilia Takukuru
 
Awaomba watanzania kufuata sheria ili kuufanya uchaguzi wa mwaka huu uwe wa amani na bila uvunjifu wa sheria na watu wasiwe na wasiwasi utaendeshwa kwa ufanisi haki na uwazi, na sheria za uchaguzi zitafuatwa.
 
Wapiga kura mkimaliza kupiga kura kwenye vituo basi muondoke msizunguke zunguke pale kisa kusubiri matokeo kwani hiyo ni kazi ya mawakala, awaomba mawakala kuwa makini ili zoezi liende murua
 
Anateleza kidogo hapa na kusema kuwa Nyerere alizungumzia watu wanaobagua wenzao kwa misingi ya dini/ukabila/rangi etc ni wa kuwaogopa kama ukoma.............ukweli ni kuwa Nyerere alizungumzia watu wanaotumia pesa kukimbilia Ikulu ndio wa kuogopa kama ukoma..!

Sijui ni tatizo la speechwriter au mkuu aliongeza mwenyewe?
 
Awaomba vyama vya siasa, wagombea, wapiga kula na viongozi wa dini kuwe kampeni zifanyke kwa amani kwani ni jambo la msingi sana kwenye kampeni, wagombea watumie lugha nzuri na siyo za matusi na kebehi kwani lugha za namna hiyo ni hatari kwa amani na umoja wa Tanzania.
 
Tarime, busanda kampeni zilikuwa siyo nzuri, vyama viache kuandaa magenge ya wahuni zidi ya vyama vingine.
 
Mzee muda mfupi ni upi kwako ?
Au una edit na kuweka mbwebwe teh tehe tehe ,usijali na ktk kusubili.
 
Akishaongea inatusaidia nini watanzania?

Ni rais so lazima usikilize anachoongea kama pumba upate sababu ya kushawishi wengine wasimchague.
Na mengi ataongea kujipapa so inabidi ukanushe kama anajipamba uongo , its war man!!!!!!!!!
 
Ni rais so lazima usikilize anachoongea kama pumba upate sababu ya kushawishi wengine wasimchague.
Na mengi ataongea kujipapa so inabidi ukanushe kama anajipamba uongo , its war man!!!!!!!!!

Unategemea cha maana kutoka kwenye hotuba yake ambacho hujakisikia na kukipata kwa miaka mitano iliyopita?
 
Sielewi ni kwanini Kikwete ameona kuwa anawiwa maelezo na wa Kenya kuhusu barabara inayopita Serengeti iliyoko Tanzania?
 
Mkulu anaonekana hana raha kabisa. Kuna kitu kinamsumbua ama ana homa ya uchaguzi.
 
Mwanakijiji nakusikia unaguna "hah!" baada ya rais kusema "mfumo wa serikali ya umoja Zanzibar siyo wa milele" unajua hata mimi nimeshangaa yaani unapoitisha referendum si maana ya kubadili katiba? na anaposema kila baada ya miaka mitano watakuwa wanauangalia huu si uhuni?, yaani kila miaka mitano wazanzibar wawe wanapiga kura za maoni?. Maana kama jambo limeingizwa kwa kura ya maoni basi halilatoka pasi na kura hiyo hiyo kupigwa tena. Kwa mtazamo wangu hakukuwa na haja ya hii kura kama mtazamo ni huu wa kureview every five years.
 
Back
Top Bottom