Elections 2010 Kikwete ahutubia Manzese

Du sijawahi kusikia kampeni ya uraisi CCM Manzese, kweli mambo ni tait kwa jK.
 
Du sijawahi kusikia kampeni ya uraisi CCM Manzese, kweli mambo ni tait kwa jK.

Siku hizi picha za mgombea wao JK hadi milango ya kuingia maliwatoni tena baa, yaani wamechanganyikiwa kabisaaaa!

Na siku hazigandi, 31 hiyooooo inatinga!
 
Coaster zipo mitaani kubembeleza watu wapande waende kwenye mkutano wa ccm!jamani mnatulipa kiasi gani kutupeleka kupamba kampeni zenu?
 
Bharkresa pale kwenye biashara ya huduma kwa wakubwa tu au? Angalieni pale huwa hawakawii kuchoma mtu kisu. Unajimu wa Yahya usije ukatimia bureeeee
 
hahaaaa JK anapiga kampeni manzese???Duh kweli mwaka huu kampeni za shuka kwa shuka
 
Du sijawahi kusikia kampeni ya uraisi CCM Manzese, kweli mambo ni tait kwa jK.

hii ndio tofauti ya washindi na walalamikaji, washindi hufuata wapiga kura walalamikaji kazi yao ni kulia lia tu.
 
Rais Kikwete atangaza mipango Kabambe kumaliza kero ya maji Dar

  • Atangaza pia ujenzi wa Machinga Complex tano zaidi
Oktoba 17, 2010

RAIS Jakaya Mrisho Kikwete na Mgombea Urais wa Tanzania katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) ameelezea mipango kabambe ya Serikali yake ya kuboresha upatikanaji wa maji kwa wakazi wa Jiji la Dar Es Salaam.

Aidha, Rais Kikwete ametangaza kuwa Serikali yake itawezesha kupatikana kwa nafasi 40,000 zaidi za wafanyabiashara ndogo ndogo kufanyika shughuli zao kwa kuhakikisha kuwa kila moja ya wilaya tatu za Mkoa wa Dar es Salaam inajenga majengo makubwa (Machinga Complex) mawili kwa ajili ya wafanyabiashara hao.

Vile vile Rais Kikwete amethibitisha kuwa hospitali tatu za sasa za wilaya – Mwanyamala, Amana na Temeke – zitapandishwa hadhi ya kuwa na hadhi ya Hospitali za Mikoa katika kutekeleza azma ya Serikali yake kuboresha huduma za afya kwa ajili ya wanachi.

Rais Kikwete ameeleza hayo leo, Jumapili, Oktoba 17, 2010, wakati alipohutubia mamia kwa mami ya wananchi katika mkutano wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu uliofanyika kwenye Viwanja vya Bakharesa, Manzese, Jimbo la Ubungo, Wilaya ya Kinondoni.

Rais ameaambia wananchi hao waliojawa na shamrashamra za kila aina: “Najua kuwa maji bado ni tatizo kubwa kwa Mkoa na Jiji la Dar Es Salaam. Lakini na hili tunayo mipango na majawabu yake. Kwanza, tutaongeza upatikana wa maji kutoka lita milioni 18 hadi milioni 60 kutoka chanzo cha maji cha Ruvu Juu. Pili, tutaongeza upatikana wa maji kutoka lita milioni 40 hadi milioni 90 kutoka Ruvu Chini na Wamarekani wanatusaidia katika mradi huu mkubwa.”

Ameongeza: “ Tatu, tutalipa Jiji maji kutoka chanzo kipya cha Kimbiji ambacho kinadadiriwa kuwa na uwezo wa kutoa maji kiasi cha lita milioni 260.”

Kuhusu ujenzi wa majengo makubwa ya wafanyabiashara kufanyika shughuli zao, Rais Kikwete amesema:

“Tayari tumekamilisha ile Machinga Complex pale Ilala. Sasa mipango ni kujenga majengo mawili ya namna hiyo katika kila moja ya wilaya za Dar Es Salaam na pia kujenga jumba la viwanda vidogo vidogo katika eneo lililokuwa mali ya TTCL Barabara la Sam Nujoma katika Wilaya ya Kinondoni.”

Ameongeza katika wilaya ya Temeke, majengo hayo mawili yatajengwa eneo la Temeke Stereo na eneo lililoko nyumba ya TBC Barabara ya Nelson Mandela, katika Wilaya ya Kinondoni majengo hayo yatajengwa eneo la DDC Magomeni Kondoa na Mbezi Louise wakati katika Wilaya ya Ilala jengo la pili la namna hiyo litajengwa Buruguni Sokoni.

Amesisitiza: “ Ujenzi huo utatuwezesha kuwa na uwezo wa kutoa nafasi kwa wafanyabiashara kiasi cha 40,000. Lakini kama nilivyopata kusema majuzi, ni lazima nafasi hizo zigawiwe kwa haki kwa wakubwa kuacha kujipendelea katika kujipa nafasi wao na jamaa zao.”

Amesema fedha za ujenzi wa majengo hayo, kiasi cha sh bilioni 100 tayari zimepatikana kutoka Serikali ya Jamhuri ya Wananchi wa China.

Kuhusu maboresho ya huduma za afya, Rais Kikwete amesema kuwa ili kuongeza ubora wa utoaji huduma kwa wakazi wa Dar es salaam hospitali tatu za sasa za wilaya zitapandishwa hadhi na kuwa hospitali za hadhi ya mikoa na vitajngwa vituo vya afya na zahanati mpya.

Mapema kabla ya kuhutubia mkutano wa Manzese, Rais Kikwete amefungua Shina la Wakereketwa wa CCM la Rashid Mfaume Kawawa katika eneo la Magomeni Mzimuni.

Rais Kikwete amesikiliza kero za wakazi wa eneo hilo ambalo zimeelezwa kuwa ni pamoja na maji, ukusanyaji taka, wingi wa mbu, na tuisheni kwa watoto wa shule.

Baadaye leo mchana, Rais Kikwete atafungua Shina la Wakereketwa la Wanedesha Pikipiki la Mbezi Tangi Bovu na kuhutubia mkutano wa kampeni katika Viwanja vya Tanganyika Packers, Kawe.
 
Rais Kikwete atangaza mipango Kabambe kumaliza kero ya maji Dar

  • Atangaza pia ujenzi wa Machinga Complex tano zaidi
Oktoba 17, 2010

RAIS Jakaya Mrisho Kikwete na Mgombea Urais wa Tanzania katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) ameelezea mipango kabambe ya Serikali yake ya kuboresha upatikanaji wa maji kwa wakazi wa Jiji la Dar Es Salaam.

Aidha, Rais Kikwete ametangaza kuwa Serikali yake itawezesha kupatikana kwa nafasi 40,000 zaidi za wafanyabiashara ndogo ndogo kufanyika shughuli zao kwa kuhakikisha kuwa kila moja ya wilaya tatu za Mkoa wa Dar es Salaam inajenga majengo makubwa (Machinga Complex) mawili kwa ajili ya wafanyabiashara hao.

Vile vile Rais Kikwete amethibitisha kuwa hospitali tatu za sasa za wilaya – Mwanyamala, Amana na Temeke – zitapandishwa hadhi ya kuwa na hadhi ya Hospitali za Mikoa katika kutekeleza azma ya Serikali yake kuboresha huduma za afya kwa ajili ya wanachi.

Rais Kikwete ameeleza hayo leo, Jumapili, Oktoba 17, 2010, wakati alipohutubia mamia kwa mami ya wananchi katika mkutano wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu uliofanyika kwenye Viwanja vya Bakharesa, Manzese, Jimbo la Ubungo, Wilaya ya Kinondoni.

Rais ameaambia wananchi hao waliojawa na shamrashamra za kila aina: "Najua kuwa maji bado ni tatizo kubwa kwa Mkoa na Jiji la Dar Es Salaam. Lakini na hili tunayo mipango na majawabu yake. Kwanza, tutaongeza upatikana wa maji kutoka lita milioni 18 hadi milioni 60 kutoka chanzo cha maji cha Ruvu Juu. Pili, tutaongeza upatikana wa maji kutoka lita milioni 40 hadi milioni 90 kutoka Ruvu Chini na Wamarekani wanatusaidia katika mradi huu mkubwa."

Ameongeza: " Tatu, tutalipa Jiji maji kutoka chanzo kipya cha Kimbiji ambacho kinadadiriwa kuwa na uwezo wa kutoa maji kiasi cha lita milioni 260."

Kuhusu ujenzi wa majengo makubwa ya wafanyabiashara kufanyika shughuli zao, Rais Kikwete amesema:

"Tayari tumekamilisha ile Machinga Complex pale Ilala. Sasa mipango ni kujenga majengo mawili ya namna hiyo katika kila moja ya wilaya za Dar Es Salaam na pia kujenga jumba la viwanda vidogo vidogo katika eneo lililokuwa mali ya TTCL Barabara la Sam Nujoma katika Wilaya ya Kinondoni."

Ameongeza katika wilaya ya Temeke, majengo hayo mawili yatajengwa eneo la Temeke Stereo na eneo lililoko nyumba ya TBC Barabara ya Nelson Mandela, katika Wilaya ya Kinondoni majengo hayo yatajengwa eneo la DDC Magomeni Kondoa na Mbezi Louise wakati katika Wilaya ya Ilala jengo la pili la namna hiyo litajengwa Buruguni Sokoni.

Amesisitiza: " Ujenzi huo utatuwezesha kuwa na uwezo wa kutoa nafasi kwa wafanyabiashara kiasi cha 40,000. Lakini kama nilivyopata kusema majuzi, ni lazima nafasi hizo zigawiwe kwa haki kwa wakubwa kuacha kujipendelea katika kujipa nafasi wao na jamaa zao."

Amesema fedha za ujenzi wa majengo hayo, kiasi cha sh bilioni 100 tayari zimepatikana kutoka Serikali ya Jamhuri ya Wananchi wa China.

Kuhusu maboresho ya huduma za afya, Rais Kikwete amesema kuwa ili kuongeza ubora wa utoaji huduma kwa wakazi wa Dar es salaam hospitali tatu za sasa za wilaya zitapandishwa hadhi na kuwa hospitali za hadhi ya mikoa na vitajngwa vituo vya afya na zahanati mpya.

Mapema kabla ya kuhutubia mkutano wa Manzese, Rais Kikwete amefungua Shina la Wakereketwa wa CCM la Rashid Mfaume Kawawa katika eneo la Magomeni Mzimuni.

Rais Kikwete amesikiliza kero za wakazi wa eneo hilo ambalo zimeelezwa kuwa ni pamoja na maji, ukusanyaji taka, wingi wa mbu, na tuisheni kwa watoto wa shule.

Baadaye leo mchana, Rais Kikwete atafungua Shina la Wakereketwa la Wanedesha Pikipiki la Mbezi Tangi Bovu na kuhutubia mkutano wa kampeni katika Viwanja vya Tanganyika Packers, Kawe.

...presha inapanda, inashuka...
 
Kumbe ni sahihi Dk Slaa kukataa kuahidi ahadi za reja reja, this is too much, kama ahadi zote hizo zipo, zitatekelezwa kwa budget gani wakati budget ya mwaka huu tumekopa kwenye benki? au ana pesa za kutekelezea haya? nimeuliza tu
 
JK hana akili kabisa..yaani hajui nini cha kuongea ...Kilichomfany a kushindwa kushugulikia tatizo la maji ni nini? Huyu mzee ovyo sana huyu sijui tulitoka naye wapi mapaka akawa rais wa hii nchi
 
Siku hizi picha za mgombea wao JK hadi milango ya kuingia maliwatoni tena baa, yaani wamechanganyikiwa kabisaaaa!

Na siku hazigandi, 31 hiyooooo inatinga!
Nyingine nimezishudia kwenye mapipa ya Takataka(dust bins) mitaani
 
Katika mojawapo ya dalili za kuzidiwa kwa sisiem mwaka huu ni JK kufanyia kampeni Manzese. Sikumbuki ni lini watu wa Manzese walikumbukwa na chama hiki wakati wa kampeni. Ama kweli nimeamini "mfa maji haachi.............". Chadema kazeni budi sisiem pumzi inaendelea kuisha.
 
Mnisamehe jana niliahidi kuwapa maendeleo ya kampeni yaliyonikuta ni makubwa kwani nilifuatwa ndani ya gari yangu na jamaa wana mashati ya kijani siwafahamu kabisa na shushu moja namfahamu wakaniambia niache kutuma hizo habari vinginevyo watanifukuza mkutanoni, walisema chama hakiitaji msaada wangu wa kufanya kampeni na kama natka kufanya hvyo niwasiliane na timu ya Kampeni ya chama
 
Back
Top Bottom