Kikwete agoma kusaini waraka kuhusu wabunge kujipandishia posho

NGOMA INOGILE...

Kwahiyo kikinuka kabisa itabidi wabunge wakwatwe mishahara kulipia posho walizochukua kutoka wizara ya fedha bila idhini ya JK?

Wanasema life is expensive in dodoma, vp kuhusu mlalahoi/mpiga kura anayeshindia chini ya dola moja kwa siku?

Hivi tunajifunza nini hapo?
 
yaani walikuwa wanaelewa kabisa kuwa ni lazima Raisi ataisaini,kwani wameshazoea kuwa Raisi husaini kila kitu wanacho mpatia bila kuhoji,hii ni hatari sana kwa mstakari wa nchi yetu,kudhani kuwa kila Raisi husaini bila shaka lolote ndio maana wakalipana kabla ya mkuu kusaini
haya yetu macho
 
Ukitaka kuamini kwamba misomi ya Tanzania ni hasara tupu, nilitegemea wangefanya maandamano makubwa hasa hawa wa UDOM kuomba nyongeza ya pesa za kujikimu maana maisha ya Dodoma ni ghali mno, na reference ni bunge.
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Tunamuomba saana Mh.saana Kikwete aione hali ya wananchi wake asikubali kusaini huo waraka kwani kama ni kupanda kwa maisha yamepanda kwa watu wote sio kwa wabunge tuu.
 
Kama ni kweli wabunge wa upinzani nao hususani CDM wamechukua hizo posho, napata hisia za siasa za ubabaishaji uliotukuka. Nimefuraishwa na TAMKO/Waraka/Msimamo wa CDM kuhusu upingaji wa hizo posho.Nimesoma kwenye sread ya mleta mada inaelekea hata watetezi wetu wetu nao wamevuta posho isipokuwa Mzito Kabwela. Imefikia wakati tuache siasa za kinafiki, kama ni kweli CDM hawajachukua hizo posho wakanushe hadharani ili wajitofautishe na wana Magamba. Vinginevyo wakisubiri mpaka taarifa za JK kugoma kusaini waraka wa kuongeza posho CDM itapigwa bao. Magamba ni wepesi kwenda vijijini na kuanza kuwapumbuza Watanganyika kwa kuwalaghai kuwa Sirikali yao inawajali na watadandia hoja kuwa Magamba wamegomea posho.
utakuwa outdated!!!!
posho hapewi mkononi bali huingizwa kwenye akaunti ya mbunge husika together with hela zingine kama mshahara nk.
hapo kila akaunti ya mmbunge imeorodheshwa na taka ustake hela huingizwa
 
trust no one in this government, bcoz no lie wl live 4eva, hilo ni chenga la macho tu ili kuavoid mass upraisal:shock:
 
  • Thanks
Reactions: Ame


i know the only man you trust ni Lowassa! sometimes Just give a guy a credit akifanya a right thing
Apewe credit kwa lipi? kwani kugoma maana yake ni kukataa? akieleweshwa si ataweka saini? atoe tamko hadharani kwamba amekataa hapo mimi bila hiyana nitampongeza.
 
sasa akigoma kusaini wenzake kule katika chama watamuelewa?maana muswada wa katiba alikubali CDM wanahoja na anasaini kwa sababu tu wenzake katika chama wasimuelewe vibaya
 
Rais kasusa Mkuu!!!! Hatukuwahi kumsikia Mwalimu hata siku moja anafanya usanii kama huu eti wa kususa!!!! Sasa Rais unasusa unamsusia nani!!!? Nchi yetu kweli imepata kiongozi!!!!


Kama watafanya hivyo itabidi waongeze mishahara ya wafanyakazi Nchi nzima kwani
mishahara ni midogo mno kama kwenye TGTS MWENYE DEGREE ANAanza na 330,000
ambayo ndio mbunge atachukua kwa siku
 
I do not trust my president any more.

Haiwezekani bunge lipeleke waraka kusainiwa na Rais wakitegemea kuwa waraka huo utakataliwa! Kikwete alikubaliana na spika Makinda kuwa moja ya njama ambazo wangezitumia kuwashawishi wabunge kupitisha muswada wa Katiba na mingine itakayofuata ni njia hii ya kuwahonga [bribery] wabunge kwa kuwaongezea posho zao; sasa kwavile wananchi na makundi mengi ya jumuiya na wanaharakati wamekuja juu ndio maana mkweree amestuka na kuvuta pumzi akiangalia upepo unavyovuma!! Msijeona ajabu keshokutwa mkasikia ameridhia uongezwaji wa hizo posho.
 
Tuiombe serikali irudishe kitu kinachofanana na SCOPO ya zamani ki-regulate mishahara na posho mbalimbali kwa watumishi wa serikali na taasisi za umma. Vinginevyo tunawaonea WABUNGE wetu tu. Mashirika ya UMMA kama NHC sasa wanalipana mishahara ya ajabu. Nenda TCRA, EWURA, SUMATRA, DAWASA, DAWASCO, NSSF, PPF, REA, TANESCO, TPDC,... Ulizia mishahara na posho zao sasa.
Nchi inatafunwa hii acheni tu.
 
Tuiombe serikali irudishe kitu kinachofanana na SCOPO ya zamani ki-regulate mishahara na posho mbalimbali kwa watumishi wa serikali na taasisi za umma. Vinginevyo tunawaonea WABUNGE wetu tu. Mashirika ya UMMA kama NHC sasa wanalipana mishahara ya ajabu. Nenda TCRA, EWURA, SUMATRA, DAWASA, DAWASCO, NSSF, PPF, REA, TANESCO, TPDC,... Ulizia mishahara na posho zao sasa.
Nchi inatafunwa hii acheni tu.

Hapo kwenye red; Nchi hii ingekuwa na Bunge linalojua kazi na majukumu yake ya msingi tusingekuwa tunafikiria "kuiomba serikali". Ni wajibu wa Bunge kuona upuuzi huo na KUIAGIZA serikali kurekebisha hali hiyo mara moja. Bunge makini na linalojua kazi zake linayo mamlaka WAKATI WOWOTE kutunga SHERIA YOYOTE KUIAGIZA serikali kutekeleza SUALA LOLOTE lenye maslahi kwa jamii pana/yote.

Lakini badala ya Bunge letu kutekeleza majukumu yake kama ilivyotegemewa kinyume chake linatamani UFISADI unaofanywa na wengine (TCRA, EWURA, BoT, n.k.); wabunge wetu wanatafuta namna ya KUTOKA. Sijui watanzania tukimbilie wapi? Lakini tuliwachagua wenyewe anyway.

TAFAKARI.
 
>> Katibu Wa Bunge (Hakuna Ongezeko La Posho)

>> Spika Wa Bunge (ongezeko La Posho Liko Tokea 8/11)

>> Rais (Agoma Kusaini Waraka.)

Nimuamini nani kati ya hawa? Nitegemee nini kutoka kwa hawa? Na Je ni kipi kinafuat?

wote vigeugeu....
 
Mkuu kama anajali matumizi badala ya kususa kwanini asitamke tu hadharani kwamba hizi posho mpya za Wabunge hazitakuwepo na wataendelea kupata posho zilizokuwepo kabla!? Msanii huyu anasubiri Watanzania tusahau labda mwishoni mwa Januaru au Mwanzoni mwa February atie wino tayari kunenepesha mifuko ya Wabunge.
Kama amepinga adharani, halafu akamwaga wino kwa siri,itajulikana tu,atabebewa bango hadharani,labda atajidai anataka marekebisho.

All in all anataka kuwaaminisha wadanganyika kuwa yeye ni mtu makini na muungwana.

Kwamba wadanganyika watasahau mapema hata akimwaga wino, hilo tusubiri.
 
Kama watafanya hivyo itabidi waongeze mishahara ya wafanyakazi Nchi nzima kwani
mishahara ni midogo mno kama kwenye TGTS MWENYE DEGREE ANAanza na 330,000
ambayo ndio mbunge atachukua kwa siku


Ningekuwa mimi Rais wala hata siongezi hiyo mishahara maana wafanyakazi wa Tanzania wako kama vile hakuna kinachowahusu kwenye nchi hii. Wakisikia police (ambao ni sehemu hiyo hiyo ya hao wafanyakazi) wanaonea wapinzani wao haiwahusu; wakisikia CCM inawatumia kukandamiza wananchi wao wako kimya kama vile siyo wao wanao lalamikiwa...Acha wakome..Rais please do us a favour sign hiyo rekebisho la posho ikibidi ongeza na nyingine labda cadre ya taaluma na wafanyakazi itatoka katika usingizi mnono waliolala wakuachia kila kitu kiamuliwe kisiasa.
 
Back
Top Bottom