Kikwete afagia tena ndani ya saa 24, Zamu hii amemng'oa Profesa Yadon Kohi

on a light note, nilidhani makanali ni watu wa vita na wamezoea mazingira magumu ya maporini? LOL

Mkuu heshima ikurudie, after 14 years ya uongozi uraiani? Mkuuu tulipitia JKT kwa hiyo we have an idea kidogo, huyu mkuu alipaswa tu kustaafishwa maaana hana jeshi tena akilini mwake, na itakuwa vigumu sana at this stage kumrudisha jeshini tena, kwa lugha za kijeshi anaitwa raia huyu!

ANKO VITUKO VYA JK HAVIISHI..USISHANGAE KUMRUDISHA B.GEN KOHI ALIYEKAA URAIANI MIAKA 14...KUMBUKA ALIMVYOAMUA KUMRUDISHA KANALI NDOMBA[RAFIKI YAKE] ALIYEKAA MIAKA 15 KWENYE VYEO VYA URAIANI..NA KUMPA KAZI NYETI CHA UTUMISHI JESHINI..AMBAYO ALWAYS WAMEFANYA HARDENED SOLDIERS KAMA MAJ.GEN LOUIS [LATE] AND THE LIKE ...SIO HUYU AMBAYE HATA ALISHASAHAU JESHI..SO USIONE AJABU KAKA ..KWA JK LOLOTE LINAWEZEKANA!!! TENA SI AFADHALI HUYU KOHI AMEKUWA AKIFANYA SHUGHULI MBILI TATU ZA KIJESHI HATA AKIWA PALE COSTECH...
 
pamoja na kuwa mkurugenzi wa COSTECH...profesa brigadier general yodan kohi...ni PROFESA WA CHUO KIKUU CHA KUMBUKUMBU YA DR HUBERT MWOMBEKI KAIRUKI...sasa labda vijana pale watuambie kama kitabu anachowapa ni safi..pia kohi ndio aliyeongoza operesheni ya kuongoza MUHIMBILI KITABIBU KIJESHI WAKATI WA MGOMO WA MWAKA JUZI WA MADAKTARI NCHI NZIMA AMBAPO JESHI LILIPEWA JUKUMU LA KUTOA HUDUMA NA UENDESHAJI ...NADHANI ALIFANIKIWA...ila kiukweli pale COSTECH..ameshindwa au wameshindwa ..

lakini tunapojadili hali hii sasa tuchukue tahadhari moja..kiini cha kushindwa pale costech ni nini? ukosefu wa ubunifu/miradi....wafadhili au serikali haitoi pesa za utafiti??? ingekuwa bora aeleze ...JE SERIKALI ANAWAJIBIKA KUWA SOLE SPONSOR WA UTAFITI PALE..NADHANI MFUMO WAUTAFITI WA MATAIFA MAKUBWA UKIZINGATIA NA ISHU YA USIRI WANAPENDA KUFADHILI TAFITI ZA KITAIFA FROM OWN SOURCE...UNAFIKIRI NANI ATAPENDA KUFADHILI UTAFITI WA NUCLEAR KWA SERIKALI KAMA YETU....

NAMSHAURI AMIRI JESHI MKUU NA MKUU WA MAJESHI WAUNDE KITENGO CHA SAYANSI NA UTAFITI..ILI TUWEZE KUTAFITI ZANA NA PROGRAM FULANI FULANI WENYEWE..KUNA ASKARI WENGINE WENGI TU WANASAYANSI AKIWEMO YULE ALIYEKUWA MKURUGENZI WA TUME YA MAWASILIANO ..KANALI ABIHUNGWA...kwa pamoja jeshi liwe la kitafiti ili miradi aliyoanzisha mwalimu ya program za kiulinzi kama nyumbu,mazao,..ets na kile KIJIJI CHA SAYANSI NA TEKNELOJIA IRUDI..

Philemon Mikkaeli,

1. I like your Patriotic reflections ndugu yangu! Nakubaliana na wewe serikali have orphaned COSTECH- ndo maana hata ukawaona VODACOM wakaja pale kupiga rangi lile jengo! Unajua mtoto yatima is so desperate to tap opportunity of any thing! Naafiki na wewe- Kohi factor- is not the only problem at COSTECH- hata akiondolewa as long as COSTECH will be starved of resources- I am pessimistic to see any meaningful changes!

2. As long as serikali inaona Investment in Science and Technology not a priority- basi sisi as a country tutazidi tuu kuwa nguma ya mataifa mengine ktk maendeleo in our region- hata Rwanda sasa pamoja na matatizo yao wanapiga hatua kubwa zaidi tena kwa haraka!

3. Kama wengine walivyosema- what is the office tenure ya Wakurugenzi Tanzania? Kohi was 14 years! Luhanga UD was over 15 years! Severe- (20 years????), and the list goes on! Hili pia ni tatizo kubwa kwa serikali- there must be a limit to office tenure- say vipindi viwili vya 4 years- making it 8 years! Sasa kama in 8 years mtu hawezi kuleta mabadiliko- do you think akikaa 15 or 20 years ndo ataleta mabadiliko?
8 years maximum kwa maoni yangu pia itatoa fursa kuwapa nafasi walio chini yao kujenga uwezo wao (Capacity building and strengthening).
 

Sasa my point ni kwamba sina uhakika kama kweli nambas, zinaweza kuthibitisha kuwa tuna percent kubwa as a nation ya walio na uwezo kiakili, lakini wakashindwa kwenda mbele kwa kukosa nyenzo, I mean sina uhakika na hilo mkuu, ila ninaamini sana kuwa huwa hatuwatupi, lakini mkuu wangu sina ushahidi wa kutosha kwenye hilo.


Mzee katika hili naungana nawe. Lakini pia hata siku hizi wanaopotea sana wanapotea kabla/katika shule za awali I mean primary school may be na secondary school sana sana vijijini.

Lakini wanaoweza kuvuka kisiki hiki kidogo wachache ambao wameweza kukosa usaidizi. Na pia wanaoshindwa kupata usaidizi ni ktk sehemu(MIKOA) zilizokuwa hivyo kihistoria.
 
Kohi sikuweza kubainisha/sijabainisha kama kweli alikuwa na uwezo/sifa waliozokuwa wakimpa.Hila niliona kama vile alikuwa Mzalendo.

Nafikiri alikuwa ameisha pafanya mahala pale kama sebuleni kwake ni vizuri naye akapumzika kama akina Prof. Luhanga. Miaka kumi na nne ni mingi mno.
 
Huyu Kohi Waziri Wake Alikuwa Profesa Msolla...je Kama Amemuondoa Mmoja Wa Wakurugenzi Wa Taasisi Zake Kwa Majigambo ....amechukua Hatua Gani Kwa Msolla ...hata Baada Ya Kuhojiwa Na Mjj Na Wananchi....kuhusu Mikopo Ya Wanafunzi Na Wale Watoto Wetu Walio Ukraine....

This Is Just A Political Catche!!!!
 
Mzalendo Rwanda Wako Mbali Kisayansi...wanayo Kigali Institute Of Technology...inafanya Maajabu...iko Funded Na Serikali ..imeajiri Hata Wanasayansi Wa Kitanzania .....wamedhamiria Kufunza Vijana Wao Technology Ili Wakaajiriwe Nje Na Kuleta Fanaka...

Nadhani Wakurugenzi Wa Mashirika Wawe Wanafanya Kazi Kwa Mikataba...say Miaka Mitatu..wanapewa Na Terms Of References..mtu Akitumika Muda Mrefu Mahali Anachika Kimawazo...aruhusiwe Ku Renew Terms Mbili Akionekana Anahitajika Anapelekwa Mahali Pengine Na Baada Ya Mzunguko Anaweza Tena Kurudishwa....

Wakurugenzi Wengi Wa Mashirika Wanaoteuliwa Na Rais Anasahau Kuwahamisha ..nafikiri Rais Hii Kazi Ya Uteuzi Awaoe Independent Body...kuna Wakurugenzi Mfano Kimei Wa Crdb ...ni Bright Na Ameleta Mafanikio Sana Pale ..lakini Kwa Muda Aliokaa Hata Kama Ni Mzuri Vipi Ataaza Ku Drop Perfomance ...sasa Hapo Ingetakiwa Apewe Shirika Lingine Lililopo Icu...ie Reli,tazara Ets Aoneshe Uwezo [ni Mfano Tu]..

Kiongozi Pekee Aliyekuwa Na Dira Ya Sayansi Na Teknelojia Ni Mwalimu..baada Ya Hapo Mashirika Ya Utafiti Yamekuwa Too Illfunded...
 
Taasisi kama NIMR inapata mapesa kibao ya utafiti kutoka kwa wadhili kama vile Bill gates kwenye mradi wa Malaria na taasisi nyingine zinazoshirikiana na NIMR kwa mambo ya utafi. Kwa hiyo sishangai NIMR is doing better than COSTECH.

Hii taasisi inaongozwa na kichwa makini sana Dr. Mwele Malecela, ambaye ameweza kuwa-convince Billl na Melinda, kwamba anaweza kufanya utafiti wa kweli, na pia ni mumainifu wa mapesa yao wanayompa, sasa haya ni matatizo makubwa yanayotusumbua kwenye utafiti bongo, mana htuaminiki na mara nyingi uwezo hatuna wa kisayansi kuweza kufanya utafiti,

Dr. Mwele, ambaye pia ni rais wa dunia wa utafiti wake, pia hufundisha special classes huko US na Europe, kuhusiana na utafiti wake, ndio mana hata kule Atlanta CDC, waliamua kumpa access ya anything kuhuisiana na shughuli zake za kisayansi, na pia mara nyingi kuna watu babu kubwa kama kina Andrew Young na Jesse Jackson ambao humsaidia ku-lobby kwa serikali ya US kuhusiana na shughuli zake, lakini cha msingi ni uwezo wa utafiti na uaminifu, na pia dedication kwa hiyo shughuli maana huyu mkali sometimes huenda kuishi Songea maporini huko mwisho wa dunia kufuatilia mbu, sasa hawa makanali wa jeshi wataweza vipi hayo? ndio maan tunashindwa!

huko NIMR, Dr. Mwele amepigwa majungu weee, fitina weee, mpaka kutumiwa majambazi, lakini haikusaidia kitu.

Mungu Aibariki Bongo Yetu!
Dr Mwele anaiongoza NIMR? I know she is one of the directors lakini sio Director Mkuu? Dr Kitua alishahama??
 
Mimi suala la kiongozi kuwa kwenye kiti 14 yrs sijalielewa, ikiwa Mkuu wa nchi mwenyewe ana ukomo . Why not others? Yaani mtu amekaa tu hana hili wala lile taasisi imekuwa kama nyumba yake sisi tunachekelea. Hiv vyeo viwe na ukomo. Two terms uondoke more people are getting PHDs na wanakuja na mambo mapya!
Mtu apewe cheo na hadidu za rejea ....5 years down theline hajatimiza apishe wengine..akionekana ana perform vizuri one more term then OUT. Hii itapunguza hata internal conflicts!
Na nafasi hizi zitangazwe....kuwe na interview the best three ndio waende kupitishwa na huyo Mkuu wa nchi. Hii biashara ya majina kutoka kusikojulikana pia ina madhara yake.
 
Sasa JK atampa nani nafasi ya Kohi COSTECH? Any suggestions? Ni nani anaweza kuleta mapinduzi katika Sayansi na Technology Tz kwa sasa? Hebu toeni mapendekezo ya watu wenye Vichwa wa kuchukua nafasi baada ya Kohi!

My opinion- let us look for a success story ya Taasisi iliofanya vizuri Tz- bila mizengwe so as to turn around COSTECH!

1. Dr. Rose Kingamkono? (Ag. DG)
2. Any success stories? (TRIDO, TAFIRI, NIMR, KCMC, UD, SUA, MU, MUHAS). TPRI- nako kuna taabu sasa- sidhani kama kuna candidate.
3. Au watachukua mtu toka Wizara Elimu ya Juu Sayansi na Teknologia?
4. Je apewe mwanamke this time?
5. Je atoke Zanzibar- as this is a Union matter?

We need a team tu turn around (U turn) COSTECH so as to restore pride to Tanzania ili hata mataifa yanayotuzunguka kama Kenya, Uganda na Rwanda iwe changamoto!

Waungwana mnasemaje? Kama mna CV za watu wenye vichwa hebu ziwekeni hapa!
 
Mzalendo,
Ni ukweli usiopindika kuwa Tz kuna wakina mama wenye uwezo mkubwa. Tunaowajua ni asilimia chache tu, kibao wako underground. Tatizo la Tanzania mwanamke mpaka awe kwenye siasa ndio apate heshima zake. Nani ambaye anajua credentials zote za Dr. Kingamkono? Huyu mama ni mmoja wa Nutritionists wazuri sana Bongo. Ameshafanya research nyingi sana kuhusu utapiamlo na lishe ya wajawazito na watoto, sio tu Tanzania, bali Africa mzima.

Shukrani Mkuu!
Hebu tuwekee basi CV yakeo hapa- hizi ndo fursa sawa za akina mama!
 
Mzalendo Rwanda Wako Mbali Kisayansi...wanayo Kigali Institute Of Technology...inafanya Maajabu...iko Funded Na Serikali ..imeajiri Hata Wanasayansi Wa Kitanzania .....wamedhamiria Kufunza Vijana Wao Technology Ili Wakaajiriwe Nje Na Kuleta Fanaka...

Nadhani Wakurugenzi Wa Mashirika Wawe Wanafanya Kazi Kwa Mikataba...say Miaka Mitatu..wanapewa Na Terms Of References..mtu Akitumika Muda Mrefu Mahali Anachika Kimawazo...aruhusiwe Ku Renew Terms Mbili Akionekana Anahitajika Anapelekwa Mahali Pengine Na Baada Ya Mzunguko Anaweza Tena Kurudishwa....

Wakurugenzi Wengi Wa Mashirika Wanaoteuliwa Na Rais Anasahau Kuwahamisha ..nafikiri Rais Hii Kazi Ya Uteuzi Awaoe Independent Body...kuna Wakurugenzi Mfano Kimei Wa Crdb ...ni Bright Na Ameleta Mafanikio Sana Pale ..lakini Kwa Muda Aliokaa Hata Kama Ni Mzuri Vipi Ataaza Ku Drop Perfomance ...sasa Hapo Ingetakiwa Apewe Shirika Lingine Lililopo Icu...ie Reli,tazara Ets Aoneshe Uwezo [ni Mfano Tu]..

Kiongozi Pekee Aliyekuwa Na Dira Ya Sayansi Na Teknelojia Ni Mwalimu..baada Ya Hapo Mashirika Ya Utafiti Yamekuwa Too Illfunded...

phillemon mikael,
COSTECH iko ICU- sasa atafutwe mkurugenzi anayefanya vizuri pengine- aje to make U Turn pale. Hata kama ni Watz wako nje ya nchi- ktk ngapi ya juu- na wana uwezo wa kufanya U turn basi wapewe nafasi! Saa ingine ukifanya tu open advert unaweaza kukosa watu wazuri wenye interest- ni bora kuangalia sucsess stories kama unavyosema!
 
phillemon mikael,
COSTECH iko ICU- sasa atafutwe mkurugenzi anayefanya vizuri pengine- aje to make U Turn pale. Hata kama ni Watz wako nje ya nchi- ktk ngapi ya juu- na wana uwezo wa kufanya U turn basi wapewe nafasi! Saa ingine ukifanya tu open advert unaweaza kukosa watu wazuri wenye interest- ni bora kuangalia sucsess stories kama unavyosema!

Sasa ile sera ilopitishwa ya kuangalia walio kwenye utumishi wa umma watanzania walio nje wana nafasi kweli?
 
Shukrani Mkuu!
Hebu tuwekee basi CV yakeo hapa- hizi ndo fursa sawa za akina mama!

Nimewasiliana na mtu wa karibu wa Mama Kingamkono kuweza kupata accurate CV ya huyu mama. Nitaiweka pindi nitakapoipata katika masaa 24 yajayo.
 
..naona tunarudi kule kule kwa "JK apagawisha", "JK hakuna mfano", "JK chaguo la MUNGU".....

..yaani mtu atolewe COSTECH apelekwe JWTZ halafu mnamsifia Raisi kwa "kufagia?"

..JESHINI ndiyo pamekuwa mahali pa kupeleka "UCHAFU" ktk hii awamu ya Lt.COL.KIKWETE

..kati ya COSTECH na JWTZ ipi ni muhimu kwa mustakabali wa Taifa letu?
 
Hivi maprofesa ndio viongozi wazuri Tanzania?

We unafikiri Tanzania kuna maprofesor wengi, wengine nasikia wakifika nchi za watu huwa wanaomba wasiitwe Maprofesor. Hata huyo Kohi nafikiri alikuwa hivyo hivyo. Wengi ni wanasiasa tu ni applied professors.

We assume mtu ni professor yuko vyuo vikuu hata mwanafunzi wa masters hajaweza kumuelekeza huyo sijui tumuiteje?.

Kwa hali ilivyo nchini Tanzania ni vigumu sana kumpata chief executive ambaye anateuliwa na Rais akawa mtu mzuri.

Mimi ningependekeza suala kama la COSTECH watangaze nafasi ya kazi watu wanaleta CV halafu interview unaita international consutancy kufanyisha interview potelea mbali gharama hila utapata mtu anayeeleweka bila hivi hakuna chochote.
 
Joka Kuu ndio hapo sasa tusiposifia tunaambiwa "hatutendi haki"...

tean utasikia wansema.Eti Jf hamuoni mazuri,IlaMganag awa CCM wa sasa ni kiboko,wameweza kuzima tuhuma za Ufisadi kirahisi sana,nasikia Walimfuata Mzee Mangula na Kumuomba msaada wa kipropaganda baada ya kuona kingunge keshashindwa,Hata Mbnu aliyoitumia Masha Mlevi kuhusu madini,Ni moja ya propaganda zao..Mtasikia Mengi sana ambayo yatawafanya muone maisha bora yamekaribia na kuwafanya msahau maneno ya mzee wa kilalacha,sasa hivi wanagonga glass.
 
tean utasikia wansema.Eti Jf hamuoni mazuri,IlaMganag awa CCM wa sasa ni kiboko,wameweza kuzima tuhuma za Ufisadi kirahisi sana,nasikia Walimfuata Mzee Mangula na Kumuomba msaada wa kipropaganda baada ya kuona kingunge keshashindwa,Hata Mbnu aliyoitumia Masha Mlevi kuhusu madini,Ni moja ya propaganda zao..Mtasikia Mengi sana ambayo yatawafanya muone maisha bora yamekaribia na kuwafanya msahau maneno ya mzee wa kilalacha,sasa hivi wanagonga glass.

Mkombozi,

Niliisha sema na wengine wakachangia, tuna ugonjwa wa kitaifa watanzania walio wengi, Ugumu kuelewa, wepesi kusahau na uhodari wa kusifia hata visivyostahirihuu ni ugonjwa mbaya sana unalishambulia taifa letu, heri hata ya ukimwi kuna ARV!! sisi ni kulalamika bila kuchukua hatua, kidogo tunasifia na kusahau...ufisadi, Buzwagi BOT, Rich man in Monduli (Richmondi) vitakufa vifo vya mende!! Thanks to the JF inasaidia kidogo kutuamsha kwenye uzingizi wa pono na giza totoro!!
 
Back
Top Bottom