Kikwete aelekea US, Pinda atangaza ongezeko la bei kwa watumiaji umeme!

Raisi kwenda nje ni muhimu na ni kwa manufaa ya nchi yake sema tu ni kwamba inatakiwa unapoenda nje manufaa yaonekane kweli sio kwenda tu kila siku kwa wenzako hata kurudi na ubunifu tu huwezi, hata kama si yeye wale wanaoambatana na Raisi wanastahili kuweka zaidi maslahi ya nchi kwenye kila safari anazofanya raisi. Rais wetu nae amezidi sana kila siku je utafikiri yeye ndo kwanza anaanzisha uhusiano wa tz na mataifa kumbe ulikuwepo
 
hapo maisha yatazidi kuwa magumu umeme bei ghali, mgawo, sukari haishikiki, sembe pia tutapona kweli? Bado wa mafuta nao watakuja kivyao
 
JK alikatisha safari ya Canada wakati wa maafa ya meli Zanzibar vinginevyo alikuwa aunganishe Marekani juu kwa juu na muda wote huo wangekuwa wanakula posho ya safari, toka wiki iliyopita. Which means alipojua General Assembly inakuja akabuni stop nyingine north America ili kurefusha safari kabla msiba haujamkatisha. Mbinu yake ni kwamba mianya ya kuiba ile kinoma noma kama EPA/Dowans watu wanamtolea macho kila kona, so the way kula na kipofu bila kumgusa mkono ni kukomba every last bit of legal money he can get his hands on.

Hana huruma na nchi.
 
Waziri Mkuu wa Jamhuri wa Muungano wa nchi za Tanganyika na Zanzibar anatarajia kutangaza kupanda kwa bei ya umeme kitendo ambacho kitaongeza makali ya maisha ya watanzania ambao wengi wetu tunaganga njaa. Hivi Vasco dA GAMA akisitisha safari mbili hiyo ela haiwezi kufidia hilo ongezeko la bei hat kwa mwaka mmoja????
 
Ndo maisha bora kwa kila mtanzania ambayo jk alituahidi? Hivyo kupanda kwa bei ya umeme nani ana mamlaka ya kutangaza waziri mkuu, waziri wa nishati na madini au Tanesco.
 
Waziri Mkuu wa Jamhuri wa Muungano wa nchi za Tanganyika na Zanzibar anatarajia kutangaza kupanda kwa bei ya umeme kitendo ambacho kitaongeza makali ya maisha ya watanzania ambao wengi wetu tunaganga njaa. Hivi Vasco dA GAMA akisitisha safari mbili hiyo ela haiwezi kufidia hilo ongezeko la bei hat kwa mwaka mmoja????

Suala hapa ni walala hoi kubeba mzigo wa ile faini iliyotakiwa kulipwa na tanesco baada ya kuvunja mkataba na dowans. Wakati umefika sasa kulipa lile deni na wanaotakiwa kulipa ni walala hoi. Tuna kasi kubwa
 
Huu uliopo tu tabu,
Kisha ndio tunapandishiwa!!
Halafu watapandishaje kitu ambacho hakipatikani??
Huo umeme una kizuri kipi kiasi cha kuuziwa kwa bei juu?
Mbona hii nchi kila kitu kinakua tabu?
Hii yote ni kwasababu ya kulipia capacity charge alizosaini JK kwa IPTL kipindi akiwa waziri wa nishati, halafu bado tunachekeana tu.
Kweli watanzania tumelogwa!!
 
huyu Mizengo Pinda simuelewi anaposema gharama za uzalishaji zimepanda, ina maana hili giza tunalogawiwa na Tanesco lina gharama zake...
Wafikirie kwanza jinsi ya kuboresha huduma zao, then hilo la kupandisha bei lifuate...haiwezekani kila siku huduma ni za ovyo, ila bei zinapaa balaa!!!nafikiri ishu za IPTL, DOWANS na UJAIRO flan wanaoupiga ndio unaotuumiza waTZ
 
Pamoja na PM kutangazia taifa kupanda kwa bei ya umeme,Mgao bado uko pale pale? Maana naona hapa A town 2na mgao kama kawa.
 
Pamoja na PM kutangazia taifa kupanda kwa bei ya umeme,Mgao bado uko pale pale? Maana naona hapa A town 2na mgao kama kawa.

mkuu upandishwaji wa umeme sio kuengezea kipato cha kununua vifaa vya kupunguza makali ya mgao tusubirini mpaka pale yesu akirudi nadhani mambo yatakuwa swafi na mkuu wa kaya toka afanye kazi ya udalali bado hajapata mteja wa kutununua..

Mungu ibariki safari ya rais
Mungu ibariki tanesco
Mungu mbariki mzee wetu wa Katavi
Mungu ibariki Tanzagiza.
 
Waziri mkuu Mizengo Peter Pinda jana alisema kuwa bei ya umeme ni lazima ipande bila kujua ilikuwa anachoma wananchi na mwiba mwingine katika maisha yao.

Kwa taarifa hiyo yalikuwa ni machungu mengine ya kuongeza kiwango duni cha maisha kw awananchi. Dola imepanda nishati ya mafuta bei juu unga bei juu maharage bei juu sukari haipatikani ikipatikana bi yake haishikiki.
 
ameenda marekani katika ufunguzi wa UNGA.vilevile atashiriki katika sherehe za kuazimisha maendeo yaliyofikiwa na nchi zinazo endelea.
wakati huo huo waziri mkuu pinda ametangaza kuwa serikali inakusudia kuongeza bei ya umeme kwa sababu tanesco inajiendesha kwa hasara.mia
Hivi ile thread ilyokuwa inahesabu safari za mkuu iko wapi vile tuongeze namba
 
ameenda marekani katika ufunguzi wa UNGA.vilevile atashiriki katika sherehe za kuazimisha maendeo yaliyofikiwa na nchi zinazo endelea.
wakati huo huo waziri mkuu pinda ametangaza kuwa serikali inakusudia kuongeza bei ya umeme kwa sababu tanesco inajiendesha kwa hasara.mia

Hapo Obama atakuwa anajiuliza, 'ataomba nini tena?". Wakati huo Bush anamsubiri akitaka kujua ule mpango wa Kigamboni umefikia wapi. Tunakutakia safari njema Jk, lakini wenzio walishachoka na ombaomba yako.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom