Kikwete adai tatizo ni ujamaa!

Kaka

The Chinese, are at the point where they invest in sport franchises, wewe unaongela ujamaa. Hawa washapita na ujamaa longtime; their soo capitalist to the point western 'left side' politacal parties seem radical in their eyes.

Watu wanafikiri ile ya kudhibiti ufisadi kule china ni ujamaa, kwi kwi kwi kwi, wale wachina sio wajamaa na wamepita huko karne kadhaa, kule china ukiongeza mtoto wa pili inabidi umlipie kodi.

Kule china karibu kila familia ina kakiwanda japo hata ka kukamua matunda. Ukoministi/ujamaa ni ile hali ya kujenga state kwa wananchi kuwa waoga wakati wote, wananchi kuwa natabia ya kidomodomo ili kurahisisha kazi ya polisi ya kuwa -tocha raia. Ukoministi/ujamaa ni hali ya kujenga FIREWALLS ambayo ni ruhusa kwa watu fulani kuwa nacho, lakini wengine hamruhusu kupata , hata kama umepata kihalali lazima waku question ama kukutaifisha kabisa huo ndo ukoministi/ujamaa

Ukoministi ni ile hali ya kumhofia mwenzako kwamba ukimtonya ktk dili fulani anaweza faidika sana, kwa hiyo hata kama wewe hilo dili huliwezi bora mlikosa wote. Huu ndo ukoministi/ujamaa.

Ukoministi ni ule kama mimi kitu fulani siwezi kukipata lazima nifanye njama za aina zozote na Mkandara asipate, na hata kama ninacho nitahakikisha Mkandara hapati ili Mkandara aendelee kunitukuza.

Nendeni mkajiulize ama mkasome mawazo ya kikoministi yanavyopinga URAIA WA NCHI MBILI. Ukoministi ni tatizo kubwa sana tena sana. JK angefanya tu kuwaoondowa wazee wote walio juu ya miaka 45 ktk nyadhifa zao.
 
Ukiritimba ndiyo tatizo na si ujamaa. Kwani si wabadili to procedures ili kuondoa ukiritimba? Mlolongo wa process na mipaper work isiyo na kichwa wala miguu ndiyo inayoondoa ile efficiency ambayo inajenga mazingira ya rushwa... Kila kitu bongo ni rushwa, everything, hakuna pahala pasipo na rushwa bongo. Ni mfumo wa rushwa ndiyo tatizo na si ujamaa.

Ujamaa labda ni kikwazo kwa wananchi na si viongozi, kwasababu wao wanagawana mali za umma kwa kudai ubinafsishaji.Nyumba za serikali kwa vigezo hivyo hivyo. Migodi nk.

Sikutegemea maneno hayo haya yangezungumzwa na mkuu. Yanaonyesha kutofahamu kabisa matatizo ya wananchi na taifa kwa ujumla. Huwezi ukawa unafahamu matatizo ya nchi na wananchi halafu ukaongea maneno kama hayo.
 
..kwa kweli inachanganya mwenyekiti wa chama kinachofuata itikadi ya UJAMAA na KuJITEGEMEA anapotoa kauli kama hizi.

..hivi inawezekana tukawa na chama tawala cha kijamaa lakini serikali yake ikawa ya kibepari?
Mkuu sio kutofautiana na itikadi ya chama chake tuu bali hata Katiba ya nchi.

Ibara ya 9 ya Katiba yetu inasema kuwa "Lengo la Katiba hii ni kuwezesha ujenzi wa Jamhuri ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar au wa chochote kati ya vyombo vyake na udugu na amani kutokana na kufuata siasa ya Ujamaa na Kujitegemea, amabyo inasisitiza utekelezaji wa misingi ya kijamaa kwa kuzingatia mazingira yaliyomo katika Jamhuri ya Muungano.

Kwa hiyo, Mamlaka ya Nchi na vyombo vyake vyote vinawajibika kuelekeza sera na shughuli zake zote katika lengo la kuhakikisha pamoja na mambo mengine kwamba nchi inatawaliwa kwa kufuata misingi ya demokrasia na ujamaa.
 
Mkuu hapa sikuelewi.. Hivi Russia bado ni Makomunist? hakuna mtu anayetetea Ukomunist hapa na nini zilikuwa athari zake. Russia, China na hata Cuba viongozi wa nchi hizo ni walikuwa matajiri chini ya mfumo wa Kikokunist na kinachoweza kulalamikiwa ni mfumo ule wa Kikomunist uliowatajirisha..Tofauti na Tanzania viongozi wetu walikuwa maskini ndani ya Ujamaa leo hii ni matajiri wakubwa sana wakitumia Ubepari kama ngazi ya kupandia. Russia na China wapo matajiri wengi wameibuka ambao wanafanya kweli lakini hatuwezi kusema mafanikio ya nchi hizi yanatokana na Ujamaa wao (Ukomunist) kwa sababu tu Tanzania tunafail ktk Ubepari na kusingizia Ujamaa. Wao hao Russia na China walikuwa ndani ya Ujamaa kwa miaka mingi kuliko sisi na walibobea zaidi kiimani, mbona wao wanaedelea na wameweza kubadilika ghafla.

Sababu ni ndogo sana, wenzetu walikuwa na uwezo (Elimu na nguvu kazi), waliweza kudhibiti mirija na taratibu za uwekezaji ili kuepuka ukoloni mamboleo kwa maslahi ya nchi zao. Wawekezaji wakubwa ni raia wa ndani na hawapangiwi masharti na wawekezaji toka nchi za nje Kifupi wao sii wahitaji bali ni washiriki ktk dunia hii ya Utandawazi na soko huria hali sisi ni consumers yaani tunategemea kulishwa..

Mwisho mkuu wangu huyo mzee wa Kikerewe ndiye nasema ataonekana kuwa na mrengo usiokubalika nchini wakati huko Ulaya Conservative ni mrengo unaokubalika kwa sababu hawa jamaa zetu wako miaka 200 mbele yetu wamisha jenga Taifa linaloitwa Marekani, Uingereza na kadhalika pasipo kujali makabila au asili za raia wake na zaidi ya hapo ni matajiri ambao wanaweza jitegemea na sii maskini kama sisi ombaomba tukaige kushuka kimba kama la tembo! Uchumi w Tanzania unapasuka msamba na hakuna sababu yeyote zaidi ya kuiga Tembo..


Mkandara
Naona hujapata jiswi na chengu siku nyingi.
Wewe unakubali kabisa mfumo wa kikoministi/ujamaa ndo umewanufaisha viongozi harafu ukifika kwa Tz unapaa vihunzi.Kifupi mfumo ndo huo huo ndo maana utaona viongozi wa kikoministi/ujamaa ndio hao hao wanaomiliki na watoto wao na kudhibiti wengine.

Ukijichanganya mitaani na ukafanya kazi ndo utagundua ukoministi/ujamaa ni tatizo kuu kwa vizee vya Tanzania, mie nimefanya kazi bongo kama fundi mchundo lakini lilikuwa tatizo kubwa sana kwa vizee vya VETA.

Ulaya magharibi hakuna ukoministi/ujamaa wala sidhani kama kuna chama chochote kinachofuata ukoministi/ujamaa kule kuna u-coservative , u-liberali nk.
 
wandugu,

..mwenyekiti wa CCM na Raisi wa Jamhuri anadai kwamba Ujamaa ni tatizo.

..upande mwingine, Nape Nnauye, ambaye ni Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, anadai chama kitaendesha mafunzo ya itikadi nchi nzima.

..nchi haijawahi kuwa na vituko kama wakati huu.
 
..kwa kweli inachanganya mwenyekiti wa chama kinachofuata itikadi ya UJAMAA na KuJITEGEMEA anapotoa kauli kama hizi.

..hivi inawezekana tukawa na chama tawala cha kijamaa lakini serikali yake ikawa ya kibepari?
Joka,
China wana elements kama hizo.Serikali yao inatumia baadhi ya sera za kibepari,west wanazitambua kama reforms.Hata hivyo serikali hiyo ni ya chama cha kikomunisti.
 
Ukiritimba ndiyo tatizo na si ujamaa. Kwani si wabadili to procedures ili kuondoa ukiritimba? Mlolongo wa process na mipaper work isiyo na kichwa wala miguu ndiyo inayoondoa ile efficiency ambayo inajenga mazingira ya rushwa... Kila kitu bongo ni rushwa, everything, hakuna pahala pasipo na rushwa bongo. Ni mfumo wa rushwa ndiyo tatizo na si ujamaa.

Ujamaa labda ni kikwazo kwa wananchi na si viongozi, kwasababu wao wanagawana mali za umma kwa kudai ubinafsishaji.Nyumba za serikali kwa vigezo hivyo hivyo. Migodi nk.

Sikutegemea maneno hayo haya yangezungumzwa na mkuu. Yanaonyesha kutofahamu kabisa matatizo ya wananchi na taifa kwa ujumla. Huwezi ukawa unafahamu matatizo ya nchi na wananchi halafu ukaongea maneno kama hayo.

Ukiritimba muasisi wake ni mkomnisti/mjamaa. Nendeni nchi za ulaya mashariki wakahadithie ukiritimba uliokuwa unafanywa na ukoministi/ujamaa. Nchi zote za kikoministi/ujamaa ndo mwake humo kila kitu paper nenda kule rudi huku, peleka pale.
 
Hivi rais anapoikosoa katiba waziwazi hajavunja katiba aliyoapa kuilinda??

KWA HIYO, BASI, KATIBA HII IMETUNGWA NA BUNGE
MAALUM LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, kwa niaba ya Wananchi, kwa madhumuni ya kujenga jamii kama hiyo, na pia kwa ajili ya kuhakikisha kwamba Tanzania inaongozwa na Serikali yenye kufuata misingi ya demokrasia na ujamaa.
 
Ujamaa/socialism huwa unapimwa kwa kuangalia government revenue as a percentage of GDP.Ukiona nchi ina kama 90% hiyo ni ya ujamaa mpevu,wengine wanaita ukomunisti,nchi hiyo haipo hivi sasa.Cuba ina kama 76% kuna nchi za kisoshalisti kama venezuela,bolivia,ecuardor,germany,china,russia,canada,sweden denmark etc... nazo zinapata kama asilimia 40% hadi 60%.....Tanzania tunapata 12%,so tell me how far are we?
 
Tatizo la Tanzania si ubepari wala ujamaa, bali ni uongozi dhaifu usio taka kufanya vitu vya maendeleo, kama tatizo ni ujamaa na hao wazee walio kaa miaka mingi basi wa kwanza kujichukulia hatua ni huyu aliye toa matamshi haya, na mtu yoyote hawezi kuniambia IPTL, Richmond, EPA, Rites, TTCL, VodaCom, Airtell, umetokana na ujamaa?

Kenya ni majirani zetu wanafuata ujamaa lakini wana Goldenberg, wana Rift Valley railways, wana serikali inayo watetea Ocampo six, dhidi ya waathirika wa vuruga za uchaguzi nk nk nao utasema matatizo yao ni ujamaa.
 
Kiranga,
Mimi nilimsikia ITV. Napata ITV kupitia Tv4africa.com. Ni kweli aliyasema hayo. Lakini hilo tisa. Nijuavyo mimi, hayo ndiyo maoni sahihi ya Kikwete ambayo huyasema privately au miongoni mwa marafiki zake. Hana hata moja la kumsifia Nyerere. They are trying so hard to kill his legacy lakini naamini historia itawaumbua.
kaka unaona mbali sana, ngoja tusubili tuone jitihada zao zitakapoishia.
 
Nchi yenye mgawo wa umeme unategemea nini?Madhara yanayotokana na ukosefu wa umeme ni makubwa sana kuzidi hata hayo ya sikukuu.
Serikali ina majukumu ya kuwajengea wananchi mazingira ya kujiletea maendeleo,ndiyo kazi yake hiyo.Tusiwalaumu wananchi peke yao.

Wananchi hao hao unaosema tusiwalaumu ndo wanaichagua serikali na kuchagua wawakilishi wao. Wanastahili wanachopata.
 
Ujamaa/socialism huwa unapimwa kwa kuangalia government revenue as a percentage of GDP.Ukiona nchi ina kama 90% hiyo ni ya ujamaa mpevu,wengine wanaita ukomunisti,nchi hiyo haipo hivi sasa.Cuba ina kama 76% kuna nchi za kisoshalisti kama venezuela,bolivia,ecuardor,germany,china,russia,canada,sweden denmark etc... nazo zinapata kama asilimia 40% hadi 60%.....Tanzania tunapata 12%,so tell me how far are we?

Mkuu,
Tanzania sio tena makoministi/wajamaa. Tatizo ni kwamba wazee walio na hatamu wanamawazo ya kikoministi na kuendesha serikali kibepari basi wanapoteaaaaaaaaa jangwani. Ndio maana JK, anasema tuwaoondoa hawa wazee na tuweke vijana wenye mawazo ya kibepari kuongoza serikali kiperi. Namuunga JK kwa asilimia 100%. Fukuza wazeeeeee wotee.

Nenda kaombe kazi serikali, teh teh teh kwanza kwenye interview itakuja panel ya watu kama 15, hawa wanalipwa posho wote kufika ktk panel, watakupitisha. na ikitoka hapo itakuja kamati nyingine ya watu 30 ili kupitisha jina lako. ikitoka hapo watapeleka jina utumishi na utumishi watakaa watu 50 kujadili jinsi ya kuingiza jina lako ktk malipo.Utumishi watarudisha jina sehemu ulipoomba nao tena wataita kamati nyingine, upuuzi tupu.
 
tatizo la tanzania si ubepari wala ujamaa, bali ni uongozi dhaifu usio taka kufanya vitu vya maendeleo, kama tatizo ni ujamaa na hao wazee walio kaa miaka mingi basi wa kwanza kujichukulia hatua ni huyu aliye toa matamshi haya, na mtu yoyote hawezi kuniambia iptl, richmond, epa, rites , ttcl, vodacom, airtell, umetokana na ujamaa?
kenya ni majirani zetu wanafuata ujamaa lakini wana goldenberg, wana rift valley railways, wana serikali inayo watetea ocampo six, dhidi ya waathirika wa vuruga za uchaguzi nk nk nao utasema matatizo yao ni ujamaa.

Nendeni hata huko ulaya mkaone ukalinganishe weusi wa mataifa mengine na watanzania, sana sana mjamaa/mkoministi mtakutana naye anapamba pamba kiswahili chake pale kosa mpe mgongo ,teh teh teh
 
Siasa za nchi hii zinaendeshwa Kitamthiliya tamthilia tu...! Huo ujamaa wenyewe ulikuwa sawa na mtu aliye vaa masurupwete, haikujulikana kama tumevaa Kaptula la Marx, au pajama lake.
 
Kiranga,
Mimi nilimsikia ITV. Napata ITV kupitia Tv4africa.com. Ni kweli aliyasema hayo. Lakini hilo tisa. Nijuavyo mimi, hayo ndiyo maoni sahihi ya Kikwete ambayo huyasema privately au miongoni mwa marafiki zake. Hana hata moja la kumsifia Nyerere. They are trying so hard to kill his legacy lakini naamini historia itawaumbua.

mhh,Jasusi mbona hivyo,kulikoni?, are u a great thinker?, acha porojo za kahawa kijiweni!,au ndondo zimekulevya?
Napita tu.
 
Hapa Kikwete kwa mara ya kwanza kaongea point yenye akili sana. wachangiaji wa mwanzo hili lililosemwa na kikwete lina ukweli midingi maofisini humo wakiritimba hata kwa wawekezaji wa ndani yaani private sector na wao ni kama paka na panya. Sijuwi kitaisha lini hiki kizaji cha Mwalimu Nyerere?.

Na kwa taarifa yenu kwa kila Mtanzania aliyefanikiwa kiuchumi kupitia private sector atakubaliana na haya isipokuwa wale mnaonufakaika na system zisizo wazi na ukiritimba, maana wao akili yao inaishia kuomba mgao eti kwa vile mtu amekuja kuchukua cheque yake.

Kikwete ni mtu asiyefaa kabisa kuwa kiongozi wa nchi kutokana na kutokuwa na vision yake mwenywe na akaisimamia kuitekeleza. Siku zote anatafuta visingizio kwa kumlumu Nyerere alieondoka madarakani miaka 26 iliyopita, mara mbili zaidi umri wa Taifa jipya la Rwanda chini ya Kagame, na vile vile sawa na umri wa taifa la Uganda chini ya Mseveni. Nadhani anatumia nafasi ya kumlumu Nyerere kwa vile anajua kuwa Nyerere huyo hayupo kwa hiyo hakuna wa kumpinga. Kama Kikwete angekuwa ni kiongozi anayejua wajibu wake, leo hii angekuwa anaonyesha maendeleo aliyoleta nchini tangu mwaka 2005; hakuna alilofanya bali kuongeza ugumu wa maisha na kuwatajirisha marafiki zake na ukoo wake tu.

Tatizo la Tanzania leo hii siyo la kihistoria bali ni la kiuongozi; Tanzania haina uongozi kabisa bali kuna wababaishaji kama Kikwete na genge lake. Wawekezaji wanaondoka kutokana na udhaifu wa serikali, rushwa na miundo mbinu mibovu; siyo Ujamaa wala babu yake na Ujamaa. Hakuna nchi zilizokuwa na Ujamaa mkali kama ule wa Urusi au China, lakini mbona huko bado kuna wawekezaji wanakwenda sana na leo hii China ni taifa la pili kwa utajiri duniani? Amesahau kuwa huko China mtu akishikwa kwa kula rushwa ananyongwa hapo hapo; na wala hakuna ukiritimba mkali kama wa Tanzania. Je Tanzania ni wangapi aliowachukulia hatua yoyote kwa kuhusika na rushwa? Tunasikia tu kuwa tangu Kikwete ameingia madarakani watoto wake wamekuwa ni mabilionea, wakati watoto wa kitanzania wa kawaida wakiwa wanakuwa maskini zaidi kutokana na kutokupata nyenzo za kupatia maendeleo, kama elimu na huduma nzuri za afya. Ujamaa huo huo wa Nyerere ndio uliomfikisha yeye hapo alipo halafu leo eti anautukana.

Nchi kama Marekani ambayo ndiyo babu wa Ubepari, bado utawasikia wana huduma nyingi sana za kijamaa ambazo Tazania ya leo hazipo kabisa; je kama ujamaa ni mbaya hivyo kwa nini nchi zote za Scandinavia ambazo zinatoa misaada sana kwa Tanzania zina mifumo yenye kutoa huduma za kijamaa? kwa mfano huduma za afya, elimu, na malipo ya kujikimu kwa wasiokuwa na Kazi.
 
Mkuu,
Tanzania sio tena makoministi/wajamaa. Tatizo ni kwamba wazee walio na hatamu wanamawazo ya kikoministi na kuendesha serikali kibepari basi wanapoteaaaaaaaaa jangwani. Ndio maana JK, anasema tuwaoondoa hawa wazee na tuweke vijana wenye mawazo ya kibepari kuongoza serikali kiperi. Namuunga JK kwa asilimia 100%. Fukuza wazeeeeee wotee.

Juma Kaseja (JK) ama unaimanisha Jakaya Kikwete? Huyu ana miaka 60 na ushee sasa yeye mwenyewe inabidi aondoke kwanza.....
 
Nendeni hata huko ulaya mkaone ukalinganishe weusi wa mataifa mengine na watanzania, sana sana mjamaa/mkoministi mtakutana naye anapamba pamba kiswahili chake pale kosa mpe mgongo ,teh teh teh

Mbona wapo tu watanzania wengi tu wanaofanya vizuri iwe ulaya au hapa tanzania kuzidi watu wa mataifa mengine, iwe mthungu/mweusi. mbona sita na uzee wakee lakini anajua baya na zuri, mbona slaa na umri wake anajua anacho taka kufanya au anacho takiwa kusimamia na kutolea uamuzi.

Serikali iliyopo imeshindwa kwenye kila kitu sasa wanatafuta mti wa kushikilia na yote ina tereza, kwa mfano suala la uwekezaji katika umeme linatolewa uamuzi na cabinet ambao wameteuliwa na aliye toa kauli na yeye ndio mwenyekiti wao, wanashindwaje kuaamua leo kwenye suala hilo, mpaka maji yakauke ndio waanze sirikali itafanya kila kinachowezekana kuleta umeme. Kushindwa kukua kwa uchumi wetu ambao ndio una leteleza mishahara midogo hautokani na hawa wazee waliopo serikalini bali linatokana na uongozi mbovu tuliokuwa nao, mbona wakati wa mkapa hali ya nidhamu ilikuwa tofauti na sasa.
 
Back
Top Bottom