Kikwete adai tatizo ni ujamaa!

Kiwete aache porojo.

Anazungumzia UJAMAA upi? Je,anataka kutuaminisha kuwa Tanzania bado tunafuata Siasa ya Ujamaa? Kila mtu anajua kuwa Siasa za Ujamaa na Kujitegemea zilizikwa pale Zanzibar baada ya CCM kufutilia mbali sera za Ujamaa na mambo yanayohusiana na Azimio la Arusha.

CCM kutoka hapo waliibuka na Sera mpya ya UBINAFSISHAJI na UGENISHAJI. Kwamba kutoka sera ya Kumilikisha njia zote kuu za Uchumi kwa Wazawa(Wakulima na Wafanyakazi) sasa njia kuu za Uchumi zimemilikishwa kwa Wageni al-maarufu WAWEKEZAJI.

Kwa sasa Raslimali zote ikiwemo MIGODI,VIWANDA na BIASHARA zote muhimu zinamilikiwa na WAGENI pengine tuwaite WAKOLONI!
Mwalimu JK Nyerere(RIP) alichukua au ali-copy sera hizi toka kwa Wachina miaka ya 1960s mapema tu baada ya kuungana na Zanzibar. Nyerere alikuwa na nia njema kabisa kwa Watanzania kwa sababu yeye alikuwa na maono ya mbali.

Leo Wachina wanaofuata sera hizo za kijamaa wamekuwa ni tishio kwa dunia katika nyanja zote. China kwasasa inashindana na USA,JAPANI,UK,Germany,France na nchi zingine za kibebapari1

China huwezi kusikia habari au neno FISADI.Ukipatikana na tuhuma za Ufisadi unakula shaba on the spot! Hakuna longolongo na ndiyo maana wenzetu Wachina leo wako hapo walipo.

CCM wamekataa UJAMAA wakakumbatia UBEPARI na UFISADI wa kutisha!
Kikwete awambie Wa-tz ubaya wa UJAMAA na uzuri wa UGENISHAI/UBINAFSISHAJI ambao umekuwa ni kichocheo cha UFISADI na RUSHWA ndani ya CCM!
 
nakubaliana na wewe 101%

Na wala hawaumizi vichwa wale wazee wanaoitwa watumishi wa umma tena wao wakishapata pesa kupitia huo urasimu wa kijima wao hutumbua tu kwa mibia, magari, vimada na simu za bei kubwa siku hizi wala hawawekezi wanaona ni unyama. Mi naomba kizazi chao kiishe tu tena ningemshauri JK asiwateue tena wenye above 45.
 
Ni kweli kabisa, kila siku nasema humu, tatizo la Tanzania ni wazee wanamawazo ya kikoministi. wakoninisti ni wao tu kupata wengine njaa kali, mwangalieni Putin.

Na ukoministi idea yake imejikita kiwivu wivu, yani ukionekana unakula mayai lazima wenzako wakukuchongee kwa polisi. Angalieni tu na mentality ya watanzania ilivyo wivuuu sana. Miaka ya nyuma ilikuwa hata mtoto wako akipata nafasi ya kwenda sekondari wivuu wa hapo, ila siku hizi imekwisha kwa sababu kila mmoja anaenda.

Kwa msingi huo, ukoministi umejikita ktk mizizi ya kwamba lazima wote muishi maisha sawa, ukichomoza kichwa lazima wewe ni jambazi ,mwizi nk.

Angalia tu URAIA wa nchi mbili, watu walivyo na wivu kwa wenzao, kuna mtu mwingine amejenga hoja eti walio na uraia wa nchi mbili wanapata ile pesa kutoka nchi waliko kwa hiyo wakiruhusiwa kuja watanunua ardhi wao wakose. MTAHANGAIKA mno, lakini msipoona ukoministi ni tatizo basii tena.

Sehemu kulipo na ukoministi, kunatabia ya UMAFIA, yani kuumwagiana acid ninyi kwa ninyi ama kupigana risasi, pia kutengeneza ajali na kuuwa watu.
 
Moja ya tatizo ni hili: leo sikukuu, kesho hakuna kazi, Jumapili hakuna kazi, Jumatatu ni siku ya mapumziko, Jumanne nayo ni siku ya mapumziko. Sasa niambieni, kwa hali tuliyonayo sisi tunaweza kweli kumudu kutokufanya kazi siku zote hizi?

Kwa hiyo hapo utaona kwamba moja ya matatizo yetu ni kuendekeza starehe na uvivu.
Nchi yenye mgawo wa umeme unategemea nini?Madhara yanayotokana na ukosefu wa umeme ni makubwa sana kuzidi hata hayo ya sikukuu.
Serikali ina majukumu ya kuwajengea wananchi mazingira ya kujiletea maendeleo,ndiyo kazi yake hiyo.Tusiwalaumu wananchi peke yao.
 
Nadhani rushwa ni kikwazo kikubwa zaidi kuliko hiyo hoja ya mentality ya ujamaa.Sasa wewe ni rais,mara ya kwanza umewagwaya mafisadi,na sasa unalalamika,kwani hao watendaji si una uwezo wa kuwabadili?Na semina huko Ngurdoto ilikuwa ya nini?Acheni porojo viongozi.
 
Sasa kama sisi kazini kwetu tuna umeme masaa mawili tu! Mgao unatufanya tukae tu! Sasa kama tutakuja kazini siku hizi zote, hli si ile ile? Mie naona sikukuu zinapunguza kuumwa na dhamira yaani ninapokea mshahara bil kufanya kazi!

If this is the attitude then we are toast!
 
Ni kweli kabisa, kila siku nasema humu, tatizo la Tanzania ni wazee wanamawazo ya kikoministi. wakoninisti ni wao tu kupata wengine njaa kali, mwangalieni Putin.

Na ukoministi idea yake imejikita kiwivu wivu, yani ukionekana unakula mayai lazima wenzako wakukuchongee kwa polisi. Angalieni tu na mentality ya watanzania ilivyo wivuuu sana. Miaka ya nyuma ilikuwa hata mtoto wako akipata nafasi ya kwenda sekondari wivuu wa hapo, ila siku hizi imekwisha kwa sababu kila mmoja anaenda.

Kwa msingi huo, ukoministi umejikita ktk mizizi ya kwamba lazima wote muishi maisha sawa, ukichomoza kichwa lazima wewe ni jambazi ,mwizi nk.

Angalia tu URAIA wa nchi mbili, watu walivyo na wivu kwa wenzao, kuna mtu mwingine amejenga hoja eti walio na uraia wa nchi mbili wanapata ile pesa kutoka nchi waliko kwa hiyo wakiruhusiwa kuja watanunua ardhi wao wakose. MTAHANGAIKA mno, lakini msipoona ukoministi ni tatizo basii tena.

Sehemu kulipo na ukoministi, kunatabia ya UMAFIA, yani kuumwagiana acid ninyi kwa ninyi ama kupigana risasi, pia kutengeneza ajali na kuuwa watu.
Mkuu hata huku majuu wapo viongozi na vyama vya Kijamaa na hawana mawazo kama yako..Kwa nini mnapenda sana kushirikisha Ujamaa na Ukomunist hali ndani ya Ubepari kuna Ujamaa pia..
Na iweje hao viongozi mnaowasema wao ni wajamaa ndio Mabepari wa Tanzania leo hii. JK yeye asema Ujamaa ndio tatizo, kwa huo utajiri wake wa 10% toka Barricks na Sinclair ndio unahesabika kuwa Ubepari?

Wananchi ni wavivu kutokana na mfumo mzima wa kiutawala kwa sababu nchi ni maskini..Leo hii ukichukua maana halisi ya Conservative na kui apply Tanzania tutaitwa wabaguzi na siasa ambayo haifai kabisa, lakini Ulaya ndio sehemu ya Ubepari wenyewe. Pengine jifunzeni zaidi tofauti za mrengo badala ya kutumia siasa za Ukomunist dhidi ya Capitalism wakati wananchi wote leo hii wanapinga serikali kuhodhi njia kuu za uchumi lakini bado mnawaita wajamaa kwa tafsiri ya Ukomunist. Nani leo hii bado anataka Ukomunist?
 
Jokakuu,
Mkuu kwa maneno ya JK sidhnai kama anastahili hata kuwa mwenyekiti na kiongozi wa CCM kwa sababu amepinga hadharani mrengo wa chama chake. Na labda kashindwa kuelewa vizuri kwamba hao wawekezaji wanapoingia nchi wameshafanya utafiti wao kuchambua baina ya siasa za Ujamaa na policies za uwekezaji..Kwa nini mnaendelea kuvuta Ujamaa ule hali viongozi wote wa Tanzania na watumishi wake ni Mabepari kupindukia, tena mirija isiyotakiwa ndani ya Ubepari wenyewe.

Mtumishi wa Umma atamwona mwekezaji kama mwizi tu pale alipoona mkataba wa huyo mwekezaji hauna manufaa kwa nchi na hili halina fikra za Kijamaa au Kibepari. Pengine JK anahitaji kujifunza yeye nini maana ya Ubepari na tofauti zilizopo leo ktk mfumo huo tofauti na ule wa wakati wa vita baridi. Hakuna Mtanzania ambaye hapendi wawekezaji lakini sii kwa mtindo huu wa Ukoloni mamboleo kuuza na kuinadi nchi ichukuliwe pasipo manufaa kwao. Hata Mabepari waliobobea hao Marekani, Uingiereza, Japan na Canada wanapiga vita uwekezaji wowote ambao hauzingatii national interest bali kufuata na kupangiwa masharti na mwekezaji..

Tanzania tunakabiriwa na Ufisadi uliopita mipaka yote ya uwekezaji kiasi kwamba kila mwekezaji kutoka nje huona watu wamelala..Lazima awe mwizi au fisadi vile vile kwa sababu wao ndio wenye kauli. hatuwezi kujifananisha na nchi zilizoendelea ambazo Ubepari kwao wanapanga masharti kwa wawekezaji hali sisi na umaskini wetu tunapangiwa masharti.

UBepari nchi za Ulaya unategemea wawekezaji wa ndani yaani wananchi raia wa nchi hizo hali sisi tunategemea bepari ni mwekezaji kutoka nje kwa sababu wananchi wenyewe hawana uwezo huo...Haya tu yanatosha kuona tofauti za kitaalam ktk kuendesha Ubepari nchi zetu na hizo za Ulaya badala yake tunajaribu kuiga Ubepari wa Ulaya kwa sababu ndivyo tulivyofundishwa darasani..

JK ameshindwa kabisa kufahamu tatizo la Tanzania ktk uwekezaji ila ametafuta visingizio pasipo kufanya utafiti wa kina kufahamu nini matatizo yetu haswa..UFISADI... Ufisadi ambao ndio mbegu ya kuimarika kwa Urasimu na ukiritimba ni sababu kubwa ya wawekezaji wenye nia nzuri kutowekeza Tanzania, kwani hakuna hata kitu kimoja ambacho kipo huru, rahisi na taratibu zake zinamwezesha mwekezaji kuweka makadirio ya investment, matumizi, muda na hata uwezekano wa kufanikiwa kufungua biashara aliyokusudia.

KIla hatua ya uwekezaji nchini ina Ukiritimba unaojenga nafasi kubwa ya urasimu kwa sabahu ya mfumo duni wa kiutawala....Maadam kila mbuzi atakula kwa urefu wa kamba yake hakuna sheria tena inayoweza kudhibiti wanachokula mbuzi hawa.. Ni lazima uhonge kupata hata TIN namba, vibali, eneo na kama anategemea zana za uzalishaji kutoka nje atakwama bandarini kwa muida usiojulikana. JK katembelea wizara na kutazama tu utendaji kazi wake ktk nafasi ambazo tayari zimesimama badala ya kutazama sababu ya sehemu ambazo zimeshindikana..

Kama angechukua muda kuwauliza wawekezaji hata kupitia balozi zao tu angepata upeo mzuri zaidi wa jinsi Ufisadi ulivyokithiri nchini kiasi kwamba wawekezaji wanashindwa kupata picha halisi ya uwekezaji in term of success. Hata mwananchi akitaka kuwekeza ktk jambo dogo sana inampa shida kufuatilia taratibu za upatikanaji wa vibali.. paper work ni nyingi zisizokuwa na msingi na kibaya zaidi ni ofisifi nyingi zinahusika na kibali kimoja tu hii ikiwa na maana mfumo za taratibu za kiuchumi nchini zimejenga zaidi nafasi za urasimu na ulaji kwa wafanyakazi wake.

Lleo hii Tanzania hata mlinzi (gatekeeper) anataka apewe chochote ili upate kuingia ofisini na akikataa huna pa kwenda kulalamika. Na kila hatua unayokwenda lazima utoe hongo tena kwa kiwango wanachokijua wao kinyume kabisa na taratibu. Na usipofanya hivyo, kazi yako imelala na huna pa kwenda kulalamika..No one give a damn!..

Nilipokuwa Bongo mshikaji wangu mmoja aliibiwa laptop yake toka ktk gari lake mitaa ya O'Bay.. tulipokwenda kutoa report polisi waliandika kesi ya jamaa kwenye jarida la kitabu using a pencil..Na tulipouliza walisema hawna karatasi hivyo tukaenda kununua karatasi na kalamu..Just imagine kituo cha O'bay polisi hakina karatasi achilia mbali kuwa na computer wala data base na leo tunazungumzia miaka 50 ya Uhuru. Je kutokuwa na vitu hivyo ni mawazo ya kijamaa au Wajamaa ni wao viongozi ambao wameshindwa kutoka ktk mfumo duni wa kizamani.Barabara zinajengwa kabla ya mifereji ya majitaka, umeme na njia za simu na maji.

Miji mipya unajengwa na wananchi pasipo kupimwa lakini utakuta tayari Tanesco wameisha sambaza miti ya umeme wakati hakuna ramani za barabara..Again Tanesco wanatumia miti badala ya Aluminium poles zenye thamani ndogo zaidi na zinazodumu kuliko hiyo miti. Leo hii hatuna maji, Umeme na mvua kidogo tu iliyonyesha Dar mji mzima unanuka, kinyesi kinaelea barabara kuu utafikiri ni part of mapambo ya barabara.

Jamani mwekezaji gani kweli atapenda kuwekeza Tanzania na sii Rwanda, Kenya au Uganda ambako kidogo wameweza kudhibiti urasimu ktk nafasi nyeti za uwekezaji. Makusanyo ya kodi bado ni ya kukadiliwa ina maana hakuna sheria wala utaratibu unaotoza mtu kulinganana kipato isipokuwa makisio..

Hili tu linamfukuza mwekezaji yeyote kabla hajafahamu kuna njia za mkato..Katika business plan yeyote ile kiwango cha tax kinachotakiwa kulipwa kinatakiwa kiwe wazi kulingana na mapato ya mwekezaji lakini inapofikia mwekezaji kuanza kubishana na afisa wa TRA kuhusiana na kodi hapo tena huwezi kulalamikia Ujamaa bali sisi wenyewe kukurupukia Ubepari pasipo kujua kwamba Ujamaa wa leo ni part ya Ubepari vile vile, hivyo hauwezi kustafrika kama ni fikra finyu za watumishi wa umma wanapowatazama wawekezaji kama ni wezi wa mali zao.

Mmh nimesoma post hii ya Mkandara kwa kweli inaelimisha sana tu na ina taarifa nyingi za kutosha. Lakini kama mtu mwenye mawazo kama haya atakuwa kwenye nafasi ya kufanya maamuzi ili nchi yetu isonge mbele naweza sema ni afadhali ya statement za KIKWETE zina pakuanzia kuliko hii yako mkuu.
 
Kiwete aache porojo.

Anazungumzia UJAMAA upi? Je,anataka kutuaminisha kuwa Tanzania bado tunafuata Siasa ya Ujamaa? Kila mtu anajua kuwa Siasa za Ujamaa na Kujitegemea zilizikwa pale Zanzibar baada ya CCM kufutilia mbali sera za Ujamaa na mambo yanayohusiana na Azimio la Arusha.

CCM kutoka hapo waliibuka na Sera mpya ya UBINAFSISHAJI na UGENISHAJI. Kwamba kutoka sera ya Kumilikisha njia zote kuu za Uchumi kwa Wazawa(Wakulima na Wafanyakazi) sasa njia kuu za Uchumi zimemilikishwa kwa Wageni al-maarufu WAWEKEZAJI.

Kwa sasa Raslimali zote ikiwemo MIGODI,VIWANDA na BIASHARA zote muhimu zinamilikiwa na WAGENI pengine tuwaite WAKOLONI!
Mwalimu JK Nyerere(RIP) alichukua au ali-copy sera hizi toka kwa Wachina miaka ya 1960s mapema tu baada ya kuungana na Zanzibar. Nyerere alikuwa na nia njema kabisa kwa Watanzania kwa sababu yeye alikuwa na maono ya mbali.

Leo Wachina wanaofuata sera hizo za kijamaa wamekuwa ni tishio kwa dunia katika nyanja zote. China kwasasa inashindana na USA,JAPANI,UK,Germany,France na nchi zingine za kibebapari1

China huwezi kusikia habari au neno FISADI.Ukipatikana na tuhuma za Ufisadi unakula shaba on the spot! Hakuna longolongo na ndiyo maana wenzetu Wachina leo wako hapo walipo.

CCM wamekataa UJAMAA wakakumbatia UBEPARI na UFISADI wa kutisha!
Kikwete awambie Wa-tz ubaya wa UJAMAA na uzuri wa UGENISHAI/UBINAFSISHAJI ambao umekuwa ni kichocheo cha UFISADI na RUSHWA ndani ya CCM!
Kaka

The Chinese, are at the point where they invest in sport franchises, wewe unaongela ujamaa. Hawa washapita na ujamaa longtime; their soo capitalist to the point western 'left side' politacal parties seem radical in their eyes.
 
Kwa sheria hizi za uwekaezaji tulizonazo......lazima muwekezaji tumuone kama mwizi tu.... hana faida hata chembe kwa wananchi......lazima turekebishe sheria ndiyo muwekezaji tutamwona ni mwenzetu.....

Sijui kwanini wengine hawajaona hili, ukweli mwekezaji hapa hapendwi kwasababu ya sheria za kifisadi zilizowekwa, ukienda Botswana utashangaa jinsi wanavyonufaika na rasilimali, hapa kuna mdudu gani tushindwe? Kama ni rasilimali tunazo nyingi kushinda wao lakini kwa sheria hizi za kifisadi wawekezaji hatuwataki mpaka hapo sheria zitakapokuwa za kizalendo..
 
I think we put too much expectation to people who by all standards they dont know if they dont know. Kati ya rushwa ya kitu kidogo na ujamaa upi unakimbiza wawekezaji?

Dr. Slaa have already put it right hata kama wanadai CCM ina practice ubepari basi hata huo bado maana yake hawajaijua vizuri.

Capitialism is not synonimous to ufisadi neither to wizi nor to holela. It is more on proper property rights definition and lowering of transaction cost. It is more based on legal payment of the efforts spent based on demand and supply principal. It is more on capital investment of private entities than the government involvement in investments.

Hata siku moja capitalism haijakataa kuwa kuna public goods and bads. What CCM and its government is doing is not found in any mode of production's and governance dictionaries labda kama wata kuwa founders wa new Ideology ambayo tutawaomba watupatie na jina lake. Kwasababu iko centred kwenye ufisadi na confusion which has resulted into cheos.
 
Mmh nimesoma post hii ya Mkandara kwa kweli inaelimisha sana tu na ina taarifa nyingi za kutosha. Lakini kama mtu mwenye mawazo kama haya atakuwa kwenye nafasi ya kufanya maamuzi ili nchi yetu isonge mbele naweza sema ni afadhali ya statement za KIKWETE zina pakuanzia kuliko hii yako mkuu.
Mkuu ni kweli kabisa maneno yako..Maadam umejifunza mengi sii rahisi kutoa maamuzi yenye busara ili nchi ikasonga mbele wakati unajifunza ila pale utakapo elimika na kuelewa nini ni nini.
Nchi yetu inatawaliwa na Ubepari uliopitiliza..Kwa imani kwamba - Ufisadi ni part ya Ubepari, hivyo sii rahisi kabisa kuelewa kwamba hata Ubepari una taratibu na haramu zake sii kila kitu RUKSA!
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Ndiyo matatizo ya kukurupuka na kutoa kauli bila kutafakari kwa kina. Dunia ya sasa anayoizungumzia ndiyo ipi? ya kuwakaribisha wawekezaji wasiolipa kodi? Wanaoruhusiwa kuchimba rasilimali na kutuachia 3% tu!? Au wawekezaji wa kutoka Houston, Texas Richmond/Dowans ambao ni matapeli tu na kumbe ni wa Kariakoo tu? Au wale wahindi wa RITES ambao walipewa 51% ya hisa za TRC bila kutoa hate senti moja na sasa wanatakiwa kulipwa $87 millioni, au hawa Wahindi walionunua Zain na Serikali kukosa kodi ya shilingi bilioni 500 kwa uzembe wao wa kufikiri?

Ni aibu kuwa na mtu kama huyu katika nafasi yoyote ile ya uongozi.

Bubu ataka kusema ni kweli wale wahindi wa airtel hawakulipa bil.500 lakini kuna vile vijisenti huwa wanawekewa kwenye a/c zao kama kule kisiwani kwa chenge
 
Moja ya tatizo ni hili: leo sikukuu, kesho hakuna kazi, Jumapili hakuna kazi, Jumatatu ni siku ya mapumziko, Jumanne nayo ni siku ya mapumziko. Sasa niambieni, kwa hali tuliyonayo sisi tunaweza kweli kumudu kutokufanya kazi siku zote hizi?

Kwa hiyo hapo utaona kwamba moja ya matatizo yetu ni kuendekeza starehe na uvivu.
Nchi tajiri hazina long weekends?
 
Jamani mwekezaji gani kweli atapenda kuwekeza Tanzania na sii Rwanda, Kenya au Uganda ambako kidogo wameweza kudhibiti urasimu ktk nafasi nyeti za uwekezaji. Makusanyo ya kodi bado ni ya kukadiliwa ina maana hakuna sheria wala utaratibu unaotoza mtu kulinganana kipato isipokuwa makisio..

Hili tu linamfukuza mwekezaji yeyote kabla hajafahamu kuna njia za mkato..Katika business plan yeyote ile kiwango cha tax kinachotakiwa kulipwa kinatakiwa kiwe wazi kulingana na mapato ya mwekezaji lakini inapofikia mwekezaji kuanza kubishana na afisa wa TRA kuhusiana na kodi hapo tena huwezi kulalamikia Ujamaa bali sisi wenyewe kukurupukia Ubepari pasipo kujua kwamba Ujamaa wa leo ni part ya Ubepari vile vile, hivyo hauwezi kustafrika kama ni fikra finyu za watumishi wa umma wanapowatazama wawekezaji kama ni wezi wa mali zao.
Mkandara, you have summed it up.

Hivi JK hajui hayo yote uliyoandika hapo juu? Hopefuly anatembelea hapa asome hii posting yako. Ndo ukweli, no body gives a damn bongo. Kipindi kile cha kubadili passport, ilikuwa inacost $ 50 dollars hapa marekani. Kipindi hicho nilikuwa na safari ya bongo, nikaamua niende kuibadilisha bongo, ilinikosti laki mbili na elfu hamsini.

Rushwa ni utaratibu wa kawaida kabisa bongo na ni utamaduni wetu. Na kipindi hicho umeme ulikuwa hakuna, ukiingia hapo jengo la wizara ya mambo ya ndani ni kama jehanam. Na rushwa utatoa tu, maana hiyo foleni na hiyo sweating na vikwapa humo ndani hata kupumua yenyewe ni tabu. Nchi imeoza kabisa. Yani hapo ni wizarani. Kila pahali pameoza bongo.

Kui-fix bongo ni kazi. Kwanza pa kuanzia tu penyewe inahitaji utafiti. Kuufuta utamaduni wetu wa rushwa si kazi ndogo.
 
Mkuu hata huku majuu wapo viongozi na vyama vya Kijamaa na hawana mawazo kama yako..Kwa nini mnapenda sana kushirikisha Ujamaa na Ukomunist hali ndani ya Ubepari kuna Ujamaa pia..

Na iweje hao viongozi mnaowasema wao ni wajamaa ndio Mabepari wa Tanzania leo hii. JK yeye asema Ujamaa ndio tatizo, kwa huo utajiri wake wa 10% toka Barricks na Sinclair ndio unahesabika kuwa Ubepari?

Wananchi ni wavivu kutokana na mfumo mzima wa kiutawala kwa sababu nchi ni maskini..Leo hii ukichukua maana halisi ya Conservative na kui apply Tanzania tutaitwa wabaguzi na siasa ambayo haifai kabisa, lakini Ulaya ndio sehemu ya Ubepari wenyewe. Pengine jifunzeni zaidi tofauti za mrengo badala ya kutumia siasa za Ukomunist dhidi ya Capitalism wakati wananchi wote leo hii wanapinga serikali kuhodhi njia kuu za uchumi lakini bado mnawaita wajamaa kwa tafsiri ya Ukomunist. Nani leo hii bado anataka Ukomunist?

Mkandara
Ujamaa ndo huo ukominist walioumodify. Ujamaa mie pia nauita ukoministi ndo ujinga wake huo wa kupumbaza watu wakati wachache wanajilimbikizia.

Mkandara unaongea nini, umeshifika moscow kwa waasisi wa ujamaa? kuna matajiri balaa na masikini balaa wanaodanganywa na ujamaa aka ukoministi.

Wewe unafikiri viongozi wa urusi ni masikini, unafikiri akina PUTIN ni masikini , unafikiri Medvedved ni masikini? lakini nenda kule SEBERIA jimbo moja urusi utatoa machozi wewe.

Wewe unachanganya u-Conservative sio ujamaa/ukoministi, u-conservative ni kutokubali mabadiliko. Mfano kule NANSIO ukerewe kuna vijibabu ni vi-conservative ukiwapelekea mke wa kizungu wanakukana wewe sio mtoto wao. huo ndo ukosevertive, na ile mlengo mwingine ni kukubali mabadiliko kwendana na wakati, Mfano kwetu nikienda na mzungu wale mamba hawawezi kuleta fujo maana wanakubali mabadiliko kulingana na wakati.

Ukoministi ndo ujinga wake huo, umekaa kaa kuogopana kuchongeana ninyi kwa ninyi wakati maviongozi yanafaidika na huo ujinga, wajamaa wote Tanzania wakitupwa nje, tukaiingia vijana Tz itapaa.
 
Hapa Kikwete kwa mara ya kwanza kaongea point yenye akili sana. wachangiaji wa mwanzo hili lililosemwa na kikwete lina ukweli midingi maofisini humo wakiritimba hata kwa wawekezaji wa ndani yaani private sector na wao ni kama paka na panya. Sijuwi kitaisha lini hiki kizaji cha Mwalimu Nyerere?.

Na kwa taarifa yenu kwa kila Mtanzania aliyefanikiwa kiuchumi kupitia private sector atakubaliana na haya isipokuwa wale mnaonufakaika na system zisizo wazi na ukiritimba, maana wao akili yao inaishia kuomba mgao eti kwa vile mtu amekuja kuchukua cheque yake.
je suis d’accord , nakubaliana kabisa mkuu.
 
Mi nadhani JK hajuhi yupo wapi na wala hajui kutofautisha kati ya Ujamaa na mifumo mingine ya kisiasa, kama nchi ingekuwa kwenye ujamaa basi angelisema hilo na tungemuelewa, Ujamaa na Azimio la Arusha lilikufa Zanzibar na tukaingia kwenye siasa nyingine isiyo na jina, malengo wala Mwelekeo, na hapo ndipo lilipo tatizo.

Ujamaa ulikuwa na Direction na zilisimamiwa japo zingine zilifail, lakini zilifail zikiwa kwenye kutekelezwa,
JK anashindwa kujua sasa nchi ya Tanzania inaongozwa na Sera/Slogan za uchaguzi ( kasi zaidi, nk) bila kuwa na vipaumbele na msingi wa kusimamia hivyo vipaumbele

cha muhimu pia JK inampasa kujua hata hao Mabepari anaoprefer nao pia wana practice ujamaa, maana bila kuwa mjamaa Bepari hawezi kusimama
 
Mkandara
Ujamaa ndo huo ukominist walioumodify. Ujamaa mie pia nauita ukoministi ndo ujinga wake huo wa kupumbaza watu wakati wachache wanajilimbikizia.

Mkandara unaongea nini, umeshifika moscow kwa waasisi wa ujamaa? kuna matajiri balaa na masikini balaa wanaodanganywa na ujamaa aka ukoministi.

Wewe unafikiri viongozi wa urusi ni masikini, unafikiri akina PUTIN ni masikini , unafikiri Medvedved ni masikini? lakini nenda kule SEBERIA jimbo moja urusi utatoa machozi wewe.

Wewe unachanganya u-Conservative sio ujamaa/ukoministi, u-conservative ni kutokubali mabadiliko. Mfano kule NANSIO ukerewe kuna vijibabu ni vi-conservative ukiwapelekea mke wa kizungu wanakukana wewe sio mtoto wao. huo ndo ukosevertive, na ile mlengo mwingine ni kukubali mabadiliko kwendana na wakati, Mfano kwetu nikienda na mzungu wale mamba hawawezi kuleta fujo maana wanakubali mabadiliko kulingana na wakati.

Ukoministi ndo ujinga wake huo, umekaa kaa kuogopana kuchongeana ninyi kwa ninyi wakati maviongozi yanafaidika na huo ujinga, wajamaa wote Tanzania wakitupwa nje, tukaiingia vijana Tz itapaa.
Mkuu hapa sikuelewi..

Hivi Russia bado ni Makomunist? hakuna mtu anayetetea Ukomunist hapa na nini zilikuwa athari zake. Russia, China na hata Cuba viongozi wa nchi hizo ni walikuwa matajiri chini ya mfumo wa Kikokunist na kinachoweza kulalamikiwa ni mfumo ule wa Kikomunist uliowatajirisha..Tofauti na Tanzania viongozi wetu walikuwa maskini ndani ya Ujamaa leo hii ni matajiri wakubwa sana wakitumia Ubepari kama ngazi ya kupandia.

Russia na China wapo matajiri wengi wameibuka ambao wanafanya kweli lakini hatuwezi kusema mafanikio ya nchi hizi yanatokana na Ujamaa wao (Ukomunist) kwa sababu tu Tanzania tunafail ktk Ubepari na kusingizia Ujamaa. Wao hao Russia na China walikuwa ndani ya Ujamaa kwa miaka mingi kuliko sisi na walibobea zaidi kiimani, mbona wao wanaedelea na wameweza kubadilika ghafla.

Sababu ni ndogo sana, wenzetu walikuwa na uwezo (Elimu na nguvu kazi), waliweza kudhibiti mirija na taratibu za uwekezaji ili kuepuka ukoloni mamboleo kwa maslahi ya nchi zao. Wawekezaji wakubwa ni raia wa ndani na hawapangiwi masharti na wawekezaji toka nchi za nje Kifupi wao sii wahitaji bali ni washiriki ktk dunia hii ya Utandawazi na soko huria hali sisi ni consumers yaani tunategemea kulishwa..

Mwisho mkuu wangu huyo mzee wa Kikerewe ndiye nasema ataonekana kuwa na mrengo usiokubalika nchini wakati huko Ulaya Conservative ni mrengo unaokubalika kwa sababu hawa jamaa zetu wako miaka 200 mbele yetu wamisha jenga Taifa linaloitwa Marekani, Uingereza na kadhalika pasipo kujali makabila au asili za raia wake na zaidi ya hapo ni matajiri ambao wanaweza jitegemea na sii maskini kama sisi ombaomba tukaige kushuka kimba kama la tembo! Uchumi wa Tanzania unapasuka msamba na hakuna sababu yeyote zaidi ya kuiga Tembo..
 
Back
Top Bottom