Kikwete achimba mkwara mzito!!

Na "usanii" unaendelea....nakumbuka wakati wa kampeni JK aliwaahidi wananchi nafasi za kazi milioni moja....hmmmm......ziko wapi..??
 
`` The past non-interference in member countries internal affairs has no place in our continent.´´ Jakaya Kikwete, Chair, African Union and President of Tanzania, 10-27-2008

Ni makosa kusema moja kwa moja, wazi wazi, ``kutoingilia mambo ya ndani ya nchi wanachama hakuna nafasi tena barani mwetu.´´

Hata mwanadiplomasia wa Kimarekani, nchi ambayo inaongoza duniani kwa kuchokonoa mambo ya wengine, angekuwa makini sana kutumia lugha kama hiyo. Viongozi wetu kutokuwa makini katika public communication sasa wanaenda kutuabisha katika jukwaa la kimataifa.

Ni careless, unconsidered language kwa sababu inaweza kutafsiriwa kuhalalisha kuingilia mambo ya ndani yoyote yale ya nchi nyingine. Alitakiwa katika sentensi hiyo hiyo aainishe kwa ufasaha kabisa kwamba hii international policy mpya hii ya Afrika inahusu specifically maeneo ya trammeled democracy ambapo kunatokea human crises, kama Zimbabwe. Usipoiweka wazi kwa ufasaha ndio unaanza kuwa misquoted na misinterpreted na misunderstood.

Foreign polices za kuingilia yaliyo ya ndani ya nchi nyingine zinalaaniwa duniani kama vyanzo vya vita na ukoloni mamboleo, hususan dhidi ya mataifa madogo, kwa sababu tunapigana na paternalistic hegemony ya Western imperialists. Kiongozi wa Afrika inabidi awe makini na fasaha sana akitumia lugha kama hizi za kuhalalisha kuingilia mataifa mengine.

Muda wake wa African Union sijui utaisha lini tujitoe huko kwenye kuiongelea Afrika.
 
Kuhani,

..sasa huyu ndiyo ana uzoefu wa miaka 10 kama mwanadiplomasia mkuu wa Tanzania kabla hajawa Raisi!!!

..halafu sijui huu mtazamo au uamuzi mpya wa kutokuheshimu tena mambo ya ndani ya nchi wananchama wa AU, umefikiwa na kikao gani rasmi cha AU.

..cha kusikitisha zaidi ni kwamba alikatisha ziara yake Tabora na kupanda ndege kwenda Afrika Kusini kutoa matamshi ya ajabu-ajabu kama haya.
 
Katika forum/audience kama ile......JK akiwa kama Mwenyekiti wa AU na kwa uwezo wake mlitaka aseme nini?

nadhani jk alisema haya kama mwenyekiti wa au. swali ni "jee huu ndio msimamo rasmi wa au na ulifikiwa na kikao gani cha juu cha au?" kama kuna huo uamuzi nadhani si vyema kumshambulia jk kuhusu huo msimamo

tatizo ni kama mkuu kuhani alivyosema hapo juu ni lugha aliyotumia kuwasilisha huo msimamo
 
..Kikwete amechimba mkwara wa 'kuwashukia' madikteta wa Afrika.

..hivi uwezo huo upo kweli, au ni usanii tu?


Tulishaweka hadi thread hapa JF kuhusu hali ya eastern congo kuwa siyo shwari...na kwamba ni Kagame ndiyo anacheza proxy war..lakini JK aliendelea kutalii Amerika na Ulaya...kana kwamba yanayotokea Congo ni mambo ya kawaida tu..
Sasa leo anakuja na vimaneno maneno vya kiusanii sanii ili kujaza watu tu ..kama kweli anayo nia ya kupambana na madikteta aanze na jirani yake Kagame ambaye moja kwa moja anamsaidia Nkunda na kuchafua amani mashariki ya congo.

Haya thread yenye hii

www.jamiiforums.com/internationa-forum/19079-rwanda-troops-invade-dr-congo.htm


Wembe.
 
Mheshimiwa rais wetu ni hodari kuongea tu....Kikwete has got charisma but he is not a Leader, this is to my fellow africans who think highly of The AU Chairman.
 
Back
Top Bottom