Zitto
Former MP Kigoma Urban
- Mar 2, 2007
- 1,562
- 10,880
Ninajiquote nilichosema tarehe 15/10/2009
Ninapendekeza;
Ikulu inasema wafanyabiashara ndio wamemwomba Rais. Ni sawa tu........
Ninapendekeza;
- Serikali ihakikishe mitambo ya IPTL inawashwa mara moja wakati mazungumzo yake na IPTL yakiendelea kwa kuharakishwa (fast tracking). Hali ya nchi ni mbaya, ni sawa na vita, haiwezekani serikali yenye mamlaka ishindwe kuhakikisha IPTL inazalisha umeme wakati mazungumzo yakiendelea. Haiwezekani.Labda kama haina uchungu na maisha ya watu wake.
- Sikutaka kusema chochote nikiamini kwamba Shirika la TANESCO, Serikali, na kwa upande wa bunge, Kamati ya masuala ya Nishati na Madini, wangeweza kutoa majibu ya tatizo linatukabili. Badala yake, juhudi nyingi zimetumika kutafuta chanzo cha tatizo na kuchelea kutoa suluhuInaumiza sana kuona kuwa tunaendekeza siasa rahisi tunaposhugulikia masuala mazito ya kitaifa kama Nishati. Inasikitisha zaidi pale tunapoona kuwa serikali inashindwa kuchukua hatua mahususi za kuhami uchumi wa Taifa letu. Serikali na Bunge hazitoi suluhisho la hali hii na ni wazi kuna kutupiana mpira wakati nchi inaumia. Serikali imewekwa madarakani ili ifanye maamuzi na tuihukumu kwa maamuzi hayo. Serikali ni lazima sasa iamue.
- Mazingira magumu kama haya yanahitaji maamuzi magumu (extra ordinary circumstances require extra ordinary decisions). Ninaamini serikali itazingatia ushauri wangu.
Ikulu inasema wafanyabiashara ndio wamemwomba Rais. Ni sawa tu........