Kikwete Aahidi Bajaj 400

Hivi ana washauri? Wametafakari logistics za kuziendesha na kuzihudumia hizo Bajaj? Na tatizo hilo lipo Chunya tu au ndio nchi itajazwa Bajaj za serikali? Tupo karne hii ya technolojia kweli tukiwaza kutumia Bajaj kuwapeleka wajawazito hospitali?
 
Mgombea Urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi(CCM),Jakaya Kikwete ameahidi kutoa pikipiki za miguu mitatu(Bajaj) 400 za wagonjwa(ambulance) kwa nchi nzima na gari moja la Wagonjwa kwaajili ya kituo cha afya cha Mkwajuni ili kuwasafirisha wajawazito katika Wilaya ya Chunya.

Akizungumza na Wakazi wa Mkwajuni Wilayani hapa wakati wa mkutano wake wa kampeni,Kikwete alisema ahadi hiyo ataitekeleza pindi atakapochaguliwa kurejea kwenye kiti alichonacho hivi sasa.

Chanzo:Tanzania Daima.

Mwandishi: Irene Mark.Mbeya.

My take.

Bajaj na wajawazito hii kali hata kipindi cha zama za mawe hii isingekubalika.Bado sijamuelewa ana maanisha nini!!1 kazi ipo.

Dada Regia ukiona hivyo ujue maji yako shingoni kwani hata hawezi kufikiri kuwa inawezekana?
 
Aliye nifurahisha ni mke wake, Salma, amempiga hadharani kuwa maisha bora hayataletwa na Serikali bali yataletwa na watu wenyewe! Yaani kila mtu anasema yake.

V8 ni kwa ajili ya viongozi kutanua na akina dada na mama zetu warushwe-rushwe na bajaji? HAO NDO VIONGOZI WENU WA TANGU UHURU!
 
Tokea ameanza kampeni kuna idadi ya ahadi kama 25 hivi kama sio 30 kujenga viwanja vya ndege, kununua meli, umeme na nyingine nyingi ataweza kweli huyu mkulu

Well, he dont have to!! Hiki ni kipindi chake cha mwisho kuwa madarakani, hizo ahadi utamuuliza lini wakati he will never ever go back again kuomba au kumuombea mtu kura! Mkapa kama alitoa ahadi wakati wa kipindi chake cha mwisho zilikwenda na maji--hakuna aliyemuuliza JK kuhusu ahadi za Mkapa( infact yule mzee Mkapa alikuwa hatoi ahadi, alikuwa anafanya). JK atatoa nyingi tu this time, na nyingine za kuudhi na kuchekesha, who cares, akishashinda kura October 31, ndio imetoka, wadanganyika hamtamuona tena, sana sana watakaomfaidi JK ni wabeba mabox huku majuu, manake atachanja mbuga kishenzi na kuwaachia nchi kina RA kuimaliza.
Nimeongea hivi assuming kuwa JK na ccm watapita this time!! which I do not believe so
 
Hivi ana washauri? Wametafakari logistics za kuziendesha na kuzihudumia hizo Bajaj? Na tatizo hilo lipo Chunya tu au ndio nchi itajazwa Bajaj za serikali? Tupo karne hii ya technolojia kweli tukiwaza kutumia Bajaj kuwapeleka wajawazito hospitali?
Hii ahadi ipo kwenye ilani ya uchaguzi ya CCM? I am just wondering kama ahadi hizi zote zipo kwenye ilani, mwenye kuwa aliisoma tunaomba msaada. Isije kuwa ilani ya CCM kwa sasa ni draft na wataikamilisha baada ya JK kumaliza kampeni zake
 
Ninaamini msajili wa vyama amekutana na changamoto kubwa ambayo itaamua hatima ya heshima yake kwa jamii ya kitanzania hata na nje ya nchi. Kwenda kinyume na boss wake, yaani aliyemteua kushika wadhifa alio nao au kutenda haki kulingana na sheria za nchi na uadilifu. Hoja iliyoko mbele yake ni nzito, nikimaanisha siyo ya kukurupuka kutoa majibu marahisi.

Wachambuzi wa mambo ya kisiasa wameichambua hoja ya CHADEMA na hakika kama haki itafuatwa, mgombea wa CCM huenda akaenguliwa kwenye kugombea uraisi. Lakini ni hoja ipi hasa inayomuweka Raisi Kikwete kwenye hatari hii? Kuongeza mishahara kwa wafanyakazi ndio hoja yenye nguvu. Laiti kama tungaliweza kuona nafsi za watu tungefahamu ni nini hasa lilikuwa kusudio la Kikwete, kwa kuwa uwezo huo hatunao, basi hatuna budi kuchambua na kuangalia mambo kama haya yaliyowahi kutokea siku za nyuma.

Miaka kadhaa iliyopita wahudumu wa afya waligoma na serikali iliongeza mishahara, je ongezeko lile liliidhinishwa na bunge? nafikiri haikuwa hivyo, je hela hizi zilitoka wapi na mbona wanasiasa hawakucharuka kusema serikali imevunja sheria? Nahisi Msajili anaweza kutumia mfano huu kufanya maamuzi marahisi. Nahisi akifanya hivyo atakuwa amefanya kosa kubwa mno litakalomgharimu heshima yake. Kwa nini nasema hivi?

Tuende ndani kidogo, Kwanza kabisa sasa hivi issue kubwa hapa ni uchaguzi na sheria inayosimamia uchaguzi huo. Pili, Raisi alishatoa tamko hadharani kabla ya kampeni akiwa anatumia jukwaa kama Raisi kuwa Serikali haina uwezo wa kuongeza mishahara, na hakukuwa na emergency iliyokuwepo wakati wa mgomo wa madaktari (Kuwa kuna wagonjwa walikuwa wanakufa kwa wao kugoma). Kikwete hapa hana ujanja maana wafanyakazi walisharidhia kuwa hamna ongezeko la mshahara; hawakuwa wamegoma na kulikuwa hamna emergency yoyote kama watu kupoteza maisha.

Nini hasa kilichomsukuma Kikwete kuongeza mishahara? Kwa bahati mbaya ama kwa kutokufahamu kwa wasaidizi wa kikwete, hakufahamu vizuri kundi hili lina nguvu gani katika kushawishi wapiga kura. Wafanyakazi walipoamua kuweka wazi msimamo wao na kampeni zilizoleta kuchapishwa t-shirt (Sizitaki kura za wafanyakazi) ilikuwa ni dalili mbaya kwa CCM. Hata wakati wagombea wanarudisha form Wafanyakazi walionyesha wazi ni nani chaguo lao (Dr. Slaa). Huu ndio msukumo wa Kikwete kuongeza mishahara na kuwabembeleza wafanyakazi kuwa hana ugomvi nao. Kwa nini hii ina qualify kuwa Rushwa? Angalia vizuri hapa: Raisi na Serikali walikuwa na muda mwingi mno kutoa kauli kuwa hawana ugomvi na wafanyakazi, lakini hawakufanya hivyo, walikuwa na uwezo wa kutoa ahadi kuwa wataongeza mishahara hata kabla kampeni hazijaanza lakini hawakufanya hivyo, sababu ni kuwa hawakuona impact, lakini kampeni zilipoanza waliona wafanyakazi wameelemea kwa mgombea yupi na hapa ndipo wakaamua kufanya DHAMBI YA KUSHAWISHI KWA KUONGEZA MISHAHARA KINYUME NE SHERIA YA UCHAGUZI. Timing ina qualify nyongeza ya mshahara kuwa Rushwa. Sidhani kama CCM wana ujanja hapa zaidi ya kumshinikiza Tendwa kufanya watakavyo.

Kwa upande mwingine hii ni nafasi ya Tendwa kuingia kwenye vitabu vya historia na kujulikana duniani kote kama ataamua kutenda haki. Kama akisimama kidete na kumuondoa Kikwete, huo ndio utakua mwisho wa CCM, sio hili tu, unaweza ukawa ndio uamuzi wa kuleta maendeleo kwa Tanzania, nani asiyependa sifa hii?. Hapa umakini wake na uadilifu wake upo kwenye mizani.

MUNGU IBARIKI TANZANIA, M BARIKI TENDWA NA KUMPA UJASIRI WA KUFANYA MAAMUZI MAGUMU, SHUSHA MALAIKA WAKO NA MITUME AKANENE YALE YAKUPENDEZAYO WEWE NA SIO YA WATAWALA.
 
Tokea ameanza kampeni kuna idadi ya ahadi kama 25 hivi kama sio 30 kujenga viwanja vya ndege, kununua meli, umeme na nyingine nyingi ataweza kweli huyu mkulu

kwa dalili zilizopo ni kuwa ataweza.....! LABDA WABUNGE NA MADIWANI WAWE WACHACHE
 
This is a joke ... na dharau kubwa sana kwa watanzania

Kuna watu wamempigia makofi na kushangilia ujio wa bajaj hizo wanajua watapigia dili kama wanavyo fanya kwenye Ambulance sasa hivi, zipo chache hizo hizo zinatumika kwenye kazi binafsi za wakubwa
 
Ninaamini msajili wa vyama amekutana na changamoto kubwa ambayo itaamua hatima ya heshima yake kwa jamii ya kitanzania hata na nje ya nchi. Kwenda kinyume na boss wake, yaani aliyemteua kushika wadhifa alio nao au kutenda haki kulingana na sheria za nchi na uadilifu. Hoja iliyoko mbele yake ni nzito, nikimaanisha siyo ya kukurupuka kutoa majibu marahisi.

Wachambuzi wa mambo ya kisiasa wameichambua hoja ya CHADEMA na hakika kama haki itafuatwa, mgombea wa CCM huenda akaenguliwa kwenye kugombea uraisi. Lakini ni hoja ipi hasa inayomuweka Raisi Kikwete kwenye hatari hii? Kuongeza mishahara kwa wafanyakazi ndio hoja yenye nguvu. Laiti kama tungaliweza kuona nafsi za watu tungefahamu ni nini hasa lilikuwa kusudio la Kikwete, kwa kuwa uwezo huo hatunao, basi hatuna budi kuchambua na kuangalia mambo kama haya yaliyowahi kutokea siku za nyuma.

Miaka kadhaa iliyopita wahudumu wa afya waligoma na serikali iliongeza mishahara, je ongezeko lile liliidhinishwa na bunge? nafikiri haikuwa hivyo, je hela hizi zilitoka wapi na mbona wanasiasa hawakucharuka kusema serikali imevunja sheria? Nahisi Msajili anaweza kutumia mfano huu kufanya maamuzi marahisi. Nahisi akifanya hivyo atakuwa amefanya kosa kubwa mno litakalomgharimu heshima yake. Kwa nini nasema hivi?

Tuende ndani kidogo, Kwanza kabisa sasa hivi issue kubwa hapa ni uchaguzi na sheria inayosimamia uchaguzi huo. Pili, Raisi alishatoa tamko hadharani kabla ya kampeni akiwa anatumia jukwaa kama Raisi kuwa Serikali haina uwezo wa kuongeza mishahara, na hakukuwa na emergency iliyokuwepo wakati wa mgomo wa madaktari (Kuwa kuna wagonjwa walikuwa wanakufa kwa wao kugoma). Kikwete hapa hana ujanja maana wafanyakazi walisharidhia kuwa hamna ongezeko la mshahara; hawakuwa wamegoma na kulikuwa hamna emergency yoyote kama watu kupoteza maisha.

Nini hasa kilichomsukuma Kikwete kuongeza mishahara? Kwa bahati mbaya ama kwa kutokufahamu kwa wasaidizi wa kikwete, hakufahamu vizuri kundi hili lina nguvu gani katika kushawishi wapiga kura. Wafanyakazi walipoamua kuweka wazi msimamo wao na kampeni zilizoleta kuchapishwa t-shirt (Sizitaki kura za wafanyakazi) ilikuwa ni dalili mbaya kwa CCM. Hata wakati wagombea wanarudisha form Wafanyakazi walionyesha wazi ni nani chaguo lao (Dr. Slaa). Huu ndio msukumo wa Kikwete kuongeza mishahara na kuwabembeleza wafanyakazi kuwa hana ugomvi nao. Kwa nini hii ina qualify kuwa Rushwa? Angalia vizuri hapa: Raisi na Serikali walikuwa na muda mwingi mno kutoa kauli kuwa hawana ugomvi na wafanyakazi, lakini hawakufanya hivyo, walikuwa na uwezo wa kutoa ahadi kuwa wataongeza mishahara hata kabla kampeni hazijaanza lakini hawakufanya hivyo, sababu ni kuwa hawakuona impact, lakini kampeni zilipoanza waliona wafanyakazi wameelemea kwa mgombea yupi na hapa ndipo wakaamua kufanya DHAMBI YA KUSHAWISHI KWA KUONGEZA MISHAHARA KINYUME NE SHERIA YA UCHAGUZI. Timing ina qualify nyongeza ya mshahara kuwa Rushwa. Sidhani kama CCM wana ujanja hapa zaidi ya kumshinikiza Tendwa kufanya watakavyo.

Kwa upande mwingine hii ni nafasi ya Tendwa kuingia kwenye vitabu vya historia na kujulikana duniani kote kama ataamua kutenda haki. Kama akisimama kidete na kumuondoa Kikwete, huo ndio utakua mwisho wa CCM, sio hili tu, unaweza ukawa ndio uamuzi wa kuleta maendeleo kwa Tanzania, nani asiyependa sifa hii?. Hapa umakini wake na uadilifu wake upo kwenye mizani.

MUNGU IBARIKI TANZANIA, M BARIKI TENDWA NA KUMPA UJASIRI WA KUFANYA MAAMUZI MAGUMU, SHUSHA MALAIKA WAKO NA MITUME AKANENE YALE YAKUPENDEZAYO WEWE NA SIO YA WATAWALA.

Bado sielewi ni kwa nini hii post imeunganishwa na hii thread ya Bajaj
Na bado nashangaa kuwa thread ya bajaj imeletwa jukwaa la siasa? Hata hivyo ngoja nisiwe mnyimi wa shukrani, Kazi nzuri mods
 
Sio vibaya kwa yeye kutoa ahadi hiyo ila tatizo ni kwamba ikiwa yeye ni kiongozi ambaye yuko madarakani anaomba aongezewe muda wa kuwa madarakani. kama alisha ona kuwa kuna tatizo hilo la upungufu wa viombo vya usafiri kwa wagonjwa hasa mama wajawazito, na akaliwekea ukimia ili kana kwamba atumie tatizo hilo kwa masilahi binafsi, si sahii.
Mh uwezo unao nguvu unayo tuna omba wezesha sasa ili WATANZANIA wazida kuwa na imani na ahadi

Mimi nakubaliana na wewe sio sawa kuyafumbia macho matatizo ambayo yame-exist kwa muda wote aliokuwa madarakani ili kuja kufanyia kampeni baadae. kama hakufanya hivyo for the period alikuwa madarakani atawezaje kufanya sasa hivi?????
 
Mgombea wa CCM JM Kikwete jana alitoa ahadi ya kutoa bajaj 400 kwa wajawazito huko Chunya ili ziwasaidie kuwawahisha hospitalini mara tu atakapoingia madarakani. Source: Radio Maria
Sungura

Huyu ndiye Rais wetu, kununua bajaji 400 unatibu CORE problems za kina mama wajawazito? au unaweka tatizo pending na linazidi kukomaa? kwenye Ilani yao ya uchaguzi hakuna plan kuaddress issue ya matibabu hasa kwa kina mama wajawazito na watoto? au ndiyo hivyo vyandarua kila kijiji? Ndugu zangu CCM imeshaisha, wanaweza kutuuza hata na sisi.
 
Mgombea wa CCM JM Kikwete jana alitoa ahadi ya kutoa bajaj 400 kwa wajawazito huko Chunya ili ziwasaidie kuwawahisha hospitalini mara tu atakapoingia madarakani. Source: Radio Maria
Sungura

Ongea kuhusu kuishiwa sera, kuongozwa na raisi kilaza, na thamani ya mpiga kura wa Tanzania.

Bajaj 400, are you kidding me? kwa mama wajawazito?
 
Jamaa mgonjwa wa akili hebu angalia hapa! Hes totally incapacitated

attachment.php
 
Are you whining because Bajaj are made in India? JK and CCM deserves respect and appreciation. They have done so much for this country and that's why we elect then during every election.
Vote CCM
Long live JK
 
Back
Top Bottom