Kikwete Aahidi Bajaj 400

wabunge wake wanataka 4 wheel drive ati barabara ni mbovu.....sasa hizo bajaj zitapita kwa mawingu..?????

sio vizuri kutoa ahadi kama hizo tena sehemu za baridi wakati dunia inapigana kupunguza population..!
za garama ya mil 200 wakati bajaj sijui kama inafika mil 3...
 
Naona mkakati wa kuzidi kupoteza vizazi unaongezeka!! Watu wanne wanakufa, dereva, mama mjamzito, mtoto, na aliye pembeni.. Halafu hiyo bajaj inaweza kuja kubutuliwa na yule mzee anaitwa Chenge a.k.a vijisenti..!
 
haya yameshasemwa sana na sio mapya.

ilikuwa bungeni mwaka jana na pia wakati wa kuwasilisha bajeti ya afya.

kutoka kumbukumbu za bunge Hansard,28 juni 2010
Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2009/10, katika mkakati wa kupunguza vifo
vinavyotokana na uzazi, Wizara ilikamilisha taratibu za ununuzi wa pikipiki maalum 400
kwa ajili ya wajawazito wanapopata rufaa. Aidha, Wizara kwa kushirikiana na wadau
ilinunua radio call 40 na magari 12 ya kubebea wagonjwa na kusambaza katika
Halmashauri za Karagwe, Kasulu, Kibondo, Kigoma, Nachingwea, Kisarawe, Liwale,
Ngara, Rufiji, Chunya, Ileje na Sumbawanga.
Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2010/11, Wizara itanunua pikipiki 400 kwa
ajili ya kubebea wagonjwa ili kutekeleza Mpango wa Afya ya Mama na Mtoto. Aidha,
Wizara kwa kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za
Mitaa, itanunua mtambo wa kujenga Zahanati kwa gharama nafuu​
(Ultimate Building
Machine – UBM).
Mheshimiwa Spika, tunakili kwamba tumelizungumza hapa na pesa zilitolewa
lakini hiki ni kitu kigeni, kumekuwa na utaratibu wa mlolongo kidogo, kwa sababu ilibidi
tuwapeleke vijana wetu kwenda kuangalia na kujadiliana nao hao wanaotengeneza ili
tupate chombo ambacho kinaweza kikahimili barabara zetu. Lakini ninachoweza kusema
ni kwamba kwa sasa taratibu hizi zimekamilika na hivi karibu tutaona tuna
launch na
kuzipeleka hizo
ambulance 400. (Makofi)

Kazi kweli kweli
 
Hii ni KICHEFUCHEFU Bajaj 400 kwa wamama wajawazito lol!! Tusimlaumu sana IQ yake ndipo ilipofikia :mad2::mad2:
 
Kama angekuwa serious angejenga zahanati na kupeleka wahudumu na vufaa huko vijijini ili kuwasaidia mama wajawazito.

Unakwenda kwenye zahanati mama anaejifungua anaambiwa lete vifaa kama gloves, pamba nk
 
Ahadi sasa zimefikia 63 sijui baada ya kumalizika kampeni zitafikia ngapi..............yaani ni ahadi za tamaa tu bila kujali kuwa baadaye atawaambia wananchi kuwa '''kutokana na ufinyu wa baajeti serikali itashughulikia baada ya miaka mitano''''''
mpeni tu mikura yenu kwa kubadilishana na pilau wana chunya..
 
kwanini asipunguze garama za kukukalabati ikulu kila mwaka kwa bil 26 akatumia angalau bil 10 kama alivyofanya Mkapa kipi chote cha utawala bil 16 zingeweza kununua ambulance ngapi...

Dah bili 26 kukarabati Ikulu si mchezo yaani kupaka paka rangi na kukata nyasi zinatumika pesa nyingi kiasi hicho?
 
Kama angekuwa serious angejenga zahanati na kupeleka wahudumu na vufaa huko vijijini ili kuwasaidia mama wajawazito.

Unakwenda kwenye zahanati mama anaejifungua anaambiwa lete vifaa kama gloves, pamba nk

Huyu jamaa akili zake za ajabu sana. Hivi mkewe angekuwa na mimba angempandisha bajaj kwenye barabara mbovu? Hivi kwanza anajua mimba inakaa wapi? Nahisi anadhani mimba zinakaa kwenye makapu kama nyanya
 
Mh Chenge anafurahi zaidi kusikia ahadi kama hizi maana anajua mkulu anamkumbuka!
 
Frankly speaking the time for CCM to go out of the office is now overdue … even though this depends on us as Tanzanians, our critical thinking and decision making ability on who to vote in. It is only yesterday I had an opportunity to discussion with one fellow citizen who seemed to know the way of thinking of many people in his area. He explained that the situation is getting more complicated in his area due to factors z, j, d and s. I think these factors may be true for the other regions in the Country. The factors include
z. Uzoefu:
Sisi tulishazoea CCM… habari ya CUF, CHADEMA, TLP etc bado ni ngeni kwetu, hao hatuwajuwi vizuri, hivyo tunasita kuwapigia kura zetu watu tusiokuwa na uzoefu nao.
j. Ujinga:
Tukichagua upinzani iaweza kutokea vita ya makabila!!!. CCM ni chama kilicholeta amani na kinadumisha amani.. hivyo ukichagua CCM ni kama unachaga amani badala ya vita!
d. Udini:
Kikwete ni wa dini yetu lazima tumuunge mkono dhidi ya Slaa ambaye ni Padre na atatetea maslahi ya Wakatholik zaidi … pathetic!
s. Umasikini:
Tunashukuru kwa kupewa zawadi ndogondogo kama kilo 2 za mchele au unga, kofia na fulana yenye sura ya mgombea mwenye sura nzuri…
This is a serious problem and is escalating with time (t). Na nimekuwa nikijaribu kufanya mahesabu kuona combination ya mambo haya yatakuja kuzaa nni na lini.
zt+ jt+ dt+st =???

· Because of factor z many people are in dilemma on who to vote for…mazoea ni kama sheria
· J thoughts demonstrate how shallow minded most of our fellow citizens are ready to compromise even the positive changes for their betterment. Katika hili hata baadhi ya wasomi wanaonesha dalili za factor j, hii inafanya wa-Tz tuwe a unique people... tuko tofauti hata na jirani zetu…. Uchumi wao unazidi kukua (Rwanda, Uganda & Kenya) wanaweza kufanya maamuzi magumu (radical changes) eg Kenya etc
· d reasoning is really pathetic!.. kwahiyo itabidi tuwe tunachagua dini moja tu kila mara kwa kuogopa wakatholic? Kwahiyo wakatholic hawana haki ya kuchaguliwa? Kila raia anayo haki yakikatiba kuchagua na kuchaguliwa bila kubaguliwa kwa misingi yoyote isipokuwa umri na afya ya ubongo wake. Nadhani tungejikita katika kuchagua m-Tanzania mwenye uwezo wa kuongoza na mzalendo kwa nchi yake zaid kuliko kuangalia dini ya mtu, dini ni factor ambayo ni too complicated ku-handle na imeleta shida katika nchi nyingi. Yeyote mwenye akili nzuri angejaribu kuepuka mawazo ya dini katika uongozi wa nchi.
· s factor ni tatizo linalotokana na sera, uongozi. Tunazo resources za kutosha kuboresha maisha ya watu wetu kuliko Kenya, Uingereza, Rwanda, Norway nk. Ubinafsi na ufisadi ndio unasababisha hali hii. Tukikataa sera mbovu na viongozi wabovu tunaweza kutatua tatizo.
Kwa mtizamo wangu sera za Dr Slaa ni dawa sahihi ya nchi yetu kwasasa. Sera za Kikwete zitaangamiza nchi katika miaka t = mitano ijayo. Naogopa sana…
 
kweli baada ya kusema proper ambulance unaongelea bajaji
bajaji haiwezi kuwa ambulance hata siku moja
eti mama mjamzito unampandisha bajaji
hii ukiweka na sitaki kura za wafanyakazi na mimba za wattoto wa shule unajiuliza rais wetu ni mtu wa aina gani
 
kweli baada ya kusema proper ambulance unaongelea bajaji
bajaji haiwezi kuwa ambulance hata siku moja
eti mama mjamzito unampandisha bajaji
hii ukiweka na sitaki kura za wafanyakazi na mimba za wattoto wa shule unajiuliza rais wetu ni mtu wa aina gani
its-real-bajaj1.jpg


Mjamzito unamweka humo kabla hajafika hospitali atakuwa tayari kapata uchungu na kumaliza kabisa
 
Unashangaa nini? hujui kwamba yapo maeneo ya vijijini wajawazito wanasafirishwa kwa baiskeli.Huoni kwamba bajaji zinaweza zikawasaidia zaidi wajawazito hao kushinda baiskeli wanazotumia? bajaji ni usafiri mzuri na unakubalika kulingana na maeneo husika .

Mi nafikiri Wataalamu wetu wameamua kupumzika kufikiria au wamepuuzwa sasa wamekaa pembeni na kusubir kusema '' I told you so''. Hivi ni akili au matope (ashakum) kufikiria kunua bajaj 400 kama suluhisho la kupunguza vifo vya kinamama/au na watoto wachanga wakati wa kujifungua? Hebu tuanzie hapa;bajaj 400 @2million tshs (min)= 800 mill. wataalamu wake wanasemaje kama angeamua kujenga maternity waiting home katika strategic areas jirani na vituo vikubwa vya afya (health centers na Hospitali vyenye capacity ya kufanya upasuaji wa dharura ambapo mama wajawazito wangekuwa wanatembea/wanaletwa na baiskeli (au any means ambayo ndio wanatumia sasa) muda kabla hawajawa due kujifungua, wakiwa pale watasubiri na tena hii ita create nafasi nyingine kwa wataalamu wa afya kuwapa elimu ya malezi bora ya watoto, unyonyeshaji ,uzazi wa mpango pamoja na upimaji wa UKIMWI wa hiari kwa kipindi watakachokuwa wanasubiri...unauweza kuniuliza wakati wa kusubiri wamama hawa watakula nini? Kumbuka bajaji zitaenda sambamba na kuajiriwa madereva 400 (piga heasu ya mshahara wao) pia zitahitaji kutumia mafuta na maintainance so ile pesa ambayo ingeenda kununua mafuta+mishahara ya bajaji inaweza kuwa sehemu ya fedha ya kuwatunza akina mama hawa,vyanzo vingine vitatafutwa including mapato yatokanayo na Community health fund (CHF) n.k Ni siri iliyowazi kuwa maeneo ambayo kuna maternity waiting homes matokea yanajionyesha wazi.....Kwa Bajaji I say no no no! Chukulia mkoa wa K,njaro wilaya za Mwanga, Same, Moshi Vijijini (vijiji vya Uru,Kilema, Kibosho, Marangu nk), Kuna mlima wa kupanda Bajaji?! Nenda Ngorongoro (vijiji vya Malambo, Soitsambu, Arash Piyaya nk)...si wajawazito wataliwa na Simba ?! List ni ndefu ya maeneo ambayo ni magumu kwa usafiri wa Bajaji.....
 
Kweli JK mgonjwa, hvi kwa akili zako timamu waweza kuagiza bajaji zitumike kama ambulance vijijini kwenye rough road kweliiiiiiiiii? Daaaaaaaa hata kama ni kudanganya wananchi huku kiboko kabisa, huku dar bajaji zenyewe twapandia hio shida na full kutuangusha.Jamani kweli nimechoshwa na ahadi hewa za JK hata aibu hama huyu sick man aghaaaaaaaa.HATUDANGANYIKIIIIIIIIIIIIIIIII 2010.
 
its-real-bajaj1.jpg


Mjamzito unamweka humo kabla hajafika hospitali atakuwa tayari kapata uchungu na kumaliza kabisa

Badala ya kwenda mbele tunarudi nyuma kwa mbwembwe bila hata chembe ya aibu usoni mwetu, miaka ya 1980 kila Health Centre, narudia neno hilo...kila Health Centre ilikuwa na Landrover moja na Medical Assistant mmoja ambaye alikuwa na uwezo wa ku screen wagonjwa wanaohitaji upasuaji au huduma nyeti na kumpeleka Hospitali ya wilaya kwa haraka kwa kutumia gari hiyo ya serikali aina ya Landrover
Leo
Leo ni miaka thelathini (30) toka enzi hizo hayo magari hayapo na hata baiskeli tulizopewa na wafadhili za MCH ambazo wakunga walizitumia kutembelea kinamama wajawazito na kwendea kutoa sindano za kinga zimekufa na serikali yetu haijaweza kuzirudisha, mbadala tuongelee kuwa Health Centres ziboreshwe ziwe na Theatre na kuongeza madaktari na vifaa vya upasuaji katika kila Health Center hapo nafikiri tungekuwa tumesaidia kupunguza tatizo kwa kuwafuata na kuwa karibu na hao wajawazito wetu vijijini na sio eti uwaweke kwenye Bajaj, hiyo Bajaj Mkunga atakaa wapi? vifaa vya mkunga navyo vitakaa wapi? Daktari atakaa sehemu ipi? ndugu watakaoenda kumuongezea damu huyo mgonjwa wao endapo atapasuliwa watakaa wapi? Hivi kweli hawa ndugu zetu wanataka kutuaminisha kuwa serikali haina uwezo wa kununua magari cheap badala ya kufanya mchezo na maisha ya kinamama wakitanzania? naamini kabisa kuwa kuna siku ya siku pazia walilonalo machoni watanzania litafunguka na mtajibu tu, huwezi kufuja mali za watanzania kwa ushahidi ulio wazi halafu ukapona hapo mbeleni, haya endeleeni mkizani mmevaa nguo kumbe mpo uchi
 
Back
Top Bottom