Kikwete Aahidi Bajaj 400

Mi nilikuwa mfuatiliaji mzuri wa hotuba za kikwete 2005, sikuwahi kusikia hata siku moja anasema/anaongea point ya maana zaidi ya kuwahadaa wananchi. Kusema kweli JK alikuwa anapendwaa sana enzi hizo, lakini baada ya miaka 5, ndo watu wameona JK mwenyewe. Lakini bado watu wanaimani. Ila JK huwa haonyeshi seiousness ya kufanya kitu.
 
Tokea ameanza kampeni kuna idadi ya ahadi kama 25 hivi kama sio 30 kujenga viwanja vya ndege, kununua meli, umeme na nyingine nyingi ataweza kweli huyu mkulu
Hii ndo term yake ya mwisho kwa hiyo ataahidi lolote ili aingie Ikulu, anajua hatutaweza kumkaba kwenye uchaguzi ujao.
 
Mgombea wa CCM JM Kikwete jana alitoa ahadi ya kutoa bajaj 400 kwa wajawazito huko Chunya ili ziwasaidie kuwawahisha hospitalini mara tu atakapoingia madarakani. Source: Radio Maria
Sungura
Hivi bajaj ni bei gani..Kwanza naona kawazalilisha kwanini asiwanunulie hao mawizi wake wakatembelea badala yake anataka mama zetu ndiyo watumie wakati wa kwenda kujifungua...au kwanini asipunguze garama za kukukalabati ikulu kila mwaka kwa bil 26 akatumia angalau bil 10 kama alivyofanya Mkapa kipi chote cha utawala bil 16 zingeweza kununua ambulance ngapi...aache kuwafanya watanzania wajinga...usikute walimpigia makofi, si wange mpiga mawe hata....
 
Unashangaa nini? hujui kwamba yapo maeneo ya vijijini wajawazito wanasafirishwa kwa baiskeli.Huoni kwamba bajaji zinaweza zikawasaidia zaidi wajawazito hao kushinda baiskeli wanazotumia? bajaji ni usafiri mzuri na unakubalika kulingana na maeneo husika .

Niynyi watu mnachekesha sana!! Yaani BAJAJ kwa wajawazito, kweli....?

Hivi hii nchi inakwenda wapi? Priority zao ni nini? Kweli hawa jamaa wantumia ujinga wetu kutuhadaaa!
 
Kama wananchi wanateseka na kupanda baiskeli kupelekwa hospitali nadhani bajaj ni better than hiyo baiskeli...wengine wanapandishwa kwenye mikokoteni ya kukokotwa na punda...au hatujasikia hizo? ?? zipo ndugu zangu na nafikiri ni simple logic kuwa ukiwa na bajaj ikamuwahi huyo mjamzito na kumkimbiza hospitali itamsaidia mara milioni kuliko baiskeli au huo mkokoteni..au la basi tuache wafie njiani??

Nadhani bajaj ni step nzuri kuelekea kuwa na magari coz hayo magari yaliyopo utaambiwa hayana mafuta au visingizio kibao ila bajaj ukiweka wese kidogo unazunguka hadi unasahau...nadhani hiyo ahadi ina-apply kwa maeneo yenye matatizo sugu ya usafiri so to me hiyo ahadi nadhani itawapa nafuu wanajamii husika kama akichaguliwa na kuitekeleza.
 
Mgombea wa CCM JM Kikwete jana alitoa ahadi ya kutoa bajaj 400 kwa wajawazito huko Chunya ili ziwasaidie kuwawahisha hospitalini mara tu atakapoingia madarakani. Source: Radio Maria
Sungura

Hapa bado nachanganyikiwa kwani kwa barabara za vijijini kwetu we ulete Bajaji hizo ajali atapona mtu kweli? Kubwa zaidi ingawa me si mkunga ila nadhani kama mama ana uchungu au mimba tu, atahitaji kusafirishwa akiwa amelala chali sasa Bajaji itakuwaje au zipo zenye official vitanda? Tusidanganyike!
 
Huko vijijini wajawazito husafirishwa kwenye baiskeli na mikokoteni inayovutwa na wanyama, nyie mnashangaa bajaji?

Mnaojadili hapa JF mnatoka Tanzania ya wapi?

Labda tu bajaji zisiishie kwa wajawazito tu bali hata vigogo wa serikali huko wilayani na mikoani watumie bajaji maana shangingi moja linaweza kununua bajaji zaidi ya 50.
 
Kama wananchi wanateseka na kupanda baiskeli kupelekwa hospitali nadhani bajaj ni better than hiyo baiskeli...wengine wanapandishwa kwenye mikokoteni ya kukokotwa na punda...au hatujasikia hizo? ?? zipo ndugu zangu na nafikiri ni simple logic kuwa ukiwa na bajaj ikamuwahi huyo mjamzito na kumkimbiza hospitali itamsaidia mara milioni kuliko baiskeli au huo mkokoteni..au la basi tuache wafie njiani??

Nadhani bajaj ni step nzuri kuelekea kuwa na magari coz hayo magari yaliyopo utaambiwa hayana mafuta au visingizio kibao ila bajaj ukiweka wese kidogo unazunguka hadi unasahau...nadhani hiyo ahadi ina-apply kwa maeneo yenye matatizo sugu ya usafiri so to me hiyo ahadi nadhani itawapa nafuu wanajamii husika kama akichaguliwa na kuitekeleza.

Kwa pesa iliyoibiwa Kagoda, EPA, Meremeta, Richmond, ndege ya rais, RADA, kuongelea Bajaj ni dharau kubwa kwa wananchi wa Tanzania. Uwezekano wa kununua landcruiser mkonge kwa akina mama hao upo mkubwa sana.

Mkuu hii nchi kama tutapata uongozi makini ambao unatumia raslimali kwa kuwajali wananchi wake leo tusingezungumzia bajaj. Hii ni dhihaka kwa kweli.

Ila nnalolijua ni kuwa watatuhadaa sana ila mwisho upo. History will back me up!
 
Mgombea Urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi(CCM),Jakaya Kikwete ameahidi kutoa pikipiki za miguu mitatu(Bajaj) 400 za wagonjwa(ambulance) kwa nchi nzima na gari moja la Wagonjwa kwaajili ya kituo cha afya cha Mkwajuni ili kuwasafirisha wajawazito katika Wilaya ya Chunya.

Akizungumza na Wakazi wa Mkwajuni Wilayani hapa wakati wa mkutano wake wa kampeni,Kikwete alisema ahadi hiyo ataitekeleza pindi atakapochaguliwa kurejea kwenye kiti alichonacho hivi sasa.

Chanzo:Tanzania Daima.

Mwandishi: Irene Mark.Mbeya.

My take.

Bajaj na wajawazito hii kali hata kipindi cha zama za mawe hii isingekubalika.Bado sijamuelewa ana maanisha nini!!1 kazi ipo.

Regia,

Mwogope mungu, kule Kilombero mashambani akina mama mbona wanabebwa kwenye baiskeli na pikipiki kwenda hospitali?
 
haya yameshasemwa sana na sio mapya.

ilikuwa bungeni mwaka jana na pia wakati wa kuwasilisha bajeti ya afya.

kutoka kumbukumbu za bunge Hansard,28 juni 2010

Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2009/10, katika mkakati wa kupunguza vifo vinavyotokana na uzazi, Wizara ilikamilisha taratibu za ununuzi wa pikipiki maalum 400 kwa ajili ya wajawazito wanapopata rufaa. Aidha, Wizara kwa kushirikiana na wadau ilinunua radio call 40 na magari 12 ya kubebea wagonjwa na kusambaza katika Halmashauri za Karagwe, Kasulu, Kibondo, Kigoma, Nachingwea, Kisarawe, Liwale, Ngara, Rufiji, Chunya, Ileje na Sumbawanga.

Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2010/11, Wizara itanunua pikipiki 400 kwa ajili ya kubebea wagonjwa ili kutekeleza Mpango wa Afya ya Mama na Mtoto. Aidha, Wizara kwa kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, itanunua mtambo wa kujenga Zahanati kwa gharama nafuu (Ultimate Building Machine – UBM).

Mheshimiwa Spika, tunakili kwamba tumelizungumza hapa na pesa zilitolewa lakini hiki ni kitu kigeni, kumekuwa na utaratibu wa mlolongo kidogo, kwa sababu ilibidi tuwapeleke vijana wetu kwenda kuangalia na kujadiliana nao hao wanaotengeneza ili tupate chombo ambacho kinaweza kikahimili barabara zetu. Lakini ninachoweza kusema ni kwamba kwa sasa taratibu hizi zimekamilika na hivi karibu tutaona tuna launch na kuzipeleka hizo ambulance 400. (Makofi)

Kama wananchi wanateseka na kupanda baiskeli kupelekwa hospitali nadhani bajaj ni better than hiyo baiskeli...wengine wanapandishwa kwenye mikokoteni ya kukokotwa na punda...au hatujasikia hizo? ?? zipo ndugu zangu na nafikiri ni simple logic kuwa ukiwa na bajaj ikamuwahi huyo mjamzito na kumkimbiza hospitali itamsaidia mara milioni kuliko baiskeli au huo mkokoteni..au la basi tuache wafie njiani??

Nadhani bajaj ni step nzuri kuelekea kuwa na magari coz hayo magari yaliyopo utaambiwa hayana mafuta au visingizio kibao ila bajaj ukiweka wese kidogo unazunguka hadi unasahau...nadhani hiyo ahadi ina-apply kwa maeneo yenye matatizo sugu ya usafiri so to me hiyo ahadi nadhani itawapa nafuu wanajamii husika kama akichaguliwa na kuitekeleza.

I and you and all Tanzanian (especially those with minds like yours) should think positively. Kuahidi bajaj ni upuuzi uliotukuka kama sio ushamba wa hali ya juu.

Fikiria barabara zetu za kijijini: Hiyo bajaji itapita wapi?

Mimi nafikiri angesema na hii ingelenga zaidi kenye kujenga Zahanati za kila kata kama sio kijiji! Shule za kata at least wanajaribu. Kwa nini isiwe kwa zahanati. Kwa nini asiseme kuwa atahamasisha wananchi wajijengee zahanati na serikali ichangie gharama za madaktari kama sio watabibu na madawa! Kwa nini asiseme kuwa kuanzia serikali ya awamu ijayo hakutakuwa na kuagiza mashangingi kwa viongozi wa kiserikali badala yake tutahakikisha kila Kata inapata hata ambulance used ambayo hafikii gharama ya USD 15000! Kwa nini asiwaahidi wananchi kuwa anahakikisha vijana wanaomaliza shule wanafundishwa mbinu mmbadala za kukabiliana na maisha yao baada ya kuwazuia kuchanagamana na wenzao wa mikoani na hata majirani zao? Hii ni kejeli ya hali ya juu kwa wananchi wa nchi hii! BAJAJI KWA AKINA MAMA WAJAWAZITO!

Sitaki kuamini na wala sitoamini ahadi kama hii! Tatizo letu ni kushabikia na kukenua tuambiwapo uongo! Ukisema ukweli daima utaonekana msaliti! Kwa nini tusifike mahali tuwaambie wananchi wetu ukweli! Wakati umefika sasa kwa kila aliye Mtanzania mwenye uchungu na nchi hii, mwenye uchungu na wananchi wa nchi hii apigane vita ya udanganyifu! Tuwe na uwezo wa kusema HAPANA siyo HIVI ni VILE. Kweli watu zaidi ya milioni 42 tunakubali kudanganywa!

Mimi naamini wakati umefika sasa wa KUWAKOMBOA WATANZANIA WALIO KATIKA MAKUCHA YA WACHACHE. We need to educate our people! And that begins with you!
 
wabunge wake wanataka 4 wheel drive ati barabara ni mbovu.....sasa hizo bajaj zitapita kwa mawingu..?????

sio vizuri kutoa ahadi kama hizo tena sehemu za baridi wakati dunia inapigana kupunguza population..!
 
Mgombea wa CCM JM Kikwete jana alitoa ahadi ya kutoa bajaj 400 kwa wajawazito huko Chunya ili ziwasaidie kuwawahisha hospitalini mara tu atakapoingia madarakani. Source: Radio Maria
Sungura

Hakuna lolote...............KUMBUKENI KUWA HAKAWII KUKANA KILA ANACHOAHIDI................ ahadi ZA MIAKA MITANO ILIYOPITA ALISHAZIKANA KADHAAAAA............................. ALIKANA KURA ZA WAFANYAKAZI LAKINI SASA ANASEMA HAKUKANA....................... HUYO NI MBAYUWAI HAKAWII KUGEUKA GHAFRA...........
 
Kumbe JK ni muuaji ! yaani mjamzito + Bajaj + barabara ya mashimo = kifo cha kiumbe wa tumboni.
 
Kama wananchi wanateseka na kupanda baiskeli kupelekwa hospitali nadhani bajaj ni better than hiyo baiskeli...wengine wanapandishwa kwenye mikokoteni ya kukokotwa na punda...au hatujasikia hizo? ?? zipo ndugu zangu na nafikiri ni simple logic kuwa ukiwa na bajaj ikamuwahi huyo mjamzito na kumkimbiza hospitali itamsaidia mara milioni kuliko baiskeli au huo mkokoteni..au la basi tuache wafie njiani??

Nadhani bajaj ni step nzuri kuelekea kuwa na magari coz hayo magari yaliyopo utaambiwa hayana mafuta au visingizio kibao ila bajaj ukiweka wese kidogo unazunguka hadi unasahau...nadhani hiyo ahadi ina-apply kwa maeneo yenye matatizo sugu ya usafiri so to me hiyo ahadi nadhani itawapa nafuu wanajamii husika kama akichaguliwa na kuitekeleza.

We ndugu.... KUMBUKA BAISKELI HAITUMII MAFUTA.... HUKO ANAKOSEMA ATAPELEKA BAJAJ HATA MAFUTA YA MSHINE YA KUSAGA NI SHIDA..... WATU WANATUMIA MCHI NA KINU... GEREJI YA HIYO BAJAJ..... SPEA, NA MBAYA ZAIDI VIBAJAJ HAVIKAWII KUBIDUKA...............VITAPITA BARABARA GANI...........???

VILE VINAHITAJI LAMI ILI VITEMBEE KWA USALAMA ......... jaaamaaaniiii eeeeee.........hii kweli invesare proposhenoooo................. YAANI MAWAZILI WANTEMBELEA VX KWENYE LAMI HALAFU WAJAWAZITO WAKATEMBELE BAJAJ KWENYE YALE MAHANDAKI................ hebu jaribu kuwa ule mlia wa kwenda kijiji cha Itungi ukitokea Ilula kule Iringa............... kuna bajaj itapanda pale.........???
 
Kwa ahadi hiyo ndo mjue mna mtu hasiyeona mbele, Huyu anagombea uongozi, hatuwezi kuwa na kiongozi anayethink low kama huyu, kiongozi anfikiri bajaj wananchi wake watafikiri vitu gani vikubwa kama si kufikiri kibajaj-bajaj!

what you believe is what you become, You think big you become big, you think low ...............
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom