Kikwete aagiza Nyumba za Serikali zilizouzwa zirejeshwe

nataka niwakumbushe watanzania wenzangu kuwa JK ni mwingi wa kuropokwa.....

sasa kwa hili sijui ameshalifanyia utafiti wa kiasi gani, na akaona linawezekana kiasi gani......ila kwa nyendo zake za nyuma si hasha kuwa kakurupuka tu.

naona kwa hili halitofanyika, na hata likifanyika ni kwa nyumba mbili au tatu tu.....lakini natusubiri tuone
 
Rais Jakaya Kikwete ameanza mchakato wa kuhakikisha nyumba za serikali zilizouzwa kwa watumishi wake wakati wa uongozi wa Awamu ya Tatu, zirejeshwa serikalini

Tuliwakataza kuwa wasiuze, sasa michakato ya nini tena?
 
Mie hongera zangu nitazitoa pale nitakaposikia Muungwana ametoa kauli kuhusu urejeshwaji wa nyumba hizo kwa Watanzania wote.
 
Bubu, hiyo hongera yako kaa nayo tu. Last week jamaa yangu mmoja Oysterbay kapata title deed yake baada ya kumaliza kulipia nyumba aliyonunua serkalini, na ndipo nikafahamu kuwa kwa takribani miaka 3 amekuwa akilipwa pia na serikali house allowance kwa kuwa anaishi kwenye 'nyumba yake'. Cheo chake alitakiwa apewe nyumba ya serikali, na aliyokuwa nayo ndiyo hiyo kainunua!

Just imagine, analipwa house allowance na serikali hiyo hiyo bado ilikuwa inamdai deni la nyumba!

Haya kama si mazingaombwe sijui ni nini! Maana si changa la macho tena.
 
Kama hii ni kweli; Mimi naliona hili ni zoezi lingine la kuwaibia watanzania fedha za jasho lao (kodi)....hebu angalieni kilichofanyika katika hii misheni town ya serikali

1. Serikali iliuza nyumba kwa wafanyakazi wake kihalali na kwa mujibu wa sheria.

2. Wafanyakazi walioweza wakazinunua na wengine bado wanazilipia kidogo kidogo.

3. Walionunua wakiwa wamiliki halali wamezifanyia marekebisho ya gharama hizo nyumba (mfano kule O'bay, Kinondoni, Masaki n.k)

4. Serikali ya JK inakuja na kusema HAPANA tunazitaka nyumba zetu tulizowauzia, tutawarudishia gharama zenu....!!!

5. Huu ni utapeli wa mchana maana wajanja wataongeza gharama ya hizo nyumba na serikali haina mabavu kisheria ya kuwalazimisha waziuze kwa bei ndogo. Nyumba zilizouzwa kwa Mil 10 zitanunuliwa kwa Mil 100 kila moja...mwenye nyumba anapewa Mil 50 na wafanyakazi wa Serikali wanagawana Mil 50 iliyobaki...

Watanzania tutapiga makofi JK hana mchezo amerudisha nyumba za serikali....tuhesabu tumeliwa....
 
Hawa simaanishi kama wanamaanisha hicho wanachosema eti atarudisha nyumba za serikali mbona alisema kipindi kirefu kimepita sasa hata zile za polisi walizouziana ndani ya vituo vya polisi hazijarudi bado.
 
spin! a.k.a. kiini macho. to be able to carry their functions effectively viongozi wa juu wanahitaji makazi yanayoeleweka .of course ni class issue but thats how it is.'tabaka la watawala. yes nyumba zirudishwe!
 
Kikwete: Nyumba zilizouzwa maeneo nyeti zitarudishwa
Na Jacqueline Liana(source -uhuru la leo)

RAIS Jakaya Kikwete amesema baadhi ya nyumba za serikali zilizouzwa kwa maofisa wake wakati wa uongozi wa awamu ya tatu, zitarudishwa serikalini.

Kama wameamua kuzirudisha nyumba basi zirudishwe zote bila ya kujali cheo cha huyo aliyepewa nyumba hiyo, vinginevyo itakuwa ni yale yale mabo ya usanii ya kuwaonea baadhi ya watu.

Muungwana onyesha uongozi wako katika swala hili, kama huwezi kuzichukua nyumba zote basi ni bora usiseme lolote kuhusiana na nyumba hizo.
 
Sina hakika kwamba ni kile kipindi cha wabunge kusema wajulikane majimboni au ni kweli Kimaro kaamua kuwa real na kukataa kuitwa pembeni.Mbuge huyu kaamua kupeleka hoja binafsi juu ya nyumba z Serikali kuuzwa.Sasa utata huu maana JK anayo nyumba pia .Analitaka Bunge kuunda Tume kuchunguza utata na njia za kuuzwa.Sasa sina hakika kama Hoja itapita maana iko kwanza ndani ya CCM.Kama CCM wa akili zenye akili basi wataacha iende ile ijadilike lakini wakiizima sijui itakuwa ni kwa manufaa ya nini .Copy ya hoja yenyewe nitaileta hapa ila kwa sasa naangalia upepo tokea hapa Dodoma .Es najua nyumba zile tulizipigia kelele sana sasa Kimaro aweza kuwa njia ya ufumbuzi ?
 
Bwana Luyungu nisaidie kidogo mkuu, unajua hii ishu ya ngumba sijaichimbua kiundani, sasa swala ni nyumba za serikali, nyumba za mashirika au zote mkuu???
 
Hilo Jimbo analotoka Aloyce Kimaro (ambako anajulikana kama Simba wa Yuda) ni jimbo linalosifika kwa upinzani wake dhidi ya CCM, hata wengi tulishangaa ilikuwaje CCM ikashinda huko mwaka 2005. Wengine tulidhani ni walewale wapinzani wamejipaka rangi ya kijani ili wawepo kwenye "system" kiaina. Jimbo hilo ndiko nyumbani kwa Lyatonga Mrema na James Mbatia, na mara ya mwisho lilikuwa na mbunge wa TLP Major (mstaafu) Jesse Makundi. Sasa huyu Kimaro anapomshambulia Mkapa na kupingana na CCM "wenzake" waziwazi kuhusu suala hili la nyumba za serikali (ambalo kwa hakika tulio wengi tunamuunga mkono), anajiweka pia kwenye wakati mgumu ukizingatia historia ya wenyeji wa jimbo hilo. Tunakuunga mkono Kimaro, usiogope wala usione aibu wala kutishika iwapo watakuhusisha na upinzani au kukuzulia ya kukuzulia, mapambano yana gharama zake, natumaini umejiandaa, lakini la maana zaidi ni kuungwa mkono. Songa mbele baba!
 
Sina hakika kwamba ni kile kipindi cha wabunge kusema wajulikane majimboni au ni kweli Kimaro kaamua kuwa real na kukataa kuitwa pembeni.Mbuge huyu kaamua kupeleka hoja binafsi juu ya nyumba z Serikali kuuzwa.Sasa utata huu maana JK anayo nyumba pia .Analitaka Bunge kuunda Tume kuchunguza utata na njia za kuuzwa.Sasa sina hakika kama Hoja itapita maana iko kwanza ndani ya CCM.Kama CCM wa akili zenye akili basi wataacha iende ile ijadilike lakini wakiizima sijui itakuwa ni kwa manufaa ya nini .Copy ya hoja yenyewe nitaileta hapa ila kwa sasa naangalia upepo tokea hapa Dodoma .Es najua nyumba zile tulizipigia kelele sana sasa Kimaro aweza kuwa njia ya ufumbuzi ?

Hii ni ishara kwamba vipande vya magamba vilivyomuunganisha kobe(chama cha kijani) vimeanza kuyeyuka na kubanduka kimoja kimoja na mwishowe vitatawanyika.

Kwa nini kusafiri kwenye boti iliyotoboka?hatima yake ni kuzama.Kolimba alipooona mapema sana kuwa DIRA imeanza potea aliwekwa kiti moto dodoma na mwishowe mshipa wa moyo ukapasuka.Mwisho wa yote kuwa dhahiri umewadia.Bravo, KIMARO(MB)
 
Anaonyesha moyo wa kimapinduzi hasa kuongelea swala la mkapa bungeni, hii ni hatari kwake lakini ni afya kwa watanzania na heshima tunasitahili kumpa nyingi sana.
 
Sina hakika kwamba ni kile kipindi cha wabunge kusema wajulikane majimboni au ni kweli Kimaro kaamua kuwa real na kukataa kuitwa pembeni.Mbuge huyu kaamua kupeleka hoja binafsi juu ya nyumba z Serikali kuuzwa.Sasa utata huu maana JK anayo nyumba pia .Analitaka Bunge kuunda Tume kuchunguza utata na njia za kuuzwa.Sasa sina hakika kama Hoja itapita maana iko kwanza ndani ya CCM.Kama CCM wa akili zenye akili basi wataacha iende ile ijadilike lakini wakiizima sijui itakuwa ni kwa manufaa ya nini .Copy ya hoja yenyewe nitaileta hapa ila kwa sasa naangalia upepo tokea hapa Dodoma .Es najua nyumba zile tulizipigia kelele sana sasa Kimaro aweza kuwa njia ya ufumbuzi ?

Mpaka kieleweke. Hali ikiendelea hivi kuna uwezekano kabisa baadhi ya wabunge ndani ya CCM watakataa kufuata mstari wa mafisadi ndani ya CCM na kutawaka moto ambao haitakuwa rahisi kuuzima
 
Sina hakika kwamba ni kile kipindi cha wabunge kusema wajulikane majimboni au ni kweli Kimaro kaamua kuwa real na kukataa kuitwa pembeni.Mbuge huyu kaamua kupeleka hoja binafsi juu ya nyumba z Serikali kuuzwa.Sasa utata huu maana JK anayo nyumba pia .Analitaka Bunge kuunda Tume kuchunguza utata na njia za kuuzwa.Sasa sina hakika kama Hoja itapita maana iko kwanza ndani ya CCM.Kama CCM wa akili zenye akili basi wataacha iende ile ijadilike lakini wakiizima sijui itakuwa ni kwa manufaa ya nini .Copy ya hoja yenyewe nitaileta hapa ila kwa sasa naangalia upepo tokea hapa Dodoma .Es najua nyumba zile tulizipigia kelele sana sasa Kimaro aweza kuwa njia ya ufumbuzi ?

But how clean Kimaro is??? Atumbie na yeye ile Nakara hotel pamoja na mali zake alizipata je ili tuamini kweli ana nia ya dhati ya kufichua ufisadi katika jamii. Tunakumbuka pia alivyo kuwa mstari wa mbele wakati wa uchaguzi kugawa kanga kwa kina mama na t-shirts kwa wazee wetu kule Vunjo ili apewe kura za kuingia mjengoni.

Siamini kama kweli ana nia ya dhati ya kupambana na ufisadi. Kina Lyatonga na Mh Mbatia wanazotaarifa nzuri sana za jinsi huyu jamaa alivyo wanyanganya Jimbo.

Tuwe makini na hoja za hawa watu wa mjengoni. Sio wote wanastahili kuaminiwa.
 
Hilo Jimbo analotoka Aloyce Kimaro (ambako anajulikana kama Simba wa Yuda) ni jimbo linalosifika kwa upinzani wake dhidi ya CCM, hata wengi tulishangaa ilikuwaje CCM ikashinda huko mwaka 2005. Wengine tulidhani ni walewale wapinzani wamejipaka rangi ya kijani ili wawepo kwenye "system" kiaina. Jimbo hilo ndiko nyumbani kwa Lyatonga Mrema na James Mbatia, na mara ya mwisho lilikuwa na mbunge wa TLP Major (mstaafu) Jesse Makundi. Sasa huyu Kimaro anapomshambulia Mkapa na kupingana na CCM "wenzake" waziwazi kuhusu suala hili la nyumba za serikali (ambalo kwa hakika tulio wengi tunamuunga mkono), anajiweka pia kwenye wakati mgumu ukizingatia historia ya wenyeji wa jimbo hilo. Tunakuunga mkono Kimaro, usiogope wala usione aibu wala kutishika iwapo watakuhusisha na upinzani au kukuzulia ya kukuzulia, mapambano yana gharama zake, natumaini umejiandaa, lakini la maana zaidi ni kuungwa mkono. Songa mbele baba!

Kuna wakati watu wenye chuki za kikabila hapa kina Kubwajinga wanatoa chuki zao za wazi dhidi ya watu wa Kilimanjaro ila ukweli ni kuwa ukisoma hii post ya Mwl Kithuku lazima uwape big up hawa wabunge wa hili jimbo la Kimaro.

Good job Kimaro!
 
But how clean Kimaro is??? Atumbie na yeye ile Nakara hotel pamoja na mali zake alizipata je ili tuamini kweli ana nia ya dhati ya kufichua ufisadi katika jamii. Tunakumbuka pia alivyo kuwa mstari wa mbele wakati wa uchaguzi kugawa kanga kwa kina mama na t-shirts kwa wazee wetu kule Vunjo ili apewe kura za kuingia mjengoni.

Siamini kama kweli ana nia ya dhati ya kupambana na ufisadi. Kina Lyatonga na Mh Mbatia wanazotaarifa nzuri sana za jinsi huyu jamaa alivyo wanyanganya Jimbo.

Tuwe makini na hoja za hawa watu wa mjengoni. Sio wote wanastahili kuaminiwa.

The same ol' propaganda za Kingunge.....
 
The race has been started towards achievements,why are you looking back again?Count him worth to the courage to matters he dared to present.
Encourage this man to go.

However,we cant change the past but we can make the future better.Let this matter to become mature then you will jugde the integrity of this member of parliament(A.kimaro)
 
Back
Top Bottom