Kikwete aagiza Nyumba za Serikali zilizouzwa zirejeshwe

Jasusi,
Unajua IMF na World Bank wao hutoa mapendekezo yao kama strategy ya kiuchumi..
Mfano Serikali haitakiwi kumiliki mali ambazo ni biashara ikiwa ni pamoja na upangishaji wa nyumba.
Hapo mswahili kapewa tayari mbinu!...Badala ya serikali kuziweka nyumba hizi ziwe ktk kifungu fulani cha mapendekezo ya IMF (social walfare)..kinachosisitiza ujenzi wa nyumba kwa ajili ya wananchi wenye kipato kidogo. Kifungu hicho kinawekwa pembeni kwa sababu nyumba hizi ni mtaji mkubwa sana, haiwezekani kabisa kupewa wenye kipato kidogo... pia kuendelea kuwaweka viongozi wa serikali hali wanapokea mishahara mikubwa ni tatizo jingine ambalo IMF wamelizungumzia.
Pili wanaofaidika na nyumba hizi ni wale ambao hawapo tena ktk uongozi isipokuwa walikuwa watumishi wa serikali wakati wa Nyerere!. Hii zawadi kubwa sana haiwezi kwenda kiholela namna hii!
Sasa kifanyike kipi?... Nyumba ziuzwe, kila mmoja wetu achukue chake mapema!
NI kweli kabisa hapakuwa na sababu, serikali kuziuza nyumba hizo kwani mapendekezo ya IMF huwa ktk kupunguza gharama na kuhakikisha serikali haikalii utajiri.
Akili mu- kichwaa
 
Hapa ndipo alipuuliza Nyerere kwani lazima tukubali kila sharti la IMF? Akauliza pia tangu lini IMF imekuwa International Ministry of Finance? Tuache visingizio kuuza nyumba za serikali ilikuwa ni ujinga wetu, au to be more precise, ni ujinga wa viongozi wetu. Mchawi ni sisi wenyewe, hamna cha IMF wala WB.
 
Serikali yetu iliambiwa na hao wakubwa kuwa hakuna serikali duniani inayomiliki nyumba, na kama anavyosema Mkandara, viongozi wetu kuambiwa hivyo tu, ikawa ndio sababu ya kuanza kula!

You got it right, wachawi ni sisi wenyewe, serikali yetu iliambiwa hakuna misaada mpaka kuwa na vyama vingi vya siasa, look what they did? wachawi ni sisi wenyewe!
 
Sasa kama ndio hivyo,kwa nini wajenge nyumba nyingine tena? Au sio zao hizo nyumba mpya?
 
Our memories are very short lived;houses that were built by peoples hard earned money were " Nationalised" and today we blantantly sell at giveaway prices so called Goverment Houses .Please note that the value of a house/building s not determined by size alone but more so by LOCATION ie "where it stands".No wonder we call Tz - Bongo Land
 
The best we can do in BONGO is say POLE to each other - kama tu na ibiwa au kama tunakufa na njaa ;whatever.
 
Zanaki,
Umewahi kuona bei ya nyumba zile zinavyouzwa hivi leo ktk magazeti?... bei ya chini kabisa ni kitu kama US 300,000. Hizi wanazozijenga sasa hivi zipo ktk program ya ujenzi wa affordable town houses, jambo ambalo linakupa picha kwamba hawa viongozi wetu walitumia hila...
Pia ujenzi wa hizi nyumba wanajatibu sana kutumia mashirika hali wawekeshajui wakubwa wa mashirika hayo hayo ni wao viongozi na sheria ya nchi hii inawaruhusu viongozi kuendesha biashara mbali na uongozi... hapa pia Mtanganyika kisha ona mwanga safi wa kuzoa mafedha. Waziri wa Utalii lazima ana ki-tours chake, waziri wa afya ana duka la madawa ama hospital yake na kawekesha ktk wanunuzi na waagizaji madawa nchini ili mradi tu imekuwa vurugu.
Tumekwisha jamani mweee!
 
Mzee Mkandara ni kweli tumeisha kabisa, nadhani kuna mambo tuliyoyarukia kwa pupa sana hasa lile azimio la Zanzibar. Sijui suala la conflict of interest katika kati ya viongozi wetu linakuwa addressed vipi?
 
Wanabodi,
Swala si kuwa tunarukia, sasa hivi CCM haijulikani inafata sera ipi au hakina dira tena? na tatito lingine ni kuwa chukulia chama iwe kama cell sasa kilichopote ni kuwa hii cell haina nucleus ya kuiongoza, in fact the last ten years ni much better. Wakati wa ruksa chama kiliyumba mno, mara mwalimu alipojiweka kando mpaka alipoona hali ni mbaya na kuja kuingilia kwenye mambo mengi.
Wewe jiulize jinsi katibu mwenezi aliyepita ambaye sasa ni balozi China, alivyokuwa anajiganyaga kanyaga kuhusu mgombea mara oh kuna mgombea akishindwa ametaarisha vijana wa kufanya fujo, oh na mwenyekiti wake akasema na tayari kaandaa na baraza lake la mawaziri.
Sasa unajiuliza kama huyo mtu kaanda wahuni wafanye fujo kwa nini usimtaje na aondolewe maana huyu ni mhuni, lakini kimiaaaaaaa.
Labda mzee ES atusaidie hapa.
 
Sitasema hongera hadi nione kweli kama nyumba zinarudi .JK alitamka baada ya kuchaguliwa kwamba hakuwa na mpango wa kutidisha nyumba hizo maana kufanya hivyo kungali sababisha vita .Nikajiuliza hiyo vita na nani hasa .JK ana nyumba alinunua .JK uamuzi wa kununua nyumba aliushiriki.Je kwa nini serikal inunue hizo nyumba badala ya kuwaridishia ambao wamemaliza madeni yao na ambao hawajamaliza badala ya kutafunta njia ya kuwa pooza kwa kununua hizo nyumba? Sijaona nia ya JK hadi muda huu .

Nakuunga mkono mzee,
Huenda ni porojo zingine hizi, kuwafanya watu waishi kwa matumaini ya MAISHA BORA
 
Waziri wa Miundombinu, Basil Mramba hakuweza kupatikana kwa njia ya simu kwa vile anafuatana na Waziri Mkuu Edward Lowassa katika ziara Mkoani Kigoma.

Kwani jamani hii habari ni ya lini? maana kama ninavyojua ni kuwa Mramba ni waziri wa viwanda.

Any waye kama kweli anania inawezekana kabisa kuzirudisha japo itaigharimu serikali.

Wale wote ambao hawajalipa wanatakiwa wailipe serikali Kodi ya pango kwa miaka yote waliokaa kwenye hizo nyumba maana wamekaaa bure inabidi walipe kodi.
 
mpaka sasa najihakikishia kutoamini taarifa hizi mpaka tuyaone kwa macho. Ila nahakikisha kuwa hawapati kura yangu kamwe hawa jamaa
 
Story na kudhani ni kwingi sana kwa serikali hii, hakuna utekelezaji wowote. JK hawezi kutekeleza hili ni siasa tu kwani hata yeye mwenyewe anayo alinunua. Maswahiba wake ndio wanaomiliki hizo nyumba.
 
Back
Top Bottom