Kikombe cha babu

Mkuu ukianza kumwangalia PJ hapa hautafika maana huyu jamaa mpaka Dr Ndodi alikuwa anamtetea na hili tatizo limeshatokea na linaendelea kutafuna pesa za watu maana mpaka leo raia wanatia timu Loliondo, na roho za watu zinayeyuka kama mishumaa,
Serikali ije na majibu juu ya hili jambo na kama iliteleza iombe msamaha.....

we ndio unatoka nje ya mada, ishu ni ushahidi uletwe(rea btn the lines), na PJ alipromic atatuletea, ngoja tumsubirie!!
Watu wengi washasema hapa ndugu zao wamekufa lakini kwa wale waliodai ndugu zao wamepona hawajaleta ushahidic
wa mwanzo na baada ya kwenda samunge, ndo hapo sasa watu wanahoji!!
 
Kuna watu walimtumia babu wa Loliondo ku-score religious points! Yaani kuthibitisha kuwa "mungu" wao anaponya! Niliwaonya wakati ule, kuwa huyu "mungu" wa babu wa Loliondo ndio yule yule wa DECI! Sasa kiko wapi?

mungu wao
Mungu wetu, kumbe majibu unayo
 
Magazeti na vyombo vya habari havitowi report tena...na nchi hii inaendeshwa na magazeti zaidi so kama magazeti yakinyamza na ishu zote hupotea
kwani kuna mkuu yoyote wa nchi yetu ambaye kaenda tena kwa babu na mbona watu kibao wanaenda kwa babu daily nenda mwananyamala kituo cha hospitali kuna usafiri mkuu..
 
Habari za kuaminika kwa wale wanaokubaliana na vitabu vya Vitakatifu ni kwamba dalili za mwisho watu watainuka wengine wakisema mimi ndie mliekuwa mnamsubiri, wengine watathubutu kusema wao ni manabii mfano huyo babu aliedai kaoteshwa. Jamani kama wewe ni mpendwa na unakubaliana na vitabu vitakatifu nawakumbusha kuwa hali si shwari, kumbuka ulipokosea ukatubu.
 
Mimi nakumbuka kusema kuwa "lillilo la Mungu litasimama", ila mimi binafsi sijawahi kuamini kuwa babu wa samunge ametumwa na Mungu....
 
NDUGU YANGU MBONA UMECHELEWA KUJUA? SOMA HAPA.



Na Haruni Sanchawa
MCHUNGAJI Ambilikile Masapile (pichani) wa Kijiji cha Samunge, Loliondo amebadili upepo na sasa yupo ‘bize’ kujenga nyumba yake.

Chanzo chetu cha habari kijijini hapo, kilisema Babu amekuwa akijenga nyumba yake baada ya wateja kupungua.

“Wateja wa Babu wamepungua sana wengi wanaokuja wanatoka nje ya nchi. Hivi sasa siyo yule ambaye alikuwa akifanya kazi mpaka usiku. Muda mwingi anakuwa akijenga, ni mtaalamu wa ujenzi,” kilisema chanzo hicho.

Chanzo hicho kilipoulizwa kwa wastani Babu anatibu watu wangapi, kilisema si wengi sana. “Siyo vizuri kusema idadi, lakini ukiona mtu anaacha tiba na kwenda kujenga elewa kwamba wateja ni wachache sana,” kilisema.

Hata hivyo, baadhi ya wananchi wanaomzunguka Babu wanamshukuru kwa sababu kawaletea maendeleo.

“Hivi sasa tuna minara ya mitandao, barabara kutoka Arusha imetengenezwa kwa ajili ya Babu, tunamshukuru sana. Hata akibadili upepo na kuamua kuendelea na fani ya ujenzi, sisi hatumlaumu.

Sasa afanye nini na wateja hawaji kwa maelfu?” alisema mwanakijiji mmoja aliyeomba jina lake kuhifadhiwa.

Mchungaji Masapile amejipatia umaarufu mkubwa baada ya kudai kuoteshwa dawa na Mungu ambayo alisema inatibu magonjwa sugu ukiwemo Ukimwi.
[h=1][/h]
 
Nachukulia haya maisha ni kama zama na tunaweza kusema kuwa, zama hizo tayari zimepita sasa sijui ni zama zipi zitakazofuata maana mimi tayari nlishampoteza Mjomba wangu karibu miaka miwili sasa lakini kabla ya kufikwa na mauti tayari alishashiriki kunywakikombe cha babu alifuata masharti yote tena wala hakuingilia foleni ambayo si yake alikuwa mvumilivu hadi pale zamu yake ipofika akajitwalia kikombe cha babu, lakini ki ukweli si kuona unafuu alioupata baada ya kupata kikombe hicho cha babu zaidi ya kuteseka na magonjwa yaliyokuwa yakimsonga hadi pale roho yake ili
poacha mwili wake.
 
dah kweli nimeamin biashara mahesabu (ubunifu)
utumie nauli zaidi ya laki mbili rasilimali muda zaidi ya wiki moja, malazi, chakula na mahitaji mengine meeengi alafu ukatibiwe kwa gharama ya mia tano
ahhhh kweli ndondondo si chululu na bilioni moja si bilioni hata ikikosekana mia moja
 
Mim binafsi watu kibao nawajuwa waligonga kikombe lakini wap. Katika wote utasema hawana imani .aliyepona ajitokeze atushuhudie.
 
Sijui kwanini Mungu ameumba watu wengi sana wenye upeo mdogo.....mpaka kesho kuna watu wengi tu wanaamini upuuzi wa kikombe cha babu.
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom