Kikombe cha babu

Mlachake

JF-Expert Member
Oct 13, 2009
4,412
4,558
My Dear Great Thinkers,

Mwanzoni mwa mwaka huu Karibu vyombo vyote vya habari Tanzania vilijawa na Habari za Babu wa Loliondo na Kikombe Cha Tshs.500/= habari hizi zilienea sio Tanzania Tu bali hata Nchi za Jirani.

Kulizuka hali ya kutofautiana sana katika Jukwaa hili la Magreat Thinkers, Kwakua ni sehemu watu wanaangalia mambo kwa upana na kwa Jicho la tatu, Mmoja wa member aliyekuwa akimpinga huyu babu wa Loliondo kwa nguvu zake zote Bila woga ni Miss Judith, wakiwemo wengine wengi.

Wakati huo Taifa Lilikua kwenye Mjadal mkubwa kuhusu kulipa Deni la Dowans. Kutokana na Umaarufu wa habari za kikombe cha Babu, watanzania waliipotezea habari ya malipo ya deni la Dowans ambalo mpaka sasa wengi hatujui kulichoendelea, kama deni limeshalipwa au bado.

Viongozi wengi wa siasa ambao ni kioo cha Jamii ndio walikua mstari wa mbele katika safari ya Loliondo kukifuata kikombe cha babu. Hatuna haja ya kuwataja majini ila wapo wengi.

Wengine waliichukulia hii kama nafasi muhimu ya kurudisha fadhila kwa wapiga kura wao kwa kuwagharamia safari ya Loliondo wapate kikombe cha Babu.

Wananchi kutoka kila pembe ya Tanzania walifurika katika kijiji cha Samunge, Wengi wa hawa watanzania ni maskini, waliishia kukopa angalau wapate nauli ya kwenda Samunge.

Jambo la kushangaza ni jinsi hizi habari za Samunge zimepoteza Mvuto hivi sasa.

Kwa maoni yangu ningetegemea Kipindi hiki Ndio hizi habari zishike kasi kwa Ushuhuda wa waliopona haya magonjwa sugu yanayotibika kwa Kunywa kikombe yaani UKIMWI, KANSA NA KISUKARI.

Mimi Binafsi sijamshuhudia aliyepona magonjwa haya kwa Kunywa kikombe, ila nimesikia watu wanasema wana ndugu au Rafiki aliyepona.

Je? Kuna mwana Jamvi yeyote mwenye shuhuda ya Mgonjwa aliyepona haya magonjwa sugu? Ningependa uwe ushahidi wa kujionea mwenyewe sio wa kusikia kwa watu kama mimi nilivyosikia.

Hii pia itatusaidia kuujua ukweli kuhusu hii dawa ya Babu.
 
Ndugu, Loliondo kwa sasa imekosa mvuto baada ya watu wengi kufariki(na wachache kupona), nilishawahi kumwambia PakaJimmy atuletee copy za mgojwa aliyepona, cha kusikitisha mpaka leo yupo kimya(ingawa ali-promic).

Kinachonisikitisha zaidi kupitia wizara ya Afya wamedema eti dawa ya Babu itachukua zaidi ya miaka 2 kujua kama inaponyesha au la. Huu ni uhuni!! Hapa watake wastake serikali imetugharimu sana maisha ya watz. Hii ya Samunge mi naifananisha na meli ya MV BUkoba na ile ajali ya Treni Dodoma. Watu wengi wamepotea.

Kwa hapa JF ukiidharau dawa ya babu utaambiwa huna imani, ukitoa ushuhuda watu wako wa karibu wamekufa utajibiwa dawa ya babu haizuii kifo..yaani wana majibu ya hovyo sana.

Sasa msubirie PJ usikie majibu yake lakini mpaka leo kashindwa kututhibitishia kwa docs kwa majibu eti wagonjwa wenyewe
hawataki privacy zao ziandikwe, mbona tunao wengi tu wa kisukari wamedai wamepona na wanakunywa PEPSI mbele za
watu, na still zinawamaliza kama kuku mwenye 'mdondo'. Hapa watz tumeingizwa chaka.
 
Mbali na paka Jimmy ninajua wapo wengi waliwashudia wagonjwa waliokunywa kikombe.

Kama kuna mwenye ushuhuda wowote wa mgonjwa aliyepona Tunaomba aulete. Binafsi mimi siipingi wala siisupport dawa ya babu, kwasababu sina ushuhuda wa mtu aliyepona.
 
Niliuliza hilo swali ndugu yangu, majibu niliyopata, sina hamu! Pj na wenzake walinipa majibu ya ajabu sana.
 
Mimi toka wakati huo na mpaka sasa nahisi ni usanii tu,maana hakuna mtu aliyesimama kwa dhati kuthibitisha ABC za kupona kwake.
 
Mi nimshauri tu PK kama yeye utetezi wa Babu anaona sifa atubu!! Kama kashindwa kutuletea vivid evidence, he talked in public,he must confess in public. Mi huwa namshangaa sana PJ yuko front line kutetea hii dawa ilhali haina uzima wowote. Mi namfanisha huyu PJ na Washauri wa Rais(ambao mwenyewe PJ anawaponda kila leo). PJ jiulize watu wangapi wamevutiwa na matangazo yako hapa JF na wakaenda Samunge kunywa kikombe??kwanini leo hii hutaki kuleta evidence?? Nadhani utaonekana shujaa kwa hili.

Mi nilishawahi kutoa mfano hapa anko angu kaenda Samunge na badae kama mwezi hivi hali yake ilikuwa tete kweli hadi ikamlazimu aende India kutibiwa figo, nilivyoleta hapa, nikajibiwa eti dawa ya babu haitibu figo...lol!!

Nimesikia wafanyabishara nao washaanza kukimbia coz hamna manufaa tena kule!! Watu wamekufa na miili yao imetupwa hovyohovyo, Serikali ya JK imekuwa failure kwa kuwaacha watu wakiwemo viongozi kuwa vinara. Juzi viongozi wengi
wameprovoke kwamba ule ni mkenge, wameingizwa cha kike. Yule babu ni muuaji and not otherwize, no excuse!! PJ damu za marehemu zinakulilia.
 
Niliuliza hilo swali ndugu yangu, majibu niliyopata, sina hamu! Pj na wenzake walinipa majibu ya ajabu sana.

Pole sana, wengi tulivyohoji tulipewa majibu yasiyo na tija na ya ajabuajabu!!

PakaJimmy njoo utuletee ushuhuda wa Babu wa Loliondo [/QUOTE said:
Sidhani kama ataweza kutoa ushuhuda,zaidi ya porojo tu!! maneno mengi flani kapona, lakini evidence zero
 
Ishu ni dawa ya Babu wa Loliondo ishu sio Paka Jimmy mbona mnatoka nje ya mstari?

Pole sana, wengi tulivyohoji tulipewa majibu yasiyo na tija na ya ajabuajabu!!

Sidhani kama ataweza kutoa ushuhuda,zaidi ya porojo tu!! maneno mengi flani kapona, lakini evidence zero
 
My Dear Great Thinkers,

Mwanzoni mwa mwaka huu Karibu vyombo vyote vya habari Tanzania vilijawa na Habari za Babu wa Loliondo na Kikombe Cha Tshs.500/= habari hizi zilienea sio Tanzania Tu bali hata Nchi za Jirani.

Kulizuka hali ya kutofautiana sana katika Jukwaa hili la Magreat Thinkers, Kwakua ni sehemu watu wanaangalia mambo kwa upana na kwa Jicho la tatu, Mmoja wa member aliyekuwa akimpinga huyu babu wa Loliondo kwa nguvu zake zote Bila woga ni Miss Judith, wakiwemo wengine wengi.

Wakati huo Taifa Lilikua kwenye Mjadal mkubwa kuhusu kulipa Deni la Dowans. Kutokana na Umaarufu wa habari za kikombe cha Babu, watanzania waliipotezea habari ya malipo ya deni la Dowans ambalo mpaka sasa wengi hatujui kulichoendelea, kama deni limeshalipwa au bado.

Viongozi wengi wa siasa ambao ni kioo cha Jamii ndio walikua mstari wa mbele katika safari ya Loliondo kukifuata kikombe cha babu. Hatuna haja ya kuwataja majini ila wapo wengi.

Wengine waliichukulia hii kama nafasi muhimu ya kurudisha fadhila kwa wapiga kura wao kwa kuwagharamia safari ya Loliondo wapate kikombe cha Babu.

Wananchi kutoka kila pembe ya Tanzania walifurika katika kijiji cha Samunge, Wengi wa hawa watanzania ni maskini, waliishia kukopa angalau wapate nauli ya kwenda Samunge.

Jambo la kushangaza ni jinsi hizi habari za Samunge zimepoteza Mvuto hivi sasa.

Kwa maoni yangu ningetegemea Kipindi hiki Ndio hizi habari zishike kasi kwa Ushuhuda wa waliopona haya magonjwa sugu yanayotibika kwa Kunywa kikombe yaani UKIMWI, KANSA NA KISUKARI.

Mimi Binafsi sijamshuhudia aliyepona magonjwa haya kwa Kunywa kikombe, ila nimesikia watu wanasema wana ndugu au Rafiki aliyepona.

Je? Kuna mwana Jamvi yeyote mwenye shuhuda ya Mgonjwa aliyepona haya magonjwa sugu? Ningependa uwe ushahidi wa kujionea mwenyewe sio wa kusikia kwa watu kama mimi nilivyosikia.

Hii pia itatusaidia kuujua ukweli kuhusu hii dawa ya Babu.

Magazeti na vyombo vya habari havitowi report tena...
na nchi hii inaendeshwa na magazeti zaidi so kama magazeti yakinyamza na ishu zote hupotea
 
PakaJimmy njoo utuletee ushuhuda wa Babu wa Loliondo

Hawezi kuleta...alishanipromc kitambo tu hadi leo kimya,whats wrong??

Mbali na paka Jimmy ninajua wapo wengi waliwashudia wagonjwa waliokunywa kikombe.

Kama kuna mwenye ushuhuda wowote wa mgonjwa aliyepona Tunaomba aulete. Binafsi mimi siipingi wala siisupport dawa ya babu, kwasababu sina ushuhuda wa mtu aliyepona.

PJ ndio kinara mkuu, ila kama kuna mtu basi ni vema sasa,wakati ndio huu wanaJF tujionee na vyombo vya habari
vyote vipo kimyaaa, wako bize na bunge!

Mimi toka wakati huo na mpaka sasa nahisi ni usanii tu,maana hakuna mtu aliyesimama kwa dhati kuthibitisha ABC za kupona kwake.

Huu ni usanii, hamna mtu atakyesimama kulitolea ufafanuzi hili,serikali yenyewe imeshaoza, mpaka miaka 2 babu atakuwa wapi??kama sio keshajiozea!!
 
Ishu ni dawa ya Babu wa Loliondo ishu sio Paka Jimmy mbona mnatoka nje ya mstari?

we ndio unatoka nje ya mada, ishu ni ushahidi uletwe(rea btn the lines), na PJ alipromic atatuletea, ngoja tumsubirie!!
Watu wengi washasema hapa ndugu zao wamekufa lakini kwa wale waliodai ndugu zao wamepona hawajaleta ushahidic
wa mwanzo na baada ya kwenda samunge, ndo hapo sasa watu wanahoji!!
 
Kuhusu "publicity ya Babu", ulishaambiwa ndugu zetu wa Kenya wamechukuwa fursa hiyo kumtangaza huyo mzee na wanajipatia watalii wengi tu! CC tumebaki na malumbano wenzetu ni wajasiriamali kweli.
 
Mbali na paka Jimmy ninajua wapo wengi waliwashudia wagonjwa waliokunywa kikombe.

Kama kuna mwenye ushuhuda wowote wa mgonjwa aliyepona Tunaomba aulete. Binafsi mimi siipingi wala siisupport dawa ya babu, kwasababu sina ushuhuda wa mtu aliyepona.

pakajimy alikuwa mkali sana jana kwenye post yangu,
lazima tuseme ukweli kutoka moyoni
nimefiwa na dada rafiki yangu aliyekwenda kunywa kikombe baada ya hapo akaacha kutumia arv
ugonjwa umemchukua kama kimbunga!
huo ndio ukweli hatuwezi kunyamaza
 
Kuna watu walimtumia babu wa Loliondo ku-score religious points! Yaani kuthibitisha kuwa "mungu" wao anaponya! Niliwaonya wakati ule, kuwa huyu "mungu" wa babu wa Loliondo ndio yule yule wa DECI! Sasa kiko wapi?
 
Back
Top Bottom