kikombe atumiacho babu Alikiokota nyumbani kwake!!!!!!!

Ms Judith

JF-Expert Member
Dec 24, 2010
2,563
918
Neville Meena na Mussa Juma, Samunge
................

Kikombe cha babu
Dawa yote wanayokunywa wagonjwa wanaofika katika Kijiji cha Samunge lazima ipitie katika mkono wa Mchungaji Mwasapila.

Mkono wa mtumishi huyu wa Mungu huwa umeshikilia kikombe maarufu kama "kikombe cha babu", ambacho hukitumia kuchota dawa kutoka kwenye ndoo ambazo huletwa na wahudumu. Anachiokifanya ni kujaza vikombe vingine ambavyo hutumiwa na watu kunywa dawa hiyo.

Wakati wote utamwona Mchungaji Mwasapila akiwa na kikombe hiki mkononi mwake, huwa hakiachi popote anapokwenda labda kama si wakati wa kutoa dawa. Hapa ina maana kwamba hata kama akienda kupata chakula cha mchana au chai ya saa nne, babu huondoka na kikombe chake.

Wakati akieleza kuhusu kikombe hiki, Mchungaji Mwasapila alikuwa na uso wa tabasamu kwa mbali, hii inaashiria kwamba kikombe chake kina thamani kubwa katika utoaji wa dawa au tiba kwa wengine tunavyoweza kutamka.

Anasema kwa kuzingatia kazi zake za ufundi uashi, wakati fulani alilazimika kuwepo Mjini Loliondo ambako alikuwa akijenga nyumba ya watawa wa Kanisa Katoliki.

Anasema baada ya kukamilisha ujenzi huo uliochukua siku kadhaa, alirejea nyumbani kwake, Samunge ambako alikuta kikombe ndani ya nyumba yake kikiwa kikizagaa.

"Niliwauliza wale vijana niliowaacha pale nyumbani... Jamani hiki kikombe ni cha nani? lakini kila mmoja alisema hajui na wala hawakufahamu jinsi kilivyoingia ndani ya nyumba yangu."

Anasema walijaribu kuwauliza hata majirani iwapo kuna mtu ambaye kwa namna moja au nyingine alikuwa amesahau kikombe kile, lakini hakuna aliyejitokeza hivyo kukiacha ndani bila matumizi na kwamba kilikuwa kipo kipo tu ndani ya nyumba hiyo.

Kwa mujibu wa Mwasapila, baada ya muda mrefu kupita (hakumbuki ni muda gani), alilazimika kumuuliza Mungu kipimo cha dawa aliyoonyeshwa kuitoa kwa watu na hapo ndipo alipoonyeshwa kikombe hicho ambacho anasema wakati wote kilikuwa kikizagaa ndani ya nyumba yake.

"Mara moja nilinyanyuka nikaenda kukichukua kikombe, na hapa ndipo nilipojua thamani yake, Mungu alisema kikombe ndicho kipimo sahihi na mtu anatakiwa kunywa kimoja tu na watoto ni nusu yake", anasema.
Itaendelea wiki ijayo….

source: http://mwananchi.co.tz/biashara/-/10635-usiyoyafahamu-kuhusu-mchungaji-mwasapila


haya wapendwa,

hii hapa homework mpya, kumbe babu alikiokota kikombe chake? na anatembea nacho kila anpoenda!
Mungu gani anayetenda hivi? anayenunua vikombe na kupelekea watumishi wake?

niende wapi kuukimbia uso wako?
nikipanda mbinguni, wewe uko!
nikifanya kuzimu kitanda changu wewe uko,
nikisema giza litanifunika,
giza na mwanga kwako ni sawasawa!
 
Mungu wetu ni mwema, hawezi kufanya maovu kwa binadamu, au kumpa kikombe babu ni uovu?
Kwani kitu gani katika dunia hii Mungu hawezi kufanya. Tusaidie kutafakari vizuri hili
 
Mmmmmh, utakapo fika wakati ulio amriwa mimi (Mungu), nitahukumu hukumu ya haki.
 
Judy unalo lako jambo

you wanna walk high above God

unazidi mpaka hata chembe ya nia yako njema inapotea
 
Ata Yesu alitumia vitu vilivyotengenezwa na binadamu kufanya miujiza.Mungu daima anafanya kinyume cha akili zetu.You can not connect the dot easy with matendo ya Mungu.Yesu aliongeza samaki na mikate iliyonunuliawa na mtu aliyekuja ktk mahubiri.Kule kana Altumia mkasiki ya. Watu na ata maji yalichotwa na watu pia. With God no scientific way to under stand him.
If God can be defined his power and his hollyness at the laboratory or in a test tube ,Then is not so big cause he can stay in the lab testtube
 
"Mafarisayo wkamuuliza Yesu kati ya huyu kipofu na wazazi wake nani aliyekuwa na dhambi hata akazaliwa kipofu! Akwaambia hakuna ambaye alikuwa na dhambi ila ilikuwa mipango ya Mungu ili jina lake liinuliwa. Yesu akatema mate chini akafinyanga tope na tazama akampaka machoni kisha akamwambia nenda kanawe kwenye lile bwawa. Baada ya yule kipofu kunawa na tazama alipata kuona. Watu walipomwona wakasema huyu si yule kipofu ombaomba? Wengine walikubali na wengine walikataa! Wakuu wa sinagogi walimwita na kumuuliza yule aliyekuwa kipofu naye akawaambia kuwa yule mtu aitwaye Yesu ndiye aliyemtendea haya. Wakasema hakika huyu siyo mtu wa Mungu maana anatenda dhambi".

Tuna wengi nao wanabisha kazi ya Mungu kama Mafarisayo ambavyo hawakuamini kazi ya Yesu. Sitoshangaa Kwa baadhi ya watu kutoitambua kazi ya Mungu kupitia kwa watumishi wake. Hata Yesu angerudi leo bado kuna ambao hawataamini pia. Uzao wa Tomaso bado upo.
 
Kikombe cha babu ni kitendea kazi tu Judy wala usihofu hata kama kiliokotwa au kilidondoshwa kutoka juu, cha msingi babu anakitumia kama measuring tool yake ndo mana hakiachi kisije kikapotea, kutembea nacho ni aina tu ya utunzaji na haimaanishi vinginevyo... Usiitetereshe imani yako kwa kutafuta uhalali wa kikombe cha babu kwamba ni made in where!
 
sasa kinachotibu ni dawa?
ni kikombe?
ni babu?
ni Yesu?
hayo masharti ya kikombe hayatofautiani na mashahrti ya hirizi, wake up wapendwa!
 
sasa kinachotibu ni dawa?
ni kikombe?
ni babu?
ni Yesu?
hayo masharti ya kikombe hayatofautiani na mashahrti ya hirizi, wake up wapendwa!

Miss Judith Kwanza nakupa pole kila unacho dadisi kuhusu Babu kila mtu anakupinga na kukuona MJINGA Tuliokunywa tumepona Kama wewe huumwi shida yako nini?
 
Miss Judith Kwanza nakupa pole kila unacho dadisi kuhusu Babu kila mtu anakupinga na kukuona MJINGA Tuliokunywa tumepona Kama wewe huumwi shida yako nini?

nikutoe wasiwasi kuwa hakuna haja ya kunipa pole. kila ninachokiandika hapa siandiki kwa lengo la kuungwa mkono na mtu. mi naandika kwa sababu naamini ndio ukweli na hata asiyeukiri leo atakiri kesho. mi naandika kutimiza wajibu wangu tu kama mwanajamii na mkristo. sitafuti thanks wala likes. mi naamini Bwana alikuja kutafuta na kuokoa kilichopotea. sasa ushindi ni wake Bwana na mimi nafanya tu kazi ya mjakazi shambani kwake kwa kuisema iliyo ya kweli. sitajali hata kama dunia nzima itamkataa Bwana Yesu, mimi nitaendelea kuwa naye.

hata kama umepona, ujue kuwa tunachohoji sio kama babu anatibu na kuonya watu au la, tunahoji nguvu na roho iliyo nyuma yake na kama hilo ni somo gumu sana kwako, basi siku utakapoweza kulielewa utalielewa tu.

Mungu yu mwema kwa wamchao
 
Miss Judith Kwanza nakupa pole kila unacho dadisi kuhusu Babu kila mtu anakupinga na kukuona MJINGA Tuliokunywa tumepona Kama wewe huumwi shida yako nini?

...Judith, Wewe huna imani na anayofanya Babu basi baki na werevu wako kwa Amani.
Uache ule umati unamiminika kwa Babu kupata kikombe waendelee na Ujinga wao Kwa Amani.
It is Simple as That.
Why do you get so worked Over about Babu and his Kikombe? Why??? :noidea:

 
...Judith, Wewe huna imani na anayofanya Babu basi baki na werevu wako kwa Amani.
Uache ule umati unamiminika kwa Babu kupata kikombe waendelee na Ujinga wao Kwa Amani.
It is Simple as That.
Why do you get so worked Over about Babu and his Kikombe? Why??? :noidea:


i love those people my dear,

naumia kuona wanakimbilia kikombe kama vipofu bila kujua ni roho gani wanayoikimbilia
 
mhh...hii basi sasa inaleta maswali kweli. Lakini najiuliza, kwa nini anarudisha sifa kwa Mungu kama ni muongo?
 
source: Usiyoyafahamu kuhusu Mchungaji Mwasapila


haya wapendwa,

hii hapa homework mpya, kumbe babu alikiokota kikombe chake? na anatembea nacho kila anpoenda!
Mungu gani anayetenda hivi? anayenunua vikombe na kupelekea watumishi wake?

niende wapi kuukimbia uso wako?
nikipanda mbinguni, wewe uko!
nikifanya kuzimu kitanda changu wewe uko,
nikisema giza litanifunika,
giza na mwanga kwako ni sawasawa!


Miss Judith,

Kama babu anaagua kupitia 'muujiza' Mungu kupitia ndoto, basi yeye Mungu alishusha kikombe, babu akakiokota, simple logic for believers.
 
Namuliza Miss Judith kama ana uelewa ni wapi maandiko yanaonyesha kuwa Mungu ni careless? So why does she expect watumishi wawe kuwa careless.
 
Back
Top Bottom