Kikao kati ya CHADEMA na Serikali (Ikulu) chaisha, makubaliano haya hapa!

Kweli JK kiboko , mbwembwe zote za cdm mwishowe wameishia kuandika paragraph 2 tu , na wametoka wanafurahi kwa kunywa chai ya ikulu, juice nakupiga picha na Rais.

Kweli timu hii ifuatayo ya Chadema ni ya kuandika paragraph 2 tu??? semeni nanyi hamko seriouss na suala hili la katiba na uamuzi wenu wa kuonana na Rais mlikurupuka.

Timu ya Chadema : Philman Mbowe ( Mwenyekiti ), Said Arfi ( makamu mwenyekiti bara), Said Issa Mohammed (makamu mwenyekiti zanzibar), Prof. Mwesiga Baregu, Prof. Abdallah Saffari (washauri wa masuala ya siasa), Tundu Lisssu (mnadhimu wa kambi ya upinzani), John Mrema. Timu yote hii na vigogo then paragraph 2, kwa siku 2, ur joking !
NAJUA WEWE ni Gamba(CCM) HAPA UNAFANYA KUCHOCHEA
 
Hivi mkuu ww ulitegemea kwenye haya mazungumzo chadema wangebadilisha kitu ?. Na kwa taarifa za ndani nilizo zipata ni kuwa baada ya ile jana kuahirishwa ujumbe wa cdm ulitoka na mawazo tofauti ndani ya kikao hawakuwa wamoja tena
Ndio maana nilikwambia wewe ni GeniousZero, si maghamba hao hao walikataa CDM wasiende peke yao kumuona mkulu wa Magogoni? Sasa unasema hakuna kitu na mkulu amesema hataki hali kama ya ndugu zetu jilani waliomwaga damu, ili mambo yaende kwa majadiliano! Sasa tumuamini yupi wewe au mkulu wa boma aliyekubali kuwasikiliza CDM?
 
Huu ni mfano halisi

Lakini mi naona yapo ya msingi waliyokubaliana labda ni siri lakini kwa nini iwe siri ????

Hizi tabia za kufanya kila kitu siri ndio zimetufikisha hapa tulipo wapo watu wachache wanajua siri na mabaya ya serikali ndio hawa wanatuumiza kila siku.

Hadi katiba tunaweka usiri?
 
Hayo marekebisho itafanyiwa kabla ya Rais kusaini?

Kwasababu si inasemekana muda ni mchache kabla hajasaini?

Ama ameghairisha kuusaini muswada?

Ukweli ni kubwa sheria yaweza kusainiwa na Rais kama haina vitu ambavyo say vinapingana na katiba ya sasa... lakini wabunge e.g. wa CHADEMA wanaweza kupeleka hoja ya amendment kwenye bunge la January.... So ku-signiwa kwa sheria sio mwisho ya sheria kubadilishwa au kuhuishwa.


Mungu Ibariki Tanzania
 
Tafakari hapo, kuwa kwa upande wa serikari anasain Nchimbi na upande wa chdm anasain Mnyika, hapo maana yake nn? Na uzito wa jambo lenyewe ni upi?,, tusubiri taarifa lakini kuna picha inaashiria ki2 fulani pale ambacho ni cha kawaida saana, tusitegemee mabadiliko sana.
 
Labda turudi nyuma kidogo
Kwani CDM walienda ujumbe /hoja zipi ili tutakapo letewa taarifa kamili tujadili kwa upana zaidi Yawezekana walikuwa na hoja moja au mbili tu
 
Ndio maana nilikwambia wewe ni GeniousZero, si maghamba hao hao walikataa CDM wasiende peke yao kumuona mkulu wa Magogoni?

Sasa unasema hakuna kitu na mkulu amesema hataki hali kama ya ndugu zetu jilani waliomwaga damu, ili mambo yaende kwa majadiliano! Sasa tumuamini yupi wewe au mkulu wa boma aliyekubali kuwasikiliza CDM?
Hii ni aibu kwa cdm kupeleka ujumbe mzito , maprofesa , viongozi wa juu then mwisho wa siku kuibuka na paragraph 2. Huu si wehu huu . Ndio maana nilisema tangia siku za zilizopita kabla ya haya mazungumzo kuwa viongozi wa cdm wanakwenda ikulu kunywa chai na kupiga picha mkabisha, si mmeyaona sasa !
 
Hayo marekebisho itafanyiwa kabla ya Rais kusaini?

Kwasababu si inasemekana muda ni mchache kabla hajasaini?

Ama ameghairisha kuusaini muswada?

Angalia paragraph ya kwanza

Pamoja na sheria hiyo kupitishwa na bunge ipo haja ya kuendelea kuiboresha ili ikidhi mahitaji ya kujenga kuaminiana na muafaka wa kitaifa
Hapa kuna makosa ambayo labda ni ya kifundi au ya makusudu, bunge halijapitisha sheria, bunge limepitisha muswaada ambao hauwezi kuwa sheria mpaka Rais aupitishe kwa ku sign mswada huo ili uwe sheria, kwa kifupi hapa muswada umesainiwa tayari na hakuna marekebisho yatakayo fanyika kwenye huu muswada, labda yaje kufanyika kwenye sheria.

Palagraph ya Pili

Yawepo mawasiliano na mashauriano ya mara kwa mara kati ya Serikali na wadau mbalimbali juu ya kuboresha sheria hiyo kwa lengo la kudumisha muafaka wa kitaifa kwenye mchakato wa katiba mpya

Hapa vilevile marekebisho hayatakuwa kwenye muswada, bali ni baada ya muswada ku-sainiwa na Rais kuwa sheria na marekebisho yatafanyika kwenye sheria,

Kwa kifupi hapa mswaada utasainikuwa kuwa Sheria bila ya mabadiliko wala maboresho yoyote mpaka pale utakapokuwa sheria.

Halafu wakuu mbona neno muafaka limejirudia rudia au CDM wanataka kufanya kama CUF zenj, muafaka.

Haya mufaka.

 
Sioni la maana hapo, ni yale yale ya siku zote. CDM wamewekwa mfukoni, nawapa pole.
 
Kweli JK kiboko , mbwembwe zote za cdm mwishowe wameishia kuandika paragraph 2 tu , na wametoka wanafurahi kwa kunywa chai ya ikulu, juice nakupiga picha na Rais.

Kweli timu hii ifuatayo ya Chadema ni ya kuandika paragraph 2 tu??? semeni nanyi hamko seriouss na suala hili la katiba na uamuzi wenu wa kuonana na Rais mlikurupuka.

Timu ya Chadema :
Philman Mbowe ( Mwenyekiti ), Said Arfi ( makamu mwenyekiti bara), Said Issa Mohammed (makamu mwenyekiti zanzibar), Prof. Mwesiga Baregu, Prof. Abdallah Saffari (washauri wa masuala ya siasa), Tundu Lisssu (mnadhimu wa kambi ya upinzani), John Mrema. Timu yote hii na vigogo then paragraph 2, kwa siku 2, ur joking !

Hapo kwenye blue: Freeman?
 
Back
Top Bottom