Kikao cha NEC Zanzibar: Karume hataki kuongezewa muda!

mi nashangaa sana kuona watu wapo hapa jf halafu anatoa hoja kama mtu asiyeingia hata darasa moja.imefika wakati tuanze kuona jinsi tusivyojua maana ya opportunities..wakati nchi za ulaya mashariki zilipojiunga na EU hawakupoteza muda kuchunguza faida zake bali wali-grab hiyo opportunity kwa kwenda western countries na kufaidika na resouces za huko!!!Sasa sisi uvivu wetu wa kufikiri unatufanya tusione kilichopo kwenye nchi hizo mbili(bara na zenji) Hivi mahala ambapo pana ardhi yenye rutuba na mito yenye maji ya kutosha dunia ya leo useme pana faida gani kama sio uvivu ni nini?hata mwuungano ukiuawa kesho kama mentallity ni hizihizi patakuwa kero zaidi.Wazanzibar popote walipo hata ukiwakuta ulaya ni malalamiko hayohayo tu lakini hakuna chochote wanachofanya maana.fungueni macho kuna a lot of opportunities ndani ya muungano kama hamzioni hata mkibaki na zanzibar au bara peke yake hamtaona chochote!!!!!!!

Sasa mkuu hizo opportunities za muungano wetu ziko wapi na ni zipi hebu tumwagie nakushangaa kulinganisha muungano wetu na wa EU eti nchi za EU hazikupoteza muda kuchunguza faida eti zili-grab tu usitake kutufanya wote mbumbumbu.

Huna taarifa kuwa Lisbon treaty imesainiwa mwezi uliopita Dec baada ya mvutano mkubwa usidanganye watu kule kuna viongozi wanaofuata utawala wa sheria viongozi wanaolinda EU kwa maslahi ya nchi zao si huku viongozi wanalinda muungano kwa maslahi yao binafsi.
 
mi nashangaa sana kuona watu wapo hapa jf halafu anatoa hoja kama mtu asiyeingia hata darasa moja.imefika wakati tuanze kuona jinsi tusivyojua maana ya opportunities..wakati nchi za ulaya mashariki zilipojiunga na EU hawakupoteza muda kuchunguza faida zake bali wali-grab hiyo opportunity kwa kwenda western countries na kufaidika na resouces za huko!!!Sasa sisi uvivu wetu wa kufikiri unatufanya tusione kilichopo kwenye nchi hizo mbili(bara na zenji) Hivi mahala ambapo pana ardhi yenye rutuba na mito yenye maji ya kutosha dunia ya leo useme pana faida gani kama sio uvivu ni nini?hata mwuungano ukiuawa kesho kama mentallity ni hizihizi patakuwa kero zaidi.Wazanzibar popote walipo hata ukiwakuta ulaya ni malalamiko hayohayo tu lakini hakuna chochote wanachofanya maana.fungueni macho kuna a lot of opportunities ndani ya muungano kama hamzioni hata mkibaki na zanzibar au bara peke yake hamtaona chochote!!!!!!!

You miss the point buddy. Go back to class and revisit your notice of international politics. You cant benefit from opportunities if there is no level playing field. You cant benefit from the available opportunities if the system is corrupt and rotten. Huu ndo ugomvi wetu na CCM. Period.

Make no mistake. Hakuna anayetaka serikali impe benefits au upendeleo (labda watoto wa mafisadi). Wengi tunacholilia ni serikali iweke mazingira watu tuhangaike kivyetu. Upo? Hakuna anayesema kwamba serikali italeta maendeleo. Ila tunasema serikali iweke mfumo wa kodi mzuri hata kama ukihangaika ukienda kulipa kodi isiwe kero. Itumie kodi zetu kujenga barabara..siyo kuwekeza kwenye manyumba Dubai kusudi hata mzee wangu apate sehemu ya kupitisha pamba yake. Hivi unajua mpaka leo watanzania wengi wanaamini bila RUSHWA au KUMFAHAMU mtu kwenye "system" huwezi kufanikiwa?

Unapoongelea opportunities..its a bigger word. Wazenji wanaweza kuwa wanalalamika lakini bottomline ni kwamba watu wanalalamikia injustice. And this is what the governement should address. Then ituache watu tutumie akili zetu kuhangaika.

Masanja.
 
Je kikao kipo na ajenda zile tajwa hapo juu au kimeahirishwa?

CCM ilikuwa inasema ukichagua upinzani kutatokea vurugu nchini.Je hizi za kwao ni nini?
CCM IPO KWENYE "POLITICAL SLAMP"
. Vyama vya siasa,tumieni nafasi hii ya mtafaruku wa CCM KUJIIMARISHA,MSILALE HADI KIELEWEKE.
 
Kikao kimeahirishwa kwa kuwa kuna kikao kingine kinachoongozwa na Karume huko Zanzibar, nashindwa kujua kati ya vikao hivi ni kipi kilipangwa mapema!
 
Kikao kimeahirishwa kwa kuwa kuna kikao kingine kinachoongozwa na Karume huko Zanzibar, nashindwa kujua kati ya vikao hivi ni kipi kilipangwa mapema!

Kuna tetesi kuwa wajumbe wa Zanzibar waliotakiwa waje bara kwenye kikao cha kamati kuu waligoma na wao wakaitisha kikao chao ikabidi Msekwa aende mwenyewe Zanzibar kwenye kikao chao.
 
Hakuna lolote la maana litakalotoka Zanzibar. Kwanza ni lazima tujiulize ni kina nani hasa wanakaa, inawezekana kikubwa hasa itakuwa ni kumshambulia Karume kwa kuwauza "wanaccm" au nako kutakuwa na mwanzo wa watu kujiandaa kujiunga na CCJ.

Hakuna mwenye guts za kusema Zanzibar ijitenge, akijaribu kufanya hivyo atakuwa ndio anajimaliza kisiasa. Lets wait and see, not much will come out of it, zaidi ya politiki tu.
 
- Kuna utatanishi mkubwa sana na kinachotokea au kilichotokea kuhusiana na hiki kikao kilichokuwa kimepangwa kufanyika leo, katika masaa 48 yaliyopita behind the scene kumekuwa na vuta nikivute, between vigogo wa bara na wajumbe wa Visiwani wa kikao hiki cha CC.

- Tunajaribu ku-verify kwanza dataz tulizonazo on usahihi wake, kabla ya kuzimwaga hapa, ingawa sio siri mambo hayako sawa huko ndani.

Respect.

FMEs!
 
That is your take, jaribu kujiuliza kiutu uzima wiki iliyopita kulitakiwa kufanyike kikao cha NEC Dodoma wajumbe wa Zanzibar wakagoma kuja kuwa wana kikao cha wawakilishi si kawaida yao kwanza si wawakilishi wote ambao ni wajumbe wa NEC.

Kikaitishwa kikao cha dharura cha CC-CCM Dar es salaam vile vile wajumbe wa zanzibar wakagoma bila kutoa sababu usiniulize kwa hili sijui kitu ambacho si cha kawaida kikao cha CC kimeahilishwa ghafula, kuona hivyo CCM bara wakamtuma Msekwa kuwafuata Zanzibar kujua kulikoni wewe bado unasema hakuna chochote.

Kwa mtazamo wa kawaida tu hii sinema si ya kawaida kwa CCM na wala tusidharau kwa kusema ni mambo ya kawaida, kama ni kujiridhisha kwa wana CCM ok endeleeni kujiridhisha lakini wenye akili zao wameliona hili na wanajua kuna jambo kubwa linatokea ndani ya CCM.
 
Sichezi mbali leo na mzee wa dataz! Huenda utabiri wa Mwalimu Nyerere unaanza timia....Mpasuko CCM
 
- Kuna utatanishi mkubwa sana na kinachotokea au kilichotokea kuhusiana na hiki kikao kilichokuwa kimepangwa kufanyika leo, katika masaa 48 yaliyopita behind the scene kumekuwa na vuta nikivute, between vigogo wa bara na wajumbe wa Visiwani wa kikao hiki cha CC.

- Tunajaribu ku-verify kwanza dataz tulizonazo on usahihi wake, kabla ya kuzimwaga hapa, ingawa sio siri mambo hayako sawa huko ndani.

Respect.

FMEs!

tunazisubiria mkuu wa sauti ya umeme
 
- Well the dataz ni kikao kimeahirishwa mpaka itakapoamuliwa tena, tatizo ni wajumbe wa Zanzibar wakiongozwa na Karume, wamegoma kuja kwenye kikao wakidai wana kikao chao huko cha Kamati Maalum ambacho kinawajumusiha wajumbe wa CC huko Visiwani, na pia wajumbe wa NEC kutoka huko, na wajumbe wa CC na NEC, wenye asili ya huko Visiwani kama kina Meghji na Khatibu.

- The dataz ni kwamba kuna kundi lenye mchanganyiko wa wajumbe toka CCM na CUF, likiongozwa na Maalim Seif limeanza kuwa na the uper hand over siasa za Visiwani, walianza na kile kikao cha NEC kilichombana mbavu Spika, kwenye kile kikao wajumbe wote wahusika wa hili kundi waliamriwa kuondoka mara moja kabla ya kikao kuanza baada ya kugundua agenda ya kikao dakika za mwishoni.

- Sasa kundi hili pia limekataa wajumbe wasije Bara, kwenye hiki kikao cha dharura cha leo, the dataz ni kwamba hata Karume hana ubavu kwenye hili kundi, na yeye sasa anapewa amri tu, na ni hili kundi ambalo pia linalotaka apewe term ya tatu.

- Mjumbe mmoja, aliyenipenyezea hizi toka huko Visiwani amenitaka nimsubiri kwa masaa mawili zaidi maaana alikuwa ametoka nje ya kikao kidogo tu na amerudi ndani ya kikao tena, ndio tutapata more dataz ya yanayojiri huko kwenye hicho kikao maalum na huku bara on hiki kikao kilichoahirishwa na kama kawa tutahabarishana hapa hapa JF.

Respect.

FMEs!
 
Waungwana nilikuwa zanzibar muda wa siku mbili au tatu zilizopita na nimekaa huko kama mwezi mzima. Aliyoyasema mwanakijiji yanaelezea only one part (ila sidhani kufukuzwa wabara au damu itatokea znz kwani navyowafahamu wazanzibar ni waoga sana mikwala mingi tu).

CCJ is not an issue kwa CCM kwani inaweza kushughulikiwa na usalama wa taifa na makada wa chama. Ishu ni zanzibar kwasababu mentality ya wazanzibari sasa hivi ni kwamba bara inawagandamiza kila kitu. Watu zanzibar sasa hivi wanasema kuwa hawataki kuwaona wabara kwasababu wanachukua kazi zao, rasilimali zao na ardhi zao. Sasa pana chuki ya chini kwa chini inaendelea. Na hali ya maisha imekuwa ngumu kiasi kwamba watu wamechoka na CCM si CUF bali pia wanaCCM wenyewe pia. Vilevile watu wamekosa imani na muungano ndio maana wote wamesusia sherehe za kitaifa na kichama siku hizi CCM inakodi watu toka Tanga, Arusha, Tabora kwenda unguja na Pemba kwasababu wazanzibari wenyewe wamesusia kabisa sherehe hizo kwa sababu hazina faida kwao. In summary CCM bara inalazimisha kupendwa zanzibar kwani hata wale wana CCM znz wameshaichoka pia hivyo sasa hivi sijui Halmashauri kuu ya CCM watafanya mbinu gani wapendwe znz maana wanaowasupport wenyewe wamewachoka to be honest.

Pili ishu inayomfanya Karume ang'ang'anie madaraka ni mafuta ukweli mafuta yapo na report za kitaalamu zinaonyesha 95% mafuta yapo. Tayari kuna makampuni yameanza construction ya offshore drilling sites na karume anaona hizi dili akiondoka atazikosa ndio maana inapigwa zengwe akae miaka miwili ili akishasuka mipango aishi peponi milele. Sasa akiwa hayupo atakayekuwa madarakani atakula hilo dili. Likewise wazanzibari wanaona mafuta ndio mkombozi wa umaskini unaonuka znz. Hivyo basi wote CUF na CCM wamekusudia kwakweli kuuvunja huu muungano maana inaonekana wanazidiwa nguvu na serikali ya bara the best way ni kurekebisha katiba ambapo vipengele vyote vitajadiliwa including mafuta.

Kiufupi hiyo inakupa ni jinsi gani wenzetu znz walivyojizatiti na hawa jamaa hawana maskhara this time nilipoongea nao wengi wao ni wasomi hivyo vitu vyao vinaenda si kimwinyi bali kisomi na wamejipanga kweli kweli. Kimsingi mie naona CCM ingelifanya la busara kulizungumza hili jambo wazi muungano ukarekebishwa venginevyo itaresult into blood bath kitu ambacho si kizuri
 
Tatizo ni Hamadi na Karume kukubali kwa ajili ya Zanzibar na pia baada ya hpo ndio utaweza kuona na kuona kuwa kuna watu wataanzisha mambo mengine ya ugomvi zanzibar hivyo suala ya CCJ sio sababu kabisa kwa ajili ya uchaguzi. Wataleta ugomvi na kufanya hakuna mwafaka kabisa Zanzibar. Subiri tuone huko
 
Mdondoaji, hapo kweli umetoa picha ya ndani ya halihalisi ya kisiasa huko zenji!

Na hayo mabadiliko ya katiba unayoshauri yafanywe ni ya kivipi?

Bila kuwa makini, tunaweza kufanya mabadiliko ambayo yana'nullify Muungano, maana kwa kasi ya sasa hivi nionavyo mimi, mabadiliko yanayokuwa suggested ni KUONDOA ONDOA vipengele na si kuvibadilisha parse!

Na haya mafuta kama kweli yapo, basi huu muungano hauna MBELEKO ya kuubebea!
 
.....leo mambo mtaona leo mambo mtaona x2 .....mlimchagua wenyewe, watanzania wenyewe x2.........!
 
Mdondoaji, hapo kweli umetoa picha ya ndani ya halihalisi ya kisiasa huko zenji!

Na hayo mabadiliko ya katiba unayoshauri yafanywe ni ya kivipi?

Bila kuwa makini, tunaweza kufanya mabadiliko ambayo yana'nullify Muungano, maana kwa kasi ya sasa hivi nionavyo mimi, mabadiliko yanayokuwa suggested ni KUONDOA ONDOA vipengele na si kuvibadilisha parse!

Na haya mafuta kama kweli yapo, basi huu muungano hauna MBELEKO ya kuubebea!

La kwanza muungano uliundwaje this is the heart of the debate in zanzibar kwasababu inaelekea kuna alot of vaccum kuhusiana na mazingira kuundwa kwa muungano plus inasemekana mkataba upo but ukiwauliza wazee wenyewe wanasema yalikuwa ni makubaliano ya mdomo baina ya karume na nyerere ambayo nyerere aliyageuza kuwa mkataba wa muungano ( This is the root of the problem).

Pili kuna mambo ndani ya muungano yanasemekana ni mambo ya muungano na mengine ni mambo ya zanzibar. Sasa ishu ni kwamba madini yaliwekwa katika Tanzania Bara na gesi ya asili. Na mafuta yaligundulika since Nyerere alipokuwa madarakani (This one i found out nilipokuwa znz majuzi) akaliweka faili chini ya desk akijua litafumua mgogoro wa muungano. Sasa nadhani over the past 12 months znz ilipoanza kudai rights za kuwa na mafuta muungano walipinga na rais akashindilia nyundo. Pia kulikuwa na tetesi baadhi ya vinara walioshabikia kuhusu mafuta wameshughulikiwa na hili ndilo liliowakera wengi ambao walikaa kimya kuhusu mafuta. sasa wanaretaliate kwasababu imeonekana Tanzania Bara wanataka kuyatawala mafuta kimabavu.

Ndio maana nikasema CCM wangelijadili haya mambo kiuwazi kwani kuna alot of consipiracy going on na zinajenga chuki within zanzibar ndio maana unaona kuna movement inaendelea ambapo inahitaji watu wazima (kiusomi kuihandle) na sio kiubabe kama ccm inavyofanya.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom