Kikao cha dharura cha CCM mchana huu

Hiki kiswanglish bana!! Hapa nimetoka kapa!!

Mzee Kipara naona leo huna hoja tena! Kiswanglish umekiona leo tu humu?
Tujuze basi kwenye kamati ya chama mchana huu, ndo mnaenda kuwachimba mkwara eeh?
 
wakanyamazishane tu ....... lakini kwa mwendo huu wa seriakli kuwa imeoza katika sehemu nyingi pesa za wananchi zinatafunwa bila huruma 2015 wabunge wengi wanahofu kutorudishwa tena bungeni ndio maana wanapiga kelele...... nazisifu sana kamati kuweka wazi uozo wote.
 
Hii nilitegemea baada ya kuzuiwa kusomwa kwa mawaziri wanafuja hela za serekali.
 
Toka sakata la Jairo litokee siku hizi wala hainistui kusikia wabunge wa CCM wameka kama kamati, nakumbuka waliongea hadi mapovu wakasema patachimbika, lakini leo nasikia Jairo bado analipwa mshahara, haya ni masihara sasa.
 
Kwani yupo bungeni?
ndio yupo ameongea mengi mazuri ila lililowachanganya ccm ni alipowambia serikali iliyo chini ya waziri mkuu M. Pinda ni wezi na wanatakiwa kuwajibishwa, na wakwanza kuwajibishwa anatakiwa awe Mizengo pinda kwa kutokusimamia mawaziri wake, na njia ya kumuwajibisha ni kupiga kura za kutokua na imani naye, AKAWAAMBIA WAPINZANI NI WACHACHE CCM NI WENGI NA KWA WINGI WAO WANAWEZA KUMUONDOA WAZIRI MKUU NA MAWAZIRI WEZI MADARAKANI, akawaambia kama kweli ccm wanatetea wananchi wafanye hivyo vinginevyo wasipige kelele za kinafiki bungeni. HUU NI MTIHANI KWA CCM (a) ENDAPO HAWATAMUONDOA PINDA NA MAWAZIRI WEZI hukumu yao ni 2015 (b)je wanauthubutu wa kufanya hvy?
 
Ivi wanajeshi huwa hawasikilizi bunge maana madudu yote haya watu bado wanapeta.
Yaani ata Mali wametushinda jamani!
 
My friend it to late for CCM kuwahi train
Mwalimu wangu chuoni aliwahi kusema unapoandika/unapoongea broken english, ni sawa na mtu mzima kujamba hadharani. Alitumia neno baya sana nadhan nia yake ilikuwa ni kumfanya mtu anayetumia lugha hii awe makini kwenye kutoa matamshi/kuandika hasa ukizingatia kwamba sio Lugha yetu asilia. Nashauri pia tutumie tu Lugha yetu maana nayo inasifa kubwa tu ya ukimataifa huko nje ya nchi. Sio kuwa ukitumia kiswahili utaonekana haujasoma. Wapo maprofessor wa kichina na kifaransa hawajui kiingereza kabisa so usifkirie usipoongea/kuandika kiingereza utatolewa kwenye tabaka la wasomi.Take it as a challenge and move forward, JF ni jukwaa la kufundishana na kushauriana.
 
Back
Top Bottom