Kikao cha Bunge jana jioni

mshikachuma

JF-Expert Member
Dec 2, 2010
2,853
626
Wakati akihailisha kikao cha bunge jana jioni' Naibu spika alitoa tangazo la
kwamba wabunge wote wa CCM na CUF kutoka Zanzibar wanaitwa kwenye
kikao fulani. Ndipo mh. zito kabwe akauliza kwa kuhoji, hata CDM wanawa
bunge kutoka Zanzibar mbona hamuwaiti kwenye hicho kikao? Naibu spika
alijibu kwa kupotezea......

Swali langu ni - Hivi kitu kama hicho wanamaanisha nini? Hapo kweli kuna
upinzani? - Nawasilisha
 
CUF walishazoea kushika hatamu upinzani bungeni na kusema kweli walifanya vizuri. Sasa kwa kuwa uongozi una marupurupu kibao na CUF hawakudhani wanaweza kuachia mtu mwingine wakiona ugumu wa wapinzani wa Bara kuibuka na kiwango kikubwa kama alivyopata CDM hawatko tayari kuona hilo linatokea kama ambavyo CCM wanasema piga, garagaza, ua lazima dola washike wao milele unaweza kuona utau wa madaraka kila mtu anaujua. Huyo kiongozi wao aliyejizolea sifa sana bunge lililopita ghafla kageuka pilipili maana hana chake na huenda alitarajia mwaka huu ashike kotekote.
 
Mtu na mchumba wake, acha waende faragha.
mmmh.... maana huku uraiani watu wanabishana kuhusu lile tukio la jana jioni na bado
jibu hatujalipata. kwanza walio wengi wanakataa kuwa CDM wana wabunge Zanzibar na
wanahoji wabunge hao waliwapateje na kwa sheria hipi? Na kama wapo'basi kwanini
na wao wasiitwe kwenye kikao ile jana?
 
hivi jamani kuna kosa mtu akimwita mkewe ndani wakae falagha ....
 
tuanzishe kampeni ya kuidai nchi yetu ya Tanganyika.
maana mapaka sasa Zanzibari ni kama walishajitenga kabisa sasa kilichobaki ni sisi
Wakati akihailisha kikao cha bunge jana jioni' Naibu spika alitoa tangazo la
kwamba wabunge wote wa CCM na CUF kutoka Zanzibar wanaitwa kwenye
kikao fulani. Ndipo mh. zito kabwe akauliza kwa kuhoji, hata CDM wanawa
bunge kutoka Zanzibar mbona hamuwaiti kwenye hicho kikao? Naibu spika
alijibu kwa kupotezea......

Swali langu ni - Hivi kitu kama hicho wanamaanisha nini? Hapo kweli kuna
upinzani? - Nawasilisha
 
tuanzishe kampeni ya kuidai nchi yetu ya Tanganyika.
maana mapaka sasa Zanzibari ni kama walishajitenga kabisa sasa kilichobaki ni sisi

Tanganyika mbona ipo kiaina kwa mwavuli wa Tanzania? Au unataka tupoteze muda kilijadili hilo?
 
mhhhh mambo mazito hayo. Ina maana hao wabunge wa CHADEMA toka Zanzibar si wa Zanzibari au hao wa CUF na CCM walikuwa wanaitwa kwa agenda gani hasa? mwaka huu tutaona na kuyasikia mengi
 
Mtu na mumewe wameenda kula halua nyie kinawauma nini? Waacheni jamani mapenzi yako mwanzoni lazima yawe moto moto
 
Nilisema jana,kuwa hawa wawakilish wetu wanafanya komedi mjengoni pale!
mhhhh mambo mazito hayo. Ina maana hao wabunge wa CHADEMA toka Zanzibar si wa Zanzibari au hao wa CUF na CCM walikuwa wanaitwa kwa agenda gani hasa? mwaka huu tutaona na kuyasikia mengi
 
Back
Top Bottom