Kijitabu Cha Orodha ya mafisadi wa Elimu Tanzania chagombewa sokoni

We acha tu,

Halafu watu wana nerve ya kushutumu ufisadi on the next thread.
nimejaribu kusoma kijitabu hote hajaweka mawasiliano yake wala anuani ya mchapaji ili kuona kama kunauwezekano wayeye kuruhusu chapisho lake kubandikwa humu, ila kwmujibu wake kupitia gazeti nililonalo hapa ni kua amechapa naka 89000, sasa kwa kasi ile ya manunuzi sijui kama kwa siku hizi tatu kitakua sokoni.

ila nikifika home nitapima mwenyewe kuona ni busara kubandika humu ama laah.
 
Nikingali natafakari "ukichaa" wa mwandishi wa kitabu hicho kujitoa hadharani kuwaadhiri wakulu wenye vyeti vinavyotia shaka, na nikizingatia kilichoelezwa kwenye magazeti tu, najiuliza kama ni sahihi kuandikia suala hilo kitabu. Labda kama lengo ni kutoa uchambuzi mzito na wa msingi wa tatizo hilo na jinsi ya kulitatua (zaidi ya kuwaumbua waheshimiwa na digrii zao feki).

Kama kitabu kimelenga kutaja majina na ushahidi wake tu, basi ingelikuwa bora mwandishi angetoa makala ya utafiti (investigative journalitic piece) kwenye vyombo vya habari badala ya kuandika kitabu kinachotakiwa kudumu kwa muda mrefu na kupitiwa hata na vizazi vijavyo.
 
Namfahamu Mh. Diallo, na nakumbuka nilivyokuwa namuona akipiga book. na nisikuwa nikimsifia kwamba hakika yeye unawezo mkubwa kuliko vijana wengi, kwa maana kuweza kusoma, siasa, biashara etc. But I saw that man... is extraordinary.

Jamaa amesomea degree yake... sasa kama munadhani kusoma lazima uwe darasani... kama hamtambui distance learning... that is your proble.

Mkuu, Usimtetee kwa mtindo wa mitaani eti jamaa anayapata mambo sana. Hata kama anabuni mambo usiyoweza kama Newton, maadamu hakupitia Chuo kinachotambulika, usiseme ana degree. Ni kosa kubwa kwa aliyesoma kutetea mtu kwa mtindo huo. Shule lazimaa uthibitishe kupitia chumba cha mtihani. Iwe ktk chuo kilichotambulika.

Huyo Diallo hivi karibuni katangaza kupata Ph.D sijui ni ya chuo kipi lakini ukweli ni kwamba huyu ni medical assistant. Hiyo ndo elimu aliyohenyea darasani.

Tulipofika, bora ofisi ya Bunge iamue kutoa digrii kwa wabunge wote wanaozitaka.

Wanasiasa wanaharibu Elimu nchini. Wanafanya usanii ambao wanauhamisha kuja kwenye shule zetu za Kata. Leo hii zinaongoza kwa division Zero.
 
Bigup Msemakweli..........tunataka na Tanzania Law Chambers wawafungulie kesi akina chenge....au??
 
Diallo, ni jina Sir Name iliyo maarufu kwenye nchi zilizokuwa chini ya Mali Empire. Utalisikia kwenye nchi kama Mali, Senegal, Ivory Coast, Guinea Conacry etc. Wanigeria hawana Diallo (linasomeka kwa wengine Jalo).

Kwa watu wa umri wao mtakuwa mnakumbuka wimbo wa Alpha Blondy "Fanta Diallo". Ila pana wakati nilisikia habari moja kuwa miaka ya uhuru, kuna jamaa wengi wa West Africa waliletwa Zenji na hawa waliacha majina/watoto wenye hizo sir name.

Ila Wasukuma huwa hawachelewi kujipa majina kama Carrington, MacBundala, Mzungu, Ulaya, Marekano, Meja, nk. Sintoshangaa kusikia jamaa si jina lake hasa la ukoo ila kajipachika jina la mshichana wake wa Kiguinea aitwaye Tigui Diallo (Diabate Coulibaly Keita).

Sikonge na wewe kwa fiksi umezidi!!
 
Nikingali natafakari "ukichaa" wa mwandishi wa kitabu hicho kujitoa hadharani kuwaadhiri wakulu wenye vyeti vinavyotia shaka, na nikizingatia kilichoelezwa kwenye magazeti tu, najiuliza kama ni sahihi kuandikia suala hilo kitabu. Labda kama lengo ni kutoa uchambuzi mzito na wa msingi wa tatizo hilo na jinsi ya kulitatua (zaidi ya kuwaumbua waheshimiwa na digrii zao feki).

Kama kitabu kimelenga kutaja majina na ushahidi wake tu, basi ingelikuwa bora mwandishi angetoa makala ya utafiti (investigative journalitic piece) kwenye vyombo vya habari badala ya kuandika kitabu kinachotakiwa kudumu kwa muda mrefu na kupitiwa hata na vizazi vijavyo.

Mkuu kila mtu akifanya kazi yake inatakiwa itambulike na jamii husika jamii yetu au watawala wetu hawako tayari kuangalia haya ndio maana kijana kawatia kitanzi kabisa.

Mimi naunga mkono alicho kifanya na liwe fundisho kwa wote. Hiki kitabu kitasomwa miaka nenda rudi. Na kitakuwa fundisho kwa wote wanaotaka kuwa majangiri wa Elimu.
 
Nikingali natafakari "ukichaa" wa mwandishi wa kitabu hicho kujitoa hadharani kuwaadhiri wakulu wenye vyeti vinavyotia shaka, na nikizingatia kilichoelezwa kwenye magazeti tu, najiuliza kama ni sahihi kuandikia suala hilo kitabu. Labda kama lengo ni kutoa uchambuzi mzito na wa msingi wa tatizo hilo na jinsi ya kulitatua (zaidi ya kuwaumbua waheshimiwa na digrii zao feki).

Kama kitabu kimelenga kutaja majina na ushahidi wake tu, basi ingelikuwa bora mwandishi angetoa makala ya utafiti (investigative journalitic piece) kwenye vyombo vya habari badala ya kuandika kitabu kinachotakiwa kudumu kwa muda mrefu na kupitiwa hata na vizazi vijavyo.

Thanks mkuu,

Investigative journalistic publications that has standard in it

kwa mfano reinforcement steel made in Tz should not be less than 410Mpa, and those imported should not be less than 460Mpa.Nikipata steel bar yoyote less than 410 haitakiwi nchini. This was the case ya kubomoa baadhi ya floor ya nne ya BOT(towers), steel strength was substandard.

Ukienda kwa watu wa air quality watakuambia arsenic anayotakiwa mtu kuwa exposed in for one year is 6ng/cu.m, more than that ni hatari

we are supposed to have standard (our standard) in each and everything. Unapoandika hiko kijarida unajua umesimamia wapi.

Kama ulivyosema kingekuwa kizuri kwa ajili ya kuelimisha kila raia, na hata apitie njia gani ili apate elimu fulani, na kingekuwa kizuri kutoa maelekezo nini kifanyike.

kwa mfano, mtu akishapata certificate UDSM let say, are there any peer reviewer somewhere to register it?(siyo professional board).

system yetu ya elimu na standard haviko clear kuna loop holes kibao ya watu kufanya fraud, writing that kijarida wont solve problem.

kuna watu wanataka kulazimisha mambo kuwa kila mtu awe kama wao, sheria ndio kitu pekee cha kuwaweka wote sawa.mtu kafoji degree anatengeneza mamilioni mtaanza kumlaumu, tutasema mpaka mate yakauke lakini yeye haathiriki, we need to enforce clear and known laws and standards based on our country and situation.

hao hata mkiwasoma, hawana mshipa wa aibu mpaka leo sijaona mwana CCM yeyote mwenye aibu, inakuwa kama ukiingia tu CCM unafanyiwa operation maalumu ya kuondoa nerve za aibu, mtasoma hicho kijarida tatizo litakuwa palepale!

angefanya jambo la mbolea ili vijana wetu wajue elimu si lelemama na sio mipasho
 
TCU! TCU!
Kweli ipo lakini kwa kazi ipi?
Mkuu wa TCU kwa kumbukumbu zangu ni yule aliyekuwa CACO UDSM na aliachwa. Performance yake pale chuoni haikuvutia hata kidogo.

Hapo TCU kweli ataweza?
 
wote wanao beza kijitabu hicho niwaulize mmefanya nini ktk kupambana na watu wenye vyeti feki?

Kama hakuna mlilofanya ktk juhudi hizi basi kaeni kimya.
 
Sijui nani unayemkusudia kama anabeza.

Mimi na Wabs tunachosema, kwa kuangalia posts hizo juu, ni kwamba, kama hatuna bodi ya viwango inayotoa muongozo kwamba chuo hiki au cha hivi kinakubalika na hiki au cha hivi hakikubaliki, basi tunacheza tu.

Kama huna hii standard, uta print vitabu mamilioni lakini unaacha legal loopholes kibao.Na kitabu hiki kama hakijagusia hili hakijawa serious enough.
 
Thanks mkuu,

..........................................[snip]

system yetu ya elimu na standard haviko clear kuna loop holes kibao ya watu kufanya fraud, writing that kijarida wont solve problem.
.................................................................
..........................................................................[snip]

angefanya jambo la mbolea ili vijana wetu wajue elimu si lelemama na sio mipasho

You are not wrong but you are similarly not right.

System yetu ina standards. Tangu umri wa kuanza Darasa la kwanza hadi miaka ya elimu na aina ya vyuo. Hata ajira inatambua ni miaka mingapi umekuwa chuoni na mshahara unaostahili.

Tatizo liko kwa wanasiasa. Baadhi hawana elimu ya kuwapa nguvu ya kujishikiza ktk vyeo vyao. Wameamua kufoji au kukiuka taratibu wanazotakiwa kuzilinda.

Baadhi wana familia (watoto, ndungu, nk.) ambao shule haipandi na wahusika hawa wnaamua kutafuta njia za mkato. Watawapeleka shule wanazodhani watapita bila shida ikibidi hata nje ya nchi. Hizo shule zinalazimishwa ziwe safi ili hata wao watambulike.

Tusipende kukubali makosa ya wanasiasa walioamua kuachana na standards nasi tukadhani hakuna standards.
 
Kwanza kabisa, miaka ya elimu si standard clear.

Pili, kusema nchi yetu haina standard haina maana kwamba mtu anatetea hawa wanasiasa.
 
Nashukuru umesema elimu yetu kuanzia shule ya msingi, in globalised world we dont have that 'yetu' kuna watu wanasoma abroad,wanaishia grade twelve n.k, kuna kijana mmoja alisoma uganda na alipata shida sana kuingia mlimani, alimaliza with flying colours!

Lingine ishu ya kufoji vyeti si ya wanasiasa tu you will be making a big mistake kama unasema ni wanasiasa tu, ni janga la kitaifa mkuu!

Msemakweli alichofanya ni hasira, ila angepiga mbuzi kiaina kwa kujificha nyuma ya 'standard' na angeandika kitabu chake kwa mtindo wa swali!this is another technique ya kufikisha ujumbe bila kuonekana mjinga!

unajua kabisa hatuna standard na hauwezi kuwastaki hawa watu, unauliza swali kuwahukumu wao( pasi standard) na kuwaamsha mamlaka zilizolala ziwajibike!

kwa mfano naiweka degree ya Diallo nina mfananisha na Shivji! alichofanya ni ile ua, ambayo kwa dunia ya sasa watoto wetu si wanasoma na kusikia na bado hao watu hawatachukuliwa hatua yeyote! watu angalau wakiona compariosn they think and decide!

wale walimu wa mzumbe waliofoji vyetii au sijui kusoma shule zisizojuliana ni wanasiasa? ni janga hili la kitaifa

hofu yangu ni kuwa kuna watu amewaandika wana genuine degree ambazo aidha mpya kwetu, na sheria haziko wazi, huyo mtu ukimwandika unafikiri athari zake ni nini?ndiyo nikasema anahukumiwa kwa sheria ipi?

so mjadala ni kufoji? kusoma non accredited school?, kutokukaa darasani! au ni nini hasa? maana kuna walio na notion(primitive) kuwa distance learning ni mbaya, wakati dunia ndio inakoenda huko!
 
Kwa nini usituwekee na sisi tukakisoma hapa jamvini?

Jamani si mkinunue, au hakina copyright? Nadhani jamaa aliingia gharama kukitoa nyime mnataka kuki scan na kukitoa humu, lol!
Jamaa haogopi ila namuonea huruma, sijui watamfanyaje.
 
nimejaribu kusoma kijitabu hote hajaweka mawasiliano yake wala anuani ya mchapaji ili kuona kama kunauwezekano wayeye kuruhusu chapisho lake kubandikwa humu, ila kwmujibu wake kupitia gazeti nililonalo hapa ni kua amechapa naka 89000, sasa kwa kasi ile ya manunuzi sijui kama kwa siku hizi tatu kitakua sokoni.
ila nikifika home nitapima mwenyewe kuona ni busara kubandika humu ama laah.

Usibandike. Watu watafute wanunue please, ahh
 
Nashukuru umesema elimu yetu kuanzia shule ya msingi, in globalised world we dont have that 'yetu' kuna watu wanasoma abroad,wanaishia grade twelve n.k, kuna kijana mmoja alisoma uganda na alipata shida sana kuingia mlimani, alimaliza with flying colours!

Lingine ishu ya kufoji vyeti si ya wanasiasa tu you will be making a big mistake kama unasema ni wanasiasa tu, ni janga la kitaifa mkuu!

Msemakweli alichofanya ni hasira, ila angepiga mbuzi kiaina kwa kujificha nyuma ya 'standard' na angeandika kitabu chake kwa mtindo wa swali!this is another technique ya kufikisha ujumbe bila kuonekana mjinga!

unajua kabisa hatuna standard na hauwezi kuwastaki hawa watu, unauliza swali kuwahukumu wao( pasi standard) na kuwaamsha mamlaka zilizolala ziwajibike!

kwa mfano naiweka degree ya Diallo nina mfananisha na Shivji! alichofanya ni ile ua, ambayo kwa dunia ya sasa watoto wetu si wanasoma na kusikia na bado hao watu hawatachukuliwa hatua yeyote! watu angalau wakiona compariosn they think and decide!

wale walimu wa mzumbe waliofoji vyetii au sijui kusoma shule zisizojuliana ni wanasiasa? ni janga hili la kitaifa

hofu yangu ni kuwa kuna watu amewaandika wana genuine degree ambazo aidha mpya kwetu, na sheria haziko wazi, huyo mtu ukimwandika unafikiri athari zake ni nini?ndiyo nikasema anahukumiwa kwa sheria ipi?

so mjadala ni kufoji? kusoma non accredited school?, kutokukaa darasani! au ni nini hasa? maana kuna walio na notion(primitive) kuwa distance learning ni mbaya, wakati dunia ndio inakoenda huko!

tatizo ni kusoma non accredited schools/universities
 
Kwanza kabisa, miaka ya elimu si standard clear.

Pili, kusema nchi yetu haina standard haina maana kwamba mtu anatetea hawa wanasiasa.

asante kaka maana kuna watu wanafikiri tunatetea watu hapa, we need platform ya kujudge watu, hii ishu ni very sensitive, na ni janga la kitaifa , na kuna sababu nyingi sana ya watu kufoji vyeti hapa kwetu, tafiti zinaonyesha kuwa

1. watu wanafoji vyetu kwa sababu elimu yetu inaweka kipaumbele sana swala la kuajiriwa na si kujiajiri na pia huko kuajiriwa watu wanataka vyeti

2. uibaji wa mitihani ya darasala la saba, form four na six ni alama nyingine kuwa undeground kuna watu wengi wana vyeti feki!

3. kusoma mitihani, na sio kupata elimu ni dalili tosha kuwa kuna watu wana 'maliza kabisa' mzizi wa fitina kwa kutengeneza vyeti!

4. Halafu kuna hawa, tulio nao hapa , mabao hatujui wamefoji, wamesoma non accredited school,au wamepata degree za heshima??

we need 'majembe auction mart' kukagua na kusajili kila cheti hapa nchini, but we have to have reserached and well prepared standard

kuna mmoja hapo juu anasema unasoma shule ya msingi, then secondary,.... kuna watoto kibao wanatoka darasa la tano intenational(au english media) school directly secondary form one, why? kwa sababu form one ni kama marudio ya darasa la saba na sita ila kwa kiingereza!!LOL!

kuna haja ya kurekebisha mifumo yetu
 
Back
Top Bottom