Kijarida cha "Kumekucha" => Ya Libya na PPF

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,461
39,928
Kijarida cha Kumekucha kimetoka kikiwa na habari za kina kuhusu kuanguka kwa Jiji la Tripoli na vile vile kuhusu sakata la kufukuzwa kwa watumishi wa PPF ambao wanadaiwa kuvujisha habari za ufisadi ndani ya Shirika hilo la Pensheni kwa Mashirika ya Umma.
 

Attachments

  • kumekucha3.jpg
    kumekucha3.jpg
    186.4 KB · Views: 170
  • kumekucha-3.pdf
    398.5 KB · Views: 505
Duh! Kana habari nzuri, hardcopy wap inapatikana kweli kumekucha... Gadaf out?
 
Duh! Kana habari nzuri, hardcopy wap inapatikana kweli kumekucha... Gadaf out?
Kwani Mkuu wewe huna printer ili ukiprint? Mimi huwa naviprint vingi na kuvigawa. Nawewe kama unaweza fanya ze semu utakuwa umechangia katika kuikomboa nchi hii kutoka kwenye wizi wa akina Lake Oils, ambao saa ya ukombozi ikifika tutawatia mikononi mwa sheria kama watoto wa Saadam, Gadafi na Mubarakh.
 
Du inasikitisha! Yaani mtu unafanya kazi miaka mitatu halafu unapata marupurupu na mafao kuliko yule mfanyakazi aliyechangia PPF kwa miaka 20? Kwanza aliyetengeneza scheme hiyo ya mafao ni nani na alizingatia nini? Scheme kama hizo zinatakiwa zitengenezwe na professionals wa masuala ya rasiliamali watu kwa kuangalia pia best practises. Kwa kweli hiyo formular yao ni ya Kifisadi kabisa na wala haina maana kwa watanzania wanachama wa PPF.
 
Kweli sasa kutakucha kwa wote kwa mtindo huu kama kijarida kinavyosema katika kauli mbiu yake. Atakayelala hana tofauti na ile katuni ya kajamaa kalikoshindwa kulivua Gamba Jikobe, maana limepitiliza umbo la kawaida la KOBE

Salute
 
Mwanzoni lengo letu lilikuwa kuliamsha taifa lakini sasa ni katika kuhakikisha kuwa watu hawalali tena. Kwani, mtu kulala na kupitiliza mara ya kwanza yaweza kudhaniwa ni bahati mbaya lakini kulala mara ya pili ni kutokujali. Well.. we should care..
 
Hawa wafanyakazi wa PPF waende tu mahakamani, aka CMA or Commission for Mediation and Arbitration. Hii ni unfair termination
 
Duh! Kana habari nzuri, hardcopy wap inapatikana kweli kumekucha... Gadaf out?

Hhahhaha

hardcopy inapatikana uki print hiyo soft copy? So ni wewe tu Unaweza kuamua kutoa hata hard copy 1000. Ila usifanye Ufisadi wa kuuza teh teh teh
 
Unajua watu walilalamikia sana suala la Ephraim Mrema kule TANROADS hadi bungeni likazungumzwa. Ilituchukua miaka karibu mitatu kwa waliolala kuamka.
 
Hapo ndo utajua hata ukoloni wa mwanzo uliingia vivyo hivyo kama wa Tripoli, harafu cnn na bbc za wakati huo zikaandika historia eti ya kwamba ma babu zetu walibadirishana kwa kupewa vioo na shanga.

Kuongoza nchi za kiafrika kutoka ktk umasikini kwenda ktk aghalabu hali murua si rahisi, and it is pretty much impossible unless otherwise.
 
12 Reactions
Reply
Back
Top Bottom