Kijana wa mtaani asiye na kazi anakutaka kimapenzi...

Mtambuzi

Platinum Member
Oct 29, 2008
8,810
15,398
gender-roles2.jpeg

Leo nataka kufanya utafiti mdogo kwa akina dada ambao hawajaolewa. Swali langu ni hili:

Kwa mfano una elimu ya ngazi ya shahada na unafanya kazi nzuri yenye mshahara na marupurupu si haba, halafu inatokea mvulana wa mtaani ambaye hana kazi lakini ana elimu ya wastani ukilinganisha na ya kwako anakuomba uwe na uhusiano naye kimapenzi na anakuahidi kwamba lengo lake si kukuchezea bali kukuoa kama mkikubaliana…

Je utakuwa tayari kuingia katika uhusiano huo?
 
Haya naomba kina dada mfunguke maana siku hizi mmecharuka kutafuta elimu mpaka tunaogopa kuwasogelea.......
Kwa kujibu swali hilo huenda wale vijana ambao walikimbia umande watapata ujasiri wa kuwasogelea..........................
 
mmh!.............mimi siyo mdada nilyeko mawindoni ila naomba niseme tu ambacho ni angalizo kwa wakaka wasio kuwa na ajira. jamani kuolewa na mdada mwenye kazi halafu wewe jobless ni kudhalilisha sana utu wako manake binti anaweza asikunyanyapae ila wewe mwenywe ukajinyanyapaa.
 
What?Kujidhalilisha? sijakuelewa,hebu rudi ufafanue!
 
Kidato cha nne my dear

We babu wewe sasa hapa unataka waje waanze kukudanganya tu wakisema wanatukataa wakati tunaselebuka nao tu ila kiukweli ndoa ndio huwa wanatukatalia wakidai kuwa hatuna fyucha,lakini kwenye baikoko ni mwendo mdundo tu....
 
Mi jamani nilishakuwa na mahusiano ya namna hiyo kwa kweli SITARUDIA TENA.. Huyo mkaka alikuwa anajishtukia sana japokuwa yeye alikuwa na kazi sema ndio vile elimu form four.. Uuuwi wivu na kutokujiamini nikimwambia tuu nasafiri kikazi basi ananuna balaaa kisa, eti nitatembea na wasomi wenzangu..! Kwa kweli yalinishinda mengi tuu, unakuta hata ki maongezi ham cope... Ni kazi saaaaaaaaaana!
 
kutokuwa na kazi si hoja
hoja kama ni mtu mwenye mwamko, dira, dhamira na mwelekeo wa kutafuta maendeleo yake binafsi na yapamoja.

Nikikumbuka where I came from, sioni kwa nini nimdharau mwanamme kisa yuko chini.

Mwanamme akijitambua na akajikubali ana akaamua kuwa mwanamme regardless ya kuwa hana pesa kwa wakati huo, well and good, and welcome on board.

Kuna watu wana akili na waelewa ila hajapata nafasi ya kutoka tu.
 
Ametuaibisha sana WANAUME huyo.Hivi kwanini unashindwa kuwa MWANAUME?Aaaagggrrrr!!!!
 
gender-roles2.jpeg

Leo nataka kufanya utafiti mdogo kwa akina dada ambao hawajaolewa. Swali langu ni hili:

Kwa mfano una elimu ya ngazi ya shahada na unafanya kazi nzuri yenye mshahara na marupurupu si haba, halafu inatokea mvulana wa mtaani ambaye hana kazi lakini ana elimu ya wastani ukilinganisha na ya kwako anakuomba uwe na uhusiano naye kimapenzi na anakuahidi kwamba lengo lake si kukuchezea bali kukuoa kama mkikubaliana….

Je utakuwa tayari kuingia katika uhusiano huo……………………?

Ina maana hili swali wanajibu ambao hawajaolewa tu????????Kama wote tunahusika ngoja niendelee...Uhusiano ni mapenzi na malengo...Naamini kila mdada anapotafuta mahusiano huwa anakuwa na malengo yake maalumu na sifa anazotaka kwa huyo kaka.Hivo Kama sifa zinajitosheleza then WHY NOT???
 
kutokuwa na kazi si hoja
hoja kama ni mtu mwenye mwamko, dira, dhamira na mwelekeo wa kutafuta maendeleo yake binafsi na yapamoja.

Nikikumbuka where I came from, sioni kwa nini nimdharau mwanamme kisa yuko chini.

Mwanamme akijitambua na akajikubali ana akaamua kuwa mwanamme regardless ya kuwa hana pesa kwa wakati huo, well and good, and welcome on board.

Kuna watu wana akili na waelewa ila hajapata nafasi ya kutoka tu.

u said it all!!
 
nilivyokuwa mdogo nilikuwa nasoma hadithi za binti matawi anapendana na kijana lofa!! ni hadithi tuu. kitu hiki ni kigumu sana kutokea katika dunia hii, kama gap ni kubwa lazima mmoja atakuwa na inferiority complex wakati mwingine atajiona ameshuka standard.
 
mmh!.............mimi siyo mdada nilyeko mawindoni ila naomba niseme tu ambacho ni angalizo kwa wakaka wasio kuwa na ajira. jamani kuolewa na mdada mwenye kazi halafu wewe jobless ni kudhalilisha sana utu wako manake binti anaweza asikunyanyapae ila wewe mwenywe ukajinyanyapaa.

gfsonwin aksante, mimi ni mmoja wa wadada ambao sikuwa nikiamini katika tofauti za kipato na elimu lakini kwa somo nililolipata kwa kaka yangu, I concur with you gfsonwin
 
Mtambuzi mbona umekomaa sana na WENYE KASORO aisee!! Angalia usije ukajenga unyanyapaa wa thread zako kwa baadhi ya wasomaji.
Naona majibu ya wadada wote yanakazia KUUA KABISA DHANA YA ASILI YA UPENDO.
Nakubali sasa kuwa kuna mambo ambayo nimeyaona miaka 10 iliyopita, ambayo sitakaa niyaone tena hadi niimbiwe "Si mbali...karibu"!
 
He asikwambie mtu ni wakorofi mbaya yani wana infiriority ya kufa mtu.To say few rafiki zangu wenye shahada kichapo wanachopata toka kwa waume zao dploma holder sitaki kusema yani huwa wakipigwa hawaji kazini siku mbili akija amivimba uso wote tena huwa wanapigwa usoni tu.du tisa kumi mie bwana nilikuwa namkaka ye form 4 me degree mfanyabiashara jamani sitaki kufikiria yule mkaka alivyokuwa mkorofi siku moja karibu anipige airpot kisa nilimsalimu mwanaume classmet eti ye akanisubiri.Raha iko apa baada ya kujua anacheat nilimuacha kama kawaida ya sizitaki mbichi hizi akanimwagia mitusitangu hapo sikuta kusikia la basi imepita miaka 3 sasa eti anataka kunioa nimsamehe alikuwa anafurahia ninavyompenda.hahaha na najua kupenda na nilimpenda kweli lakini nasema kulliko niolewe na mwanaume mwenye elimu ndogo sana cjui God kwows
 
Back
Top Bottom