JacksonMichael
JF-Expert Member
- Mar 22, 2012
- 339
- 61
Peoples power yamtokea puani mwanachama:
KIJANA Aludo Sanga (28) mkazi wa kitongoji cha Nelo Kiloleni katika mji mdogo wa Tunduma wilayani Mbozi, amefikishwa katika mahakama ya wilaya kwa kosa la kutishia kumdhuru Waziri wa Mambo ya Ndani, Shamsi Vuai Nahodha.
Mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya wilaya, Rahim Mushi, Mwendesha Mashtaka, John Mazwile alieleza kuwa, kijana huyo alitenda kosa hilo Februari 3 mwaka huu, majira
ya saa 3:50 asubuhi maeneo ya Mwangaza Hotel mjini Tunduma wakati Waziri Nahodha katika ziara ya kiserikali.
Mazwile alisema kabla hajatimiza azma yake ya kuudhuru msafara wa waziri huyo, mshtakiwa alizuiwa na Vijana wa ulinzi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), maarufu kama Green Guard.
Alisema wakati hayo yakitokea mshitakiwa huyo pia alikuwa ameshikilia kipande cha mti na bendera ndogo ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
Alisema kosa hilo ni kinyume cha sheria kifungu cha 89 (a) na (b), cha marekebisho ya sheria mwaka 2002 cha kanuni ya adhabu.
HabariLeo | Kizimbani kwa kutishia kumdhuru Waziri Nahodha