Kijana aukata uume wake kuepuka usumbufu wa wanawake huko Tabora...!!

Money Stunna

JF-Expert Member
Aug 9, 2011
13,054
6,281


Ayubu Mnazi Alphonce(24) ni kijana ambaye amelazwa katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Tabora Kitete akipatiwa matibabu baada ya kuamua kuukata uume wake kwa kutumia wembe mpya ili kuepukana na usumbufu anaoupata kutoka kwa wanawake ambao amekuwa nao kimapenzi...








Imeelezwa kuwa baada ya kutokea mfarakano baina yake na mwanamke mmoja ambaye jina lake halijafahamika,Ayoub aliamua kuingia ndani na kuukata uume wake kwa kutumia wembe mkali na kisha kuutupa nje..








Taarifa kutoka Jeshi la Polisi zinaeleza kuwa baba mzazi wa Ayubu baada ya kubaini kuwa mtoto wake alikuwa amejifungia chumbani kwa muda mrefu, aliamua kumgongea mlango na alipopata fursa ya kuingia ndani ndipo alipogundua ukweli juu ya jambo hilo na hivyo kumpeleka Ayubu Kituo kikubwa cha Polisi Tabora ambapo jalada la kesi ya kujidhuru lilifunguliwa.








Hata hivyo hali ya Ayubu kwasasa inaendelea vizuri licha ya kuwa amejikata na kubakisha kipande cha sentimeta 5 huku akisubiriwa kufikishwa mahakamani kwa kutenda kosa hilo la kujidhuru mwenyewe pasipo sababu za msingi.
 
Duh!
Nampa poyeeeee!
Ayayayayayayaaa!
Kasepesha kilungu!
Poyeeee!
Haki ya mama mi bora mtu anikate tu nywele na kucha!!!
Aaka! Kilungu changu naulia mbu mwenzenu Mwee!
 
ha haaa, short call kwani inahitaji hata mm kadhaa best? tundu tu linatosha, lol!

Kwa matukio ya karibuni naanza kuamini kuwa wanawake tu wavumilivu sana,hivi wanavyotutenda tungekuwa tunatoa maamuzi ya ajabu kama yao sijui tungekuwa wapi kwa sasa!
Kweli mtenda akitendewa .................;.
 
Ingekuwa kokoleo lake lina perfomance nzuri sidhani kama angelirengeta. Inawezekana lilikuwa kama urembo tu ndo maana akaamua kulikataa tu ili kuEpuka kufedheheshwa. Heri lawama kuliko fedheha
 
Kwa matukio ya karibuni naanza kuamini kuwa wanawake tu wavumilivu sana,hivi wanavyotutenda tungekuwa tunatoa maamuzi ya ajabu kama yao sijui tungekuwa wapi kwa sasa!
Kweli mtenda akitendewa .................;.
umeona eeehhh!
hawa wenzetu uvumilivu sifuri.
nakumbuka nilipokuwa labor ya mtoto wa pili nilikuwa na daktari mwanaume. akaniambia aisee nyie wanawake nawaheshimu sana. kwa haya mauchungu mnayoyapata huku ingekuwa wanaume pia tunazaa hakuna mwanaume angezaa mtoto wa pili. wenzetu hawataki maumivu kabisaaaa
 
Ingekuwa kokoleo lake lina perfomance nzuri sidhani kama angelirengeta. Inawezekana lilikuwa kama urembo tu ndo maana akaamua kulikataa tu ili kuEpuka kufedheheshwa. Heri lawama kuliko fedheha
sasa mbona kabakiza sentimita 5? angetoa lote, lol!
 
Acheni uongo nyie ukikata uume lazima ufe unafikili mchezo nn! hata kicha mwenyewe hawezi kujikata uume.Don't pray with penis, it hasn't spear
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom