Kijana apiga mbizi kutekeleza agizo la Magufuli!

Nauli ya 200/- si kigezo cha kupiga mbizi eti kwa kushindwa kulipa. Mbona ubungo Terminal tunalipa 200/- ili uvuke geti kwa miguu yako. Wasafiri na wanawaunga mkono tutafakari zaidi!
Usichanganye vitu vya lazima na visvyo vya lazima. Huwezi kulinganisha waingiaji wa stand ya ubungo na watumiaji wa kivuko. Kama unaona hamna tofauti basi tuishauri serikali iweke ushuru kwa kila mtumiaji wa barabara ili tuiongezee serikali uwezo wa kuimarisha na kusimamia barabara.
 
Huyu mtu kwa haraka haraka ni kwamba ametaka kutolewa kwenye vyombo vya habari kama JF na kadhalika na kwamba alitaka sisi tujue kwamba anaweza kuogelea lakini si kwamba kukosa sh200 ndo kumemfanya aongelee hadi ng'ambo kama hujui kuogelea kama unabisha kajaribu wewe uliyetoa thret hii kama utaweza, vitu vingine havina umuhimu wowote kuvileta humu watu mnaonekana kama hamna kazi za kufanya.

Hata hivyo siku zote naichukia siasa sana kwa maana kwenye siasa ukichukiwa na wanasiasa wenzio au chama chako kikichukiwa basi hakuna utakalosema wananchi wakaliona la maana, soma kwa makini hapa ili uelewe ninachotaka kusema, Mimi nilimshangaa sana Chapombe John waliposema alimshangaa Mh. Mnyika John, Chapombe alisema alitegemea Mnyika apeleke proposal za jinsi ya kutatua matatizo ya foleni wakat yryr mwenyewe alitakiwa kutoa pendekezo lake la kuongeza nauli kwa Project yake ya Boat kutoka Bagamoyo hadi Dar ambapo kungekua na vitua kadhaa kabla ya kufika Bagamoyo.
Aliteakiwa kuonyesha Presentation yake kwa wananchi na kuchukua maoni yao harafu ndo kupandisha nauli kungefuata sidhani kama wananchi wangempinga, maana mantiki yake inaleta maana sana kuondoa siasa, Kupanda kwa nauli ya kivuko sioni tatizo ila tatizo ni kutangazwa na mwanasiasa ambae chama chake kwa kiasi kikubwa kimepoteza mwelekeo na imani kwa Wananchi wake na hcho ndo chanzo cha marumbano yanayoendelea sasa.
Ngoja nichukulie kwa wanaokaa Ubungo ambako nimeambiwa kuna maendeleo ambayo yamesababishwa na Mh. Mnyika, ukiwa Posta na unataka kurudi Ubungo wewe mwenyewe wala bila tangazo la Chapombe unaenda akiba unapanda gari kwa shs 200 hadi posta na kisha unatoa nauli nyingine ya kwenda ubungo mbona hamlalamiki? Ukiwa Posta na unataka kwenda Gongo la Mboto ni hvyo hvyo, kipi cha ajabu ambacho Chapombe kakifanya? huwezi kupata kingine ila jambo limechukuliwa kisiasa na aliyetangaza chama chake ndo kama hvyo tena,
Ok angalia tena Ubungo terminal, kwa miguu yako mwenyewe unaingia kwa sh200 unapewa ticket na ukipoteza ticket ukiwa bado hujatoka utatozwa sh 200 tena nani alishawahi kulalamika? au watu wa Kigamboni hawatumii Ubungo Terminal kwamba hawajui haya? Yaani Watanzania bana mara nyingi tumekua kigeu geu na hatuna misimamo ya kweli kama mtu anafanya jambo la maendeleo hata kama ni wa chama gani asapotiwe huo ndio Ujamaa,
Mara nyingi nimeona threats ambazo zinatolewa na wadau mbali mbali kama ni za chama tawala zitatolewa lugha ngumu mpaka basi hii ni dalili tosha kwamba chama tawala kimepoteza mwelekeo kaabisa na imani kwa wananchi wake ila ningeona wana JF wamaana sana na watu makini kama wangekua wanachukua muda kuangalia mambo kabla hawajasema chochote na ikumbukwe pia Watanzania sisi ni wavivu saaana wa kujituma na si wabunifu ila ni hodali wa kulaaumu na kutoa visingizio.

Maelezo mareeeeeefu substance zero
 
Nikweli hapa nilipo kichwa kinaniuma sana, kwanini tumemkamata?? Yani najiuliza na kila mmoja wetu hapa anajiuliza kwanini tumemkamata? Lakini viongozi wetu wanasema afikishwe mbele ya sheria!
Ndo maana Mwigamba alisema msitii kila amri maana hapo suala liko wazi kuwa agizo katoa waziri na raia katekeleza sas nyie mnadhani huyo mtamshinda kwa sheria ipi au mnataka muoneshe mnavyoamua maamuzi ya ovyo.
 
huyo atafikishwa mahakamani kwa kuwa kesi yake inafanana sana na mtu aliyetaka kujinyonga ikashindikana,so dogo atashitakiwa kwa kosa la kutaka kujitoa uhai.hakuna lingine na hii itatoa fundisho kwa wale wote waliokuwa na nia kama yake,hahahahahaha

kazi kwelikweli tz
Kama ni hivyo basi magufuli nae jela inamwita maana nae atashitakiwa kwa kumnyonga mtu.
 
Nikweli hapa nilipo kichwa kinaniuma sana, kwanini tumemkamata??Yani najiuliza na kila mmoja wetu hapa anajiuliza kwanini tumemkamata? Lakini viongozi wetu wanasema afikishwe mbele ya sheria!
Kama wewe ni askari kamili unamsimamo gani wewe kama wewe, huoni kwamba Mwigamba alikuwa sahihi alipowaambia.."kuwa askari kunakuondolea uwezo wa kufikiri na badala yake unafikiriwa na watu wengine".
Mkufunzi: Nyinyi makruta mbona wote hamkuja na majembe?
Makruta: Ndiyo afande!
Mkufunzi: Hamkuambiwa makao makuu ya jeshi kwamba lazima mje na majembe?
Makruta: Ndiyo afande!
Mkufunzi: Kwa hiyo kwa kuwa hamkuambiwa na nyinyi hamkuyabeba?
Makruta: Ndiyo afande!
Mkufunzi: Wote ni wapumbavu pamoja na mama zenu waliowazaa.
Makruta: Ndiyo afande
 
Teheehee hiro ni tusi kwa gesi retu ra porisi! Nitakuaresti sasa hivi ovaaa!!
Kwa hiyo hutaki kuambiwa ukweli kuwa polisi wako chini sana kulinganisha na sector zingine! kama ni uongo mbona wanafanya mambo mengi bila hata kuangalia kama sheria inasemaje?
 
Atalaumiwa Magufuli kwa kuikosesha serikali mapato. Hapo ni kichwa kimoja kimepotea hivi hivi. Sasa imagine na wengine waamue kupiga mbizi. Ile pantoni si itabidi iwekwe tuu juu ya mawe?
Nadhani wanapata kiburi kwasababu hamna ushindani wa kibiashara, kungekua na pantoni la mtu binafsi pale mbona wangekua wapole. Maana watu wangehamia huko hata kama kuna foleni.
 
Nadhani wanapata kiburi kwasababu hamna ushindani wa kibiashara, kungekua na pantoni la mtu binafsi pale mbona wangekua wapole. Maana watu wangehamia huko hata kama kuna foleni.
Upo lizzy tz hii au ughaibuni?
 
Leo nitapiga Mbizi kwenda upande wa Kigamboni Katika harakati za kumpinga magufuli na serikali lege lege! shs 200 si tatizo kwangu
 
Hivi mtu anapoogelea bila nguo kuvuka ng'ambo ya pili, akifika huko ataenda uchi hadi kwao? Nguo si zinakuwa zimebaki huko alikotoka?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom