Kiingereza kinampa shida mkuu wa mkoa Arusha, aogopa mikutano ya kimataifa

Imebainika kuwa Mkuu wa mkoa wa Arusha, Magessa Mulongo, anakiogopa sana kiingerezakiasi cha kujitahidi kuiepuka mikutano mingi ya kimataifa inayofanyika mjini Arusha.

Mkuu huyo amekuwa akipata shida sana kusoma speech alizoandikiwa kwa lugha hiyo ngeni katika baadhi ya mikutano aliyoalikwa kuifungua na hivi sasa ameamua kuikacha jumla.

Hakuna dhambi kwa kiongozi kutojua lugha ya malkia lakini mtu akipewa eneo la kimataifa kama Arusha kigezo hicho kwa kweli ni muhimu maana kuna taasisi nyingi za kigeni hapa hii ikiwa ni pamoja na jiji kuwa mwenyeji wa mikutano mingi ya kimataifa.

Lakini watu wake wa karibu wanasema suala si kiingereza tu. Hata kusoma speech ya kiswahili kwa mtiririko ulio tulia huwa ni taabu kwake.

Hata hivyo Mulongo ambaye inadaiwa aliletwa mkoani hapa maalum kuja kumdhibiti mbunge wa Monduli anatekeleza jukumu hili kwa ufasaha ila kama atashinda ndicho hakijulikani.

Ki utendaji pia Mulongo ni mzuri kwani amefanikiwa kuwatimua maofisa wala rushwa na watendaji hovyo katika taasisi na ofisi za umma mkoani hapa. Hii ni pamoja na madai kuwa amekuwa akifanya hivyo kisiasa zaidi.

Wewe nini muongo sana! Kama umehadithiwa basi ujue umedanganywa.Mkuu huyu yuko njema kwenye lugha ya malkia na ukitaka kujua ni pale anapovunja jokes za hapa na pale wakati akisoma speech lol!
 
\mbona viongozi wakuu wengi wa China hawajui hata how are you bana ,muhimu ni utendaji wa kazi,kiingereza si kigezo,huko Irani wale wanasayansi wa nyukilia hawajui kiingereza lakini mambo wanayoyafanya hayana mfano.kiingereza ni lugha tu wajemeni
 
Kuna mmoja alikuwa anaitwa Said kalembo akiongea kingereza unaweza kumchapa vibao.huyu magesa malongo nliwahi mkuta Bagamoyo kule travellor akiongea kingereza haeleweki hana lafudhi nzuri kwa lugha zote mbili .
 
Rais Ahamednajad, waziri mkuu Putin, Hugo Chavez na wengine wengi hawajui kiinglish. Kimsingi kujua au kutojua kiingilish si big deal. Kama anaweza kuchapa mzigo heri yake kuliko maprofesa kama Abdulaye Wade au madaktari kama Daud Balali walioleta balaa. Muulize huyo profesa wa afya ana nini zaidi ya yes yes nyingi lakini kazi hamnei.
 
Bora achape kazi tu ila Kiingereza, inapobidi naona Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Bi Mercy Sila anamsaidia na kudai "RC has other commitments."
 
Wewe nini muongo sana! Kama umehadithiwa basi ujue umedanganywa.Mkuu huyu yuko njema kwenye lugha ya malkia na ukitaka kujua ni pale anapovunja jokes za hapa na pale wakati akisoma speech lol!

Tausi

avatar23787_25.gif
 
Back
Top Bottom