mpinga shetani
JF-Expert Member
- Nov 22, 2010
- 3,236
- 954
Imebainika kuwa Mkuu wa mkoa wa Arusha, Magessa Mulongo, anakiogopa sana kiingereza kiasi cha kujitahidi kuiepuka mikutano mingi ya kimataifa inayofanyika mjini Arusha.
Mkuu huyo amekuwa akipata shida sana kusoma speech alizoandikiwa kwa lugha hiyo ngeni katika baadhi ya mikutano aliyoalikwa kuifungua na hivi sasa ameamua kuikacha jumla.
Hakuna dhambi kwa kiongozi kutojua lugha ya malkia lakini mtu akipewa eneo la kimataifa kama Arusha kigezo hicho kwa kweli ni muhimu maana kuna taasisi nyingi za kigeni hapa hii ikiwa ni pamoja na jiji kuwa mwenyeji wa mikutano mingi ya kimataifa.
Lakini watu wake wa karibu wanasema suala si kiingereza tu. Hata kusoma speech ya kiswahili kwa mtiririko ulio tulia huwa ni taabu kwake.
Hata hivyo Mulongo ambaye inadaiwa aliletwa mkoani hapa maalum kuja kumdhibiti mbunge wa Monduli anatekeleza jukumu hili kwa ufasaha ila kama atashinda ndicho hakijulikani.
Ki utendaji pia Mulongo ni mzuri kwani amefanikiwa kuwatimua maofisa wala rushwa na watendaji hovyo katika taasisi na ofisi za umma mkoani hapa. Hii ni pamoja na madai kuwa amekuwa akifanya hivyo kisiasa zaidi.