Kiingereza cha kiTanzania

Hakuna shaka hapa. English yetu itakuja tu. Subiri tuwe na flooded graduates wa hizi academy za mara cambridge, sijue british system, wengine american system wengine, tanzania syllubus. Maana ukimpeleka mtoto kumwandikisha std one or nursery private primary schools in Tz utapata kichekesho. We are mixed up completely????!!!!!
 
Daaa!!!hapo umenipa mwanga maana nilijua ndugu ni jamaa yako,awe mtoto wa baba mdogo,mjomba au hata mliyetoka naye ukoo mmoja

Hivyo ulivyokuwa unajua awali ndivyo sahihi. Hata mtoto wa baba yako mdogo, mjombao ni nduguyo.
 
Mi nadhani kiingereza kitabaki kuwa "kiingereza" kinacho tofautisha ni matamshi na lafidhi ya watu wa Taifa husika. Kwani huwezi sema " watch-mosquito-watch = Sambusa" au " River ukamaanish mto wa kulalia". Hiyo itakuwa Swanglish ambayo tutaielewa sisi tu lakini kuhusu English "Kiingereza" kinachotumiwa dunia nzima kitabaki kuwa kiingereza tu.
 
Mi nadhani kiingereza kitabaki kuwa "kiingereza" kinacho tofautisha ni matamshi na lafidhi ya watu wa Taifa husika. Kwani huwezi sema " watch-mosquito-watch = Sambusa" au " River ukamaanish mto wa kulalia". Hiyo itakuwa Swanglish ambayo tutaielewa sisi tu lakini kuhusu English "Kiingereza" kinachotumiwa dunia nzima kitabaki kuwa kiingereza tu.

Hahahaa Mkulu Hofstede umenikumbusha mbali sana mambo ya 'Grandmother cry' =biblia,,'Katelephone don't smoke my river' =Kassim usiuvute mto(pillow) wangu,,'I waited you but where' =Nilikusubiri wee lakini wapi,,'You think the reason why' =unafikiri sababu ni kwa nini,,,au mambo ya Chonya wa Chilonwa(Riwaya ya Shida ya Ndyanao Balisidya) pale anaposema "if the police come tell him that Chonya of Chilonwa me take the girl to the hospital"...So tukitaka kuwa na kiingereza chetu waTz tutaelekea huku Wakulu...lol...
 

[ame="http://www.youtube.com/watch?v=c1rXdD7SxuY"]YouTube - Too Much Very Much[/ame]


 

Watanganyika nafikiri wameshaanza kutumia kizungu chao; Mfano ni jina la Ze Comedy.
 
Kiingereza cha kiTanzania

Wapendwa wana JF na wale wote wenye mapenzi mema na nchi yetu Tanzania; hapa ulimwenguni katika nchi zote zilizotawaliwa na mwingereza takriban kila moja ina kiingereza chake mfano kuna kiingereza cha Australia, Belize, Canada, Caribbean, Hong-Kong-S.A.R., India, Indonesia, Ireland, Jamaica, Malaysia, New-Zealand, Philippines, Nigeria, Singapore, South-Africa, Trinidad-&-Tobago, UK ,US, na Zimbabwe.

Ukifuatilia kwa makini kila nchi iliyotajwa hapo imeongeza au imepunguza au imebadili neno au herufi fulani kutoka kwenye kiingereza cha asili cha Uingereza.

Mfano Mwingereza anatumia neno POST CODE lakini mMarekani anatumia neno hilo hilo kama ZIP CODE

Kinachosikitisha ni kwamba sie waTanzania tunatumia either American English or British English.

Kuna maneno mengi ambayo wataalam wa lugha mnayafahamu (mie sio mtaalamu wa lugha bali ni Mchungaji) ambayo mnaweza kuyabainisha hapa ili tuweze kuwa na kiingereza chetu cha kiTanzania.

Mie nilikuwa ninapendekeza tuanzie hapa: - Badala ya kumuita baba mkubwa na/au baba mdogo UNCLE tuwe tunawaita ELDER FATHER na YOUNGER FATHER. Badala ya kumuita mama mkubwa na/au mama mdogo AUNT tuwe tunawaita ELDER MOTHER na YOUNGER MOTHER ... ... ... nakadhalika.

Naomba kuwasilisha.

Bwana Modest, kiingereza kinachoongewa na watanzania inategemea alipo mtu huyo.Kuna Kiswanglish ambacho ni cha wale wenye madaraka na wanasiasa wasiopenda kujieleza katika lugha ya asili ya kiswahili kwa nia ya kujionyesha tu.
Kuna pidgin english ya wale watu walio na elimu isiyo tosha lakini wanalazimika kuwasiliana kwa kiingereza.
Kuna kiingereza cha kuiga kabisa ambacho ni funky na kinapendwa na vijana na wanakipata kwenye hip hop etc
Kati ya viingereza vyote hivyo ni kiswanglish kinachoweza kusahihishwa kwa maana kiko katika mkondo wa matumizi ulio rasmi.
 
Mimi nadhani kwavile kiingereza siyo lugha yetu ni lugha ya mkoloni basi tukitumie kama mwenyewe mkoloni anavyokitumia na hayo madoido mengine yote basi tuyaweke kwenye lugha yetu yaani kiswahili.
 
Kazi ipo kujadili vya wenzetu. Nilidhani ingekuwa kheri tuakajadili Kiswahili cha Kinegeria, kIswahili cha Kongo na hata Tunisia.Tutafika tu
 
KIswahili chetu hatukiwezi tunataka kurukia kukibadilisha kiingereza cha wenzetu, ambacho hatukiwezi zaidi ya Kiswahili.
 
sasa haya ni yale ya mpiga tarumbeta unajuwa maana ya neno tarumbeta ???kazi kwako
 
[ame=http://www.liveleak.com/view?i=be6_1240308325]LiveLeak.com - Learning English is not always easy[/ame]
 
Kubadilika kwa lugha kunategemea na matumizi makuu ya hiyo lugha, ukifika nchi kama zimbabwe au nigeria utakuta kuna makabila tofauti lakini lugha ya mawasiliano kwa wote ni kiingereza kwa hiyo basi utakuta hicho kiingereza lazima kiaribike kufuatana na laaja ya wasemaji kwani wanakuwa wameathirika na mother tongue
hilo halipo kwa kiingereza tu, hata ukija kwenye kiswahili, nacho kinatofauti kwa sababu hizohizo na ndio maana kuna kiswahili cha comoro, congo,kenya, bara na pwani
 

Mkuu Max,

Nimeipenda sana hii. Lingekuwa jambo zuri kama wengi tungejua kuwa ili kujifunza lugha au kitu chochote tunahiji jitahada za ziada. Lakini wengi wetu tunachukulia vitu kirahisi sana. Baada ya kuharibiwa na walimu wa UPE na wale wa Vodavasta, ni wachache sana wanajaribu kufanya kama huyo jamaa anayesota kujifunza kizungu! Tunahitaji mkakati mpya wa kujikomboa katika uwezo wetu wa kutumia lugha, iwe kiswahili, kiingereza au Kijapani.
 
Natumai huko mahakamani, mahakimu na waendesha mashtaka huwa wanaandika maelezo kwa kiingereza.

Sentensi kama hii wataiandikaje? ........"nilitoka kwa baba mdongo na kuelekea kwa mjomba ambako nilikuta mauaji yametokea........"
 
Back
Top Bottom