Ladslaus Modest
JF-Expert Member
- Jun 27, 2008
- 635
- 20
Kiingereza cha kiTanzania
Wapendwa wana JF na wale wote wenye mapenzi mema na nchi yetu Tanzania; hapa ulimwenguni katika nchi zote zilizotawaliwa na mwingereza takriban kila moja ina kiingereza chake mfano kuna kiingereza cha Australia, Belize, Canada, Caribbean, Hong-Kong-S.A.R., India, Indonesia, Ireland, Jamaica, Malaysia, New-Zealand, Philippines, Nigeria, Singapore, South-Africa, Trinidad-&-Tobago, UK ,US, na Zimbabwe.
Ukifuatilia kwa makini kila nchi iliyotajwa hapo imeongeza au imepunguza au imebadili neno au herufi fulani kutoka kwenye kiingereza cha asili cha Uingereza.
Mfano Mwingereza anatumia neno POST CODE lakini mMarekani anatumia neno hilo hilo kama ZIP CODE
Kinachosikitisha ni kwamba sie waTanzania tunatumia either American English or British English.
Kuna maneno mengi ambayo wataalam wa lugha mnayafahamu (mie sio mtaalamu wa lugha bali ni Mchungaji) ambayo mnaweza kuyabainisha hapa ili tuweze kuwa na kiingereza chetu cha kiTanzania.
Mie nilikuwa ninapendekeza tuanzie hapa: - Badala ya kumuita baba mkubwa na/au baba mdogo UNCLE tuwe tunawaita ELDER FATHER na YOUNGER FATHER. Badala ya kumuita mama mkubwa na/au mama mdogo AUNT tuwe tunawaita ELDER MOTHER na YOUNGER MOTHER ... ... ... nakadhalika.
Naomba kuwasilisha.