Kiingereza bila pesa mfukoni ni sawa na makelele

Ok,Nashukuru kwa swali lako,Kuna msanii langa alishawahi flow hiyo line:

"SHukurani kwa nyerere alicheza utadhani pele,kuendeleza kiswahili,mikoani na mbele mbele,Tunamuendekeza mzungu wakati tuna shida tele,Kingeleza bila hela ni sawa na kupiga kelele"-LANGA
 
embu nitumie mdogo wangu huyu siku nyingi network ilikata nimemsikia kwenye redio kamrudia Mungu
kama kweli Mungu ambadilishe kikweliiii asirudie tena mambo yale..hii nimetumiwa na shemeji yangu nikajiuliza kwasababu anapesa ajasoma ananteta ama sikuelewa embu niletee kwenu
 
Kingereza ni lugha tu kama zilivyo lugha nyingine. Tatizo ni kwamba wapo waliojijengea ya kuwa anaeongea kiingereza ni msomi, na lazima atakuwa na hela ambapo ni ujinga mtupu!!
 
Kingereza ni lugha tu kama zilivyo lugha nyingine. Tatizo ni kwamba wapo waliojijengea ya kuwa anaeongea kiingereza ni msomi, na lazima atakuwa na hela ambapo ni ujinga mtupu!!

Duh!! Kweli tupu kwani kuna wazungu wanaongea hiyo lugha lakini hawakwenda shule hata kukiandika issue. Wazaramo wanaongea kiswahili laini je wamesoma na hela wanazo?? ni mawazo potofu.
 
Ni kweli mkuu. Hiyo ni sawa na mtu kuwa na para kuubwa bila pesa. Samahani kwa wenye vipara, kwa mtazamo wangu mtu kuwa na kipara bila pesa hilo litakuwa ni kovu tu.
 
Watu wanaongea kingereza wanaishi kiswahili! Japan ukija na english yako tafuta mkalimani na mwenyewe anaenglish ya kuungaunga!
 
msidanganyane hapa. Kingereza ni moja ya lugha za kimataifa. Watanzania tumeshindwa kuachieve mambo mengi sababu ya kingereza. Watanzania wengi wanapoenda kwenye mikutano na semina za kimataifa wanageuka mabubu kwaajili ya lugha alafu wakitoka wanaanza kujilaumu
 
pili kama wewe ni maskini lazima ujifunze lugha ya mtoa msaada ambao wengi wanatumia kingereza. As long as we are poor we have to understand the lg of the master
 
Ok,Nashukuru kwa swali lako,Kuna msanii langa alishawahi flow hiyo line:

"SHukurani kwa nyerere alicheza utadhani pele,kuendeleza kiswahili,mikoani na mbele mbele,Tunamuendekeza mzungu wakati tuna shida tele,Kingeleza bila hela ni sawa na kupiga kelele"-LANGA

Msanii huyu angemsoma Nyerere kidogo tu, angegundua kwamba kumuweka Nyerere katika sentensi inayoweka hela mbele ni "mental masturbation".

Angesoma kidogo tu historia ya lugha angegundua kwamba lugha zote ni kelele.

Hana kipya cha kutuambia.
 
Ok,Nashukuru kwa swali lako,Kuna msanii langa alishawahi flow hiyo line:<br />
<br />
&quot;SHukurani kwa nyerere alicheza utadhani pele,kuendeleza kiswahili,mikoani na mbele mbele,Tunamuendekeza mzungu wakati tuna shida tele,Kingeleza bila hela ni sawa na kupiga kelele&quot;-LANGA
<br />
<br />
hii ni enzi za wakilisha enhee..
 
ni ka-ugonjwa kametuadhiri hata nyerere aliwahi kusema mtu akilizungumzia jambo kwa kiingereza hata kama bovu tutalisifia si limesemwa kwa kiingereza
 
Duh!! Kweli tupu kwani kuna wazungu wanaongea hiyo lugha lakini hawakwenda shule hata kukiandika issue. Wazaramo wanaongea kiswahili laini je wamesoma na hela wanazo?? ni mawazo potofu.

angalia Familia ya mkulu isikusikie
 
Sioni uhusianao wowote kati ya lugha na hela. Kuna wenzetu wako Uingereza na Marekani na wanaongea Kiingereza kutokana na mazingira wanamoishi. Sidhani kama wote wanazo pesa kwa vile wanongea Kiingereza. Wengune ni 'choka mbaya' hasa. Halafu mafanikio siyo kuwa na pesa peke yake. Ukitimiza malengo yako na nafsi yako ikaridhika umefanikiwa hata kama haikuletei pesa. Kwa mfano, mzazi akiwasomesha watoto wake mpaka kiwango cha Chuo Kikuu anaweza kuridhika kuwa amefanikiwa. Lengo lake siyo pesa bali kuwapa watoto wake fursa za mafanikio katika maisha yao.
 
Back
Top Bottom