Kiingereza aibu kwa mawaziri wa JK

Afadhali huyo kuna siku Mkuu wa Kaya alikuwa anafanyiwa interview na Clouds Fm siku ya birthday yake. Basi msikilizaji akapiga simu na kum-wish ''happy birthday Mr. President'' jamaa akajibu ''oooh! The same to you''

Hiyo ilikuwa kali kuliko.
 
Ingawa mimi si mshabiki wa hawa wanasiasa nadhani hapa mnamuonea bure Ngeleja! Kiingereza chake ni kizuri na kinasikika kabisa hususan ukitilia maanani kuwa kajifunzia ukubwani na pia ni lugha yake ya tatu au hata ya nne!

Ndugu Ngeleja hapa anazungumza Kiingereza vizuri kuliko viongozi wetu wengi wanavyokizungumza hiki kiswahili chetu ambacho wanakizungumza kila siku na kuna sehemu nyingi za kujifunzia au kuuliza kama huna uhakika na neno linavyotamkwa au kuandikwa! Viongozi wengi tu (na pia hapa JF) wanashindwa kutofatisha L na R, A na H nk. Kuna viongozi wakiongea kiswahili unatamani kuwaambia wakae kimya wanavyokiboronga!
 
Hukuwaii kuleta mada kesho unasema Tuna matatizo ya mgao wa umeme sababu ngereja hajui kingereza
Ndio maana yake. Matatizo ya umeme yanachangiwa kwa viongozi na watendaji kutojua Kiingereza kwa sababu wanaingizwa mikenge kwenye mikataba na majadiliano ya mikataba ambayo haiendeshwi kisukuma.
 
Kwel bado tumetawaliwa. Wazir kutojua kiingereza anaonekana kama ametenda dhamb. Mzungu asipojua kiswahil je?. Acha ujinga Ngeleja na wewe tumia Kiswahili.

Na siyo kweli kuwa hawajui kiingereza.... tatizo ni kwa vile hawana 'accent" ya kimarekani au kiingereza lol! Wakisikia waarabu au wafaransa wanaongea kiingereza sijui wanapata hisia gani lol! Maana hiyo accent unaweza hata usielewe wanasema lugha gani!
 
Siyo lugha yake wala simshangai.mbona hamuwashanga waingereza wanapokosea kiswahili?

Kwanini tunapenda kujustify kiasi hiki? Matokeo yake kiingereza kitaendelea kuwa tatizo siku zote mpaka tutakapokubali kwamba ni tatizo na tunatakiwa kulifanyia kazi. Hao wazungu Fe hawakisomi kiswahili huko kwao kama sisi tunavyokisoma kiingereza, seconday mpaka University. By the way Ngeleja alisoma sheria so matarajio ya wengi alipaswa kuwa fit kwenye lugha lakini patupu. Lakini kibaya zaidi hata kiswahili huyu jamaa kinampa shida pia, rejea ile hutuma yake bungeni wakati wa mgomo wa wauza mafuta (natamani iwepo mtandaoni) kwani jamaa alikivunja kiswahili kupita maelezo, mfano kwenye dha kwake ilikuwa za n.k. At first nilidhani alikuwa Masebu, nilipokuja kutambua kwamba ni Ngeleja oh my God niliishiwa nguvu. Kwa maneno mengine waziri wetu lugha anayoijua kwa ufasaha may be ni kisukuma pekee-this is real bad wajameni.
 
Leo nimempata Ngeleja akisoma hotuba, aibu. embu soma zikiza hii.. the the the the..... Lawrence Masha (waziri mambo ya ndani) yuko juu sana kwenye kiingereza

5. Opening speaker Minister William Ngeleja part 2 (International Energy Conference 2009) - YouTube
Ingilizi ya Tanzania bado kabisa aliyekuwa anajuwa Kiingerza Perfect katika Tanzania yetu ni Baba wa Taifa Mwalim Julius Nyerere waliobakia wanabahatisha na hicho Kiingereza cha machungwa hebu msikilize Baba wa Taifa anavyozungumza kiingereza

 
Last edited by a moderator:
Achaani ujinga usilinganishe Kiingereza na kiswahili basi kama ni hivyo ukitoka Usukumani huna haja ya kijua kiswahili ongea tu kisukuma, Kuongea lugha nyingi kunakuongezea usahi na upana wa mawasiliano na kingereza ni lugha kubwa sana so ni plus kuijua zaidi ushamba huu huu ndio unatuweka hapa tulivyo, si ha hichi kinafaa tu, tunajikuta kama kisiwa.
 
am hungly. Feer rike eating lice with river. see you tomollow
 
kíingereza cha nini? Ningeshangaa kama hajuwi kiswahi na kisukuma.. Msituletee vigezo hafifu
 
Ingilizi ya Tanzania bado kabisa aliyekuwa anajuwa Kiingerza Perfect katika Tanzania yetu ni Baba wa Taifa Mwalim Julius Nyerere waliobakia wanabahatisha na hicho Kiingereza cha machungwa hebu msikilize Baba wa Taifa anavyozungumza kiingereza



weka na link ya Mkapa akiitema lugha ya Malkia!
 
Last edited by a moderator:
Lugha yoyote kama huitumii kwa mawasiliano ya kawaida inakuwa ngumu kuitawala.
Kizungu Tanzania kinatumiwa kwenye taaluma tu.
Not easy to be fluent if you don't use it in normal conversation.
By the way, Tanzania utaongea kizungu na nani?
Hata watoto wanaosoma english medium schools, wakirudi nyumbani wanatumia Kiswahili.
Tanzania is not an English speaking nation per se.
It is a predominantly Swahili speaking one.
 
serikali yetu ndio inasababisha yote haya inatakiwa ichague moja lugha ya kiingereza itumike mashuleni au kiswahili mimi simshangai ngeleja ingawa inachekesha lakini watanzania tulio wengi kiingeleza ni kigumu kwetu kwa sababu sio lugha yetu watanzania lugha yetu ni kiswahili, hii lugha inatufanya tusijiamini tunapotakiwa kuongea mbele ya watu kwa sababu wanaokusikiliza wanajifanya wanajua zaidi kuliko wewe, inabidi tubadilike jamani kiingeleza sio lugha yetu watanzani tunalazimishwa
 
Back
Top Bottom