Kigwangalla Kimyaaaa! Usicheze na CCM Bana!

Le Grand Alexei

Senior Member
Nov 9, 2011
116
83
Hivi karibuni mbunge wa Nzega (CCM), Dkt. Hamisi Kigwangalla amekuwa kwenye kurasa za mbele za magazeti mbalimbali na mitandao ya kijamii kuhusiana na misimamo yake madhubuti isiyoyumba iliyopelekea kutaka kufukuzwa kwenye chama chake. Tukasikia kuwa yuko mbioni kujiuzuru yeye mwenyewe kabla ya kusubiri ahukumiwe kufukuzwa. Amekuwa mstari wa mbele kupinga ongezeko la posho ya wabunge kutoka 70,000 hadi 200,000 kwa kila kikao akidai ni aibu kwa wabunge kukubali dhulma hiyo wakati wao wanafanya kazi masaa 8 tu ukilinganisha na madaktari wanaokesha kwenye mahospitali na kufanya kazi masaa 36. Mbunge huyu pia msimamo wake kwenye suala la madaktari umekuwa wazi sana. Yote haya yamepelekea kuwa tofauti na wenzake na hata kupelekea kuzomewa, kuzongwa na wenzake na kuambiwa akae chini kwenye vikao.

Wachunguzi wa mambo ya siasa wanaona Kigwangalla amekuwa kimya mno bunge hili ikilinganishwa na mabunge mengine ambapo alikuwa maarufu kwa kuonyesha umahiri wake wa kutumia vizuri kanuni za bunge kwa kuomba mwongozo wa spika na kuonesha upana wa uelewa wake wa mambo mbali mbali kwa kutoa taarifa kwa wabunge wenzake wakiwa wanaongea. toka bunge hili lianze, katika hali ya kushangaza, Kigwangalla amekuwa kimya kabisa! Ndiyo kusema wamefanikiwa kumnyamazisha ama hana hoja tu? Ametuacha na maswali mengi zaidi ya majibu. hebu aibuke hapa atoe majibu.
 
hana lolote attention seeker tu

Ni bora kama ana seek attention kwa mambo ya msingi kama kupinga ongezeko la posho za wabunge, kuliko kutafuta umarufu usio na kichwa wala miguu kama wa Nape kusema kwamba atawashughulikia mafisadi kwa kuwavua gamba
 
....Nakubaliana nawe Mkuu
 
i hope kamati yake inamfanya awe busy haswa ukizingatia mbinu wanazotumia madaktari kuendeleza mgomo ni za hali ya juu sana hivyo ni lazima wawe makini ili kuja na kitu na sio siasa.
 
Mbona tunamsikia ata leo ktk vyombo vya habari kaongea....weulikua unataka aongelee wapi na uku hoja hiyo bungeni ilipingwa na spika/naibu spika akipata muda wa kuongea mbona ataongea....huyu ni msomi tofauti na BEATRICE SHELUKINDO mpaka ameanza kuingia choo cha kiume......ungesema yuwapi ANNE KILANGO MALEC....... Ungeeleweka
 
Ni bora kama ana seek attention kwa mambo ya msingi kama kupinga ongezeko la posho za wabunge, kuliko kutafuta umarufu usio na kichwa wala miguu kama wa Nape kusema kwamba atawashughulikia mafisadi kwa kuwavua gamba

hata mie ninakuunga mkono mkuu.. mradi suala la msingi analolipigania..
 
Vipi kwani na yeye wameshamlisha sumu, masikini weeeeeeee angojee kupukutika nywele na ngozi.
 
Wachunguzi wa mambo ya siasa wanaona Kigwangalla amekuwa kimya mno bunge hili ikilinganishwa na mabunge mengine ambapo alikuwa maarufu kwa kuonyesha umahiri wake wa kutumia vizuri kanuni za bunge kwa kuomba mwongozo wa spika na kuonesha upana wa uelewa wake wa mambo mbali mbali kwa kutoa taarifa kwa wabunge wenzake wakiwa wanaongea. toka bunge hili lianze, katika hali ya kushangaza, Kigwangalla amekuwa kimya kabisa! Ndiyo kusema wamefanikiwa kumnyamazisha ama hana hoja tu? Ametuacha na maswali mengi zaidi ya majibu. hebu aibuke hapa atoe majibu.

Kweli ukistaajabu ya Mussa ........, Katika Bunge la JMT mbunge maarufu na mahiri ni yule anayeongoza kwa kuomba miongozo ya Spika?! This is Only Possible in Tanzania.

Wenzetu wabunge mahiri ni wale wanaojenga hoja za nguvu wakati wa kuchangia mijadala mbalimbali bungeni, hasa ile inayolenga kuisimamia serikali na kutetea masilahi ya wapiga kura.

Kama umahiri wa wabunge tunaupima hivyo na wonder wabunge "Mahiri" wa bunge la JMT wanapitisha rasmu ya mabadiliko ya sheria na hata kabla sheria hiyo haijaanza kutumika wanarudishiwa tena kuifanyia sheria husika mabadiliko.

Nafikiri watanzania tafasiri ya misamiati ya u-maarufu na u-mahiri ni tofauti kabisa na watu wengine duniani kote!
 
nataka nimtetee kidogoooo.... anapisha mwanaharamu apite...nadhani anaogopa kufanya conflict of interest...udaktari wake na uanasiasa wake..... nayo hii ni proffessionalism
 
Tulishamshauri siku nyingi kuwa huko aliko siko kama alivyopafikiria, he was going deep in shallow water!
 
hivi karibuni mbunge wa nzega (ccm), dkt. Hamisi kigwangalla amekuwa kwenye kurasa za mbele za magazeti mbalimbali na mitandao ya kijamii kuhusiana na misimamo yake madhubuti isiyoyumba iliyopelekea kutaka kufukuzwa kwenye chama chake. Tukasikia kuwa yuko mbioni kujiuzuru yeye mwenyewe kabla ya kusubiri ahukumiwe kufukuzwa. Amekuwa mstari wa mbele kupinga ongezeko la posho ya wabunge kutoka 70,000 hadi 200,000 kwa kila kikao akidai ni aibu kwa wabunge kukubali dhulma hiyo wakati wao wanafanya kazi masaa 8 tu ukilinganisha na madaktari wanaokesha kwenye mahospitali na kufanya kazi masaa 36. Mbunge huyu pia msimamo wake kwenye suala la madaktari umekuwa wazi sana. Yote haya yamepelekea kuwa tofauti na wenzake na hata kupelekea kuzomewa, kuzongwa na wenzake na kuambiwa akae chini kwenye vikao.

Wachunguzi wa mambo ya siasa wanaona kigwangalla amekuwa kimya mno bunge hili ikilinganishwa na mabunge mengine ambapo alikuwa maarufu kwa kuonyesha umahiri wake wa kutumia vizuri kanuni za bunge kwa kuomba mwongozo wa spika na kuonesha upana wa uelewa wake wa mambo mbali mbali kwa kutoa taarifa kwa wabunge wenzake wakiwa wanaongea. Toka bunge hili lianze, katika hali ya kushangaza, kigwangalla amekuwa kimya kabisa! Ndiyo kusema wamefanikiwa kumnyamazisha ama hana hoja tu? Ametuacha na maswali mengi zaidi ya majibu. Hebu aibuke hapa atoe majibu.
u know kobe akitulia ujue anatunga sheria so usiwe na wasiwasi na kingwala coz kwa sasa anajipanga kusudi asije kurupuka kama wenzie wengi wa magamba.
 
Tulishamshauri siku nyingi kuwa huko aliko siko kama alivyopafikiria, he was going deep in shallow water!

Shida sasa ni namna ya kutoka huko aliko, ukizingatia kwamba ubunge wake aliupata baada ya sisiem (isomeke mwenyekiti wa sisiem)kumvua uraia Husseni Bashe, ambaye alimshinda Kigwangallah kwenye kura za maoni
 
mi namkubali kigwangalah kwa misimamo yake...!

mnyonge anyongwe tu lakin haki yake apewe
 
kigwangala hajamaliza intern,alitaka kuutumia mgomo huu ili nae apate mwanya wa kufanya inten awe dokta kamili.hana lolote yule.
 
ulitaka awe anaropoka ovyo kama mponda au?kumbuka an empty can makes the most noise
 
Back
Top Bottom