Kigwangalla atangaza nia kuutaka Urais 2025!!!

Kuna watu wanaogopa sana kuwaza vitu vitu vikubwa, mimi si mmoja wao. Hata kufika tu hapa kwenye udaktari haikuwa rahisi (jambo lenye kuwezekana) lakini mimi niliamini inawezekana na nikapigana mpaka nikafika - na kwa hakika halikuwa jambo la ghafla, ama la kufikirika tu, lilikuwa ni jambo lililohitaji discipline, bidii na umakini wa hali ya juu - qualities ambazo nilikuwa nazo na hivyo sikupata tabu sana kufikia ndoto ile...leo ni daktari! Rafiki yangu George McKenzie na mke wangu (toka akiwa Girlfriend wangu) anafahamu, kuwa niliwaza sana kuwa Mbunge siku moja na ndoto hii ni ya siku nyingi, na ndiyo maana ilipokamilika nikaamua kufanya kazi kwa bidii kwelikweli, haikuwa rahisi kuwa Mbunge, ilihitaji uwe na pesa nyingi, uwe maarufu, uwe na nguvu na uvumilivu wa kutosha ili uweze kuwa Mbunge (mtu yeyote mwepesi wa kukata tamaa angeweza kuacha kabisa kuota kuwa MB) - sifa hizo nilikuwa nazo na sasa nimekuwa Mbunge! Leo hii nimeona watu wengi tu wa ajabu ajabu wanatamani kuwa 'Rais' wa nchi, nikaogopa na kushangaa sana, kwamba hata hawa wanatamani kuwa 'Rais' mbona ni wa ajabu ajabu sana, mbona hawafai kabisa - nikaona kama mimi ninawaona hao hawatoshi kuwa 'Rais' wa nchi yangu na mimi nimetulia tu sifanyi lolote, basi kama nilivyojaaliwa kuwa Doctor, na baadaye Mbunge, mambo ambayo katika hali ya kawaida ni magumu kwa mtu mwenye background kama yangu, haitoshindikana kwa hawa jamaa (japokuwa hawatoshi) kufanikisha ndoto zao na siku moja kuja kuwa 'Rais'. Mimi hupenda kuchukua hatua, na huwa sipendi kuwa mtazamaji tu ama mlalamikaji! Niko serious, naota ndoto ya kuwa Rais wa nchi yangu, Mungu nisaidie!
https://www.facebook.com/hamisi.kigwangalla
 
Acheni ujinga wenu who is kigwangala? Tulete hoja za kujenga nchi siyo upuuzi wenu Oh Kigwangala eti awe rais!
 
Wakati tukienda mitamboni nimepata habari kuwa Kigwangalla akiwahutubia wananchi wa Nzega leo jioni ametangaza kuwa na ndoto za kuwania Urais 2025! Alisema:
'Kwa hakika dunia inakuwa mahala. Pabaya pa kuishi si kwa sababu ya watau wabaya bali kwa sababu ya ukimya wa watu wazuri..watu safi na wazuri kama mimi, japokuwa tuko wachache, ni lazima tujipange na tusimame imara kuutafuta uongozi wa nchi yetu la sivyo kundi kubwa la watu wabaya litatutawala na tutabaki tukisaga meno - wanaodhani watanitoa ubunge kirahisi wanaota ndoto za fisi, wanasubiri nyuma ya mtembea kwa miguu wakidhani atadondosha mkono, sina mpango wa kuachia ubunge hata kidogo, wajiandae kupambana na mimi ndani ya chama na hata wale wa upinzani na nina hakika nitawashinda tu, maana safari hii haikomi mpaka 2025 nitakapogombea Urais'

Alitoa kauli hiyo huku akishangiliwa na umati mkubwa wa wapiga kura wake. Sikuwahi kujua kama huyu dogo anapendwa na watu wake namna hii!! Wamemshangilia mpaka nikaogopa. Anaongea kwa kujiamini sana kiasi cha kumuaminisha kila anayemsikiliza

Jamani nyerere alisema ni bora kujipima mwenyewe kabla HUJASIMAMA mbele ya kadamnasi. Yeye mwenyewe ni kituko, itakuwaje siku akianza kutoa maneno ya vituko mbele ya hadhara?
 
Back
Top Bottom