Kigwangalla atangaza nia kuutaka Urais 2025!!!

Le Grand Alexei

Senior Member
Nov 9, 2011
116
83
Wakati tukienda mitamboni nimepata habari kuwa Kigwangalla akiwahutubia wananchi wa Nzega leo jioni ametangaza kuwa na ndoto za kuwania Urais 2025! Alisema:
'Kwa hakika dunia inakuwa mahala. Pabaya pa kuishi si kwa sababu ya watau wabaya bali kwa sababu ya ukimya wa watu wazuri..watu safi na wazuri kama mimi, japokuwa tuko wachache, ni lazima tujipange na tusimame imara kuutafuta uongozi wa nchi yetu la sivyo kundi kubwa la watu wabaya litatutawala na tutabaki tukisaga meno - wanaodhani watanitoa ubunge kirahisi wanaota ndoto za fisi, wanasubiri nyuma ya mtembea kwa miguu wakidhani atadondosha mkono, sina mpango wa kuachia ubunge hata kidogo, wajiandae kupambana na mimi ndani ya chama na hata wale wa upinzani na nina hakika nitawashinda tu, maana safari hii haikomi mpaka 2025 nitakapogombea Urais'

Alitoa kauli hiyo huku akishangiliwa na umati mkubwa wa wapiga kura wake. Sikuwahi kujua kama huyu dogo anapendwa na watu wake namna hii!! Wamemshangilia mpaka nikaogopa. Anaongea kwa kujiamini sana kiasi cha kumuaminisha kila anayemsikiliza
 
I could say a few things about plagiarism, but this is Kigs, what do you expect.

After all anafuata nyayo za baba yake Nyerere.

Nachukia sana nikiona wanasiasa wanatumia maneno ya Bertrand Russell huko, au St Augustine, au Martin Luther King, halafu hawatoi attribution. Wanataka kuonekana kama ndio wao waliosema kwa mara ya kwanza maneno hayo.

Natumai mbio za urais hazijaanza na plagiarism.
 
Nilivyokuwa mdogo zamani sana nakumbuka kuna mtu aliwahi niambia kuwa kuna watu WANAOTA wakiwa wanatembea, hawajalala , yaani wakiwa kwenye shughuli zao za kawaida. Nilijiuliza sana inakuaje mtu anaota bila ya kuwa amelala??

Sasa siku hizi ndio naanza kuuelewa huo msemo

Huyu jamaa ni aina ya watu waliokuwa wanazungumziwa na yule mzee

ANAOTA HUKU AKIWA KATIKA SHUGHULI zake za kila siku ambayo matokeo ya ndoto hiyo ni
KUJIDANGANYA
 
Wakati tukienda mitamboni nimepata habari kuwa Kigwangalla akiwahutubia wananchi wa Nzega leo jioni ametangaza kuwa na ndoto za kuwania Urais 2025! Alisema:
'Kwa hakika dunia inakuwa mahala. Pabaya pa kuishi si kwa sababu ya watau wabaya bali kwa sababu ya ukimya wa watu wazuri..watu safi na wazuri kama mimi, japokuwa tuko wachache, ni lazima tujipange na tusimame imara kuutafuta uongozi wa nchi yetu la sivyo kundi kubwa la watu wabaya litatutawala na tutabaki tukisaga meno - wanaodhani watanitoa ubunge kirahisi wanaota ndoto za fisi, wanasubiri nyuma ya mtembea kwa miguu wakidhani atadondosha mkono, sina mpango wa kuachia ubunge hata kidogo, wajiandae kupambana na mimi ndani ya chama na hata wale wa upinzani na nina hakika nitawashinda tu, maana safari hii haikomi mpaka 2025 nitakapogombea Urais'

Alitoa kauli hiyo huku akishangiliwa na umati mkubwa wa wapiga kura wake. Sikuwahi kujua kama huyu dogo anapendwa na watu wake namna hii!! Wamemshangilia mpaka nikaogopa. Anaongea kwa kujiamini sana kiasi cha kumuaminisha kila anayemsikiliza

Kwa CCM BADO kuna ULE MKONO WA SHOKA ndani ya CCM hata ukipata kura Milioni 40 utanyimwa na aliyepata kura elfu 3 na anamjua MAMA WAMA atapewa hicho kiti; GUESS WHAT na atashinda huyo aliyepata kura elfu 3; Wewe Nenda kazini UDAKTARI au KULIMA ikishindikana ANZA kuongea Mwenyewe...
 
Mr. Dhaifu amefanya mpaka urais umekuwa taasisi cheap kila mtu anaitaka! Nami natangaza nia kuwa nitagombea urais mwaka 2015 kupitia CHADEMA. Khaa! Hata wewe unayesoma hapa changamka tangaza NIA.
 
Nina hofu anaota ingali amesimama!

MUNGU mwenye mamlaka atupe kutufikisha hapo 2015 na tumwone katika kauli hii kama hajakimbilia ughaibuni mchana kweupe!

Hv anafikiri watu wamelala eeeeehh!
Atashanga!
 
Mleta mada ameandika ni mwaka 2025 na wala sio 2015 kama watu wengi wanavyonukuu humu.

Halafu kila mtu anajua mazishi rasmi ya CCM ni mwaka 2015, huyu jamaa atagombea kwa chama gani?

Wakuu embu nisaidieni kwanini huyu jamaa anamwogopa sana Hussen Bashe?
 
Jamani hata mm Chinga boy natangaza kusimama kama mgombea binafsi inaelekea uraisi ni kazi rahisi mno nina uhakika Tandahimba watanipa kura mwana wa pakaya teteteeeeh JK Wee
 
Hata mimi nilipokuwa darasa la kwanza mwalimu wetu alisema mmoja wetu atakuwa rais, yaani kiguundala ndo anakumbuka leo, shithead.
 
mtu anashinda facebook muda wote kubishana na watu halafu nae anataka urais! Rais anaewaza kusomea watu al badil!
 
Back
Top Bottom