Kigwangalla apinga Spika kuleta madaktari wa India Apollo, apingwa na wenzake!

Hii Apolo ni hospitali ya CCM huko India nini? Maana hata EPA ilikuwa na mambo mambo ya India. Wakishikwa na kifua wanaelekea mara moja. Nasikia Ikulu ikikupatia kikaratasi unapata matibabu haraka.
 
Hivi hiyo hospitali ya Apolo nani anaipigia chapuo kila siku maana inaonekana kama ni tawi la Muhimbili kila kiongozi akijisikia mafua breki ya kwanza ni hapohapo wagonjwa wa moyo wa Dr Kanabar ni Apolo nadhani hata Makinda alienda kuchekiwa afya yake palepale hivi majuzi.
Why is it always Apolo ina maana hakuna hospitali nyingine India zaidi ya hiyo picha inayoonekana kuna mtu hapa katikati anajitengenzea mkwanjwa toka serikalini kwa kufanya uwakala na hawa wahindi.
Kwa hili nampa big up Kigwangwala kwa kuliona hili nakuwashauri wenye nazo kumpotezea Lusinde kwa walioona CV yake hapa jamvini ni mtu aliyebobea kwenye shughuri za utumbo kwa hiyo haishangazi kusikia anaongea utumbo kila anapochangia maada.

Being a male is the matter of birth being a man is the matter of age but being a gentleman is the matter of chioce.
 
hakuna sheria kweli ya kuwang'oa wabunge kama hawa madarakani kweli? this is too much hizo hela wangetengeneza madawati mangap? yani watu wabafeli maisha ambao tayari wanamaisha wanazidi kukandamiza wananchi? hawa dawa yao ndogo tu... ni wakati media sasa iamke bila kuhofia kufungwa wala nini wafanye kama wanavyofanya bbc ama aljazeera wabunge kama hawa unamchambua siku nzima ili watu wapate uchungu.... yani unaanza kuchambua maisha yake toka mwanzo maisha kabla na baada ya ubunge mbona watajirekebisha.
 
Nahisi kama jambo linataka kufichwa juu ya afya za wabunge wetu na ndiyo maana wazee wa Apollo wanapigiwa chapuo.
 
Ndugu zangu, nchi hii ni kama imeingiwa na laana! Spika wa Bunge anataka madaktari wa kuwapima afya wabunge watoke Apollo, India. Mbunge wa Nzega, Dk. Kigwangallah amepinga. Wabunge kadhaa wamepinga pia. Lakini inaelekea Makinda ni kama vile ana 10% ndani ya ujio huo wa madaktari. Ameshupalia suala hilo kwa nguvu zote.

ushauri wangu: Watanzania wote, bila kujali itikadi na imani zetu, tushikamane kupinga upuuzi huu kwa nguvu zote. Makinda akilazimisha, tuhakikishe kuwa tunaandaa mabango ya kutosha, na hata kuwazuia kabisa hao madaktari kutua hapa nchini. Ujio wao ni fedha nyingi sana kutoka kwa walipa kodi. Isitoshe, hii ni fedheha kubwa sana kwa madaktari wetu ambao shida yao ni vifaa tu! Tukiendekeza tabia hii ya kuleta madaktari kuwatibu viongozi, kamwe huduma zetu za afya hazitaboreshwa. Tushikamane kama tulivyofanya kwenye Fao la Kujitoa.

nawasilisha.
 
nakubaliana na wewe na tuwapokee na mabango yaliyoandikwa kuwa "wanasiasa wanakuja kuwapima wanasiasa" watakuwa na matatizo ya kiafya ambayo wakipimwa humu nchini lazima siri zitamwagika ndio maana kasimamia hilo. Babu wa samunge hakuwasaidia.
 
We yanakuhusu nini? Wapimwe wasipimwe utafaidika na nini?ni sawa na mtoto aandamane na mabango kumzuia baba yake asipitie bar kupata moja moto moja baridi baada ya kutoka ofcn badala ya kukaa ndani na kusoma,mind your own business.
 
Wabunge wakiumwa hao india! hao madaktari waende hosptali za rufaa watibu watanzania wanaoteseka.
 
Tupinge kwa kufikiri wakuu, mna hakika gani na afya ya huyo mama aliyependekeza hivyo?

Yawezekana ana magonjwa tata yasiyo na idadi kiasi asingependa siri zake zigunduliwe na Mtanzania, hususan ambaye anakerekwa na baadhi ya mambo ya ajabu ajabu anayofanya mjengoni, hili likiwa mojawapo.
 
We yanakuhusu nini? Wapimwe wasipimwe utafaidika na nini?ni sawa na mtoto aandamane na mabango kumzuia baba yake asipitie bar kupata moja moto moja baridi baada ya kutoka ofcn badala ya kukaa ndani na kusoma,mind your own business.

Sina hakika na IQ ya huyu mtu! Haya ni matatizo ya madarasa ya kata! Lazima ujue kuwa hao madaktari wanaletwa na kutunzwa kwa fedha ambazo zingesaidia masikini wa nchi hii. Siwezi ku-maind my business wakati fedha zinazotafunwa ni zetu!
 
Eti zinazotafunwa ni hela zetu?wamekubrainwash mpaka ela za serikali wanazonunulia magari ya serikali unasema yenu,mbona huwa yanakupita stand ukiwa unasubiri daladala kama ni ya kwenu?
 
Eti zinazotafunwa ni hela zetu?wamekubrainwash mpaka ela za serikali wanazonunulia magari ya serikali unasema yenu,mbona huwa yanakupita stand ukiwa unasubiri daladala kama ni ya kwenu?

Una akili za kuazima wewe! Bangi la mchana halifai!
 
Sioni wanachokuja kufanya kwani hao si wahindi sawa na wale wa pale agha khani?mbona weupe tuu hao?mbona ndugu zetu wanafia pale huku wao wakiendelea kutengeneza bill?
 
Hakuna haja ya sisi kuandamana hao wabunge kama hawataki kupimwa wenyewe ndio wanatakiwa wagome kupimwa, watampima Makinda peke yake.
 
Eti zinazotafunwa ni hela zetu?wamekubrainwash mpaka ela za serikali wanazonunulia magari ya serikali unasema yenu,mbona huwa yanakupita stand ukiwa unasubiri daladala kama ni ya kwenu?
Pole sana, yawezekana hata elimu ya upili hujaipata. Hivi huwezi kujua kwamba shughuli za serikali zinaendeshwa na kodi za wananchi?
 
Hakuna haja ya sisi kuandamana hao wabunge kama hawataki kupimwa wenyewe ndio wanatakiwa wagome kupimwa, watampima Makinda peke yake.

Sa wakigoma kupima wakati wapimaji washafika Bongo ndio hawatalipwa kodi zetu? Tunahitaji kudemonstrate kabla hawajaja, zaidi ya hapo na sie tutakuwa mapunguani tu!
 
ndugu zangu, nchi hii ni kama imeingiwa na laana! Spika wa bunge anataka madaktari wa kuwapima afya wabunge watoke apollo, india. Mbunge wa nzega, dk. Kigwangallah amepinga. Wabunge kadhaa wamepinga pia. Lakini inaelekea makinda ni kama vile ana 10% ndani ya ujio huo wa madaktari. Ameshupalia suala hilo kwa nguvu zote.

Ushauri wangu: Watanzania wote, bila kujali itikadi na imani zetu, tushikamane kupinga upuuzi huu kwa nguvu zote. Makinda akilazimisha, tuhakikishe kuwa tunaandaa mabango ya kutosha, na hata kuwazuia kabisa hao madaktari kutua hapa nchini. Ujio wao ni fedha nyingi sana kutoka kwa walipa kodi. Isitoshe, hii ni fedheha kubwa sana kwa madaktari wetu ambao shida yao ni vifaa tu! Tukiendekeza tabia hii ya kuleta madaktari kuwatibu viongozi, kamwe huduma zetu za afya hazitaboreshwa. Tushikamane kama tulivyofanya kwenye fao la kujitoa.

Nawasilisha.



nimemfatilia vizur sana kuhusu hilo
nahis ana asilimia flani kwa ujio huo,,sion mantiki yake kbs
2015 laiti iwe kesho tuondokane na uozo na fedheha za kuwa na viongozi kama hawa
hapendezi kwa kujenga HOJA yule mama kama vile asivopendeza yeye mwenyewe
sijui anatambia kitu gani gwinji makinda,sijui kasahau kua kufa kupo??
Tupeni nafasi ya kuondokana na hizi stress zenu..
 
Watu wengine wana magonjwa ya akili sijui? Wewe unashindwaje kuona logic iliyopo hapo? inamaana hulipagi kodi au? Yaani hata huna uchungu na jasho lako? au wewe nawe ndo wale wale? Ama kweli mtii huu una mizizi mikuu na matawi yamekuwa mengi!
 
Back
Top Bottom