Kigwangalla apinga Spika kuleta madaktari wa India Apollo, apingwa na wenzake!

Huyu Spika naye na akili ya aina gani jamani!! Yaani hata kwa kutumia elimu yake ya diploma, hawezi kuelewa kwamba uamuzi kama huo hauna tija kisiasa?
 
HUYU dogo kaongea ukweli mtupu, panapo stahili heshima basi tumpe pongezi zake, thanks Huyo mshenzi Lusinde atakiona cha moto
 
HUYU dogo kaongea ukweli mtupu, panapo stahili heshima basi tumpe pongezi zake, thanks Huyo makalio Lusinde atakiona cha moto
 
Siamini kama hii statement imetolewa na mtu kama makinda. Kweli ukistaajabu ya musa..............
 
Spika anajua madaktari wetu hawana morali na pia wengi wameikimbia nchi.
 
Kwa mara ya kwanza Dr. Mhe. Kigwangwala amesema jambo la maana, ndiyo maana wahenga walisema usitupe mtoto akikuwa utaona umuhimu wake big up K.
 
*Moja ya madai ya msingi ya madaktari walipogoma ilikuwa ni
''KUPINGA MTINDO WA VIONGOZI WA KISERIKALI KWENDA NJE YA NCHI KUTIBIWA AU KUCHUNGUZWA AFYA ZAO KWA MAGONJWA AMBAYO YANAWEZA KUTIBIWA AU KUCHUNGUZWA HAPA HAPA NCHINI NA MADAKTARI WA KITANZANIA''

*Baadhi ya watu waliwabeza na wengine waliamini propaganda za JK kuwa madaktari wanagoma ili kulipwa pesa nyingi sana na sio kitu kingine chochote.

*Huu ni mwanzo tu wa mauzauza mengi kwenye sekta ya Afya ambao tutaendelea kuyashuhudia siku kwa siku.

*Sasa madaktari wa India wanakuja kuwachunguza waheshimiwa wabunge afya zao hapa Tanzania!!!!!
 
Kigwangalla ni member hapa, kama chanzo cha taarifa ni sahihi nakupongeza japo kushindwa ''uzalendo' wa mjengoni.
Mh Anne Makinda kuyasema haya sidhani kuwa ni ajabu kubwa, anachofanya ni kuungana na akina Sophia Simba kuendelea kututoa wasi wasi wa aina ya viongozi tulio nao.

Lakini pia hayo kama aliyasema basi anatutoa hofu zaidi kuhusu viti maalumu na uwezo wa akina mama.
Nasema uwezo wa akina mama kwasababu akiwa mwanamke wa Tanzania alitakiwa aelewe hili vema zaidi kuliko Lusinde.
Alitakiwa aelewe uchungu wa vichanga vinavyofariki kwa kukosa Oxygen au mja mzito kununu viwembe vya kukatia vitovu.

Kibaya zaidi tulidhani wale wanaosema watatusaidia kuikomboa nchi nao pia waungane na Makinda.
Linapokuja suala la masilahi binafsi vyama pembeni masilahi mbele.

Wataalamu wapo, kama hakuna vifaa basi tujiulize zinatoka wapi pesa za kuwaleta Wahindi au kuwapeleka viongozi Apollo.
Hakuna hesabu yenye jibu sahihi kwa mwenye akili timamu isipokuwa waheshimiwa tu wanaweza kuja na formula.

Tuangalie bajeti ya bunge halafu tuilinganishe na ya Hospitali ya Muhimbili.

Wenzetu wa Kenya wao walisimama kidete dhidi ya 'wanyang'anyi' hawa wanaoitiwa waheshimiwa.
Sisi wakati madaktari wanagoma, tulisema wamekosa uzalendo,hawana utu ni wahuni n.k.
Leo tumebaki tumeduwaa, tunashangaa nini? Hivi utapanda mahindi utegemee kuvuna maembe?

Demokrasi haifanyi kazi bila enforcement, na hiyo enforcement haiwezekani kwa kutumia sheria walizoziweka wao.
Huwa najiuliza Watanzania tumelogwa au tumelishwa limbwata gani?
Nawapenda sana wakazi wa mkoa wa Mbeya!! I truly love 'em
 
alimjia juu Lema kwa kumwambia ukweli pinda kuwa serikali ni wauaji kuletewa usahahidi kimya.hakutegemea kuwa spika mchumia tumbo matunda ya siasa za visasi za ccm
 
Ndugu zangu , hii inaonyesha wazi jinsi ambavyo tatizo la msingi tumeshindwa kulibaini katika mfumo wetu wa afya. Wataalamu wetu ni wazuri sana tena wana uelewa mpana sana.

Tatizo moja ni vifaa hamna kama Citscan, MRI n.k. Wenzetu wamewekeza huko kwenye tiba. Spika wetu na wabunge wanaomuunga mkono walipaswa wafahamu kuwa wanahitaji kuishinikiza serikali kuelewa madai ya madaktari juu ya vifaa vya tiba.

Hawa madaktari wetu waliopo Muhimbili, Aghakhan, TMJ , nk wanafahamika hata huko Apollo kwa umahili wao wa kugundua matatizo bila ya kuwa na vifaa vya kupimia.

Serikali inatakiwa ifikie kuwa na Diagnosis Centre moja at least kwa nchi nzima.
 
Ndugu zangu , hii inaonyesha wazi jinsi ambavyo tatizo la msingi tumeshindwa kulibaini katika mfumo wetu wa afya.

Wataalamu wetu ni wazuri sana tena wana uelewa mpana sana. Tatizo moja ni vifaa hamna kama Citscan, MRI n.k. Wenzetu wamewekeza huko kwenye tiba.

Spika wetu na wabunge wanaomuunga mkono walipaswa wafahamu kuwa wanahitaji kuishinikiza serikali kuelewa madai ya madaktari juu ya vifaa vya tiba.

Hawa madaktari wetu waliopo Muhimbili, Aghakhan, TMJ , nk wanafahamika hata huko Apollo kwa umahili wao wa kugundua matatizo bila ya kuwa na vifaa vya kupimia. Serikali inatakiwa ifikie kuwa na Diagnosis Centre moja at least kwa nchi nzima.
 
Hakuna ubaya madaktari wa nje wa kija mbona hata ccbrt kuna wataalaam wa kitanzania lakini mara kwa mara tunaona wataalaam wa nje wakija?

Madaktari wa India pia si mara ya kwanza kuja Tanzania, huletwa mara kwa mara kuja kupima afya za Watanzania, isiwe mwao kualikwa na Anne Makinda. hiyo ni moja ya kuzidisha mahusiano mema na kubadilishana uzoefu na madaktari wetu.

Anne anawatakia mema wabunge ambao wengi hawako fit.

MamamMakinda, Kigwangallah saa ngapi atapima waginjwa saa ngapi atapiga porojo za siasa? ni vyema ulivyofanya.
 
Jamani hivi kweli tunaipeleka wapi hii nchi yetu?nadhani kuna viongozi hawana uchungu kabisa na rasilimali za nchi hii,kiufupi hakuna haja ya kuleta wataalam Madaktar from India kwani hapa Tanzania hayo yanawezekana.Lusinde ana kichaaa nadhani yeye na bi Kiroboto.Tuipende nchi yetu na tujiepushe na matumiz mabaya ya pesa JK amka mbona unakua kama umetoka Msoga Leooo.

Kuna mambo mengine bwana yanatia kichefuchefu hata ukiyasikia tu, hivi kweli mtu hafikirii kufanya vile wataelewekaje kwa watanzania? wao wanaona ndo wenye umuhimu mkubwa kujua afya zao na kuwaacha wapiga kura wakigombea Panado 2 kwenye zahati!! ubinafsi uliovuka mipaka hata hivyo haishangazi maana hata posho na mishahara mizuri wanajilimbikizia wao
 
Kama ni kweli, basi Anne Makinda anatakiwa awaombe radhi wakina mama wa Tanzania. Ukatili ulioje? Huyu Anne Makinda hana huruma? Ameenda Mwananyamala na kujionea wagonjwa wanavyopata taabu? Hata huko Jimboni kwake huduma za afya ni mgogoro! Wamama wamekuwa wahanga wakubwa wa huduma mbovu za afya hapa Tanzania. Wanajifungulia chini - tena wakiwa wamebanana kama dagaa. Halafu Spika 'mwanamke' kakazana kuwapa 'anasa' wabunge?

Naiita anasa kwa sababu tayari waheshimiwa hawa wanapata huduma za afya kwenye hospitali za private i.e Agha Khan, na hata wakienda Muhimbili wanakwenda sehemu tofauti na walala hoi. Huu ni usaliti na ukatili wa hali ya juu wa mama huyu kutelekeza wanawake wenziwe na kukumbatia wabunge. Ukatili, ukatili, ukatili...!

Wananchi tunatakiwa kudai sheria mpya -tena haraka. Kodi ya watanzania itatumika kwa matibabu kwenye hospitali za umma ndani ya ardhi ya TANZANIA. Anayetaka kwenda hospitali ya private ndani na nje ya nchi aende kwa hela yake. (ONLY SPECIAL CASES kama ile ya Dr Mwakyembe ndiyo kodi ya watanzania itatumika kwa matibabu nje). Bila ya hawa 'wasaliti' kuonjeshwa makali wanayokumbana nayo walalahoi wananchi, sekta ya afya itakufa, wagonjwa wataendelea kulala sakafuni, na vifo vitazidi. Lazima tukomeshe hili. Inakera sana.
 
Back
Top Bottom