Kigwangalla adai mkataba wa mgodi anajitakia mema kweli?

Mh mbunge afafanue why 20% na sio 50%.hata hivyo this is a good start!

kwa nini iwe hisa na isiwe kugawana matofali ya gold pasu kwa pasu yakishazalishwa ili tuwe na reserve ya gold na tuwasiliane na wateja sisi wenyewe?
 
Igwara gwara is working. Hii ni asimia 20% unayodai, bila kujali itikadi nakupongeza. kumbuka wala wanapata asilimia 3. mimi kweli kabisa siamini, lazima kuna asilimia nyingine zinavuja. Hata kule mwadui ni 49. Hii laana ya viasilimia mchwara, kwa nchiya masikini karibu kupita zote. Jamani hata sisi CCM tuna akili timamu, wabunge katika hili amkeni. Madini ya Tanzania ni ya watanzania, sio wasaini mikataba vyumbani.

wakipatikana 20 CCM Wabunges namna hii, tutakwenda mbele. hawa wala Ruzuku bungeni ndo wanadodesha CCM.

Igwaragwara.
 
Say ye all that you feel, its your right, use it! But note all you my brothers and sisters, that 'Nothing is impossible under the sun!' I am determined to do this and I feel responsible to do good to my country and I will do it...kuna falsafa moja mimi huiamini, kwamba ukichukia jambo lipiganie physically, ukiona hauwezi likemee kwa sauti kali, ukiona hauwezi basi hata walau nuna tu...na hii ya mwisho huwa haipendezi kwa kuwa unakuwa umeonesha unyonge wako! Mimi ntaanza na hiyo option ya katikati kwanza (maana inakubalika na ni njia ya wastaarabu na nina nguvu ya kufanya hivyo), kisha hiyo ya pili kama itabidi...ya tatu sitegemei kuigusa...maana ni njia ya mnyonge na mimi si mnyonge...kwa kuwa kuna wanaNzega na waTanzania nyuma yangu!

Leo hii kila mtu atapenda kui-criticise CCM na viongozi wake lakini kuna tatizo kubwa zaidi ya CCM, tatizo lenyewe ni la kimfumo na kifikra (a system and mindset problem among our people) zaidi miongoni mwa watanzania na bahati nzuri, kama inavyotegemewa, viongozi wetu (watoke CCM au hata CDM) wanatoka miongoni mwetu...kama source/pool ya viongozi ina matatizo, je itakuwaje viongozi wawe Ok? [sipendi kuwatoa kwenye mada!]
 
Say ye all that you feel, its your right, use it! But note all you my brothers and sisters, that 'Nothing is impossible under the sun!' I am determined to do this and I feel responsible to do good to my country and I will do it...kuna falsafa moja mimi huiamini, kwamba ukichukia jambo lipiganie physically, ukiona hauwezi likemee kwa sauti kali, ukiona hauwezi basi hata walau nuna tu...na hii ya mwisho huwa haipendezi kwa kuwa unakuwa umeonesha unyonge wako! Mimi ntaanza na hiyo option ya katikati kwanza (maana inakubalika na ni njia ya wastaarabu na nina nguvu ya kufanya hivyo), kisha hiyo ya pili kama itabidi...ya tatu sitegemei kuigusa...maana ni njia ya mnyonge na mimi si mnyonge...kwa kuwa kuna wanaNzega na waTanzania nyuma yangu!

Leo hii kila mtu atapenda kui-criticise CCM na viongozi wake lakini kuna tatizo kubwa zaidi ya CCM, tatizo lenyewe ni la kimfumo na kifikra (a system and mindset problem among our people) zaidi miongoni mwa watanzania na bahati nzuri, kama inavyotegemewa, viongozi wetu (watoke CCM au hata CDM) wanatoka miongoni mwetu...kama source/pool ya viongozi ina matatizo, je itakuwaje viongozi wawe Ok? [sipendi kuwatoa kwenye mada!]

Umesema vyema, tatizo ni mfumo, mfumo ambao umeasisiwa,kuekwa na unaokingiwa kifua na chama chako, CCM ..sasa ni vema ukaacha ku-beat around the bush mzee. Otherwise matokeo ya zoezi unalolianzisha yameshajulikana kabla hata zoezi kuanza.
 
Dr. Natoa maoni yangu tu. wewe umesomea MBA, je unaonaje ukiwakilisha Bungeni kuwa Wawekezaji wa madini wanapowekeza lengo kubwa ni market ya nje ya nchi na siyo domestic market. Je unaonaje governmentikitengeneza Government godowns kwa ajili ya monitoring productions na ulipaji wa hizo tax au gharama zingine kulingana na production na pia itakuwa rahisikulinganisha import doc kama b/l, bank details, port of exit, details za vessel carrying cargo(land , air or sea).
yaani iwe tunatumia njia ya kuwakilisha amount ya dhahabu iliyonunuliwa toka nchi za nje(Bank proof ya either TT or L/C by buyers into TZ banks for the investor),shipping order from either Airlines or shipping companies in TZ , then the amount of gold can be released from the monitored govenment godown under TRA. Kuliko hii inayotumika wanachimba wao na kuondoa kwa ndege zao. Nataka kusema hivi, hata kama wanatoa1%, basi kawepo kanidhamu fulani kwa serikali kusimamia hata hako ka 1%. Kwa njia wanazo tumia Bank zetu hazipati ingalau ka interest kidogo ka transfers. Think about it Sir, before terminating present that at least kuwe na kafaida kwenye ka Bank ka NMB hapo Nzega. Nakutakia mafanikio mema kwenye kazi hiyo na kwenye maendeleo ya jimbo lako. Tatizo la maji ni sugu sana Nzega, kumbuka na hilo, ndiyo maana Nzega ikaitwa Nzega kwa sababu ya MzegaMzega. Naomba sana Mungu aweze kutupatia mwamko wa kushirkiana nawe kuleta mabadiliko Nzega.
 
Nakuonya dr kigwangalah,usifanye haya kwa ajili * kutafuta sifa au umaarufu,selele alianza kama wqewe,tena alifika mbali zaidi akawa hata hawasemeshi jamaa wa resolute aliishia kupewa zira za kwenda nchi mbalimbali.Nataka nikuulize wewe kwa akili yako unadhani tatizo la nzega ni maji tu?je unadhani kuwa madini ya nzega yatamaliza matatizo maji?tafadhali sana kabla huona boriti kwenye jicho la mwenzio toa kibanzi kwenye jicho lako,unajua kuwa vijana wote wa nzega hivi sasa wanakuchukia sana kwasababu huwajali unapita na gari lako umewafungia vioo.huwasikilizi na hata viongozi wa ccm wilaya huna mahusiano nao mazuri,angalia dosari zako zote ulizonanazo kabla hujaanza kupaparikia mambo mengine
 
Hahaha aa this is a good one!
Government godown for monitoring the whole project is important. Introduce Bungeni. Hii itasaidia at least either Shipping companies au agents na Bank zetu kufaidika na TRA kufaidika zaidi and on top of that kutakuwa na Storage fee kwenye godown.
 
say ye all that you feel, its your right, use it! But note all you my brothers and sisters, that 'nothing is impossible under the sun!' i am determined to do this and i feel responsible to do good to my country and i will do it...kuna falsafa moja mimi huiamini, kwamba ukichukia jambo lipiganie physically, ukiona hauwezi likemee kwa sauti kali, ukiona hauwezi basi hata walau nuna tu...na hii ya mwisho huwa haipendezi kwa kuwa unakuwa umeonesha unyonge wako! Mimi ntaanza na hiyo option ya katikati kwanza (maana inakubalika na ni njia ya wastaarabu na nina nguvu ya kufanya hivyo), kisha hiyo ya pili kama itabidi...ya tatu sitegemei kuigusa...maana ni njia ya mnyonge na mimi si mnyonge...kwa kuwa kuna wananzega na watanzania nyuma yangu!













Leo hii kila mtu atapenda kui-criticise ccm na viongozi wake lakini kuna tatizo kubwa zaidi ya ccm, tatizo lenyewe ni la kimfumo na kifikra (a system and mindset problem among our people) zaidi miongoni mwa watanzania na bahati nzuri, kama inavyotegemewa, viongozi wetu (watoke ccm au hata cdm) wanatoka miongoni mwetu...kama source/pool ya viongozi ina matatizo, je itakuwaje viongozi wawe ok? [sipendi kuwatoa kwenye mada!]
contact zako mkuu naomba, i have package for development for your constuence.
 
Kuna mambo mengi sana kuhusiana na huu mgodi wa Golden Pride ambayo wapiga kura wa Nzega wamekuwa wakiyalalamikia kwa zaidi ya miaka kumi na tatu sasa, na haya mambo yanajulikana kila ngazi ya watendaji wa serikali na hakuna jitihada za kuyatatua...mimi Muwakilishi wao nimeamua kuyafuatilia na kwa hakika sintowaangusha wanaNzega wenzangu...nitayafuatilia mpaka pale nitakapoona yanatatuliwa la sivyo hapatatosha Bungeni!

Hivi juzi, baada ya utafiti wa muda mrefu, nimekabidhi kwa Katibu wa Bunge kusudio la kuliomba Bunge lipitishe azimio la kuufunga mgodi huo kwa kuwa hauna manufaa kwa Taifa, pamoja na mambo mengine mengi!

Kuleta mapinduzi ya kifikra siyo lazima uwe upinzani; wengine tunaamini katika kuleta mabadiliko 'from within the system' na there is plenty you are yet to see from people like me...naanza na hili na kuna mengi yapo njiani! Na siyo lazima kila mtu mwenye fikra mbadala basi ajiunge na CHADEMA...

Stay put,
HK.


Dr. Kigwangall, sikubaliani na wewe kwa hali hali ya Tanzania ya sasa, hakika nakuambia hakuna mwanaCCM yeyote anayeweza leta mbadiliko ya kweli Tanzania, siyo kuwa mtu huyu hanadhamira ya kweli, la hasha, la msingi hapa ni system husika iliyopo ndani ya CCM na watekelezaji wake wote, ni watu ambao wapo kiabishara zaidi, huwezi kuwa na jambo la kulete maendelea kwa watanzania kwa kuwa ndugu zako CCM wezako watakupinga na wakiona unaleta za kuleta watakutafutia sehemu wakuondoe kwenye system yao, kwani wapo kimasirahi zaidi na wala si kwa ajili ya kuwaletea maendeleo watanzania.

Migodi mingi iliyopo Tanzania mikataba yake ni siri kubwa baina ya wawekezaji, serikali na ndugu zetu, wanaojiita wazalendo, ambao ndiyo local share holders na wenye sauti kwenye makampuni hayo na wapo hapo kuhakikisha mambo ya kampuni katika kuwanyonya watanzania yanakwenda sawa, je nao wapo tayari kukuona ukikiwekea kitumbua chao mchanga? hakika hawata kuwa tayari watafanya wawezalo kukondoa kabisa.

Unaweza kuwa na dhamira ya kweli, tatizo ni system nzima ndai ya CCM, haipo tayari kuleta maendeleo kwa taifa hili, ndiyo maana siamini kuwa mtu anayetaka kuleta maedeleo kwa taifa hili au sehemu ya taifa hili atatoka CCM, hakika lazima atoke nje ya corrupted system, lazima awe ni mtu ambaye hafanyi jambo kwa masirahi ya wakubwa wake, hakika lazima mtu huyu atoke nje ya CCM, na wala siyo CHADEMA, chama chochote kile ambacho kipo kwa ajiri ya kumukomboa Mtanzania na matatzio yanayomsonga.

Nashukuru hata wewe umesema kuwa si lazima awe chadema, hii inaonyesha ni IMANI KAISI GANI UNAYO KUKATIKA CHADEMA NA MUSTAKABARI WA MAENDELEA WA NCHI HII, na ndiyo maana hukusema chama kingine.

Hakika, ndugu yangu, unaweza kuwa na moyo mzuri kama wengine wengi, ila system uliyopo ndani ndiyo itakayo kuangusha kwani hawana dhamira sawa na wewe, MAPINDUZI YA KWELI YATALETWA NA WATU WENYE NIA NA MOYO SAFI, NA WATU HAWAO HAWAPO CCM, WAPO NJE YA CCM. muda unakaribia na si muda mrefu.




 
Nguvu ya soda in action a.k.a moto wa kifuu kwenye mapishi ya marage.huwezi mshtaki nyani kwa tumbili atanaswa vibao balaaa.usituongopee mheshimiwa hilo swala liko nje ya uwezo wako tena ukizidi kulichokonoa yatakutokea ya bashe.shauri yako.
 
Hivyo ndivyo Mkwere alivyowadanganya, mbona nchi nyingine wanafanya bila kujali mikataba iliyopo. BTW, mikataba yenyewe ni mirefu zaidi ya miaka 20 kipindi hicho kikifika yatabaki mashimo tu wenyewe watakuwa walishajiondokea...

Angalia nchi kama Zambia, Guinea, Ghana, Zimbabwe, Venezuela wame/wanabadilisha sheria ili rasilimali zao ziwanufaishe zaidi bila kujali kama mikataba ya awali ime-expire au la....

Akina Pinda watamuambia kuwa madai ya Dr Kigwangallah hayatekelezeki MAANA eti ni kinyume na UTAWALA BORA!!
 
Monday, 31 January 2011 20:14 (Mwananchi) Boniface Meena na Sadick Mtulya
MBUNGE wa Nzega (CCM), Dk Hamisi Kigwangalla, amewasilisha hoja binafsi kwa katibu wa Bunge, akitaka Bunge lijadili na kuridhia kufungwa kwa mradi wa kuchimba dhahabu wa Golden Pride, ulioko mkoani Tabora.

Katika hoja hiyo, Dk Kigwangalla amesema mgodi huo unapaswa kufungwa mara moja kwa kuwa una madhara mengi, kuliko faida kwa nchi nchi na Jimbo la Nzega.

Dk Kigwangalla pia ameitaka serikali iwalipe fidia wachimbaji wadogo na wenyeji wananchi waliokuwa wakiishi katika maeneo yanayozunguka mgodi huo, ambao alisema wamenyanyasika na kusumbuliwa kwa ushirikiano wa serikali na wamiliki wa mgodi.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari jana, mbunge huyo alisema mradi huo unaharibu mazingira na hasa ya vyanzo vya maji.

Alisema mradi huo pia unatumia maji mengi zaidi kuliko yanayotumiwa na wenyeji wa eneo hilo.

Alisema "wawekezaji wote kwenye migodi nchini, bila kuangalia makubaliano ya huko nyuma, lazima waigawie nchi hisa na haki ya kumiliki migodi hiyo kwa asilimia isiyopungua 20 vinginevyo, wafunge migodi hiyo na waondoke.".

Katika hoja yake hiyo, mbunge huyo pia amewataka wawekezaji wote wapewe muda usiozidi miezi sita, kukamilisha mchakato huo na kuchukua hatua za kutekeleza azimio la hoja yake.

Pia ametaka katika kila mgodi kuwe na utaratibu wa wazi wa kutangaza mapato na matumizi yanayotokana na shughuli za uchimbaji wa madini.

Hali kadhalika, imetaka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), kutengeneza utaratibu mzuri na wa uhakika wa kujua wawekezaji na mitaji iliyotumika katika kuwekeza na mapato yanayotokana na uchimbaji wa madini katika migodi.

"Kwa pamoja sasa serikali na mgodi watekeleze miradi ya kuendeleza jamii zinazozunguka migodi ili kuwafanya wananchi wauone mgodi iliyoko katika maeneo yao kuwa ni yenye manufaa kwao," alisema Dk Kigwangalla.

Dk Kigwangalla pia ametaka uwekezaji katika sekta ya madini usimame hadi hapo nchi itakapokuwa tayari kuchangia kuwekeza na kumiliki asilimia kubwa ya rasilimali za nchi na kufaidika nazo.

Dk Kigwangalla alisema amefanya utafiti kuhusu hoja hiyo na kwamba ana nyaraka nyingi na uthibitisho juu ya mambo anayotaka yafanyike.

Kwa upande wake, Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR- Mageuzi), David Kafulila, jana aliwasilisha rasmi hoja binafsi ya kutaka serikali iwajibike, kwa kukukubali kuilipa mabilioni ya fedha, Kampuni ya Dowans na kuliingiza taifa hasara kupitia sekta ya umeme.


Hatua hiyo inakuja baada ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), kushindwa kesi, katika Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Migogoro ya Kibiashara (ICC) na kutakiwa kuilipa Dowans Sh 94 bilioni, kwa kosa la kuvunja mkataba.



Katika hoja hiyo, Kafulila anataka serikali , kutoa maelezo ya kina kuhusu sakata hilo , kwa sababu haitakuwa sahihi kulipa mabilioni ya fedha kwa kampuni aliyodai kuwa mmiliki wake hafahamiki. 



Kafulila pia , kulitaka Bunge liazimie kupiga kura ya kutokuwa na imani na Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, kwa madai kuwa ameshindwa kusimamia utekelezaji wa Sera ya Nishati na Mpango Kabambe wa Usambazaji wa Umeme nchini.



Mbunge huyo aliwasilisha hoja yake jana katika ofisi ndogo ya Bunge akiwa ameongozana na Mkurugenzi wa Sheria na Haki za Binadamu wa NCCR Mageuzi, Dk Seng'ondo Mvungi.

Alisema kulingana na jinsi alivyoiandaa, anaamini itafanikiwa na kujadiliwa katika kikao cha Bunge, kitakachofanyika mwezi huu.

Dk Mvungi ambaye ni mwamazuoni aliyebobea katika masuala ya katiba, alisema pamoja na kwamba Dowans imekwisha wasilisha tuzo ya hukumu Mahakama Kuu lakini akasisitiza hakuna kizuizi kwa Bunge kujadili hoja hiyo.

"Kujadili hukumu ya Dowans mahakamani si kigezo na kizuizi cha mhimili wa Bunge kutojadili suala hili.
"Hii ni hukumu na si kesi, kisheria hakuna pingamizi lolote kwa Bunge kushindwa kujadili suala la Dowans,'' alisema Dk Mvungi.

Katika hoja yake hiyo, Kafulila alisema kuwa mgogoro wa nishati ya umeme unaelekea kukomaa na kuwa sehemu ya maisha ya Watanzania.
 
Kuna mambo mengi sana kuhusiana na huu mgodi wa Golden Pride ambayo wapiga kura wa Nzega wamekuwa wakiyalalamikia kwa zaidi ya miaka kumi na tatu sasa, na haya mambo yanajulikana kila ngazi ya watendaji wa serikali na hakuna jitihada za kuyatatua...mimi Muwakilishi wao nimeamua kuyafuatilia na kwa hakika sintowaangusha wanaNzega wenzangu...nitayafuatilia mpaka pale nitakapoona yanatatuliwa la sivyo hapatatosha Bungeni!

Hivi juzi, baada ya utafiti wa muda mrefu, nimekabidhi kwa Katibu wa Bunge kusudio la kuliomba Bunge lipitishe azimio la kuufunga mgodi huo kwa kuwa hauna manufaa kwa Taifa, pamoja na mambo mengine mengi!

Kuleta mapinduzi ya kifikra siyo lazima uwe upinzani; wengine tunaamini katika kuleta mabadiliko 'from within the system' na there is plenty you are yet to see from people like me...naanza na hili na kuna mengi yapo njiani! Na siyo lazima kila mtu mwenye fikra mbadala basi ajiunge na CHADEMA...

Stay put,
HK.

we kigwangalla acha kuwadanganya wana nzega, umewekwa hapo na JK kwa nini usimuulize yeye mwenyewe direct kwani alipokuwa waziri wizara ya madini ndipo madudu kuhusiana na mgodi huu yalipofanyika.

kama ni manufaa kwa taifa - mgodi gani tz unamanufaa kwa taifa. Should we expect another Zitto kabwe??
 
by the way nani alikuwa waziri wa madini aliyesimamia mchakato wa kuanza mgodi huu?
 
Na kama wasipompa?atawafanyaje?
Acheni kutafuta cheap popularity jamani deal za watu izo
 
Back
Top Bottom