Kigwangala: Atangaza VITA na Media

Dr. HK Kigwangalla [MP] on Igunga: Media zimetuonea sana! CCM tutatumia wingi wetu bungeni kuubana Uhuru wa Media, hauna maana! about 3 hours ago

Source: twitter

HK nadhani alikuwa mvuta bangi sekondari, kauli na hoja zake hazijatulia.

Anadai Media haziwatendei haki, ana vyombo vyote vya habari vifanane na tbc, uhuru, na habari leo!
 
Kigwa ni big baby. Ni dr wa nini huyo? Kweli you become what you eat, hizo ndo fikra hafifu za ccm walio wengi. Huwezi kupiga watu mikwara ya namna hiyo karne hii.
 
Walewale wanaona mfumo huu mbovu wa utawala unawanufaisha wanajiapiza kuulinda,huyu anajiita Docta na watu wamembaini kuwa ni Docta feki jina si lake na cheti si ajabu kanunua sasa unategemea nini kutoka kinywani mwa mtu kama huyu??ndoto zake ni siku moja awe naibu waziri au waziri kwenye mfumo huu wa kuinyonya nchi kwa watu wachache,acha apeleke bungeni aone media itakavyo mmaliza.
 
Ile alama ya dole inamaana ya tumbo mbele maendeleo nyuma usituludishe enzi za ujima mageuzi daima
 
naona jamaa anajisahau kwamba ni mbunge wa term moja tu, kama angekuwa hatumii masaburi kufikiri angejiuliza Ben Ali na Mubarak walikuwa wamebana saana vyombo vya habari but at last waliondoka madarakani kwa aibu

Hii mijitu badala ya kuwajibika na kuwaletea wananchi wanaowawakilisha maendeleo wao wanataka kutumia ujinga wa hao wapiga kura wao kujinufaisha wao na familia zao,,ni vema watambua muda wa siasa uchwara umekwisha
 
Prodi,

Sasa kwani nani amekwambia nitagombea tena Ubunge? Mimi ni Mbunge wa 2010 - 2015. Ikifika hiyo 2015 nitaamua kama nigombee tena ama la!
 
Dokta Hovyo Kichwani (HK) tushamzowea maana daima yupo hovyo. Sasa hiyo twitter siyo media? Halafu anajisumbua tu kwani wanamageuzi wameshaanza kuacha kutumia media zinazodhibitiwa kirahisi kama tv, magazeti na redio. Sasa watu wanahamasishana kupitia intaneti. Mie sikumbuki mara ya mwisho nimesoma gazeti lini, wala sitazami tv,,redio ndo hakuna lakini napata habari kila dakika. Sasa wewe Dokta Hovyo Kichwani na magamba na huo wingi wenu baneni uhuru wa media ili muwanyime habari wapiga kura wenu vijijini ambao ndo mnajivunia. Watu wa mjini hawana taabu tutaendelea kuhamasishana. Kwanza unastahili kuwa Profesa wala si Dokta, ila Profesa wa Vilaza.
 
kama ndivyo kesho asishiriki kipindi cha power breakfast.
 
Dr. HK Kigwangalla [MP] on Igunga: Media zimetuonea sana! CCM tutatumia wingi wetu bungeni kuubana Uhuru wa Media, hauna maana! about 3 hours ago

Source: twitter
Madaraka bwana. Ukiwa ndani kiza, ukiwa nje, mwanga. Siku akirudi uraiani kwa kuanguka ubunge au kustaafu, atagundua kwanini wasomi kama yeye ndio kikwazo cha taifa hili kusonga mbele.
 
Back
Top Bottom